Michuzi na wadau,
Blog hii ya jamii kwa sasa inaendelea kujadili mada nzito ambazo zinawasaidia wadau mbalimbali katika maisha yao ya kila siku.
Mimi leo naleta mada inayohusu kabila liitwalo 'Wachagga' na kama kweli lipo kihalani. Kwa kuanza naomba wasomi, wana zuoni, na hao waitwao wachagga wawe ndo wachangiaji wakuu katika maelezo nitakayotoa hapa chini.
Ni ukweli kwamba kabila lolote linaundwa na watu ambao wanazungumza lugha moja, na kuwa na mila na desturi zinazofanana.
Kwa kimombo "A CERTAIN TRIBE IS MADE UP OF PEOPLE WHO SPEAK THE SAME LANGUAGE, AND ALSO SHARE THE SAME CULTURES AND TRADITIONS.'
Sasa kwa hawa wanaojiita wachaga waishio mkoani Kilimanjaro wengi wao hawazungumzi lugha moja na mila na desturi zao ni tofauti.
Mfano ni kwamba Warombo wana lugha yao na tamaduni zao tofauti. Hali ni kama hiyo hiyo kwa watu wa Vunjo(watokao Mamba, Mwika, Marangu, Kilema na Kirua, Old Moshi, Uru, Kibosho, Machame, Lyamungo, na Sanya Juu).
Wote hawa wana mila, desturi, na tamaduni zao TOFAUTI. Sasa ni kwa nini wote hawa kwa wingi wao waitwe 'WACHAGGA?'.
Makabila mengine nchini kila moja yana lugha moja, ikiwa ni pamoja na desturi na mila zisizotofautiana miongoni mwa watu.Kwa sasa najitahidi naandika kitabu kuonyesha kuwa hakuna kabila liitwalo
WACHAGGA, bali kuna warombo, wakibosho, wamarangu, wamachame, wauru na wa old moshi. Wadau nipo sawa? Naomba michango...
DEO MUSHI
DAILY NEWS - ARUSHA OFFICE
Haya tena wataalamu wa lugha na makabila, huyu jamaa kwa kiasi yuko sawa na kiasi hayuko sawa.
ReplyDeleteNasema hivyo kwa sababu moja kubwa naomba Deo ufuatilie historia ya haya makabila yote na namna yalivyoanza, ndio uamue kama kuna kabila litwalo wachaga au hakuna.
Then ni wachaga na sio wachagga.
tukiacha wachaga tukangalia makabila mengine kuna wamasai na waarushawote hao ni kabila moja. Tofauti ni kuwa katika miaka fulani wamasai walichanganyika na wameru ndio kukawepo kabila linalojiita waarusha. Then kuna wapare na wagweno wote ni wapare lakini wagweno ni kabila lilokuja baada ya wapare kuchanganyika na wachaga.
Hivyo ukifuatilia kwa undani utakuwa unakosea kwa kusema hakuna kabila la wachaga.
Ushindwe na ulegee wewe unayejiita Deo Mushi...Wachaga tupo na mila zetu zinafanana ila ni lafudhi tu zinatofautiana.Kichaga ni kile kile.
ReplyDeleteDeo mushi naons hujafanya utafiti was kutosha kuhusu mada yako.Hawa watu wanaoitwa wachsgga ni kabila moja na lugha yao no moja inayoitwa kichagga.katika isimu au linguistic,kitu kinachoinisha kwamba lugha no moja ni mizizi ya maneno yanayotumika katika lugha yenyewe,inafanama hata kama kusemwa kwake kisauti kunatofautina.Angalia waswahili wanazungumza viswahili tofauti kuna kimtangata,kipate,kiunguja,nk.hivi vyote ni viswahili kwa sabanu chimbuko lake ni moja.Na hii haivifanyi viwe lugha mbalimbali ila zinaitwa lahaja za kiswahili.
Delete😌😌
DeleteMichuzi aka mithupu aka mishusi aka mkuu wa 'ulaya' ya tegeta,
ReplyDeleteAsante kwa nafasi hii.
Binafsi mimi naona kama huwajali wadau wa blog hii, kuna vitu ambavyo watu wamekuwa wakikuomba uwatafutie au uvitundike ili waweze kuvifanyia kazi lakini unaonekana kupuuzia. Mfano ulipotundika ile picha ya mfano wa jengo la chuo kipya cha utalii watu walikuomba uwatafutie namna ya kuwasiliana na wahusika lakini hukuonekana kujali, je ni kuwa unaona mchango wetu hauna maana au na wewe ni mmojawapo wa hao jamaa wa mipango mijiunaogopa kulipuliwa?
Naomba kutoa hoja
Ndugu mwana blog, swali zuri. Jibu kwa swali lako ni ndiyo na hapana, kutegemea utachukua msimammo upi.
ReplyDelete1) Kwa wataalamu wa lugha, hasa wana lugha na jamii (social linguists) wanasema kuwa kuna vigezo kadhaa vya kuelezea kuwa kundi fulani ni kabila moja au linazungumza lugha moja, Njia mojawapo ni 'GEOGRAPHICAL CRITERIA' kuwa watu wanaoishi sehemu fulani moja saa zingine hujiita kabila moja. Mfano, wahehe-Iringa, Wachagga -Kilimnajaro, wahaya-Kagera, wakikuyu-kenya highlands, nk.
2) Pili, watu kuzungumza lugha moja. Lugha moja kwa kipimo chao ni kuweza kuelewana kwa kiwango cha asilimia angalau 60%. Hii kwa kimombo huitwa INTELLIGIBILITY. Kama Mchgga wa marangu na wa Machame wataongea na kuelewana kwa angalau kiwango hicho, basi unawaita kabila moja.
3) Kitu cha tatu wengine wanaongelea utamaduni, ukiachilia mbali kipengele cha lugha. Watu huongelea kuwa hilo kabila watakula chakula kinachofanana, uvaaji nguo, desturi katika kuoa na kuolewa, nk.
