Wapendwa mabibi na mabwana, Jumuiya ya Watanzania Michigan (TAMI) kwa kushirikiana na KLH News International na Bongo Radio itakuletea matangazo ya moja kwa moja toka Detroit watakapomkaribisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe (CHADEMA) kwa chakula cha jioni.

Matangazo hayo yatarushwa kupitia tovuti ya http://www.bongoradio.com/ toka KLH Mobile Unit kutoka eneo maarufu la Eight Mile (lililopewa umaarufu na filamu ya EMINEM ya "Eight Mile").

Shughuli yote itakuwa kuanzia majira ya kama saa moja hivi (EST sawa na -5GMT, masaa saba nyuma ya Tanzania) na kuendelea.

Tunawakaribisha Watanzania wote, marafiki na wale wote wanaoitakia mema nchi yetu katika shughuli hii ISIYO ya kisiasa, kichama au mrengo wowote wa kiitikadi zaidi ya Watanzania kukutana na Mbunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa TAnzania ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma.

Kwa hivyo ni nafasi ya kutembelewa na kiongozi wa kitaifa na heshima kubwa. Karibuni wote.

KLH News
Editor in Chief

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2008

    Nyie watu wa Michigan acheni ushamba . nani kasema zitto ni kiongozi wa KITAIFA ? mbona mnataka kumtukuza ajione kama Rais WAKATI BONGE LA MSHAMBA TU .. Hakuna chochote anchofanya jimboni kwake Kigoma

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2008

    Aaha.. KUMBE KISWAHILI UNAKIWEZA!
    NYAU WE!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2008

    Huko kwao Ujiji majani mpaka kati kati ya barabara anashindwa hata kuhamasisha watu walime mbele ya nyumba zao kwenye barabara zao a mitaa ili kutumia nguvu za wananchi kama mamlaka husika zimeshindwa kutengeneza barabara za mitaa. Yaani ukienda mabarabara yote ya mitaa yamekufa nyasi ndefu hata simba anaweza jificha.

    Lakini ni muhimu kumsikiliza tumsikie anasema nini huko ili akija jimboni tumbane vizuri kwa kushadadia ya kitaifa wakati jimbo lake halikumbuki.

    Angalizo sio kurudia hoja iliyopita!
    Naona sasa mmejifunza mmeleta tangazo kwa kiswahili hilo ndilo tunalotaka. Mwanzoni si mlijidai wajuvi kuwa ooh huu mkutano hauwahusu unawahusu waingereza wa Michigan mwapiga kelele ya nini. Kiwapi sasa mbona mnatangazia watanzania wote wamsikilize. Mwanakijiji kama ulivyo hodari wa kukosoa ukikosolewa kubali sio kuja na utetezi kibao kama wanasiasa! Kiwapi sasa mbona unawaalika watu waje wasikie na tangazo lilikuwa kwa wabongo wa Michigan na waafrika wengine. Acheni madharau, ni sisi sisi mnaotudharau kwa kutokujua kiingereza ndio tutakaopiga kura!

    Je sie tusiojua kiingereza tufungue hiyo redio kusikiliza huo mkutano? Maana tuliambiwa utakuwa wa lugha ya kiingereza kwa sababu kuna waafrika wengine wanashiriki ambao hawajui kiswahili.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2008

    tunaomba basi utupe adress kamili ya hiyo sehemu

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2008

    Mheshimiwa lakini unchapakazi jimboni kwako au kutafuta umaarufu tu wa nje na kuwasahau waliokuwezesha? Angalia usije kuleta vijisababu visivyo na msingi 2010 pale wananchi watakapo kumwaga. maana nyie hamuishi kulalamika, mara oh! tumibiwa kura, wapiga kura mamluki! Kumbuka ubunge ni ajira tena inayolipa sana kuliko hata ualimu chuo kikuu hivyo watu wengi wanajiandaa kwenda kwa wananchi 2010 ili waajiriwe

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2008

    HEY, JAMANI, SISI WATANZANIA TUNA ROHO ZA 'DIZAINI' GANI? MAFISADI TUNAWACHUKIA, VIONGOZI KAMA ZITTO WENYE MWELEKEO MZURI KUSAIDIA WANANCHI NAO TUNAWACHUKIA. TUNATAKA NINI? AMA KWELI NIMEAMINI WANAOSEMA WATANZANIA TUNA ROHO MBAYA NAKUBALI. JAPO WAPO WAZURI, LAKINI TUNA WENGI PIA WEHU.

