mfano wa jengo jipya la kitachukuwa chuo kikuu cha utalii barabara ya shaaban robert karibu na makumbusho ya taifa na chuo cha ifm jijini dar
mkuu wa chuo cha taifa cha utalii mama agnes mziray akiangalia mfano wa jengo jipya linalojengwa mtaa wa shaaban robert street jijini dar ambalo litakuwa chuo kikuu cha utalii nchini katika azma ya serikali ya kuiboresha sekta hiyo nyeti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2008

    Ni hatua nzuri kuwa na chuo kikuu cha utalii, hongereni sana kwa hilo ila nina maoni tofauti ya kiutaalamu kuhusiana na hilo jengo! At the moment jengo linaonekana vizuri tu ila mimi nafikiri ingekuwa idea nzuri hilo jengo lingejengwa nje ya mji kidogo even eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Ardhi University kwa sababu kuu zifuatazo
    1.Hapo mjini parking ni mgogoro, hata kama wana basement parking, haziwezi kuwatosha lecturers na wanafunzi. Take an example from IFM
    2.Accomodation for students, sijaona michoro ya hilo jengo, may be iko included ndani ya jengo, kama haijawa included sijui wataiweka wapi manake naona site yote imejaa.
    3.Future expansion- sijui itakuwaje manake naona site yote iko covered, na vertical expansion sijui kama ni possible manake naona hiyo roof inaonekana kutoruhusu jambo hilo.
    Apart from the above comments, the design looks good, the architect tried hard, but future sustainability and expansion of the entire project might be at stake.
    Experienced Architect.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2008

    Sasa kaka MICHU, kwanza Hi? Pili kuna kitu kianivunja chaga zangu Neno Mtaa wa Shaaban Robert Street, uko wapi huo hapo DSM?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2008

    Wabongo kweli tu wabongo! mwaka huu wa 2008 bado tunapanga kujenga chuo kikuu cha whatever katikati ya jiji wakati tunayo maeneo makubwa nje ya jiji ambayo yanafaa sana hata kwa upanuzi na mandhari ya vyuo kama hivyo. ninashangaa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2008

    yaani tafadhari kinapofunguliwa lazima somo la kwanza kabisa kufundishwa nakutiiwa mkazo liwe costomer care! duuuu wadau twende sambaba na mama mkuu wa chuo anapashwa kuanza kuwapeleka shule walimu wachuo wapigwe msasa kwani wao mbuuuuuuu si kwamba tunawacheka lakini ni ukweli lazima ngumbalu iwepo kuboza resha maisha, waliojifunza enzi yamepitwa na wakati sasa mteja ni mfarume lazima uwe na njia za kumbembeleza!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2008

    Suala la walimu halina noma manake tz ina wanafunzi wengi wanakula kitabu kwenye sekta ya tourism nchi za nje big up sana tz big up ila chuo kimekaa sehemu ambayo sio naomba wasije wakafany mistake kukiweka hicho chuo town

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2008

    Namuunga mkono anon wa kwanza hapo juu..kwa kweli eneo lilichaguliwa kwa chuo litakuwa usumbufu hata wakati wa ujenzi inabidi barabara kadhaa zifungwe ili kupitisha vifaa vya ujenzi na pia tunalia msongamano wa magari kuelekea mjini na bado tunajenga vyuo vikuu 'city center'...nawapongeza wale waliokuwa na idea kule mwanzoni kujenga Chuo kikuu Dar kule mlimani. Mawazo yangu chuo kikuu cha utalii kijengwe nje ya mji wa Arusha au Morogoro

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2008

    .....Najua hoja hii haitakuwa na uzito kwa wahusika kwa sababu fulani fulani .
    MICHUZI, PICHA HIYO YA CHUO NI NZURI SANA .

    BUT, NANI ASIYEJUA KUWA MSONGAMANO KATIKATI YA JIJI NI MATOKEO YA NGURUNDIKA HUDUMA ZOTE HAPO MJINI. AU HIYO INAHITAJI DEGREE KUFIKIRIA ??????
    KWA NINI CHUO HIKI KISIJENGWE MAENEO NJE KIDOGO KAMA VILE KILIVYO CHUO CHA DIPLOMASI AU USTAWI WA JAMII ?????????????
    INAKATISHA TAMAA, TUNAWEZAJE KUSEMA TUTASAMBAZA MAENDELEO SAWI KTK NCHI NZIMA KAMA TUNASHINDWA HATA MAMBO MADOGO KAMA HAYA?