Lakini mwisho tukumbuke kuwa, kabila moja si lazima waongee lugha moja. Kuna vitu vinavyowaunganisha watu kuwa kabila. Kwa fano historia yao. Kama wamasai wa Kenya na wale wa Kilosa, si lazima waongee lugha ya kufanana, lakini cha muhimu ni historia yao. Utakuta wote wametoka sehemu moja. Nadhani kabila ni swala la kihistoria kuliko lugha wanayozungumza.
Asante,
Mark,
USA.
Mkuu upo sahihi
Deletewhat are you up to? where are you up to? hata kama halipo hilo kabila still linaleta unifications of people,and obviously with some common things, so you research will end up kuwatenganisha watu badala ya kuwaunganisha! which is of no one interest
ReplyDeletemangi
UK
i don't see what you try to say but find samething else to do. maana uwezi kubadili kwani imeshakuwa ni wachagga ni wachagga tuu end for story.
ReplyDeleteWEWE DEO MUSHI, UNAJUA YALIYOTOKEA KENYA JUZI, RWANDA NA BURUNDI,ETHIOPIA NA ERITREA, SUDAN NA KWINGINEKO DUNIANI NI SHAURI YA UKABILA?IDEA ZA KIPUUZI NA POOR KAMA HIZI NDIO ZINASABABISHA VITA!!!!!!NIMESIKITISHWA NA MWANDISHI MZIMA KAMA WEWE KUANDIKA MAMBO YA KIPUUZI KAMA HAYO.WATU TUNAPAMBANA NA UFISADI, WEWE UNAANZISHA MAMBO YA UKABILA NA KUTENGANISHA WATU.WACHAGA, WAPARE, WAMASAI, WAMATUMBI,WAMAKONDE, LET THEM BE!SIO MUDA WA KUJADILI UKABILA NA KUTENGANISHA WATU HAPA.KUPANDIKIZA IDEA KAMA HIZI AKILINI MWA WATU NDIO KUANZISHA UKABILA NA UTENGANO.WAKIANZA KUCHINJANA UTACHEKELEA USHINDI KUWA WEWE NDIO ULIANZISHA HIYO DISCUSSION KWENYE BLOG NA KUANDIKA KITABU?WATANZANIA SASA HIVI TUNATAKIWA KUUNGANA, KAMA MWALIMU ALIVYOTUUNGANISHA.DISCUSSION KAMA HIZI ZA UKABILA HATUZITAKI, SASA NA SIKU ZOTE.TAFADHALI!
ReplyDeleteivi wewe DEO kunawapemba pia ila nao wanamakabila vile vile
ReplyDeletekama wakojani....mtumbatu kwa hiyo neno wachaaga inamaanisha kwamba ni
watu wanaotoka moshi jamani.... mimi ni MCHAGA ila natokea ROMBO kuna ubaya gani kujiita MROMBO
Huna points kabisa unatafuta umaarufu na kitabu chako hatutanua ngoja sasa upate majibu ynayoyataka nina hisi wewe ni MPARE
Mushi hujatulia.Ebu tupe reference of where did you get that definition of Tribe?
ReplyDeleteanyway...kwa ujumla wanaitwa chaggas..ila tofauti lafidhi na maneno ya kichagaa kama ulivyosema kulinga na maeneo yao....hao ni wakulima na wafugaji wadogo wadogo.inawezekana kuna mchanganyiko wa wataita.wapare.wameru.wamasai...katika desturi na mila zilizoingiliana.
ReplyDeletemtoa maoni
Mtoa mada nakusalimu.
ReplyDeleteMi naona "wachagga" ni makabila madogomadogo yote yaliyopo mkoani Kilimanjaro kwa ujumla wao ndo unapata "wachagga" Hiyo si kwamba ni issue ya Kilimanjaro pekee kwani hata mikoa mingine ipo mathalani ukisema wagogo, wapo wa aina nyingi, kuna wa mpwapwa wanaongea tofauti na wale wa bahi wanaongea tofauti na wa mvumi nao tofauti ila kwa ujumla wao tunasema wagogo. Hali kdhalika kwa wanyakyusa wapo wasafwa na wengine lakini kwa ujumla wao tunasema wasafwa. Wasukuma nao kuna wanyantuzu na wengine pia kwa ujumla wao tunaita wasukuma. Hivi ndivyo ninavyoelewa mimi.
NAWASILISHA
nadhani hao uliowataja hapo wanaitwa WACHAGGA sababu wako tofauti tofauti mfano wa chagga za kitanda.Chunguza Chagga za kitanda chako(kama unalalia kitanda cha mbao,sio teremka tukaze) utaelewa nasema nini.
ReplyDeleteMAELEZO YAKO UMEYABANIA KWA KUWA UMEANGALIA KADIKSHENARI KAMOJA TU , SASA SOMA HAPA TUJIFUNZE
ReplyDeleteMoja Kibiblia
--Tofautisha rangi na kabila....Tribe: family divisions, usually within Israel, but also of other ethnic peoples.
Mbili Kisomi zaidi
jisomee hapo
Tatu Ikusaidie zaidi
....Tribe - A group of people who live in one part of a country and are ruled by a chief.
Nne, Unachanganya Lugha na Dialect, Kabila hushea Dialect...??
In common modern understanding the word tribe means a social division within a traditional society consisting of a group of interlinked families or communities sharing a common culture and dialect.
...sasa angalia neno DIALECT ni :The usage or vocabulary that is characteristic of a specific group of people kwa taarifa yako wachaga wanashea Dialect (MMARANGU ANAONGEA NA MROMBO na WANAELEWANA,
Sita
A tribe, viewed historically or developmentally, consists of a social group existing before the development of, or outside of, states, though some modern theorists hold that contemporary tribes can only be understood in terms of their relationship to states.
Saba, Mkishibana sana eneo lenu hahahah..
...A group of people able to support a level of subsistence in a permanent settlement.
Nane..unajua machifu MANGI?
...A group of people who live in one part of a country and are ruled by a chief.
Tisa, hata mkitambuana kiusiriazi tu
Kumi..mwisho na wengine wachangie... angalia neno COMMON LANGUAGE na SIO SAME LANGUAGE
Mwisho kabisa...kwa walio na muda...au basi tosha
Ila Nimeipenda sana hii topic, tano nimeruka!
