tatizo sugu la bangi a.k.a ganja ni mojawapo ya mada zitazotawala na kuzungumziwa katika siku hii. ila ripoti iliyopo sio nzuri kwa bongo. anti subi katukumbuesha hili kwa kutuwekea linki hii:
http://dailynews.habarileo.co.tz/home/index.php?id=5447

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kamwe sitayasahau madhara ya matakataka haya ya kulevya.
    Yameniharibia binamu alikyekuwa mwanafunzi bora darasani na kijana chapakazi kujenga maisha. Amebaki kuwa msumbufu na aliyeharibikiwa kabisa, kwa ufupi, mgojwa wa akili.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2008

    Haka kammea ni katamu ukatumiapo kama mboga za majani.wanaokataza kulima wanatunea sisi tukose virutubisho. kwa kukavuta mi simo.
    Nantombe
    Moshi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2008

    CAN I GET THAT WIZZY EAZYYY EAZZZYY...OOOOH ...W£££D...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2008

    subi ndugu yangu hauko peke yako kwenye tatizo hili, wengi limetugusa na na kweli linarudisha nyuma sana maendeleo ya mwathirika na familia yake kwa ujumla. leo ukienda muhimbili ward ya magonjwa ya akili utaona jinsi ilivyofurika vijana kati ya miaka 18 na 30. na kutokana na wingi wa wagonjwa, imefikia hatua wauguzi huwapa ruhusa wagonjwa baada ya muda mfupi sana. ndugu yangu alikuwa serious sana lakini walimlaza kwa siku tatu tu na aliporudi nyumbani akafikia maskani moja kwa moja kuendeleza libeneke la kuvuta. kinachokatisha tamaa ni kuwa hata wakipata nafuu baada ya mfupi wanarudia kuvuta tena, kwa kifupi mtu anakuwa mzigo mkubwa kwa familia. nadhani kama tunaweza labda tuanzishe jumuiya ya marafiki wa watu wenye matatizo ya akili ambapo wana jumuiya wanaweza kukutana na kubadilishana uzoefu jinsi ya kuwasaidia waathirika kwani kuna baadhi yao baada ya kupona leo hii wamekuwa watu safi kabisa na wanafanya shughuli za kujiingizia kipato.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2008

    hii kitu imeharibu wengi saaana.jamani ipigwe vita.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 26, 2008

    Marijuana is NOT A DRUG!!!!!!!! It is something that grows naturally from the earth, and it just so happens that when the smoke is inhaled it creates a sense of relaxation! You sound absolutely ignorant!!!!!!!!!!!! Smoking pot has never been connected to causing any types of syndromes or diabilities! You shoul probably go roll one and CHILL OUT!!!HAHAHAAAA

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2008

    Mimi nadhani tuache unafiki kama tunataka kupambana na hii vita ya dawa za kulevya. Waingizaji, wasambazaji na wauzaji wa dawa za kulevya wanafahamika lakini wanaachwa kwa sababu hii kazi licha ya kuleta utajiri mkubwa kwa wauzaji lakini pia inawaongezea kipato polisi kwani ndiyo wanaotumika kuficha huu uoza. Ili tukomeshe kabisa hii hali na kuwanasuru vijana inabidi sheria za adhabu kwa wauzaji wa madawa ya kulevya irekebishwe ili iweze kuwabana lakini ikibaki kama ilivyo tutakuwa tunapoteza pesa pamoja na muda na hakuna mafanikio mpaka yesu arudi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2008

    Weed haina noma tatizo ni watumiaji wake,ukizidisha sana kuvuta jani lazima likuzingue sana.Mimi ni mwenyeji wa Iringa,kule kwetu tunaitumia hii kama kiungo cha mboga kama ukipikwa mrenda tunapiga miksa na hii kitu,ukitoka hapo unaenda kupiga kazi kama huna akili nzuri,imenisaidia sana kujiamini na kufanya vizuri darasani toka nilipoanza kuitumia darasa la sita hadi chuo kikuu,imenisaidia sana kujiamini ,kujenga afya,na ni pain killer nzuri ninayoitegemea.Soma link hii ujue habari kuhusu utafiti uliofanya unavyoonesha faida za dawa!
    http://www.norml.org/index.cfm?Group_ID=347

    wengine inatusaidia jamani,hakuna asiyefahamu busara za hayati Bob Marley,ni kwa sababu ya doping,US pres. used to smoke that thing! ila kwa wengine siwashauri hasa kids kwa sababu wengi wao wakifanya doping sana vichwa vyao vinadhulika ,sababu ni moja tu,kama ilivyo doping kwenye semicondoctor lengo ni kuifanya semicondoctor iwe conductor kamili ya umeme,kadhalika ukizidisha doping katika hali ile lazima semiconductor ile iwe defected same applies to human head,so doping kiasi kwetu sie sio mbaya,inatujenga!
    So don't give marijuana a bad name!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 27, 2008

