KUNA RAFIKI YANGU ANAKUJA BONGO MTASHA(MZUNGU)ALIKUWA ANATAKA KUJUA GHARAMA ZA USAFIRI WA NDEGE DOMESTIC FLIGHTS MFANO ATC WEBSITE YAKE AIFANYI KAZI NA PRECISION AIR IKO ON AIR LAKINI BEI HAKUNA JE INAKUWAJE SASA KUTATUA TATIZO.MAANA JAMAA AMEENDA EMBASSY PIA ANASEMA AMESHINDWA KUPATA JIBU MSAADA. NI NGUMU SANA MAISHA YA NAMNA HII BILA KUANGALIA VITU MUHIMU KWA JAMII ASWA KARNE HII YA 21.

MDAU
Janeth

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2008

    sasa yeye anataka kujua bei za nini,wakati ukidondoka bongo na $ au £ kila kitu ni ubwete au ana ajenda ya siri

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2008

    Njia rahisi ni kutafuta kupitia mtandaoni makampuni yaliyopo Tz yanayoshughulika na biashara ya uwakala wa usafiri na kuwauliza. Baadhi ya makampuni hayo yana tovuti zake.
    Njia mbadala ni kuwapigia simu ATC na Precision Air moja kwa moja.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2008

    Kwa kukusaidia dada Janeth sijui anaenda wapi na wapi labda? ndio tuweze kukusaidia kujua bei

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2008

    we unakuja kulalamika tu hapa oh hawatoi infor, we mwenyewe mbona hutoi infor???
    nauli ya kwenda wapi?? hujui bongo kuna mikoa kibao? anaenda znz? mwz? arusha? musoma? kigoma? bukoba? etc
    Unaona sasa? kila sehemu inanauli yake, next time usije kukoroma koroma hapa bila kuleta infor au ulidhani ukisema mzungu tutaogopa
    tena kwa vile umesema mzungu labda ningekunyima infor hata kama ningekuwa nazo

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2008

    Kwa kawaida ninavyofahamu mimi bei za ticket za ndege huwa zinatofautiana hazipo fixed kama ticket za mabasi au garimoshi. Kwa mfano unapokuwa kwenye ndege unaweza shangaa tofauti ya ghara uliyolipa kati yako na abiria mwigine hata kama kiti chake kipo pembeni yako. Wewe unaweza kuwa umelipa $300 na yeye kalipa $500. Ticket za ndege zinategemeana na destination na siku uliyonunua hiyo ticket, na pia maagent wanatofautiana bei.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2008

    ndio walewale. Kwani wewe Janeth hujui hizo bei au ?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2008

    Janeth, bei za ndani(Local Flight) kati ya ATC na Precision zinafana. Mfano Dar-Mw-Dar ni $300. So bei inakuwa inarange kati ya $200 hadi 400. MAK

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2008

    yaani watu humu ndani majibu yake yamekaka Ki- CCM CCM TU !! Mtu anataka kujua kwa nini Hizo tovuti za mashirika hayo hazina bei? na ni mashirika makubwa, hajauliza wapi atapata bei. Inashauriwa upate bei sehemu OFFICIAL , siyo uchochoroni !!Na majenti wenyewe wabongo wengi ni makanjanja.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2008

    MWAMBIE HUYO MTASHA AWASILIANE NA WAGANGA WA KIENYEJI ANAWEZA KUSAFIRI USIKU KWA BEI POA KWA USAFIRI WA UNGO ANACHO TAKIWA KUFANYA NI KUPATA SEHEMU ZA SIRI ZA ZERUZERU. USAFIRI WA UNGO USIKU INASEMEKANA NI WA AINA YAKE HAKUNA FOLENI NA NIWA HARAKA KULIKO WA NDEGE NA HAIJAWAI KUTOKEA UNGO UKAWA ADIMU AMA SAFARI KUWA CANCELLED KUMBE NI VIZURI UKAMPA HIZI TIPS AKAE MKAO WA KULA AKIJA BONGO

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2008

    Ndugu Mdau,
    Mwambie mtasha wako kuwa mashirika mengi ya ndege hawaweki taarifa za bei za tiketi za ndege kutokana na ushindani mkali wa biashara.

    Mweleze mtasha apitie webusaiti ya http://en.wikipedia.org halafu agonge 'Tanzania' halafu ashuke kwenye 'Sub-headings: Geography/Economy.