    UTAKE USITAKE, ZITTO NA AKINA DR. SLAA NDIO WAMEBADILI HALI YA HEWA BUNGENI KUANZIA MAAMUZI YA SERIKALI KWA RAIS HADI WABUNGE WA CHAMA TAWALA. UKIBISHA BISHA TU.

    KWANZA, ZITTO NI KIONGOZI WA KITAIFA KWA WANAOJUA MAMBO. YEYE NI MWENYEKITI WA KAMATI INAYOSHUGHULIKIA MAMBO YOTE YA UWEKEZAJI NA MIKATABA. UNAFIKIRI ANAONGOZA MIKATABA YA CHADEMA? LA HASAHA!

    PILI, ZITTO NI KIONGOZI WA KITAIFA SABABU SASA HIVI AMEHUTUBIA WANANCHI KARIBU PANDE ZOTE ZA NCHI WAKATI NCHI IKITAFUNWA NA RICHMOND NK. NA NDIO AMESAIDIA UELEWA KWA WANANCHI WENGI. MFANO MZURI WATU WA BUKOBA WALIMWELEWA VIZURI SANA.

    TATU, ZITTO KACHAGULIWA NA UBALOZI WA MAREKANI KUJA USA KAMA KIONGOZI WA TANZANIA NA SI KAMA MBUNGE WA CHADEMA.NAFASI HII ILIKUWA WAZI KWA KIONGOZI YEYOTE YULE WA CHAMA CHOCHOTE. LENGO LIKIWA NI KULETA MANUFAA KWA NCHI NA KWA KIONGOZI BINAFSI.

    MWISHO, NAOMBA WENZANGU TUSOME AINA ZA UONGOZI. UKIZIJUA UTAONA NI WAPI ZITTO ANASTAHILI NA NI KIONGOZI WA KITAIFA. ACHANA N KATIBA YETU INASEMAJE, SOMA NADHARIA ZA UONGOZI KWA JUMLA. UTAONA Uongozi wa Kiimla, uongozi wa Kidemokrasia, Uongozi wa Kikarisma nk. To me , Zitto falls under CHARISMATIC LEADERSHIP, ambayo inatokana na influence ya mtu kwa nchio yetu.

    MDAU

    ReplyDelete
  7. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kiongozi wa kitaifa; Mbunge yeyote wa Bunge la Muungano ni kiongozi wa kitaifa ndio maana wanapokuwa kwenye magari yao haipepei bendera ya Kigoma Kaskazini! (kama ipo)

    Na kutumia kiingereza au kiswahili is just a matter of choice for Tanzanians are bilingual and others tri-lingual.. so if I were to switch in either language I would not find it offensive to anyone.

    So for some of ya'll who are somewhat offended I got one thing to say 2 u.. you'll be just fine stop whining and crying.

    Nadhani tumeelewana kwani you don't need to gambila me stupid infront of my waifu wangu.

    Tunatarajia kuanza shughuli mapema zaidi kuliko tulivyotarajia na mipango ya kurusha matangazo hayo iko pale pale.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2008

    Wewe mwanakijiji hakuna mtu aliyekuambia stupid wala nini nafikiri katika hizo comment zote hapo juu sijaona hata moja ambayo umeambiwa kuwa u stupid, ila naona kuna mahali umeambiwa ukikosolewa kubali makosa usiwe kama mwanasiasa, anasema hili halafu baadae anarudia kulifanya lile ambalo amesema amepinga. Kuhusu kiswahili kwa taarifa yako ni lugha ya taifa ila kiingereza ni lugha ya kiofisi na si ya taifa, ndio maana Chadema ilishindwa kupata kura kutokana na arrogance ya watu wake kama wewe unafikiri hicho kiingereza chako zaidi ya huku kwenye mtandao kitawafaa nini wakati asilimia 95% ya watanzania wanazungumza kiswahili na asilimia ambayo haifiki hata 5% ndio wanazungumza kiingereza muda wote. Kwa mtindo huu wa arrogance zenu na kujiona mko juu mtaifanya CCM iendelee kututawala milele mpaka tupate watu walio na nia ya mabadiliko ya kweli na inayotoka mioyoni mwao kwa ajili ya watu masikini, wengine wote ni opportunists tu ambao nao wanatafuta kutafuna na kula bila kuzasa, hakuna mpinzani wa kweli ambaye ana nia ya dhati ya kuwafikia masikini huko waliko na kuwapa muongozo. Hapa tu watu wamezungumzia lugha tu na mmekuja juu ka moto wa kifuu! Watu wa dizaini yenu mkipata madaraka ndio mtatemea mate watu usoni kisa hawafanani na nyie.