Hii mada baab kubwa Michuzi. Hebu angalia mchanganuo ufuatao.
ReplyDeleteWAROMBO -- They really help each other socially and in business, but both men and women from there are sexually inactive.
WAVUNJO --(Wamarangu, Kirua etc) Wasafi na wapenda majumba mazuri though very proud people, waongo, and jeolous.
WA-URU -- Wasomi wazuri sana and their women are sexually very OK (watamu sana), lakini wanaume wao pamoja na elimu yao ni matondo (wajinga). They love keeping their diplomas and degrees in their kabatis.
WAKIBOSHO: Wanapenda sana wake zao, hasa wanapojifungua.
Very aggressive people in business but wachoyo na individualistic. Hawataki wengine wapate. Pia ni waizi pia.
WAMACHAME: The most religious and developed people in chagga land, though their women love men, not because of what they are, but what they have.
WA OLD MOSHI-- Wasomi wazuri and their women morally OK but men finish their vihambas (mashamba) erecting big houses inhabited only during christmas time.
Wa SANYA JUU -- Agressive people in everything, though they don't value education very much. Mashamba na ng'ombe ni mali sana kwao.
NAWASILISHA, MDAU WA HIMO AMBAYE SIO MCHAGGA LAKINI KAISHI SANA UCHAGANI
ww ni vuvuzelaa
DeleteMtori, Mbege, Migomba, kahawa Biashara, shule, Kanisa/msikiti, Nyumba ya mtaofali na ya nyasi. Biashara, kufuga mbuzi ngo'mbe na kondoo.Kuweka mbolea kwenye migomba. Kulima zao la ulezi kunde mahindi na maharagwe. Vyakula vinafanana na tabia na values zinafanana sana. Kabila la Wachagga lipo. It is has so much diverse and uniqueness. So don't try to eliminate its uniqueness and call it it differences. Unaweza ukaliita kabila teule kama lilivyoitwa taifa teule la Waisrael. Kwani neno Wachagga lina maana gani. Kuna kabila lolote lilikuwa na watawala waitwao mangi? Wachaga ni Wachaga na ndio hao kina Mangi Horombo mangi Sina,n.k.
ReplyDeleteWewe unatumia methodology potofu kuharibu historia. Kama kungekuwa na Wachagga wa Songea na Wa Iringa ungesemaje? Unataka kulisambaratisha kabila. Da! Unahitaji phDs 1500!!
Nani alikwambia wachaga ni kabila, au unajichanganya??
ReplyDeleteWewe kweli umekosa kazi.... unahitahi JEMBE ukalime!!
ReplyDeleteSwali la kwanza "wewe ni kabila gani"..??
ReplyDeleteUnajua wachaga ni watu wa mkoa wa Moshi, na wote (isipokuwa wamachame na wakibosho), huwa wanasikilizana. Yaani, mmarangu hamsemi hatofautiani na mchaga wa mwika, wala mamba, wala old moshi, na kidogo sana na mrombo. So, ukienda Rombo, mchaga wa huko anaweza ongea na anasikika na wa mwika. Mmarangu anasikika perfectly na mtu wa mwika. Hali mtu wa Mamba naye anasikiwa vizuri kabisa na Mmarangu.
Fanya research zaidi. Nitashukuru pia feedback yako kwani inaweza nipa mwangaza tofauti na ule ninavyofikiria.
kAMA UNAADNIKA KITABU fuatilia historia ya hao watu na hilo eneo kisha ndio u-conclude hao watu kabila lao linaitwaje. tafadhali kama unaandika kitabu cha kiswahili usianze kujichanganya kwa tafsiri za maneno ya kizungu. Usidhani neno kabila na tribe yote yana maana moja. maana zinafanana lakini sio kopy right. kwenye utafiti wako pia chunguza matumizi ya lugha utagundua zipo tofauti.
ReplyDeleteTafuta misingi ya kabila si kwenye mila na lugha tu chimba zaidi. Usianze ku-conclude kwa kusema HAKUNA KABILA LA WACHAGGA NA HATA KAMA HIYO NI HYPOTHESIS YAKO haijakaa sawa kwani utauwa biased.
Kila la kheri. Usishangae ukijagundua kuwa hata waafrika wote wanaweza kuwa kabila moja let alone warombo, wamarangu, wamachame etc. Usisahau kuchunguza hayo maeneo nani aliyagawa na sabb ni zipi. Hivi hao ni watu wameunganika kufanya kabila moja la 'wachagga' au ni watu wamegawanyika. au pengine ni kabila moja kubw la 'wachagga' limegawanyika likazaa hao warombo, wamarangu etc?
Nadani pia utagundua utaweza kujua wenyeji halisi wa eneo hilo kwani hao hao wachagga wanaasili y awakikuyu, wamasai, wahabeshi etc
kazi kwako ni ngoma nzito kama unatoka kutoka na kitu kilichokwenda shule. Labda kama unaadnika hadithi. KILA LAKHERI.
Haaya kazi kwako kama unaandika intellectually kazi unayo lakini kama unaandika hadithi basi hata kwenye blog watakusaidia.
Pole mdau maana utakuja sema hakuna mtu ni mtanzania! Rejea watu waliotokea Mkoa wa Mara....koo hata kaya zimejifanya kabila. Wamefaidika na nini? Au kuwa mchaga na kuwa moldimoshi mtu atafaidika na nini?
ReplyDeleteNashindwa kuelewa unataka nini hasa kwenye mada hii. samahani.
Habari pevu hii,sina comment kwani habari tayari ina hitimisho. Hakuna kabila la wachaga
ReplyDeleteauwiiiiiiiiiii !!! aiseee mangi sina leoooo naona umeamkia huko kibosho sasa hii imekaaje ??? kaka Mithupu wewe sasa unataka kuleta ishu na hizi posti za kutuambia eti mimi sina kabila jamani itakuwaje nii mu-old-moshi ?? wakati najulikana mcha- mchagga kweli . Sisi kabila letu kam hujafahamu ni one thing in common tena ile kitu ina maana kuliko ingione ni woooote tunajali pesa na tunapenda pesa kuliko maisha yetu sasa wewe utasemaje hatuna kitu "in common "? hebu sogea uchaggani tukujaze mbege na mtori ..... !!!!!
