Wafanyakazi wa Kampuni ya TATEPA wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika sherehe za MEI MOSI kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2008

    Haki ya nani I bet hawa wafanyakazi wote watafukuzwa kazi J'tatu hivi wamejiamini nini since when mabango yanafanya kazi za kurekebisha tabia za watu no wonder mvumbuzi amegoma kwenda huko maana hicho ni kiti moto si mchezo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2008

    Televisioni za Tanzania za binafsi na serikali hovyo kabisa.

    Nimekuwa nikitafiti jinsi vyombo vya habari hasa Televisioni za mataifa makubwa duniani zisivyojali habari za mataifa madogo maskini duniani hata ziwe kubwa vipi hawazitoi.Jana nimethibitisha kuwa hata Tanzania hali ni hiyo hiyo.Hakuna tofauti.

    Jana nilifuatilia siku ya Mei Mosi nilifuatilia Taarifa za habari zote kupitia Sattelite na Internet kuhusu sherehe za Mei Mosi Iringa nikaona hakuna hata Television moja iliyokuwa Iringa kulionyesha lile tukio ambalo lilifanyika kitaifa kule na kurusha picha zake kuanzia maandamano hadi hotuba.


    Badala ya kuonyesha Lile Tukio kule Iringa Television zote zilijazana uwanja wa Taifa Dar es salaam Zikamwonyesha maandamano ya Mei Mosi pale na hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akihutubia kwa mbwembwe kubwa wakaacha kuonyesha Waziri Mkuu Pinda Aliyekuwa kule Iringa.

    Television zote hazikuona umuhimu wa kuonyesha matukio ya sherehe hiyo ya kitaifa mkoa maskini wa Iringa.Wamegeuka na wao kuwa kama BBC,CNN,n.k ambao huwa ni vyombo vya kusemea matajiri hasa tu.Na vya kwetu vimekuwa midomo ya miji tajiri tu kama Dar es salaam.

    Hata blog zote za watanzania nilipitia ikiwemo ya Majid Mjengwa ambaye yuko kule Iringa hakuna hata moja iliyotoa picha za mei mosi kule iringa wakati matukio hata ya mchawi kuanguka dare s salaam huchapishwa hapo hapo kwenye blog

    Hata Televisioni ya Taifa hawakwenda kurusha moja kwa moja matangazo yao kule wakati wanaishi kwa kutegemea kodi za watu wa Iringa.Walichokifanya badala ya kuonyesha picha za kule walionyesha picha moja ya Mgando ya kamera ambayo ni ya siku nyingi sana zilizopita ya Waziri Mkuu panda wakaanza kusema aliyosema Iringa!!!!

    Kama mkereketwa wa kujitegemea wa mikoa maskini Tanzania nalaani kitendo cha Televisheni zote za Tanzania kutorusha picha za sherehe za mei mosi kitaifa Iringa na badala yake kurusha picha za mei mosi kimkoa za Dar es salaam.

    Mkoa wa Iringa umeonewa kwa hili na naviomba vyombo ya habari uombeni samahani huo mkoa kama kweli mumepania kutokuwa kama BBC na CNN .Televisioni ya Taifa (TBC) mumewaonea walipa kodi wenaolipa mishahara na marupurupu yenu kupitia kodi zao wa Iringa.Na bloggers watanzania wenye blog mumekosa uzalendo kwa kutoonyesha kilichokuwa kinaendelea kitaifa kule Iringa siku ya Mei mosi mkashindwa kuleta kwenye blogs zenu picha live! Hamjui umuhimu wa vitu au sherehe za kitaifa mumekalia umbeya tu kuujaza kwenye blogs zenu!

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2008

    Koloboi nakubaliana na wewe.Sijui ilikuwa ni dharau ya wazi kwa Waziri Mkuu Pinda kwasababu ni mgeni katika nafasi yake au ilikuwa dharau kwa wenyeji wa Mei Dei wenyeji wa Iringa?Au wanahabari walikosa Mshiko?Au hawakupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Uongozi wa Mkoa wa Iringa?Maana tumeshindwa kuwaelewa.Kutwa nzima katika TV tunaona matukio ya Mei Dei ya nchi zingine za nje.Pamoja na sherehe zilizofanyikia kimkoa tu Dar es salaam.Za Kitaifa Iringa hapana hazikuwa na maana yoyote!Na Waziri Mkuu aliyekwenda Iringa kumwakilisha Rais naye hakuwa na umuhimu wowote wa kuonekana jana ileile akihutubia wakazi wa Iringa na wafanyakazi wote kwa ujumla.Ni aibu sana.Huu ndiyo ufanisi tunao waagiza wafanyakazikote nchini wautekeleze?Au kuna kinacho fichwa?Je,kulikuwa na mgomo baridi wowote katika maandalizi ya Mei Mosi Iringa tokana na sababu zozote?Labda Mjengwa kupitia Blogu yake atatuhabarisha kwa kina zaidi.Mimi nilitegemea Uongozi wa Mkoa wa Iringa ungeitumia fursa ya sherehe hizo kuutangaza Mkoa wa Iringa pamoja na vivutio na rasilimali zake ili kukuza uwekezaji mkoani humo?Lakini hilo halikufanyika.Tatizo lilikuwa nini?Ukosefu wa fedha za maandalizi au serikali ilipuuzia sherehe hizo?Waziri Mkuu kauli yake kuhusu Viongozi wala rushwa haikuwa na uzito uliostahili.Chama cha wafanyakazi nacho kipokipo tu kama hakipo.Utadhani kama mwaka huu hakuna sherehe zozote zile za wafanyakazi zilizofanyika bali mzaha mtupu!Mjengwa tupashe habari kulikoni sherehe hazikwenda tulivyotarajia mambo yawe?Tatizo lilikuwa nini?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2008

    naam kweli kabisa, ufisadi ndio adui wa nchi yetu, mafisadi wote huwa wanapata protection toka serikalini, vipi ufisadi wa balali umeishia wapi, inaonekana habari zake zimezimwa, tunataka balali arudishwe bongo na kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuiba pesa za umma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...