    PENDEKEZO: wajenge hicho chuo maeneo yanayopita Port Access rd(mandela Rd). Hususan maeneo ya buguruni .
    wengine nanyi toeni maoni ya location, tuwaachie wahusika maamuzi .

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2008

    location ya ovyo kabisaaaaaa!!
    wanapoteza hela.
    Sikutegemea kama kuna watu walio na post kubya ya kufanya maamuzi serikalini kuhusu mambo ya yalio dynamic kama utalii wanaoweza kufiri upuuzi kama huu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2008

    jamani! nchi hii mbona watu wanafanya mambo utadhani bongo zao zimebana haziwezi kufikiri hata kidogo, kwani ni lazima majengo yote yabanane sehemu moja? maeneo yote tuliyonayo. Nafikiri sasa ni wakati mzuri wa kueleza office sehemu nyingine kama kibaha, bagamoyo na kwingineko.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2008

    Mimi napendekeza Chuo Hiki kijengwe Kwanza kabisa Arusha Au kama wanataka kuwa karibu na Dar es salaam wakijenge Morogoro ikishindikana kabisa kabisa yani basi Bagamoyo na Kisarawe pia. Tumechoka mrundikano huu jamani. Hata utoke kwako saa 12:00 kumi na mbili kamili asubuhi bado foleni ipo!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2008

    Kama sikosei katika vyuo vyetu vikuu hakuna chuo kinachofundiha mambo ya utalii i.e Hospitality Industry. Jambo muhimu baada ya hiki chuo kuanza kufanya kazi na kupata wahitimu ni serikali...Kwenye mahoteli yetu wamejazana, wahindi, wakenya, wasauzi na wazungu kibao ambao hawajui fani hii...waswahili wanakuja na vyeti vyao vya cambridge wanaambiwa wewe bado, unakula 150 wakati mkenya anakula kama 1,000 ivi na incentives kibao. Kwahiyo tuangalie jinsi ya kuboresha kunufaisha wazawa katika sector hiyo unless itakuwa haina maana. Wakenya wengi wanakimbilia huku kwasababu wanalipwa package za maana, Huko kenya hawa jamaa hawana ishu, nenda wewe sasa mbongo hiyo ajira ya kufagia parking hutopata lkn huku tz kuna mahoteli mpaka wabeba mizigo ni wakenya...kudadadek Bongo.
    Zanzibar kuna wazungu wana kuja kama tour leader baada ya muda unasikia kala shavu la umeneja mara kajenga vibangaloo vyake ghafla mchizi anakuwa milionea ivi ivi wkt sie tunakimbiza na mishahara ya elfu 80...inaniuma sanaaa

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 25, 2008

    MPANGO MZURI SANA ULIOCHELEWA, WAPINZANI WETU WA JADI WANA UTALII COLLEGE INAYOVUMA SANA MIAKA MINGI.
    MAONI YANGU HICHO KI-BLOCK CHA GHOROFA TATU NI KIDOGO SANA UKIZINGATI UKUBWA WA SEKTA YENYEWE NA ENEO KILIPO.
    LAZIMA MAHITAJI YA CHUO HIKI YATAONGEZEKA SANA SIKU SI NYINGI KUTOKANA NA KUKUA KWA KASI KWA SEKTA HII NA PUNDE JAMAA WATAANZA KUHANGAIKA KAM WAFANYAVYO MUHIHMBILI SASA HIVI. KWANINI WASINGEENDA MBALI KWENYE ENEO LA KUTOSHA, WAWE MPAKA NA HOSTELI?
    KWANINI JAMAA ZETU WANAKOSA UPEO? ANGALIA NYERERE ALIKOKIPELEKA CHUO KIKUU, WANA MAENEO MPAKA WANATOA KWA WAWEKEZAJI.
    TATIZO LANGU NI ENEO, HAMNA HATA MAHALI HAO JAMAA WATAWEZA KUWEKA HOTELI YA MFANO KWA AJILI YA MA-TRAINEE...
    KWELI TUNAONA KWENYE NYAYO ZETU TU MAANA UTALII NDIO SEKTA KUBWA YA TATU DUNIANI BAADA YA MIHADARATI NA MAFUTA.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 25, 2008