ReplyDeleteDuuh!! Hiyo inaukweli kabisa I never thought of it...JOOMEK
ReplyDeletehuyu mtu anasema kuwa yuko daily news arusha nahisi bosi wake huwa atembeleagi hii blog kwani huyu jamaa inatakiwa kibarua chake kiote majani.kwani inaonyesha hafanyagi kazi huyu.kwani kuwa na kabila au kuwa na mila na desturi zimekunufaisha nini wewe, wenzetu huku USA hawana cha makabila wala lugha zenu mbali mbali za kienyeji sasa sijui nyie na wao ni akina nani wanachechemea kinyumenyume? kwani naona kinachofanyika bongo kila leo ni kutaka kuwa kama wamarekani(namaanisha kuwaiga kwa kila kitu)sasa nashangaa kama unapenda kuwa kama watu ambao hawana kabila(wamarekani)sioni ni kwanini usiwaige wachaga kwani kwa madai yako wewe hawana kabila.na halafu waambie wabongo wenzio wapunguze usumbufu ubalozi wa marekani bongo na wahamie ubungo kwenye mabasi yaendayo kilimanjaro
ReplyDeleteMbega hapa
in other way round unataka kusema hakuna ukristoila kuna usabato,catholics,protestants,lutheran, etc. it doesnt make any meaning for me.
ReplyDeleteNa huko Tanga utasemaje? hakuna wasambaa ila kuna wazigua,na wabondei.
Mzee deo angalia hicho kitabu chako usije ukakinunua mwenyewe
Kwa kweli nimefurahishwa sana na topiki hii - na ninasema haya kwa nia nzuri tu. Ni hivi - ukiendelea kuchambua sana basi utakuta mengine zaidi.
ReplyDeleteMfano - tofauti nyingine ni ndogo. Mfano Wachagga wakutoka Kilema, Marangu na Mwika wanafana mno. Halfau utaona kuwa mchagga wa Rombo na wa Kibosho na Machame wanatofautiana sana.
Then kuna kitu mimi nikiita mchanganyiko - hapa utakuta kundi la wakibosho, wamachame, wa uru - ukienda kwenye mashina yao - utaelewa zaidi.
Halafu ukizingatia utaona Wachagga wana mchanganyo wa kimaasai - siyo wote lakini kuna makundi fulani fulani. Mfano wa Machame wengine wanaomchanganyo na Wamaasai na kabila la Wameru - Warombo wana mchanganyo na waMaasai na wataita.
Sasa tuchukue mfano - katika kuoana mkilema na Marangu Uchagga unarudi tena (things come to full circle). Mchanganyo unakuja kutokana na jinsi tunavyochukua mila za upande wa akina Baba. Kwa maana kwamba mfano Kama Mrombo siyo mchagga halisi na ni mwanamke - akiowana na mfano mtu wa Kilema ambae anaonekana kuwa mchagga halisi - basi mtoto ataitwa mchagga.
Ninachotaka kusema ni makubaliano fulani ya desturi zetu zaki Tanzania ndiyo zimechangia katika hilo kundi zima kuitwa wachagga. Na Uchagga kwa sehemu kubwa umetokana na makundi fulani fulani kati ya wa chagga kuona.
Sasa changa moto ni - kwako wewe mwandishi - tofauti kweli zipo, ila ni jinsi ile mila na desturi zilivyokubalika wakati ule ndio imefanya ikabakia vilivyo leo hii.
Wachagga wengi ukipenda kujua zaidi fuatilia mashina yao (roots) utakuta wana mchanganyiko mwingi - wengi siyo "wachagga pure." Angalia mashina (roots) yao kuelewa zaidi.
Mfano mimi ni moja wa mchanganyiko kama huo nilioeleza. Na katika wajomba na mashangazi wa akina wazazi wangu - kwenye mashina kuna wataita, kuna wa Maasai, kuna warombo, kuna wakilema, kuna wamachame, na kuna Marangu. Shangaa wewe hapo. Halafu kila baada ya kizazi ama kitu kama hicho, mchagga anaenda kuoa Maasai, ama Mu Uru (hawa ni mchanganyo wa Maasai pia), ama Mrombo.... so ndio Uchagga unabakia kukubali yote hayo.
Haya ni maoni yangu mimi - siyo ya kila mchagga.
Make some Noise for Deo Mushi of Daily Noise Arusha Bureau!Nafikiri Bro baada ya kuku wa Sullivan sasa kama Bored ile mbaya!Not Bad!Sometimes inabidi utoke offpoint Meku!Mchagga ni Registered Mzee!Nothing you can do about it!Kama umechoka Uchagga unawesa kujiita Maasaai tu naruhusiwa haiko mbaya!Hapa Deo Mushi anatafuta Umaarufu kwa kutumia Turufu ya Kichagga!Aikaambe Meku!
ReplyDeleteHapa kuna jambo moja linalo changanya watu wengi kuna majina ya makabila yanayo meza makabila mengine katika mikoa yetu kwamfano watu wengi wanajuwa wakazi wa kilimanjario ni WACHAGA lakini yapo makabila mengine ndani yake au ukija IRINGA kabila linalofahamika ni WAHEHE lakini kuna makabila mengine kama WAZUNGWA wanaopatikana maeneo ya MWAGIDAVA NA IKOVERO na koo zao za KINA SANINGO NA MCHAVALIKUNGU,pia wapo WABENA,WAKINGA,WAPANGWA NK.Sasa hili jambo lipo ktk mikoa mimgi kwa hapa nyumbani kwetu TANZANIA.
ReplyDeletewatu wote mnakwepa ukweli wachaga ni wale wanaokaa mlimani mapolini ni wamasai na mjini ni wenyewe wapale
ReplyDeleteau kunaatakaebisha????
