Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (katikati) akishuhudia upasuaji wa moyo ulioongozwa na Daktari, William Mahalu wakati alipotembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2008

    Loh,kwanza nampa pole mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji.Pili, Waziri mkuu umeshuhudia kwa macho yako ,wenyewe, kazi ya madaktari wetu na hao wasaidizi wao ilivyokuwa ngumu na hatari,siyo wanaleta malalamiko yao halafu mnawatimua kazi.Picha tu inaonyesha hawa watu wanavyokuwa 'bize'.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2008

    Does the patient knows that, a public officials(prime minister and his entourage) will pay a visit while he/she is having a heart bypass operation, I mean was there a consent there.

    Myself I would not want anybody apart from the doctors and nurses while i would have any operation even an appendix one, let alone a heart operation.


    Would you ??
    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2008

    Hela kuliko kufisadi mngewalipa hela nzuri jamani afya,walimu,polisi ni sekta muhimu yaani sidhani kama wananchi wangelalamika kama wangeona hawa wenzetu wanajaliwa na serkali mimi nilipangiwa kusoma udaktari nikamwambia baba yangu unataka niishie kuendesha baiskeli maish a yangu yote no way na wala sijilaumu mpaka leo kwa uwamuzi wangu binafsi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2008

    Mgonjwa pole sana. Sasa hapo Pinda ndio yupi?

    -Kaka.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2008

    Hili ndilo jambo tulilokuwa tunalisubiri.Matibabu ya moyo ni gharama sana hivyo kitendo cha muhimbili kuanzisha huu upasuaji utaokoa maisha ya wengi kwani serikali itawekeza kwa kiasi kikubwa ili wananchi wapate huduma nafuu. Ombi langu kwa madaktari ni kuwa wazalendo kwani kazi mnayofanya hailingani na malipo na hivyo epukeni kuikimbia muhimbili ili muende private mkapate pesa nyingi. Nina imani kwa kazi zenu kila mtu anawaombeeni kwa mungu ili muishi vizuri hapa duniani na ahera. Kwa upande wa serikali naiomba iwaangalie wahudumu wa afya na pia iwekeze kwenye vifaa vya tiba ili kuboresha matibabu kwani hii ndiyo njia pekee ya kuokoa pesa za watu kutibiwa nje ya nje wakati nchi ina wataamu. Kwa watalaamu wa sekta zote waliopo nje nao nawashauri waangalie namna ya kushirikiana na wataalamu waliopo nyumbani ili kuboresha maendeleo ya ndugu zao na nchi yetu. MJENGA NCHI NI MWANANCHI.
    PS: Mafisadi msituangushe kwani watu kama hawa wamajitolea kuokoa maisha ya wengi lakini nyinyi mnaiba rasilimali ambazo zinahitajika katika kusukuma maendeleo ya watu wote. Pia pesa zenu za wizi zinawakatisha tamaa watu wanaofanya taaluma nguma ambao wengi wao kipato chao ni kidogo na hivyo watu wengi hukimbilia nje au huacha kufanya kazi za taaluma zao na pia watoto wengi kuacha masomo ya sayansi kwa sababu hayalipi. Msipoiba tutaweza kugawana tunanchokipata kulingana na kazi ya mtu. Naiomba serikali iwe macho ili hiki kituo kisihujumiwe maana watanzania utawasika mara mashine fulani imeibiwa, mara mbovu ilimradi wagonjwa waende wakapasuliwe nje ya mumbili ili wahusika wapate pesa nyingi

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2008

    Hivi wameruhusuje watu kibao kuingia kwenye operating room?? This is not safe for the patient, wajameni kwani wamesikia hiyo movie?? Nchi za wenzetu huwaga wana viewing room, so watu wanaobserve through the glass na sio kwamba wanaingia na mikamera kibao this is not right.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2008

    Anony wa juu. Unasema Pinda anashuhudia kwa macho. Maelezo yanasema Pinda (katikati) na mimi nikiangalia katikati naona mikasi na na gloves. Hivi Pinda ni yupi hapo?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2008

    Ili kupunguza contamination, kwa nini hospitali yetu kuu ya muhimbili haija-design observation area ambayo inakuwa separated from the main operating area na kioo? This is the right time to do it. Otherwise, mnaweza mkawa mnajitengenezea lawsuits kirahisi kama watanzania wakija kustukia rights zao

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2008

    Hivi ni kweli kuwa mshahara wa daktari hata milioni moja haufiki huko bongo? Kama kweli basi this is an insult. Maana hata huku nje madaktari na manurse wanalipwa mishahara mikubwa kuliko profession nyingi. Wanazingatia risk ya kazi yao na muda waliochukua kupata hizo degree zao, it is not less than 7 years. Jamani mishahara africa inabidi iangalie na jinsi kazi yenyewe ilivyo. siyo wabunge kukaa na kutoa hoja wanalipana mahela kibao per day, ndiyo maana kila mtu anataka kuwa mwanasiasa maana huko ndiko kuna pesa na matokeo hatuyaoni bali ni uhujumu wa uchumi.