    Chuo kikuu huria kinaomba ruhusa ya kuanza kutoa shahada kwa kiswahili na kinapeleka mapendekezo serikalini kuwa wawekezaji wajifunze kiswahili ili waweze kuwasiliana na asilimia kubwa ya watanzania ambao ni tabaka la watu wasiojua kiingereza.

    Sasa wewe unatuletea eti Tanzania ni bilingual ili? wakati kuanzia primary mpaka sekondari ni kiswahili tu labda asilimia chache ya wtau wenye uwezo wanapeleka watoto wao private school kusoma kwa kiingereza. Nafikiri huelewi hali halisi ilivyo huku nyumbani ndio maana uko katika tabaka jingine kabisa.

    Ila waswahili wanasema kulonga mbali kutenda mbali! Njooni na vilugha na arrogance zenu 2010 muone kama kuna mtu atawasikia na hizo ahhm aahm, you know! me! you see! zenu! Kama mtaweza kuwafikia wananchi wa kawaida, kulonga mbali, kutenda mbali, mwe!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 05, 2008

    Hee kumbe ulikuwa mwalimu au mwalimu sasa? Eti nadhani tumeelewana he basi huko nyumbani kwako kuna kazi amri moja! ' mimi nimeshasema na sitaki kusikia mwingine akisema, nadhani tumeelewana, haya wote kwenda kulala! Heheehhee! Ama ukipata uongozi wewe mwanakijiji itakuwa kazi kweli kweli, uanaanza kuonyesha udikteta mapema, hakuna mtoto humu au mwanafunzi wa kumpa oda kama darasani. Hivi uko tofauti sana na watu wengine? Mbona u kawaida tu sawa na watu wengine wenye blogu, au una mamlaka fulani hivi ya kuamrisha watu! Hehehee makubwa wajameni! Baelezee hao hao bantu bako!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 05, 2008

    sawa tunalewa zitto ni mwenyekiti wa kamati inayoshughulikia mikataba na uwekezaji,naomba kuhoji hapo pamoja na kuwa mweneykiti mbona juzi juzi tumeona wawekezaji feki malofa tu toka india waliochukua TRL mpk wanashindwa kulipa wafanyakazi kima cha chini laki 1 na 60?inabidi serikali ibebe huo mzigo wa kuwakpesha bilioni kadhaa hao TRL? jimboni kwake kwenyewe hamna cha maana.ndo wale wale tu wanashibisha matumbo yao.bado sijaona kiongozi nchi hii mwenye uchungu na wananchi wenzake

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2008

    Anon may 4, 7:48 pole kwa kuwaelewa vibaya baadhi ya wadau/watanzania, mpaka kuwaweka kwenye fungu la roho mbaya au wehu, ninachotaka kukushitua juu ya muonekano wa hao unaowadhania hivyo, kuwa ni hali ya nchi ilivyo sasa watu wamechoka na blah blah za baadhi ya viongozi wetu, imefikia sasa wanashindwa kukaa na joto vifuani na wanatapatapa kutafuta ahuweni, na ahuweni hiyo ni pale wanapogundua kiongozi huyu kidogo anaweza kuongea na kujaribu kutusafishia njia katika baadhi ya kero, kwa maana ya ujasiri wa kukaripia anapoona mahali hapako sawa, hivyo wanataka kuona vitendo katika baadhi ya kero angalau ndogondogo basi hasa kwenye majimbo wanayotoka watu waone okombozi kutoka kwa wawakilishi wao wanaowachagua. Yote hayo ni misisitizo na jinsi mdau anavyowakilisha, wengine kwa uchungu,jazba wengina maskhara wengine kwa dharau, na upole.lakini wote ukiwaangalia wanalengo sawa wanatetea tanzania na mtanzania mwenyewe.