Deo Mushi you are a great thinker.!Lakini kumbuka kwamba Nabii hawezi kupendwa nyumbani!. Utapingwa na Wachagga wenzio wote, na usitegemee wao kukuunga mkono sababu tu wanahisi kama "amewavua nguo". Kuna mnajimu wa kale alikatwa shingo kwa kusema kuwa Dunia inalizunguka Jua!. Waheshimiwa walitaka abaki na msimamo kuwa ni Jua ndio linazunguka Dunia.!Hao wanaosema kuwa wachagga wanasikilizana kwa asilimia fulani ndio maana wote ni kabila moja, wanasahau kuwa suala la kusikilizana liko kwa makabila yote yanayopakana.Wakwere wanasikilizana na Wazigua. Wazigua wa Segera wanasikilizana na Wabondei wa Mombo na Korogwe. Wabondei wanasikilizana na Wasambaa, Wasambaa wanasikilizana na Wapare. Ukienda kusini nako ni hivyo hivyo, Wayao wanasikilizana na Wamwera. Nao wanasikilizana na Wangindo na Wamakonde.n.k.Hii hali inaendelea nchi nzima. Je hamjui kuwa tofauti ya makabila ya Musoma ni ndogo sana kuliko nyie wa K'njaro?. Lakini wao hawatumii jina moja. Huyo huyo Baba wa Taifa aliyekataza ukabila, hakuwahi kujiita Mkurya hata siku moja. Alijulikana ni Mzanaki kamili!.Sababu alijua kuwa Wakurya na Wazanaki ni makabila tofauti.!!. Kusikilizana kwa asilimia fulani, hakuna maana kuwa ni kabila moja. Kwa hiyo ndugu zangu mnaojiita "Wachagga", hata kama hampendi, nyie sio kabila moja. Huo ndio ukweli, japo hamtaki ujadiliwe. Mushi tunakikaribisha sana kitabu chako na kitakupa umaarufu sababu ume-"thubutu" kuwa muwazi.
ReplyDeleteMdau,
Dar
mila za wachaga ni sawa na za wakulwa na wagogo sema kihistoria walisambaana hasa ktk upande wawanawake kwaanayejuwa makabila haya mila zao hatabisha sema wachaga wanafanya siri na wakulwa wanafanya sifa na wagogo wamebaki katikati.
ReplyDeleteIt's united Chagga kama hautaki kajinyonge seems kama ujiita Mushi utape kazi kwa mengi na huko uliko Wales Sctoland na hapa Engand tamaduni tofauti ila wote nii..?? nakuuliza nii USA kila state ina sheria zake ila wote niii...??? siku nyingine usilete mawazo ya vikao vya pomve huku tunaitaji muunganiko na developments sio kinda bulshit ya researching IoI
ReplyDeleteNi kama vile unasema hakuna dini ya UKRISTO, kwa maana kwamba kuna walokole, walutheri, wasabato, anglican, catholics etc. Ni kwamba wanaunganishwa na common denominator being Yesuuuu. Sio tu wachaga wako around mt Kil. lakini life style, lugha za watu around this area zinaingiliana kwa kiasi kikubwa. Wote wanaamini katika mbege, mtori, kisusio na kutafuta hela na kujenga mabungaloo kwao. Nimeishi na hili kabila na kwa kweli is among the best people in the world.
ReplyDeleteNatoa definition ya wachaga kama ilivyoandikwa kwenye ecyclopaedia britannica (UK)
ReplyDelete'Bantu-speaking people living on the fertile southern slopes of Mount Kilimanjaro in northern Tanzania. They are one of the wealthiest and most highly organized of Tanzanian peoples'
Link ya enclopaedia britannica online http://www.britannica.com/EBchecked/topic/104317/Chaga#tab=active~checked%2Citems~checked&title=Chaga%20--%20Britannica%20Online%20Encyclopedia
.
Bwana Michuzi naomba kuwasilisha
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.
ReplyDeleteWachagga ni kabila tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.
Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine na ndiyo sababu lugha yao, Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea, Rombo magharibi ya Kilimanjaro mpaka unapofika Siha, Machame magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika makundi ya Kichagga cha Rombo, Marangu, Old Moshi,Kibosho, na Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vonjo, Wa-Uru, na Wa-siha. Baadhi ya wachagga walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wachagga wa Machame ingawa lafudhi zao zinatofautiana desturi na mila zao ziko karibu sana.
Historia ya elimu kati ya Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Kikristo walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kati ya kabila lenye watu wengi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro kuwa unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania.
Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamishinari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi. Wakati wakazi wa mikoa mingine walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1,2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro vimezidi sana idadi ya shule katika miko mingine yote.
Ni vema pia kusema kwamba shule hizi kuvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi wachagga tu.
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.
ReplyDeleteWachagga ni kabila tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.
Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine na ndiyo sababu lugha yao, Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea, Rombo magharibi ya Kilimanjaro mpaka unapofika Siha, Machame magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika makundi ya Kichagga cha Rombo, Marangu, Old Moshi,Kibosho, na Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vonjo, Wa-Uru, na Wa-siha. Baadhi ya wachagga walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wachagga wa Machame ingawa lafudhi zao zinatofautiana desturi na mila zao ziko karibu sana.
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.
ReplyDeleteWachagga ni kabila tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine na ndiyo sababu lugha yao, Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea, Rombo magharibi ya Kilimanjaro mpaka unapofika Siha, Machame magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika makundi ya Kichagga cha Rombo, Marangu, Old Moshi,Kibosho, na Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vonjo, Wa-Uru, na Wa-siha. Baadhi ya wachagga walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wachagga wa Machame ingawa lafudhi zao zinatofautiana desturi na mila zao ziko karibu sana.
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.