    ReplyDelete
  10. Very good step forward, je ilikuwa operation with or without cardiopulmonary bypass?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 27, 2008

    WEWE UNASHANGAZA UMUONI PINDA UYO APO SURA KAMA MIMI, MWEEE

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 28, 2008

    Mchangiaji !!Does the patient knows that.

    Naona unajifunza lugha ya kiingereza kwa bidii kubwa, naomba nikusahishishe makosa ya uundaji wa sentensi zako.Grammatical error je does inakwenda na knows ama know.

    Napenda kuwasilisha

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 28, 2008

    Ingekuwa fresh kama wangemtumia Mkapa kwa haya majaribio.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 28, 2008

    Jamani inatisha,kwa sababu bwana Michuzi hajataja jina la aliyekuwa anafanyawia oparation na wala sura yake kuonekana nadhani hii picha haitam-affect.Good step ahead.Upasuaji ulifanikiwa michuzi?
    Kuna mtu amewataja na polisi na walimu.Hata mimi huwa nawaza sana hizi kazi za afya,ualimu na police.Ni moja kati ya kazi ngumu sana.Ualimu huwezi kuuona kama kazi ngumu lakini hata huyo Dr.Mahalu ni kazi ya mwalimu!Nani hakukutana na mwalimu?Labda enzi zileeeee.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 28, 2008

    Huyu Daktari ni ndugu yake na yule 'mtu'wetu aliyekuwa balozi wetu ITALIA,Profesa Costa Mahalu?Au ni majina tu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 28, 2008

    yani hapo jamaa hajui hata nini kinaendela duniani, mpaka azinduke kwenye huo usingizi nusu kaputi si mchezo inanikumbusha feb nilipofanyiwa operation sikujitambua mpaka nilipozinduka baada ya masaa 3.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 28, 2008

    wewe ndungu yangu zemarcopolo yanakuhusu nini,au unataka kujionyesha tuu kuwa unajua matatizo ya moyo?

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 28, 2008

    Doctors siku hizi,baada ya ule mgomo wamepandishiwa mshahara angalau kwa mwezi wanafika gross salary ya "Mega shs" hivi na ushee,ila inategemea na dokta kama docta ni "bingwa" ye anakula shavu zaidi,nao pia wana"ndondo" kibao,si ajabu kuona dokta wa muhimbili yupo muhimbili saa 0700-1100, TMJ hospital 1200-1500,Lugalo hospital 1600-2000,ili kuongeza kipato na pia kusaidia wananchi.
    Ila tuseme ukweli Tanzania hatujui kutumia wataalamu wetu ipasavyo sasa ona Profesa Kapuya anavyotumika visivyo,mara leo waziri wa ulinzi,kesho waziri wa kazi na ajira na maendeleo ya vijana,wakati yule ni daktari bingwa si ajabu keshokutwa utaambiwa yupo Tamisemi,ndio maana Bongo hatuendelei
    g

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 28, 2008

    madaktari wenyewe wa muhimbili kugoma hovyo na operesheni hizo huchukua masaa kibao watakuacha solemba hawa. dont trust them. baadhi yao hawana wito wala maadili. hata hivyo kwa kuwa mi ni mlalahoi sina pa kwenda ni vema maslahi yao yakaboreshwa ili waweze kutuhudumia vizuri.

    ReplyDelete
  20. Anonymous wa May 28, 10:15 AM, nataka tu kujua kiasi ch progress tulichofikia kwa sababu sio kila operation ya moyo ni big deal!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 28, 2008

    Cardiopulmonary bypass (CPB) ni utaalamu unaochukua kazi za moyo na mapafu wakti mgonjwa akifanyiwa upasuaji wa moyo. wakati wa upasuaji wa mfnao kubadili mirija ya moyo ni vigumu kufanyika wakati bado moyo ukipiga. hivyo mtambo unatumiwa kufanya kazi ya moyo na mapafu ili huo upasuaji uendelee bila mgonjwa kuathirika.
    Hiyi machine inaitwa Heart-Lung Machine au pump (Mashine/pampu ya moyo-mapafu)

    Hizi ni operation kubwa ambazo mgonjwa anaweza kutolewa mshipa kwenye mkono au mguu ili kuwekwa kwenye moyo wakati mshipa halisi wa huo moyo unapokuwa na matatizo.