    kweli kabisa location matters, anon aliye sema arusha amepatia saaana kwani practical nyingi zitafanywa bila kuongezea ghalama nyingi kwa wanafunzi na arusha ni mji wa kitalii kwa hali hiyo itakuwa bore zaidi kijengwe hapo na kusema kweli hayo maeneo yaliyo lengwa ni bomu kabisa sehemu kama kigamboni kuna ardhi, kibaha, hata mbezi pls mbona ma Town planner mnatuangusha itakuwaje mnazamisha akili na kuendelea kuubana mji, my suggetion ni kwaba hapo town iwe kwe tu aministration lakini chuo chenyewe kitafutiwe sehemu nyingine!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 25, 2008

    Viongozi wetu bwana.Kwanini hiki chuo hakikujengwa ARUSHA??sababu ameshazitoa rafiki yangu June 25 11'43a.m hapo juu.Habari ndiyo hiyo.Mijitu imekomaa na Daresalaam,mijengo ya kubanana,car park ya shida n.k

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 25, 2008

    Hengera kwa wadau wote walioweza kufanikisha kuanzishwa huu mradi. Naamini huu ni mwanzo mzuri wa kuendeleza sekta ya utalii Tanzania na pia kuwawezesha watanzania kujiendeleza kielimu.

    Pendekezo langu, kwa sababu DSM center imeshajaa saana, ni bora kutafuta maeneo mengine nje ya jiji kama vile Kibamba kuanzishwe campus itayokua na uwezo wa kupanuka na kuudumua wanafunzi wengi. Na siku za mbeleni hapo panaweza kuwa sehemu ya administration....

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 25, 2008

    Napendekeza kijengwe Arusha au Bagamoyo, city centre ni kutuongezea msongamano.

    ReplyDelete
  17. Hivi jamani kwani lazima chuo kijengwe katikati ya mji? Mimi ninashauri kingejengwa Kisarawe kingesaidia kupanua mji maana Kisarawe ni mji wa zamani lakini haundelei aliyeenda Kisarawe mwaka 2000 akienda tena leo atakuta mabadiliko madogo mno. Inachosha hii, anyway nice building though.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 25, 2008

    whats the point???there are no jobs in tanzania??

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 25, 2008

    Hebu wadau jaribuni kutafuta email na simu ya wizara ya utalii tuwaandikie au kuwapigia simu kila mtu afanye hivyo,tuwaambie waache kufanya mambo ya ajabu ajabu ya kujenga hicho chuo eneo hilo...yaani kweli city planner na hao utalii sijui wamechanganyikiwa au hawajui kazi yao,jiji limejaa ile mbaya lakini bado wanarundika mijengo amabayo ingeweza kujengwa nje ya mji...its a disaster hawa city planner!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 25, 2008

    we mla vumbi acha kula vumbi,we mtu wa kisarawe nini?bongo pale posta mpya majengo sio mengi,embu jengeni hapo hapo kupendezesha mji..cheki nairobi

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 25, 2008

    wewe anon 3:58 whats the point of you being a human being then?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 25, 2008

    Mi nafikiri chuo hiki kingejengwa Singida sio lazima Arusha au Dar

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 27, 2008

    Jamani ,hata mimi naungana na watanzania wenzangu, hivi hawa watu wa City Development plan hawaigi nchi nyingine,hivi mpaka sasa bado wanasongesha majengo tu katikati ya mji?barabara ziko wapi, parking je?Jamani tubadilike ,tuanzishe miji mipya na yenye mpangilio, katikati ya jiji hilo sasa zitafutwe pesa za kujenga flyover,na joto litapungua.

    ReplyDelete
  24. me nasema chuo kimeyengwa mahali pazuri tu ila kuna kitu kimoyo michuzi naomba ukaulizie kuhusu hiki chuo mbona hawasamini wanafunzi wanao soma hapo haswa wanafuzi wa wanao soma utalii maana kuna rafiki yangu kamaliza hapo lakini amekataliwa kujiunga na elimu ya juu sasa huoni kama huo mradi utapotea bure kama hatuwapi nafasi watu wasome?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...