ReplyDeleteWachagga ni kabila tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine na ndiyo sababu lugha yao, Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea, Rombo magharibi ya Kilimanjaro mpaka unapofika Siha, Machame magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika makundi ya Kichagga cha Rombo, Marangu, Old Moshi,Kibosho, na Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vonjo, Wa-Uru, na Wa-siha. Baadhi ya wachagga walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wachagga wa Machame ingawa lafudhi zao zinatofautiana desturi na mila zao ziko karibu sana.
thanks
Fanya research yako vizuri kabla hujaanza kukurupuka na kudanganya wadanganyika. Ati hakuna kabila la wachagga na kigezo ni lugha ...utamaduni wetu ni mmoja....Na hao wapare nao hakuna kabila lao...???? Kama lugha tofauti ndio inakufanya useme hakuna kabila la wachagga ..kwa taarifa yako Wapare wa usangi hawaongei kama wapare wa Gonja au visiwani...Je ulijua hayo...Kipare ni kimoja lakini kuna maneno mengi sana tofauti the same applies to wachagga kichagga kipo tofauti lakini kama unasikia cha mmarangu hata mrombo utamsikia na tamaduni zeti ni sawa....inabidi utembee tembee kidogo huko uchaggani ujifunze yote....
ReplyDeleteWachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.
ReplyDeleteWachagga ni kabila tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.
Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine na ndiyo sababu lugha yao, Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea, Rombo magharibi ya Kilimanjaro mpaka unapofika Siha, Machame magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika makundi ya Kichagga cha Rombo, Marangu, Old Moshi,Kibosho, na Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vonjo, Wa-Uru, na Wa-siha. Baadhi ya wachagga walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wachagga wa Machame ingawa lafudhi zao zinatofautiana desturi na mila zao ziko karibu sana.
thanks
Wajameni
ReplyDeleteIsiwe mada hii ni sababu ya kumrushia makombora mwenzetu huyu, kwani alichosema, kwa mujibu wa marejeo yake, yana ukweli mtupu.
Lakini labda hii kwake ingekuwa nafasi ya kujiuliza kama kila tunachosoma kina ukweli, au kama labda kinahitaji marekebisho. Na hiyo ndiyo maana ya maendeleo. Sio tu kuamini kila kilichoandikwa. Jamii zilizoendelea hapo ndipo zilipotupiku, watu hawadumai wakaamini kila andiko. Nawe bwana Deo, kabla ya kuamua kuwasilisha kadamnasi mada yako ungejiuliza, je, definition uliyonayo haikupitwa na wakati?
Jawabu ni kwamba imeachwa nyuma sana na zama. Ni maelezo ya kizamani, na kwa sasa, kwa mujibu wa dhahiri ya mambo, hayafunction.
Kumbuka kuwa kwa mfano katika jamii za kimagharibi ukabila si kitu maarufu sana kwani kwao hakuna makabila, watatwambia nini sisi. Na hata kama hiyo definition yako hukuipata huko, wewe umeona mtaalamu au mtafiti gani akaegemea kwa definition moja tu?
Huo ni usomi wa kitoto, haukidhi ukweli uliopo duniani sasa.
Tatizo uliloliona kuhusu uchaga kama ni kabila au la, ukianza utafiti utagundua kuwa makabila mengi ya Tanzania yana kasoro kama hizo. Sasa tusemeje? Hayo mengine pia si makabila?
Ila namalizia kwa kusema hongera bwana Deo kwa mada yako chokozi, na naamini itaibua mijadala ya KIELIMU zaidi (kuliko ya jazba) kuhusu maana hasa ya neno KABILA, na si kuishia hapo tu, bali kupembua kama hii elimu kwa kutegemea definition za kale inafaa kuendelea kutumika. Nadhani utafiti na tathmini za mara kwa mara ndio chachu ya maendeleo na weledi.
Afrika/Tanzania hakuna makabila. Kuna mataifa tu. Wachagga ni taifa. Hii dhana ya ukabila ni matokeo ya ukoloni. Ndio maana mzungu mmoja anakiita kitendo hiki cha kikoloni 'invention of tribes', yaani, 'kubuni makabila.'
ReplyDeleteKwa mujibu wa kamusi yangu, taifa ni "mkusanyiko wa watu ambao wana asili, historia, lugha au utamaduni mmoja n.k." Kwa mantiki hii hizi nchi zetu nazo ni mkusanyiko wa mataifa mbalimbali.
Hivi hatujiulizi kwa nini kitu kilekile ambacho wamagharibi wanakiita 'tribe/kabila' hapa Afrika huko Ulaya wanakiita 'nation/taifa'; kitu wanachokiita 'dialect/kilugha' huku Afrika kule Ulaya wanakiita 'language/lugha'; na wanachokiita 'customs/mila' na 'traditions/desturi' za Waafrika kwa Wazungu wanakiita 'culture/utamaduni'?
Aisee Deo babangu, kama wote huchinja mburu(mbuzi) au umbe(ng'ombe) chrismass au kama wachaka wose hunywa kisusio na kama wote wafanyapo sherehe kule mgombani na kunywa mbeke(mbege)na kama wote wamepanda masale na kukuelezea maana moja wanayoibelieve na kama wote wanamuita mungu (Rua oko mndumi)na mengineyo meengi iweje ushindwe ku conclude kwamba wachaga r there na ni tribe ambalo halitakaa litokomee kutokana na jinsi wanavyo sheherekea chrissmass na easter miaka nenda rudi hata sie tulio huku ughaibuni tunarudi uchagani kwa ajili ya hayo. hivyo basi naomba urecognize wachaga and i hope Mr. Mushi doesn't see your comments or thought.
ReplyDeleteAika sana na rua oko mndumi naku bariki kofia le oiyo ni mana mtuntu na nuichi kindo pfo.
LAKUCHA.
Moja katika maafa ukoloni uliotuletea ni kasumba ya kudhani kuwa ulimwengu umeanza wakati wa ujio wao. Hili ni upotofu. Kwa bahati mbaya hata wana historia huanzia hapo, na labda ndio sababu wengine wanaamini maneno kuwa dhana ya ukabila imeletwa na ukoloni.
ReplyDeleteMiongoni mwa vitabu nilivyovisoma kinathibitisha kuwa, si tu kwamba neno makabila limetoholewa kutoka katika lugha ya kiarabu, bali pia kwamba makabila na mataifa ni vitu viwili tofauti. Kwamba binadamu wameumbwa na Muumba wao na kufanyiwa mataifa na makabila tofauti ili wapate hutambuana. Na hiki kitabu kitukufu nilichokisoma kimelitumia neno makabila wazi wazi, na neno mataifa wazi wazi.
