.jpg)
.jpg)
leo hii jengo moja lililopo makutano ya mtaa wa Zanaki/kisutu limeporomoka kwa kile kinachohisiwa kuwa ujenzi usio makini. inasemekana jengo hilo ambalo bado lilikuwa likiendelea na ujenzi lilikuwa limeshafikia ghorofa kumi kabla ya kuporomoka lote.habari ambazo bado hazijathibitishwa wakati uchunguzi ukiendelea zinasema kuwa baadhi ya mafundi waliokuwa wanalijenga jengo hilo ambao bado idadi yake haijajulikana wamefukiwa na hicho kifusi.
tutaendelea kufahamishana kadri habari zitavyopatikana.


Unajua hii Nchi unajua cjui tunakoenda wapi?Kwani nilisoma juzi cjui Mjegwa Blog au Michuzi Jr blog alisema kwani mijengo hii kwa nini isibaki kam kumbukua kuwa na Old Town na nyumba zake sio kila mahali jiji linakubali linakula hela tu sasa mnaona hiki tunaomba Misoup mshauri Meya na yeye alizungumzia Dar iwe mji wa Tourism hata Ulaya Uk kuna miji imewekwa kwa kumbukumbu ,Watanzania wachache wanajali mitumbo yao!!!!!!!!Hii ni Tanzania zaidi tuijuavyo jamni STOP Kuvunja majengo wakitaka wajenge Tegeta huko Kimara ,Tabata ili wapanue mji sio Town na kkariakoo tu jamni
ReplyDeleteuo ni ujenzi olela,cement mfuko mmoja,matofal 900 kubana bajet,uo ni upumbavu,msajil wa ujenz ni nan iv?
ReplyDeleteinabid haadabishwe kama yule wa wilaya ya temeke,jengo lilivyoanguka.
Mdau mm naona huyo Mdau wa kwanza kaongea point kabisa ,Wakajenge migorofa Mbagala huko ili mji upanuke sio Town na Kariakoo hii Ishu ni Mafisadi wala Rushwa wapenda matumbo yao mnaona sasa Wasajili wa Ujenzi na Manispaa husika ,Meja wa jiji Mr Kimbisa amka sasa mwisho vibali kujengwa Town na kariakoo migorofa wajenge huko ili Mbagala majengo kuya kaz,Kisarawe huko Kimara ,Tabata huko ili Town iwe ndo Old Town oneni Zanzibar wana Stone town za kale hadi raha
ReplyDeleteMIMI NATUPA LAWAMA KWA MAOFISA WA ARDHI.NI WALA RUSHWA SANA HALAFU NI WAVIVU,SWALA LA BUILDING PERMIT WANALICOMPLICATE SANA.ILI UPATE KIBALI CHA KUJENGA LAZIMA UTO RUSHWA. MATOKEO YAKE NI MIPANGO MIJI MIBOVU,MSONGAMANO BARABARANI,MIUNDO MBINU MIBOVU YA MAJI TAKA N.K.ASILIMIA KUBWA YA WAKAZI HAPA DAR HAWANA HATI MILIKI ZA VIWANJA VYAO.KWA SABABU YA UFASADI NA UKIRITIMBA WA MAAFISA WA WIZARA YA ARDHI
ReplyDeletePoleni sana
ReplyDeleteDuh! haihitaji elimu ya Chuo kikuu kujua kinini kinaendelea katika sekta yab mipango mini.
Polisi msicheze mbali kabisa na tukio hili wahandisi wakamatwe na wafikishwe mahakamani pia vibali vyao vifutwe ni wauwaji hao, kama hilo jengo lingeporomoka wakati watu wanaishi humo inekuwa vipi?
ReplyDeleteNilishawai kusema kwamba development pasipo standard ni sawa na maendeleo hewa. Tanzania hakuna watu wanaoenforce good standard kwenye huo ujenzi.
