Mwanamziki wa kizazi kipya Ali Kiba Amewasili Ujerumani 25.06.08 Tayari kabisa kwa show ya Miss Tanzabia EU 2008 inayotegemewa kufanyika Jumamosi 28.06.08 mjini Essen germany.
Ali ambaye aliwasili pamoja na promota wake Kassim wakitokea Oslo - Norway.

Wakati huo huo mtanange wa Ulaya kati ya Uturuki na Ujerumani ulikuwa hewani, ambapo Ujerumani Ilishinda 3-2. Ali kiba alipata nafasi ya kushangilia Mjini Essen na baadhi ya washabiki wa Ujerumani wa mpira wa miguu.

Wakati huhuo warembo washiriki wa Miss tanzania EU wako kambini na tayari kabisa kwa mchujo wa round ya kwanza pre-selection utakaofanyika ijumaa 27.06.08.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2008

    Ali kibahiyo kofia yako sasa basi tumeichoka kila siku???
    unajizeesha....

    ReplyDelete
  2. Mkuu hiyo Tanzabia hapo juu ni ya bahati mbaya au umemaanisha? Najua B na N zipo karibu sana kwenye keyboard, nadhani uanweza kuhariri hapo kidogo.
    Nawakilisha

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2008

    mdogo wangu Ali...huu ndio wakati wa kumake cash....life span ya wanamziki wa Kitanzania ni fupi sana.Kesho na keshokutwa ma-tour kama haya uyafanyayo yanaweza yasiwepo. Ule wimbo wako wa MACK MUGGA naomba uwe angalizo kwa yote uyafanyayo ili ile story ya mACK MUGGA isije ikakugeukia na ukawapa nafasi watu kusema kuwa kumbe alipotunga ule wimbo alikuwa anajitabiria yeye mwenyewe future yake. GOOD LUCK mdogo wangu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2008

    Michu!Twaomba mawasiliano na ALI KIBA tuko Marekani..! Haswa namba ya promota wake!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2008

    Michuu, ulimpeleka mdogo wako Ali Kiba, kule mlingotini uliposhauriwa kuhusu kafulana kako nini?? Maana that kofia imekua kama trademark sasa...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 26, 2008

    duh mshikaji noma na wewe kula bwana naona unashindana na Mkuu wa Wilaya ya Tegeta!!!!!!!muda wako dogo.
    2ladies.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2008

    Nyie watu wa US hampatikani kwa simu wala ur not serious kwenye maswala ya promotion.

    If you want the promoter check BongoFamily webtsite au Bongodjs. Tumetafuta promoter US mpaka tushachoka.

    Mapromoter was Europe wote walichangamka na wameshamkamata kufanya shoo katika hizo nchi zao. Nyie vipi ??

    Show some commitment please otherwise mwache Ali atengeneze hella while he can. Shoo zake nzuri na zote FULL house.

    No one will be able to beat his shows in a very long time. Hata Jide yuko hapa UK lakini hatomfikia Ally K.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2008

    hahaha eti tanzabia..walahi michuzi we basi tu!!

    warembo kila konaa...waaoo..anon wa 1 umenichekesha,ila ali kiba vipi hapo?kofia kila cku..aah!

    aisee mi nipo UK,ali kiba kapapatikiwa sana..unlike jide n tid..tunamsubiria mr blue sasa tuone kama atavua nanga au vp..GO ALI KIBA..LONG LIVE MA MEN..JITAHIDI SANA MTOTO WA KIGOMA..ITS ABOUT TIME YOU GET RICH

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 26, 2008

    Sasa huyo binti anayetuonyesha vidole viwili maana yake nini?Goli 2?Huna adabu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 26, 2008

    DC.WA TEGETA NA FULANAZZZ ALI KIBA NA KOFIAZZZZ.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 26, 2008

    Ali Kiba atakapo maliza tour lako la kiwanja pls tunamuomba promotor wako akulete hapa KIMANZICHANA tunakusubiri kwa hamu sana karibu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 26, 2008

    nyie watu mnaosema ali kiba is rich mnanichekesha sana!sasa kama angekua rich si angekua na mansion na mercedes benz...anataabika tu,na ndio maana anafanya tour apate hela

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 26, 2008

    Haki watu wana wivu jamani, yani hamkosi kukoso kitu ilimradi mumwaribe huyu kijana.
    Alikiba ni sexy ndio mana sisi twambabaikia, kijana mzuri kajaliwa kila kitu ,wenye wivu mjiue.

    Wewe uliye sema eti Alikiba awe na mercedez, kafie mbele, kama uko Ulaya beba box ,kama uko Bongo taabika na jua likukupige na upande daladala mbaka uzeeke uso , utamwona hivi hivi Alikiba ana kanyaga nchi kibao ambazo unadoto kuzifikia na hujui utafikaje maana buddget na Visa hazikuruhusu mchawi wewe.

    Sisi twamsupport Alikiba kwa hali na mali na nilijua tuu huyu ni funga la mwaka hakuna msanii atakaye mfikia na Akija USa ndio itakua show ya millenium, maana Alikiba yuko Juu kote duniani anako julikana ,mtake msitake hiyo ni kweli.
    Alikiba ni total package , sura ,umbo, sauti na mvuto anao, yani kila kitu anacho na hakuna anye weza kumfikia , kama mwenzangu alivyo sema ..Go Ali, go Ali goo! we love U

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 26, 2008

    hivi hao wanaoshiriki huo umiss hawana picha? mbona hatuoneshwi picha zao japo wakiwa kwnye maandalizi? mbona mashindano ya mamiss wengine huonyeshwa picha au hao wamefichwa....

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 27, 2008

    Lakini Ali Kiba na hiyo sweta ndio nayo ni trade make yako?

    Maana nakuona toka ulipotoka nalo Bongo na tu ulipokuja hapa UK lilikuwa kama kauka nikuvae.....na sasa tukueleweje?

    Mwambie au waambie hao mapromota wako wakubadilishie usha kuwa SUPER STAR unahitaji mtu wa kukutayarishia pamba za kubadilisha kila siku mara tatu

    Aaaaah usitie aibu kunuka jasho na sweta moja tuuu!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 27, 2008

    wewe anon 10:31 acha utumwa wewe..ali kiba anakujua???

    ReplyDelete
  17. Mdau hapo juu nikusaidie, hiyo style ya vidole aliyoonyesha huyo dada ni ishara ya amani, inajulikana kitaifa. nikama chadema kama sikusei wanakitu kama hicho katika bebdera yao.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 28, 2008

    Hamna lolote ni wivu tuu unawasumbua, mwacheni Alikiba atanue ni kijana kajaaliwa..nasema tena KAJAALIWA , mta muona hivi hivi tuu wabeba box nyie, msiopenda maendeleo yamtu kwa jasho lake , kijana ana sauti tamu vile kwanini asituchengue? Ali kamua tuu tutalipa bei yeyote kukuona handsome!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 29, 2008

    nyie mbona mna mdomo na mna hio?
    goli mbili za nini sasa wakati vidole viwili inamaanisha peace na hata mandela anafanya hivyo hivyo.
    wabongo tusiwe tuna roho mbaya lasivyo hatutaendelea...

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 29, 2008

    mkitaka kuona mamiss walioshiriki wapo www.misstanzania.eu na mshindi kashapatikana jana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...