Ni dhahiri vitu hivi vipo leo na vilikuwepo hata kabla ya mkoloni wa kwnza kuja Tanganyika hajazaliwa.
Tusidhani hawa ndio mwanzo wa dunia, wao walitueleza tu walivovijua, vingine tutafiti wenyewe.
Na tukirudi kwenye mada, naona hii ni hoja nzuri inayohitaji kuibua maoni ya kisomi yatayoleta faida si katika dhana ya ukabila tu, bali katika dhana nyingine pia, mfano ile maarfu ya kudai kuwa watu wa mwanzo walikuwa masokwe!
hawa wazungu, labda si kwa nia ya kutupotosha, huko njyuma walikuja na dhana za ajabu ajabu, mauzauza matupu. ufike wakati tukusanye fikra na kujenga taswira mpya.
UKABILA SI DHANA YA MKOLONI, NI MAUMBILE ASILI YA BINADAMU.
Ahsante, nawasilisha.
Tribe- any aggregate of people united by ties of descent from a common ancestor, community of customs and traditions, adherence to the same leaders, etc.
ReplyDelete2) a local division of an aboriginal people.
3) a division of some other people.
4) a class or type of animals, plants, articles, or the like.
tuambie kingine sio kutuelezea ukabila unaoujua wewe.
Mushi Mushi Nuamba kura mleu?
Donald Mmbando
Mushi kapfo mleu, nkiki ukundi bana? Poo mbaka, ruwa oko mndumi, ruwa oko mangi. Nonyo wari mleu? Warumu wakumbore, ambia mrocho. Enda upfule isale uwatake wachaga wote radhi aisee, unataka kuleta mgawanyiko bwana mdogo? Kuore mdau naamba iwe mana mtuntu, iwe mana mtuntu chaloi. Ruwa nakutarame akuenenge meso uone mambo mengine ili uachane na hili, ulae necha bana
ReplyDeleteMushi,
ReplyDeleteKama huu ni utafiti, basi wadau wenye majibu ya ndiyo, hapana na ndiyo/hapana wanaweza wakawa wameelewa topic. Wengine wanajaza kurasa tuu.
Pia majibu ya utafiti wako siyo lazima yakubalike kwa wachangiaji ili yawe valid bali yakipitishwa na wasomi madktari itatosha.
Cha muhimu ni analysis nzuri ya hoja na critique.
Unless if you are simply trying to count how many comments you will get dear friend....I think your thinking is clouded in "lanmguage". Otherwise,where that is, that you were "educated" a "Tribe" has anything to do with "the same language"?. When you dip a little deeper, you will see that Tribe is "a race of people, or a family, who are all descended from the same ancestor or ruled by a chief" example, if you please, will be the tribes of Chagga. I will let those from the "Royal Mangi" blood take it from here. I should also, echo the following contributors (all for June 27th): June 27, 2008 1:57 PM, 2:24 PM, 2:26 PM nothing but love for June 27, 2008 2:50 PM comments,
ReplyDeleteand of course Mmbando at
June 28, 2008 12:18 AM. Bin Michu, see to it that you post my comments as well. Kaka Yenu
Michuzi,
ReplyDeleteTatizo la kwanza ninaloliona hapa ni kwamba tumeshakubali kwamba maana ya kabila kwa mujibu wa kiingereza au wazungu ndio sahihi.Hata bwana Deo Mushi mwenyewe ametohoa maana kutoka kwenye lugha ya kiingereza na sio kiswahili au kichaga ambazo ndizo lugha husika hapa na kwa msingi huo mada nzima ilitakiwa iambae hivyo hivyo.
Hayo ndio yamekuwa makosa yetu mara kwa mara.Maana zetu,kutokana na sisi wenyewe tunavyozielewa au kwa mujibu wa simulizi za mababu zetu,kila mara tunaziona hazifai.Badala yake tunaona wanazotuletea wenzetu(ambao hata hawajui makabila wala asili zao) ndio tunaziona sahihi.
Ukichunguza sana utaona hata watoa hoja au wachangia maoni wengi,nukuu wanazoziweka ni kutoka kwenye kamusi za kizungu au taarifa zilizopo mtandaoni ambazo nyingi zao zimeandikwa na wazungu hao hao wasiotujua tunakotoka haswa badala yake wamekuwa wakiokotezakoteza barabarani.
Kabila ni kundi la watu wenye asili inayofanana au moja.Lugha na taratibu fulani fulani tu haziwezi kutosheleza kusema kwamba wachaga sio kabila.Kumbuka makundi haya yote huanzia kwenye familia kwanza na ndipo kukua na kuwa koo au kabila.Kwa maana hiyo,kutokana pia na mazingira(muhimu sana hii) ni lazima kuwepo na vitu fulani fulani(kwenye lugha au mila na desturi) ambavyo vitatofautiana.Lakini kutokana na asili yao,wanabakia kuwa wachaga.
Mwisho,ni lazima tujifunze historia zetu kupitia simulizi za mababu zetu kwanza kabla hatujakimbilia maktaba kuona anachokisema bwana Smith.Huyu aliandika historia kwa jinsi ambavyo itamnufaisha yeye na vizazi vyake.Tunahitaji kuandika historia yetu/zetu sisi wenyewe.Hii haimanishi kwamba tusiangalie chochote walichoandika wenzetu,hapana,tuchungulie kisha tupime.
Leo hii nchi zetu zina matatizo mengi kutokana na masuala ya kutojitambua kwetu.Viongozi wetu ndio kabisa.Hata habari hawana.Wamekuwa vibaraka wa wazungu nambari moja.Ah..ngoja niishie hapa ili nisije zua zogo lingine.Tuonane Columbus,Ohio mwezi ujao.
LoL! halafu eti unaitwa Mushi:-( au hiyo Mushi ni nickname yako? And to add insult to an injury, unaishi Arusha, technically 1 hour away from K'njaro...
ReplyDeleteFanya research... tena nakushauri anzia kwa wazee wa familia yako (kama kweli wewe Mushi) kisha tembelea sehemu zote za hao wachagga in question... Actually kun mtu hapo juu anaejiita mchagga halisi at least amekupa constructive critisism, read his/her points again, of all the responses s/he's the only one making sense... halafu usisahau kupitia Arican languages movements from Nilotics,Bantu, et al...