ReplyDeleteMajengo mengi ya Kariakoo yanajengwa ovyo, kwa kigezo cha Low cost na madhara yake ndio hayo. Kuna mengi tunaweza kujifunza kutokana na hili. Kwanza ni serikali kusitisha ujenzi wote wa high rising builidings wakati unatafuta good standard sababu they don't have one.
Ujenzi wowote wa in the city unatakiwa uende sambamba na ujenzi wa parking sababu parking ni kichwa cha mwenda wazimu.
Na expect serikali kwanza itamtaka mkaguezi wa majengo aleze kwa startment kwamba mara ya mwisho alivyokwenda kufanya inspection kwenye hilo jengo what was his suggestions? Na kama hatuna wakaguzi wa majengo then kwa nini tunajenga?
Mdau wa US tawi # 1
Michuzi, katika habari yako waeleze wasomaji kuwa jengo hili liko jijini Dar es Salaam na ajali hii imetokea hapa Dar es Salaam. Sio wote ambao wanafahamu mtaa wa Zanaki/Kisutu uko sehemu gani.
ReplyDeleteyataporomoka mengi sana huo ni ujenzi poa inabidi msajiri wa majengo wawe makini sana na hii mikataba wanaoingia na baadhi ya wafanyabiashara walio wengi ukwei hawana uwezo wa kujenga maghorofa kwa kiwango cha bora......
ReplyDeletemkandarasi afungiwe hafai bora limeanguka kabla halijaisha manake ahiia ni balaaaaaaaaaaaa!!effect zakuiba mitihani hiyo
ReplyDeleteITV inaonyesha kwa sasa Mhandisi wa manispaa ya Ilala amekamatwa na polisi, hii ni kutokana na jamziba ya wananchi kuwa mara nyingi alikuwa akija hapo na kuchukuwa vijisenti na kutokomea lakini ukweli umebaini jengo lilikuwa na nyufa wataalum wamesema kiasi cha cementi kilikuwa kidogo sana.......
ReplyDeleteWewe Anon wa kwanza unaongelea nini? Hivi unajuwa kinachoendelea ama unapiga domo tu?
ReplyDeleteSoma habari uielewe kabla haujaropoka.Hilo jengo si la zamani(kama habari inavyosema).Lilijengwa bila kufuata kanuni za ujengaji ndiyo maana limeporomoka na sio limuvunjwa kama ufikiriavyo.Halafu kuna majengo(maghorofa) ndani ya Dar ambayo yamejengwa bila kufuata kanuni za ujenzi wa maghorofa.Kuna jamaa mmoja alijenga jengo la shule(kule Tegeta) ambalo lilikuwa mbioni kuporomoka wenyeji wa Tegeta ukiwemo DC Michuzi nadhani mnaelewa ni jengo naloongelea.Sijui hali ya lile jengo lilivyo sasa maana mara ya mwisho kuliona ilikuwa miaka 2 iliyopita,sasa watu kama hawa wakiendelea kujenga majengo sijui kama kuna mtu atasalimika.
We anon wa kwanza unasema nini? Yaani hata huwezi kuandika kitu kikaeleweka? Anony wa pili si ajabu wewe ni Mhaya kwani h zote umezitoa na kuziweka zisipotakiwa mf. huo wewe unaita uo, aadabishwe wewe unasema haadabishwe ali mradi kasheshe tupu.
ReplyDeleteHii ni hali ya kusikitisha na kama kawaida hii ni Tanzania. Kuna jambo la kushangaza hapo? Everything is possible katika hizi nchi zetu ali mradi uwe na hela.
Semeni wenyewe sasa maana kila siku tunawalaumu wanasiasa kwa utendaji wao mbovu na kutofuata ushauri wa watalaam sasa hapa nani alaumiwe, engineer, mmiliki au?