    Hapo atapata taarifa nyingi kuhusu masuala ya usafiri mbadala wa ndege kama barabara, boti, meli na kadhalika. Kwenye webusaiti hiyo kuna link nyingi kuanzia TCAA(Tz civil avuation authority), SUMATRA, TANROADS, TANAPA, Tanzaniatouristboard.com n.k ili huyo mtasha aweze kuifahamu TZ vizuri na namna ya kusafiri toka mkoa mmoja mpaka mwingine ndani ya Tanzania.
    Mjaze huyo mtasha na taarifa hizo awapelekee wenzake.
    Mdau
    SeniorJunior
    London

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2008

    jamani janet anamaana kua tanzania tuko nyuma kwenye mambo ya information haitasaidia kama janet akiwaeleza huyo mtu anataka kwenda wapi na wapi anachomaanisha nikua ATC does not have a website of its own to give people info PERIOD.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2008

    huyo mdhungu anakuja kutafuta kazi? maana hana uhakika na fweza zake, nawewe mbona hujui wakati ni mtz? yaani huyo mzungu mjinga kwani ndie angekuwa wa kwanza kukustukia km huna mpango,huna kontakti bongo,hata kupiga simu kwa marafiki? sijui wewe umetoka wapi? i ken not biliivu iti!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2008

    Michuzi andika barua umwombe Bill Gate msaada uone ka atakupa. Kuna level ukifika unaanza kutoa msaada kwa mass na sio individuals (jamii na si mmojammoja). Inaboa kuona topik km hii, mtu shida hii ya kuleta blogini kweli? We nawe unaendekeza mambo sio. Watu na midevu yetu tunakuja kuskiliza nini? Anajua internet, anajua watu, hajaenda precision wala atc anang'aka tu. Na we michuzi unajua maana ya 'mud slinging?' ni kesi? Mi kampuni yangu ukiifanyia hivi sikuachi ng'o.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 07, 2008

    Wewe JANETH umesoma hujasoma maana swali lako kama la mtoto wa dara la kwanza maana inaonekana shuleni kwenu hujafundishwa kiswahili kwanza ukitaka kuuliza swali uliza swali ambalo kila mtu ataweza kukujibu ndio hata usipotuambia kuwa ni black au mzungu sisi haituhusu wewe nia yako ni kutaka kujua cha kuuliza tuambie atataka kusafiri kwenda wapi kutoka wapi sasa wewe unataka si tu guess anatoka canada kwenda arusha uliza na tuambie sehemu anayokwenda anayotoka tutaweza na sisi kukujibu kama mimi hii messeg naiignore tu maana hujaeleza kitu zaidi ya kuweka kwa msisitizo jina lako hapo chini ok thank.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 07, 2008

    Ukisoma hizi comments direct utajua mtu anayejibu yupo nchi gani na ana maisha gani. Yaani kumpa tu general idea inakua big deal acheni hizo jamani.

    Afadhali ya huyo aliyemwambia price range ya Dar Mwanza ni $200- $400 sasa atakua na idea.

    Na mimi nakumbuka Arusha - Manyara ilikua price range ya $150 - $250 na Arusha Dar ni $210 and up


    Good luck

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 08, 2008

    http://www.waljistravel.com/customersspeak.php

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 08, 2008

    Anataka dezo? Mi ntampa nipe namba yake na picha yake. Sisi Wabongo ni waungwana sana lazi bure ndege bure popote pale atafikishwa. Asiwe mchoyo na vitu vyake. Ntampa vyangu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 08, 2008

    hee we kama upo serious na safari si utumie hizo contact zilizopo kwenye website ulizofungua..kama ya precision ni www.precisionairtz.com na pia e mail ni info@precisionairtz.com na waweza kupiga simu no +255222860701-10 utapewa fare zote za safari unazotaka.
    nadhani nimekusaidia kutatua tatizo lako.
    mdau R

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 08, 2008

    Huyo mzungu aache ubahili kampuni za travel agancey zipo kibao Tanzania kwa nini asitumie hizo?au anapenda vitu vya bei rahisi?huku ulaya tunalipa kodi kibaooo!!mwache na yeye alipe nauli kubwa huko bongo...mdau mwenye hasira

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 08, 2008

    NASHUKURU SANA KWA WALE WALIONIPA JIBU NA KUELEWA HII MSG ILIKUWA NI KUTUMA UJUMBE GANI KWA MLENGWA.

    NIMESHAPATA JIBU AKILI YA WANANCHI KWA UJUMLA KUNA MAKUNDI MAWILI HAPA KWETU

    LA KWANZA WADANGANYIKA (WAKURUPUKA)AMBAO NI RAHISI SANA MTU MWENYE AKILI KUFANIKIWA MAISHA KUPITIA WAO MAANA AKILI ZAO NA UWEZO WAKUFIKIRI HARAKA HARAKA NI MDOGO/TO MAKE A DECISION PIA NI NGUMU MPAKA WEWE UWAONYESHE NJIA WAO NDIO WAFUATE MKUMBUKO.

