Mkuu wa kitengo cha teknolojia ya habari cha NBC Pete Novat (shoto) akipeana mikono na mkuu wa kitivo cha teknoljia ya habari chuo kikuu cha dar Dr. Alfred J Mwambela baada ya kumkabidhi kompyuta 25 za msaada kwa chuo hicho. habari kamili soma hapo chini


Benki ya Taifa ya Biashara - NBC - kupitia kitengo chake cha teknolojia ya habari na mawasiliano imetoa msaada wa kompyuta kwa kitivo cha infomatiki na Elimu kwa Compyuta cha chuo kikuu cha Dar-es-Salaam

Aina hiyo ya msaada ni sehemu ya mpango wa kutoa huduma kwa jamii mpango ambao umewahusisha wakurugenzi pamoja na watumishi kutoka matawi ya benki - NBC - yaliyopo nchini,mpango ambao ulianza tangu benki ya NBC ilipoadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake.

Kuwashirikisha watumishi wa NBC katika miradi ya jamii dhumuni likiwa ni kuitumia faida inayopatikana kwa jamii iliyolengwa ambapo itaiwezesha benki kufanya biashara.
.
Msaada huo ni sehemu ya mpango wa miezi mitano ya huduma kwa jamii ambao utaonesha ushiriki wa watumishi wa NBC katika miradi mbalimbali ya elimu nchini inayogharimu kiasi cha fedha za kitanzania milioni120.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2008

    Dezhaaa! Hongera victor hapa...Can call 832 292 8296.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2008

    hembu tuijadili hiyo aina ya computer inayooonekana hapo,ni msaada au damping?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2008

    computer zilizochoka ndio wanazitoa misaada. Ukiona hivyo ujue wao (NBC) wanabadili compyuta za maofisi yao na hapo wanatafuta pa kuzipeeka (sema) kuzitupa) hizo za mionzi.

    Natka tuone watu ambao kweli wananuanua compyuta kama wanazotumia wao na kutoa kama msaada si hizo mlizozichoka.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2008

    mkuu Mchuzi,

    Dr mwambela siyo mkuu wa kivo cha FIVE,ni Assocociate Dean-Academic.mkuu wa kitivo anaitwa Pof. Ikingura.

    Baada ya kusema hayo,mbona hizo kompyuta zinaonekana ni za zamani sana na wala isyo za kisasa,isije wwakawa wanatoa used.

    mdau wa jamiiforums.

    www.jamiiforums.com

    ReplyDelete
  5. HII INASIKITISHA SANA WADAU YAANI HIZI KOMPUTA ZA JALALANI, VIMEO MNAZIPELEKA SEHEMU KAMA CHUO KIKUU.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 20, 2008

    Waosha vinywa mshukuru hata hizo za jalalani ambazo serikali yenu imeshindwa kuwanunulia zitawasogeza kidogo.... watu wanamaliza chuo hata kutumia computer matatizo kutype 10wpm....
    msaada ni msaada chukuaaaaaaa na mjifunze kushukuru na si kulalamika kwa kila kitu khaaaa

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 20, 2008

    Wabongo bwana ...Hivi computer hiko wapi katika hiyo picha ? Mimi naona monitor tuu hapo . Jee monitor peke yake inatosha kujudge kama computer ni nzuri au lah ?....We still have long way to go.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 20, 2008

    Tusitake kuzinguana hapa,ukweli uko wazi kabisa.Kwani hata kama ni msaada ndiyo wawasaidie watu kwa kuwapa vitu vibovu,vilivyochoka na viliyopitwa na wakati?tena sehemu yenyewe chuo kikuu!Halafu hata hawaoni aibu kupiga picha tena wakiwa wanatabasamu!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 20, 2008

    Desha usimshushie huyo profesa mizigo ....by the way umemwomba Mzee Galusi ruhusa kabla ya kutoa huo msaada?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 20, 2008

    Acheni ujinga nyie wazalendo. Hizo Compyuta zinafaa kabisa kwa matumizi ya shule. Kama unfanya programming, hauhitaji top of the line.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 21, 2008

    Computer zenye screen ya box!! old fashioned, zinachukuwa nafasi kibao mezani, hizo ni za zamani wanachofanya ni damping kwa vile hawana technology ya kuzi-destroy hivyo wanahamishia mzigo kwenu, life yake ikiisha mtajuwa wenyewe kwa kuzitupa kama mtawapa watoto zenu kuchezea haya.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 21, 2008

    Wee anoni wa June 20, 2008 10:49 PM, Acha hizo! Haangushi mzigo wowote pale!Ulo**i!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 21, 2008

    Ukiskia mtu anakupa zawadi kisha unamtupia usoni ndio hapo maana hiyo ni dharau na sio msaada.Hata chekechea hawaitaji hizo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 24, 2008

    KAKA MICHUZI HII SI KARNE YA MIKOMPYUTA ZENYE VICHOGO, NAONA HAWA NBC WANADHARAU, NAOMBA CHUO KIKUUU WAANDAMANE NA KUWARUDISHIA MAJESUSI HAWA MADUBWASHA YAO WAKAYAPIKE SOUP.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 16, 2009

    Hamjui mlisemalo, hizo computer siyo kwa ajili ya kujifunzia Microsoft word, ni kwa ajili ya electronics (component level), muelimishwe siyo mnalipukalipuka tu bila hata kujua madhumuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...