wadau wakiwa karibu na eneo ambako jengo la ghorofa kumi lililokuwa linajengwa lilipobomoka lote leo.
habari mpya toka sehemu ya tukio zinasema watu wanne wameopoloewa na kukimbizwa hospitali. habari za awali ambazo hazijathibitishwa bado zinasema wanasadikiwa kufa baada ya kufunikwa na kifusi cha jengo hilo.
inasemekana watu hao wanne walikuwa ndani ya nyumba ya ghorofa tatu iliyo jirani na hilo ghorofa, ambapo baada ya kuangukiwa na kifusi wakawa wamenasa ndani.
hadi milango ya saa kumi watu watatu walikuwa wameshatolewa, na juhudi za kumpata aliyesalia ama waliosalia zinaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2008

    Dah! habari inasikitisha hii, sipati kusema. Utakuta majengo yote mapya yanayochipua katikati ya jiji la Kandoro ni mwendo huu huu. Nasikia mhandisi wa jiji katiwa korokoroni. Hii sidhani kama inasaidia. Hizi taasisi za usimamizi wa majengo, ikiwa ni pamoja na vyama vya wahandisi, nazo ziwajibike. Maana sidhani kama wanafanya wajibu wao wa kukagua ujenzi unaoendelea zaidi ya kula vijisenti.

    Halafu nashangaa Haki hajachota habari hii hadi saa hizi. Kaka Mithubu humemuwekea biti nini, maana jamaa kwa kukopi na kupesti habari za wenzie hajambo. Najua Mithubu utaibania hii kumlinda Haki hambaye nasikia ni rafikiyo. Ukweli saa ingine uwe unaachiaga, mana jamaa anaiga kila ufanyalo, tena kwa kubembea mgongoni kwako tehe tehe tehe. Usibane Mithubu kama kweli unajali uhuru wa habari na habari ndiyo hiyo...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2008

    Poleni sana kwa tukio hili la kusikitisha sana. Nilikuwa nasikiliza Radio Maria Nimemsikia Kamanda wa Polisi kanda maalumu Dar akisema watu watatu waliopatikana wamepelekwa hospitali, ingawa hakutumia kabisa neno wamefariki. Tuombee wawe wazima

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2008

    poleni sana waathirika. inawezekana wapo hai kwani niliona kwenye picha moja ktk mtandao wa global pulihers tanzania ukimuonyesha kamanda kova akiongee kwa simu na watu waliofukiwa na kifusi hivyo kama waliwahi kuwatoa huenda watakuwa hai

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...