ReplyDeleteHii nchi bado inasafari ndefu, majengo yetu mengi hayana ubora na siku tetemeko likibip Dar basi mjue yatakuwa ni maafa makubwa. Mainjinia wetu wanataka akimaliza ghorofa alilopewa ajenge naye apate la kwake kwa bajeti hiyo hiyo inayotolewa na mmiliki na badala yake bosi anapata jengo lisilo na ubora yeye anapata nyumba bomba. Hii tabia imeenea hasa kwa watalaam wa fani zote na matokeo yake ni kupata vitu ambavyo havilingani na gharama halisi na pia kuchelewa kwa miradi kwa sababu pesa nyingi zinatumika kuwalipa watu kama rushwa. RUSWA NDUGU ZANGU ITATUMALIZA, usimnyoonyeshee mwenzio kidole, anza wewe kwa kusema rushwa NO hii itasaidia kuinusuru nchi kwa majanga. Nadhani sasa tuwe na mijadala ya wazi ili tujadili kila sekta na changamoto zake pamoja na kufichua njia zinazochangia rushwa kwani huenda watu wataona aibu na kuinusuru nchi na matatizo
Mi naomba serikali itangaze hali ya hatari maeneo ya kariakoo na mjini, maana huu ujenzi wa majengo unavyofanyika ni hatari, kuna jeno jingine liko mkono wa kulia ukitoka roundabout ya uhuru ukiwa unaenda ilala kabla hujafika TBL, lile jengo limepinda kabisa (jengo lina langi ya bluu). Vyombo vinavyohusika huwa havijali mpaka ajali kama hii itokee.
ReplyDeleteMungu atusaidie tu, maana hali tunakoenda sijui itakuwaje. Tanzania mambo yanaenda utafikiri hamna wasomi au vyombo vya sheria.
jamani wadau nadhani hapa sasa tujifunze kupitia kila mahalihasa Rushwa,POLENI wahanga wa tukio sie hapa Musoma tumestuka sana.
ReplyDeletekwanza nadhani.
rushwa toka Vyoni hasa kuwapa degree wahandisi,Rushwa juu ya usalama wa majengo,Rushwa juu vifaa vya ujeni vinaingia nchini vikiwa katika hali Duni.
Pia Bei ya vifaa vya ujenzi viko Juu hadi inapelekea watu kujenga majengo Duni ili kwa gharama Nafuu
kiwepo kitengo cha ukaguzi maaluma ya Majengo ili isitokee tena Hapa Tanzania.
pia kumeibuka kampuni Nyiiingi za ukandarasi zisizo na kiwango,nadhani tathmini ya kina Ifanyike Haraka
mfuko mmoja matofali 900 nimekusoma mkuu.
ReplyDeleteSupprise , suprise !
ReplyDeletePoleni sana.Na hapo si tetemeko la ardhi wala kimbunga.Huu ubaniaji wa sementi utaleta hasara kubwa sana baadae kwa matukio hata kama ya vimbunga n.k kama yakitokea.Makampuni ya ujenzi yaache tamaa zisizo na faida kwa maisha ya binadamu.
ReplyDeleteTuombe Mungu azidi kutunusuru na majanga zaidi tunayojitakia,lakini ukweli ni kwamba jiji letu maghorofa mengi hasa yanayojengwa maeneo ya kariakoo na sehemu za katikati ya jiji,mengi yanajengwa juu ya mitaro ya zamani ambayo ilijengwa enzi ya wajerumani,na ishara nzuri mnayoweza kuthibitisha ni wakati wa mvua jiji linavyogeuka bahari.
ReplyDeleteHapa wa kwanza kulaumiwa ni jiji kwani hili wanalijua wazi na wanahistoria hii kuhusu kupotea kwa ramani iliyokua ikionesha mitaro mfano ule unaoishia pale posta ya zamani.
Nilishawahi kushuhudia mkandarasi pale kariakoo(jengo kapuni) wakati timu yake wanaandaa msingi,baada ya kufukua sana chini(kariakoo ardhi yake ni mchanga,udongo upo chini sana) ulikutwa mtaro lakini jamaa waliamua kudrili na kunyenyua pillars baada ya kuufunika.Leo jengo likidondoka utasikia anakamatwa mkandarasi pekee,wakati kosa limeanzia jiji.
