Orchestra Vijana jazz Wana-Pambamoto wakiwa .Morogoro siku Mandela alipotembelea baada ya kufunguliwa. Waliokaa mbele kushoto Mpenzi, Baker Semhando (Bassist), Juma Choka (Drummer) sasa yuko Sikinde, Waliosimama toka kushoto, John Kitime(guitaa na kuimba),sasa yuko Kilimanjaro Band-Wananjenje, Dereva wa msafala,Marehemu Aggrey Ndumbalo (Rhythm gitaa, Mhasibu), Abuu Semhando (Drummer) sasa yuko Twanga Pepeta, Maerehemu Freddy Benjamin (Muimbaji), Said Mnyupe (Trumpetist) sasa yuko msondo, Saidi Ndula (Saxophone, Rashid Pembe (saxophone), Hassan Shaw (keyboards).....Pambamoto awamu ya pili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2008

    Du nakumbuka mengi, nilimpata mke wangu wakati huu katika dansi la vijana jazz, maarufu kama vijana day

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2008

    Nakula futari bila kuswali (jamani sijui hata maneti alikuwa anaimba nini yarabi) umenikumbusha mbaali kweli!Kumbe academia zilianzia zamani

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2008

    Picha inakumbusha mbali, enzi hizo mwinjuma road.

    Mbona Papa Kisoka (Erasto Mzee wa PR-Cha Matusi) haonekani maana anadai aliwahi kuiimbia Vijana Jazz!!

    Palipali Kolokwiti

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2008

    michuzi umenikumbusha mbali sana,hiyo ni bendi yangu ya nyumbani.Hivi wapi naweza kupata cd za Vijana jazz? enzi hizo kina maneti nyimbo kama Maria,Bujumbura etc

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2008

    Bro Michuzi kwa kuwa mpiga trumpet umemuita TRUMPETIST basi na mpiga Saxphone tungemuita SAXPHONIST. Au?
    Mie nakumbuka ule wimbo.

    "Nenda upesi, nenda ukamwambie,
    Tokea leo, asinifwatefwate,
    Kitendo kile, alichonitendea,
    Kingenifanya, nipoteze maisha,
    Kunidanganyaa kwamba hajaolewa,
    Na chumba kile amekipanga yeye,
    Kumbe uwongo, Ale nidanganya..."

    Mwanawane...!

    ReplyDelete
  6. Tuache utani, hii Sagha-Rhumba ya awamu ya pili kabla Maneti hajafariki, na hii ya sasa ni tishio katika muziki Bongo. Watu wanasema Msondo ni Baba ya muziki bongo si kweli. Sababu ni hizi; kama ni tungo, Sagha Rhumba nao wana tungo safi sana za kuelimisha jamii. Katika upangaji vyombo na sauti, achana na sagha rhumba...sikilizeni muziki wa sagha rhumba toka miaka ya mwishoni 80 mpaka sasa, halafu pimeni na ya Msondo...mtaona hawa jamaa wako mbali saaana tena kinoma ile mbaya. Kidogo kwa sasa msondo wanajitahidi kupiga muziki wa international standard. Mzee Kitime wapi Malaine, Penzi halina shule, Mtatumaliza, na nyinginezo nyingi tu. Nyie bwana ni wababe wa muziki Afrika, si bongo tu. Wapi tunaweza pata CD zenu?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2008

    Aaah kaka Mithupu mbona hujatuambia mzee wa maprosoo yupo wapi siku hizi?

    Huyu ni bendi inaitwa Mkorogo anaimba na mkewe huyo wimbo wao maarufu wa maprosoo

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 08, 2008

    na we na mi! bara mpaka pwani pambamoto shambulia! hii ilikuwa imetulia sana

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2008

    Hivi haya majina ya bendi zetu za bongo ni kweli wanapiga miziki ya aina hiyo au ni mbwembwe tu? Kwa mfano hawa Vijana Jazz Orchestra, were they in fact a jazz orchestra?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 09, 2008

    Nimeminya kutoa maoni lakini nimeshindwa. Wanakokakoka - kamata Sukuma, Air Pambamoto awamu ya kwanza na ya pili - Saga Rumba walikuwa kiboko. Niliwahi kwenda gig zao kibao. Nakumbuka nyimbo zao za siasa na kijamii zilikuwa hazina mfano. Bendi hii wamepita wanamuziki wengi sana maarufu wa muziki wa dansi nakumbuka kina Hamza Kalala, Benno Villa Anthony, Cosmas Chidumule, kuna yule mpiga gitaa akiitwa Wanted kama sikosei Mmakonde mwendawazimu yule alikuwa analifumua gitaa utafikiri kaligundua yeye na wengine wengi tu. Halafu na wapulizaji matrampenti baadhi yao wakitokea Morogoro kwa Father Canute.

    Nyimbo za kisiasa ilikuwa bomba kama ile ya Tutaendelea kutokana na kukosoana. Japokuwa maudhui yake yalikuwa siyo ya kikweli sana yalifit propaganda za wakati ule. Halafu ukija nyimbo za kijamii unakutana limbukeni Ngoma, baharia Amba, na halafu mambo ya makanyaboya, Matapeli. Nyimbo hizo zilikuwa zinakupa picha Vijana Jazz ni vijana wa downtown hasa. Halafu kulikuwa nyimbo za mambo binafsi kama Shoga Kidawa, Ninapokula wananisema, na zinginezo ambazo sasa hivi sizikumbuki. Halafu jamaa walipatwa kudakwa kimapenzi na mademu wa Msasani Mikoroshoni kina Filomena wakakubali mapenzi mpaka wakawatungia nyimbo.

    Hizo ndizo zilizokuwa siku za muziki Bongo. Taka usitake, penda usipende rumba la Bongo litakuingia tu. Radio moja idhaa mbili Taifa na Biashara. Chagua mwenyewe. Hakuna cha FM wala TV wala wadhamini wa kutuletea mauzauza ya kina Senti Hamsini sijui Sumni sijui nani. Kulikuwa hakuna cha machekibob wala nini ukiingia kwenye madansi unawakuta na ukienda kwenye madisko unawakuta na mademu zao wa ushuani.

    Muhidin, mwaga series za old is gold. Wastue na wakuu wengine watuletee za Super Bomboka, Msondo ngoma, Nginde, Dundadunda, Hama hama, Kimbunga, Chaka chua, Kamanyola,na wengineo.

    Shukrani jaazillah, asante sana, ndaga fijo, thank you very much.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 09, 2008

    MICHUZI YUKO WAPI SHOW HASSAN SHOW,TULIKUWA WOTE ENZI HIZO DARAJANI PRIMARY 1972 MARA YA MWISHO TULIKUTANA AKIWA NA SAFARI SOUND (POWER IRANDA)PALE TANZANIA REGION AKIWA NA KINA FRESH JUMBE,BUSHOKE,KUNYATA,DEE,GURUMO,SKASS KASAMBULA,LISTER,CHIPEMBELE,TOTO TUNDU,MAREHEMU ABEL.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 14, 2008

    nilikwapo hapo jamhuri stadium mji kasoro,ndio nyumani,1990,nilikuwa darasa la saba nafikiri,siku zimepita kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...