    Sina hakika kama Tanzania au hata Kenya wanayo labda afrika kusini. Hiliwanajua muhimbili wenyewe. Ninachojua utaalamu upo shida ni huo mtambo hadi hapo tutakapoweka kipaumbele kwenye afya.

    Watu wengi hawajui kuwa Muhimbili wapo wataalamu wakubwa na wenye uwezo kinachogomba ni hawana vifaa. Ni kweli matatizo mengi (80%)yanayokuwa reffered India, ulaya au afrika kusini yangetibika Muhimbili kama wangekuwa na vifaa kwani utaalamu upo. Ndo maana watalamu wetu wana soko zuri sana nje amabko vifaa ni bwerereeeeeeee.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 28, 2008

    Kuna mahali nilisikia kuwa operation ya moyo hufanywa mgongoni yaani ili kuufikia moyo basi mgonjwa hulazwa kwa tumbo na kupasuliwa mgongo ili kukwepa vizuizi vya mbavu. Naomba anayejua anijulishe hata kama ni Pinda PM au walinzi wake walioshuhudia jana.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 28, 2008

    we zemarcopolo, vitu vingine uwe unafikiria, moyo ni moyo tu, sio sawa na kidole. kwa nchi kama tz tunakuwa tumepiga hatua sana, kwetu operation ya kidole ndo sio big deal.ifike mahali tushukuru kwa pale tulipofikia. mi naona we mpoki tu.kama ulitaka tujue ungeeleza kidogo unamaanisha nini by hayo materm, thn watu wanakuelewa kidogo. mi naona umejishaua tu!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 28, 2008

    kumbe tuna madaktari humu ndani,naona mambo kibao!

    mnaomuattack zemarcoplo shindweni,legeeni na oneni aibu...LOH..kwani yeye kauliza tu,sijui mmeamua kumshapalia nini!

    and anon wa may 28 7:41 wewe ndio unajifanya unajua english sio??mbona hujaandika kitu in english,we mwenzetu tu hapa,hata usijifanye kumuattack 'mchangiaji' kwani english siyo lugha ya taifa

    AMINA YUSUF

    GIRL POWER!!!!!!!! - siogopi kituuu!

    ReplyDelete
  25. Anonymous wa may 28, 2005. 5:04 PM
    Mimi niliuliza swali tu na nilitegemea kujibiwa na mtu anayeelewa. Kama umeshindwa kuelewa maana ya nilichoandika ujue hilo swali halikuwa lako.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 29, 2008

    Hiyo operesheni maanoni wanaiongelea inaitwa CABG wanatamka "kabeji".Coronary Artery Bypass Graft.Ni expensive na inahitaji utaalamu mkubwa.Bei yake ni around $50,000-60,000.Insurance companies huwa zinapiga mtungo kulipa , usually medicaid/medicare na private insurance na mgonjwa naye hana sehemu yake, co-pay ,ambayo kwa mwananchi wa kawahida huwa ni shughuli.Sidhani kama hiyo ndiyo prosija hambayo mheshimiwa Pinda anahobsavu.
    Mdau, Mtoni kijichi.

    ReplyDelete
  27. KULIKUWA NATATIZO KUBWA KWAMBA WALE WALIOKUWA WANAANDAA SAFARI ZA NJE KWA MATIBABU WALIKUWA WANAPATA ULAJI SASA WAKAMUEKAMUEKEA KIWINGU DR MASAOE ILI ULAJI WAO UENDELEE

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 29, 2008

    asante mganga kwa kutoa ufafanuzi wa kina, na wewe zermacopolo ungebainisha kuwa anaejua akuelekeze,vinginevyo wadau wanakuvaa tu, haya cheki huyu mtalaamu wa kabeji anavyopenda herufi H! hata ambapo haitakiwi ye yuko nayo tu!sasa hambayo ndiyo nini? au anahobsavu!! aa...yani tuko mbali sana kama inabidi tuanze na matamshi!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...