Ushauri wangu ni kwamba ujenzi mpya wa maghorofa kariakoo na katikati ya jiji usitishwe na kwa watakaotaka waende nje ya jiji kama walivyofanya watu wa ubungo plaza,milleniam tower,ili pia kupunguza msongamano,badala ya kuchukua uamuzi wa muda mfupi tu wa kumshitaki mkandarasi au kumfukuza mtu kazi
Ni rahisi sana kuwapata ma-"experts" baada ya tukio!!!!!
ReplyDeleteUtaalamu wenu uonekane kabla ya tukio.
Tanzania ni lazima iamuke bila kungoja "kifo cha mzaliwa wa kwanza", mithili ya hadithi ya Mfalme Firauni wa Misri ya zamani!
Kwani lazima kujenga Dar tu? Kwa nini tusiendeleze miji mingine ya tanzania, hasa miji ya mikoa?
ReplyDeleteMungu awapumzishe pema marehemu, amina.
ReplyDeleteHapa nawalaumu wanasiasa. Walileta bajeti mbovu ikasababisha ongezeko la ajabu la bei ya saruji. Unajua tena wabongo, bajeti lazima ikubali. Si ajabu mmiliki akaibuka na "mfuko matofali 900". Si ajabu wakachukua saruji ya Mbeya inayoonekana nyeusi. Mhandisi naye akakubali shinikizo. Kwa elimu aliyopewa kwenye mazingira yetu ya elimu si ajabu. Kama tunavyofahamu bajeti ya mashangingi ni kubwa kuliko ya madarasa hadi imebidi tuchangishane kujenga madarasa KINGUVU. Matokeo ndio hayo.
Haya mambo hayajaanza leo, majengo kibao yameanguka lakini bado tumeng'ang'anepo tuuuu.
wewe vipi? Kinachozungumzwa sio kujenga Dar. Hata mkijenga huko kwenu ujenzi ukiwa kama huu wa ufisadi majengo yataporomoka tuuuu!!!!
ReplyDeleteTukisema wenye hela tumieni mainjinia hamtaki , haya sdasa, nyie laumuni mainjinia tu , lakini hakuna injinia amabye anaweza kugfnya utumbo huo, injinia wa DSM ni wazuri, na kama hawawezi huwa hawafanyi nyie subirini msikie
ReplyDeletembona majengo yaliyojengwa zaman yanadumu sana,kuliko majengo yanayojengwa sasa hiv,ina maana wahandis wa zaman ni bora kuliko wa sasa
ReplyDeleteTATIZO NI KWAMBA HAWA VIBARUA WANANYANYASWA SANA,WANAPOPATA NAFASI HAWAFANYI KOSA. NA HAYA MAGOROFA NI HAKI ZETU WATANZANIA CHAAJABU WAHINDI NDIO WANATUZULUMU HAWALIPI KODI, INAVYOTAKIWA UKICHUNGUZA MAKAMPUNI MENGI YA WAHINDI KODI WANAYOLIPA NI KIDOGO SANA NA HAWA WATU WA TRA HUWA WANAJIFANYA KUFUATILIA LAKINI WANAPOKUJA JUU BASI ANAZIBWA MIDOMO. TUNA MIFANO YA MAKAMPUNI AMBAYO HAYAWAKILISHI KODI KAMA INAVYOTAKIWA. MMILIKI WA HILO JENGO UNGEJUA ANAVYONYAYASA WATANZANIA NAONA SALA ZAO ZIMEFIKA MSHAHARA KIDUCHU KAJAZA NDUGU ZAKE KUTOKA INDIA ETI EXPATRIET ELIMU HAWANA ILA MISHAHARA MIKUBWA. IPO SIKU MUNGU ATARUDISHA HAKI ZETU MIKONONI MWETU HAWA WAHINDI SIO WATU KABISAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA, MBONA HAYA MAGOROFA YATADONDOKA MENGI WASIWALAUMU MAKANDARASI WAJILAUMU MISHAHARA WANAYOWAPA.
ReplyDelete