    Watu kama hao unaowatafsiri wana roho mbayaau wehu, kwenye jamii na wapenda maendeleo ni CHACHU NA USHINDANI WA KULETA MABADILIKO NA MAENDELEO. Na ni jinsi yao ya kutuma ujumbe ili kuleta changamoto la kuweza kusukuma gurudumu la kuijenga na kuisimamia nchi kwa mawazo au vitendo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2008

    Huyu annon wa 8:17 AM ana mwelekeo hasi watu wa namna hiyo ni siyo wajinga ni wapumbavu ni watu wa kuwaepuka. hakuna asiyeelewa ZITO ni nani katika Tanzania yetu ya sasa. Bado anastahili kufuatilia sana nyendo za kisiasa katika nchi yetu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 05, 2008

    Tunawashukuru watu wote waliojitokeza kwenye shughuli yetu fupi. Mambo yalienda more than expected ilikuwa ni kama "meet and greet" session lakini pia ilifanywa kwa mtindo wa kubadilishana mawazo.

    Mhe. Zitto katumegea mambo mengi mazito na yenye hamu kubwa hasa kwa wale ambao wanasubiri kwa hamu ile ripoti ya madini. Lakini alizungumzia mambo mengi sana kutoka masuala ya kiuchumi na kisiasa. Na alitoa kauli kadhaa nzito ambazo natumaini mtazisoma kwenye magazeti ya nyumbani siku chache zijazo.

    Tafrija yetu ilimalizika kwenye saa tano za usiku na tulimfikisha Mhe. Hotelini kwake umbali wa kama saa moja hivi kwenye majira ya saa sita za usiku.

    Tunamshukuru sana kwa kutuheshimu na kutukubalia mwaliko wetu. Na sisi tulimuonesha shukrani ya watanzania Michigan na ni matumaini kuwa tumeweka alama ya kukumbukwa moyoni mwake.

    Mkutano uliendeshwa kwa lugha ya Kiswahili huku wachache wakitumia maneno kadhaa ya kiingereza. Tulijaribu kuwasihi watumie lugha yao ya Taifa lakini kulikuwa na ugumu wa aina fulani.

    M.M.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 05, 2008

    MM shukrani kwa taarifa, tumefurahi kusikia kuwa mkutano ulienda vizuri na mambo yote yameenda kama yalivyopangwa. Kubwa zaidi ni kutumika kwa kiswahili, ingawa watu wanaweza kuniona mwehu kwa kushadadia hiki kiswahili lakini ni ukweli usiopingika kuwa ni watanzania wachache sana wanakielewa kiingereza kwa ufasaha maana huwa inawafanya watu wengine wakae kimya na washindwe kuchangia mada mahala au kwenye mikutano kwa kukwazwa na lugha. Usione watu wanajidai wanajua kiingereza lakini kiukweli tunajua kiingereza kidogo sana kwa sababu wengi hufikiri kwa lugha zao za asili walizojifunza kwanza utotoni na wanazotumia kila siku, kisha hutafsiri kwa lugha hiyo ambayo inabidi awasiliane na mtu. Sio kwamba sijui kiingereza la hasha ni mtaalamu wa lugha na ninajua umuhimu wa kukazania au kuprommoti lugha yetu wenyewe ili iwe chachu ya maendeleo nchini mwetu. Natumai hata waliosikiliza kwenye podcast wamefaidi kwa kuwa lugha ilikuwa ya kueleweka. Tuzungumze kiingereza pale inapobidi kuwasiliana na watu wasiojua lugha yetu lakini sisi wenyewe tuzungumze lugha yetu na tujivunie hiyo lugha inayowezesha makabila 120 kuwasiliana bila kutumia lugha ya mzungu! Natumai na watanzania wengine walio nje wataiga huo mfano. Marehemu Shaaban Robert alisema katika moja ya mashairi yake kuwa 'Titi la mama ni tamu'katika kuthamini chetu tulichonacho.

    ReplyDelete
  15. Kaka nimerudi na nakupa pongezi za dhati kwa kuamuwa kutumia lugha yetu kwa kuwasiliana na wote kwani hata west afrika kiswahili kinagonga hivi sasa,na m-west africa akiona taarifa ya kiswahili na kuna neno afrika ndipo atakapo tafuta kamusi,inakuwa ushaitangaza lugha.Mambo ya sisa siyavai kwani sina uwezo nayo,lakini ulichokifanya kufuta kosa kiaina,inahitaji mwanamme au mwanmke wakweli kuyafanya,hongera ndugu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...