    KUNDI LA PILI:-
    NI LA WALE AKILI ZAO NI SHAPU KAMA MSHALE YAANI AFIKIRII MARA MBILI YEYE YUKO TAYARI KUCHUKUA RISK KAMA ANAONA 80% YA MAFANIKIO HIKO NDIO WAO WANATUMIA AKILI YAO KUFANIKIWA MAISHA KUPITIA KUNDI LA KWANZA(WADANGANYIKA)


    KWA JIBU LA HARAKA HARAKA UNAWEZA KUANGALIA NA KUANALYZE MWENYEWE HAPA.


    Asante sana wenu katika ujenzi wa Taifa

    Janeth(UK)

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 08, 2008

    Respect kwako Mdau Senior Junior wa London,wa May 07,2008,8:58 pm.Majibu yako yamenifurahisha sana.Trully you sound like a typical Tanzanian Character!Tunataka Vijana kama wewe huko Majuu!Shikamoo zako nyingi mze!Wengine wajifunze kutoka kwako.Mimi nipo Bongo.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 08, 2008

    Janet,
    Pole na mihangaiko. Bei ulizopewa na jamaa ni kweli kabisa ziko kwenye range hiyo. Mie nilikuwa na shida hiyo na niliwaandikia Precisionair na wakanijibu siku hiyo hiyo na kunipa nauli. Hadi Tabora ni $300 na Arusha $250. Ila nafikiri bei za ndege zinategemea na MSIMU na pia kumbuka WESE kila siku linapanda mlima Kilimanjaro... Air Tanzania sina uhakika sana nao na nafikiri wao ni email tu ingawa ni bora upige simu. Ili kupunguza bei kama uko nje basi heri ununua UNITS ONLINE kwenye makampuni kama SKYPE, REBTEL nk. Sikonge.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 08, 2008

    mdau Janet kwa mchanganuo wako naona wewe ndo uko kwenye kundi la kwanza umekurupuka tu na kuleta pumba kwenye blogu
    95% ya comments inaprove hivyo, ungekuwa kwenye kundi la pili(sharp and ready to take risk) ungewaandikia airline company ongea na marketing manager wao or something to bring about changes lakini kwa vile uko kwenye kundi la kwanza umekurupuka na kuja kwenye blogu kudhihirisha kiasi gani cha pumba unacho kichwani
    ni hayo tu

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 08, 2008

    HUYU JANETH NI WAKIZAMANI KWELI 2ANATAKA TUJUE ANA RAFIKI MZUNGU,ANAONA AKISEMA MZUNGU BASI TUTATETEMEKAAA!!AMEPEWA MAJIBU MAZURI BADO ANAPONDA,ANATAKA TUJUE KUWA YUKO ULAYA..TENA ULAYA KWENYEWE LONDON..KYEKUE

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 08, 2008

    poa tu mimi sijali kukandiwa mdau hapo juu na MKYEKUE yaani atamkikusanyika wote uwanja wa taifa mnipake still hakuna atakae niweza.nasema nashukuru walio lielewa swali nimegundua kuelewa ni kitu kigumu sana haya wengine wawili wameongezeka kyekue na mwenzie (walilekundi la juu)walimu wana kazi sana no wonder watu wanafeli

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 08, 2008

    MZUNGu!! mzungu!!heri ungesema nina rafiki yangu black american kidogoooo tungetetemeka!!mzungu???acha ushamba JANETH...SEMA NINA RAFIKI YANGU MCHAGGA ANAKUJA dar au nina rafiki yangu mpare anakuja dar,mambo ya kuogopa wazungu yaalisha zamani sana,,naona hata wewe mwenyewe umeona wazungu wengine walivyo choka mbaya...Mwambie afika dar atapokelewa na atapata ndege kama kawa..

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 09, 2008

    Janeth!
    Nakuunga mkono asilia 100%.Websites zote walizotaja baadhi ya wachangiaji za Precissionair, na ATC.Hazionnyeshi bei/nauli.Suala la msimu kama ni high season ,au low season ni irrelevant.Websites za mashirika ya ndege zinatakiwa zionyeshe hizo bei ili watu wapange safari zao kwa uhakika.
    Michuzi ,baadhi ya wachangiaji wako hawana busara , wala uwezo wa kuelewa.Hebu mniambie nani kafungua website ya ATC, au Precissionair akaona kuna mahala wameandika nauli?
    Then fungua BA, DELTA, AIRCANADA, na mashirika mengine yenye watu/viongozi makini ndio mtaona ninachozungumza, na anachozungumza Janeth.
    Kama huna cha kuchangia juu ya hoja au shida za watu humu ndani,Please do us a favour DO NOT COMMENT!!

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 11, 2008

    HAHAHAHAHA JANETH YAANI UMEPATIA KWELI!!HAYO MAKUNDI ULIYOYATAJA NI KWELI MTUPU,NA MIJITU MINGINE INAZIDI KU~PROVE YOUR POINT RIGHT!!...MA MDOGO UK!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...