    Hello Michuzi na wengine.
    Yawezekana ni kweli kuwa matumizi ya "madawa ya kulevya" kama Bangi yakawa na athari kubwa kwa jamii yetu japo kuna utata wa athari za bangi ukilinganisha na zile za Sigara. Niliwahi ongea na mwanafunzi mmoja wa udaktari akasema bangi si nzuri ukii"abuse" nami nikamuuliza ni kipi unachoweza kuki"abuse" kikawa kizuri? Kuanzia Sukari, Maji hata Imani. Anything. Hakuweza kunipa athari za wazi ama niseme kunielimisha kwa kina athari za Bangi dhidi ya sigara.Sasa kama kuna yeyote anayeweza kuoanisha madhara ya Bangi na Sigara akaja kwenye suluhisho kuwa Bangi ni mbaya zaidi ya Sigara? Nauliza hivi kwa kuzingatia uwiano wa matumizi na kemikali zilizomo ndani ya bidhaa hizi mbili. Ningependa kujua kwa undani maana kuna wakati nahisi Siasa na Maslahi ya Viwanda na Sera fulani zinafanya watu kuangukia kule "kwenye nguvu" hata kama hakuna ukweli. Wenye kulaumu naamini mmefanya tafiti na mmegundua kile ambacho pengine baadhi ya wakuu wa Amsterdam na baadhi ya sehemu za Canada hawajakijua. Ila napenda kupata linganisho la kitaalamu baina ya Sigara na Bangi lenye kunipa suluhisho kuwa bangi ni mbaya kuliko Sigara.
    Nawakilisha

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 27, 2008

    oyaaaah bangi haina madhara yoyote nikiwa kama mvutaji najisikia niko dunia ya kutulia na ninafanya kazi na familya sioni madhara yoyote naitumia kama kunipa mapumziko na kutuliza kichwa changu kwa kazi ngumu ninayofanya jioni najiburudisha na panton simsumbui mtu wala siwehuki ni miaka kumi sasa so watoto msilete nuksi hapa mtaandaoni kama madhara ni mabaya ni pombe wacheni pombe mtaadhirika jaribu bangi utaona utamu wake naomba mungu kila siku bongo watuwekee panton huru kwani ni dawa .oh hii ni safi hasa ya home na nyumbani wanawehuka kutokana jua kali na kama huna kazi inakuchangu lakini kumi panton hoyaaa idumu maisha mzizi kauleta mungu babu zetu ndio zilikuwa sterehe zao idumu panton.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 27, 2008

    watu wengine bwana, eti mtu anatetea bangi na kulinganisha na sigara. Madhara ya bangi inaenda kwenye ubongo, inafanya watu wa hallucinate.hivyo inamaana inaingilia judgement yako kichwani na ndio maana the more you use it, you develop psychotic symptoms, eventually unaanza kuweweseka na kichaa kabisaa. Hizo nchi walizoruhusu wamefanya hivyo kwa lengo la kupunguza matumizi ya kujificha, wanataka wawamonite watumiaji ili waweze kuwapa misaada ya kisaikolojia na kuua soko la magendo,kwa sababu hata ukiikataza watu bado wanatumia vilevile. Hakuna mtaalamu wa matatizo ya akili anayekubaliana na jambo hili.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 27, 2008

    mimi sijawahi kutumia wala sina ndugu aliyeathirika na MSUBA lakini nasikia Msuba hivi sasa unatumiwa kwa dawa ya kutibu/kupunguza maumivu ya Multiple sclerosis.Kuna watu wengi maarufu waishio hivi sasa mfano Montel williams anatumia kupunguza maumivu hayo na sio yeye pekee.Mfano mwingine Queen Elizabeth alitumia MSUBA kutibu maumivu ya kike(menstrual cramps).Pia jimbo la California hapa Marekani limeruhusu watu kutumia Bangi kama dawa kutibu/kupunguza maumivu mbalimbali endapo tu watakuwa wameruhusiwa na DAKTARI.
    Kusema kweli kila kitu hapa duniani kina FAIDA NA ATHARI zake kama kitatumiwa ipasavyo/kupindukia.
    Tatizo vijana wengi hasa wabongo(tunaowazungumzia)wanatumia bangi kujionyesha wao ni wajanja/wamekuwa kiumri as a results matatizo ya kiakili yanatokea.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 27, 2008

    smoke ssshpp errdayy!

    haina madhara!ukijiendekeza lwako

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 27, 2008

    wewe nani kakuambia bangi inaharibu watu? watu wanajiharibu wenyewe pili pili iko shambani wewe inakuwashia nini,kama utaki kupata ukimwi inabidi utulie, ukitumia ushauri huu bangi nayo haiwezi kukuharibu.kwani bangi hata siku moja haimfuati mtu watu ndiyo huifuata sasa kama unajua inaharibu inabidi utulie, waachie watu starehe zao. kila siku unasikia kuna miradi kibao ya kuzuia ukimwi hebu nihesabie kuna miradi mingapi ya kuzuia bangi,kama italingana na ya ukimwi. ulishawai kujiuliza ni kwa nini? kama ulikuwa hujui basi na uelewe kuwa waanzilishi wengi wa miradi wanakula msuba

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 27, 2008

    PLEASE,PLEASE DON`T SHOW THIS AGAIN,PLEASE.I miss the really Arusha shit.Wadau nani anajua Orkokola?Niko ugaibuni ila hua hiyo bangi nikiikumbuka na Gomba kidogo(Mirungi) hua natamani niwe Arusha right away so I get some.This shit changes your perception completely bro,it makes you a happy person all day everyday.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...