Mndengereko dondoo kutoka kwa msomi wa Kiafrika hii hapa:
ReplyDelete"Indeed most speakers of African languages would agree that the term "tribe" is not directly translatable into their own indigenous languages. For instance, in English the Zulu are referred to as a "tribe", in the Zulu language, however, the word for the Zulu as a group is "isizwe", which more closely translates to "nation" or "people"; hence, "Umkhonto weSizwe" is "Spear of the Nation" not "Spear of the Tribe." - http://www.zeleza.com/blogging/african-affairs/interrogating-tribe-more-just-semantic-argument
Msomi mwingine wa Kiafrika naye anasema hivi:
"Whereas in other parts of the world issues and conflicts may be named as political, economic, social, environmental, class, gender, religious, or cultural, in Africa they are almost invariably about tribes and tribalism. Nobody of course talks of tribes in Europe, except in reference to the remote past, of contemporary tribal conflicts in the Balkans, in Northern Ireland , in Spain . European groupings are defined as `nations`and their conflicts deemed national or nationalist conflicts and accorded specific characteristics, combatants, causes, closures, and consequences. In Asia people are often divided into ethnic or communal groups and their conflicts termed ethnic or communal. Nations for Europe, ethnicities for Asia, tribes for Africa , a sliding scale of civilizational status and possibilities...
"Tribes may have long been banished from the academic vocabularly in Africanist discourse, but they are alive and well in the mass media. But even in the academy the term sneaks in from time to time as I discovered at a party when I first arrived at Penn State when a head of a certain otherwise progressive department who had done a little comparative research in Africa asked me: What tribe are from? My shocked gasp said it all, but just to make sure that she got the message, I sent her an e-mail explaining the politics of the term `tribe` to which she responded with a groveling apology. But many a western journalist assigned to the hardship African beat defend the use of the term `tribe`on account that Africans themselves use it. One student of mine returned from a four week study abroad in Kenya feeling empowered to use the term and challenged my allegedly western liberal antipathy to it. There was a time when African `groupings`were called `nations` before the rise of colonial racism and academic anthropology, and in my language the term used for African and European groupings is the same, `mtundu`. `Tribe` is an acquired term of colonial self-denigration, not self-definition, let alone self-empowerment." - http://www.zeleza.com/blogging/u-s-affairs/angelina-jolie-discovers-africa
Mada nyingi hapo juu zimejaribu kufafanua na nyingine zimelichukua swala hili kama utani.Kwanza kabisa nawalaumu wadau wote wale wanaopenda kuchanganya lugha yetu na kizungu wanapojieleza-huo ni ufinyu wa lugha na ni aibu.kama wataka kuandika kwa kizungu basi andika hadi mwisho kwa kizungu. Pili wengi wana makosa tele kwenye miandiko yao.Hizo ni tabia za kasuku-wanaandika bila kurudia kusoma waliyoaandika.
ReplyDeleteSwala la wachaga ni la kipekee na wengi wetu hata sisi wenyewe wachaga hatulielewi kwani hatuna manukuu ya historia yetu. Tunategemea kule kusimuliwa tu.Kutokana na masimulio niliyoyanukuu mimi ni kwamba Uchagani (kwa kichaga ORUKA) hapo awali kulikuwa ni sehemu ya fujo sana. Makabila mengi kama wamasai, wasambaa yalikuwa yakivamia sehemu hii kwa nia ya kuitawala sehemu hii yenye rutuba,kutwaa mifugo,watoto hasa wa kike nk. Baadhi ya makabila hayo yaliweza kuteka na kuchukua sehemu mbalimbali na kuanzisha tawala zao wakichanganyika na wenyeji. Hizi tawala nazo zikawa zinazidi kuleta mgogoro kwa kuendelea kuvamia sehemu nyingine. Hivyo vurugu ikazidi.Ikabidi kila sehemu kujaribu kujitenga ili kujilinda. Kujitenga huku na kuingia watu wa kabila nyingine kulileta mabadiliko katika maendeleo ya lugha waliyokuwa wakiitumia sehemu na sehemu.Kulizidisha uhasama kati ya sehemu na sehemu, hata mila zikaanza kubadilika kufuatana na mazingira.Ili kujaribu kukabidhi madhara haya watu wakajaribu kujizatiti kwa kuwa kwenye jamii na kiongozi mmoja-MANGI.Jamii ndogondogo-KOO.Ukoo ulikuwa na nia ya kuhakikisha kuwa ndugu wasipoteane kabisa.Hii ni kiasi tu cha yote yale yanayochangia swala la tofauti za wachaga. Mbali na tofauti zao wachaga ni mfano mzuri sana kwa wote.Wachaga wote pale walipo wanaelewana na kusaidiana. Hizo tofauti mnaziona ninyi tu msio wachaga.Nawashauri muige umoja wa wachaga.KABILA LA WACHAGA LIPO NA LITAENDELEA KUWAPO!
MALISA-KILI wa URU
Deo mushi, swali lako ni relevant. Na michango hadi sasa ni mizuri. Lakini pia inasaidia ukieleza lengo la swali lako. Mie nahisi ni kwaajili ya utafiti wa ki-elimu (research).
ReplyDeleteKama ni hivyo naona michango mingi imekua ina argument za "sitaki jua" (fear-mongers), " biblia inasema" (abstractions) au "wataalam wanasema" (bila kutaja who exactly)...
Mjomba usisahau kumtaja Michuzi kwenye acknowledgements maana noana anamaliza utafiti wako bila kuwa na haja ya reference yeyote zaidi ya blogu hii ;).
Dalili ya mvua ni mawingu. Naungana na watoa maoni wengi waliosema kuchokonoa makabila kunasababisha fujo katika jamii na nchi kwa ujumlam Tangu enzi historia ya mababu zetu Tanzania haijawahi kuwa katika vita vya kikabila ila huyu kaka angu Mushi naona anafatuta mambo.
ReplyDeleteKama walivyosema wengine yawezekana anafanya Research sawa ila yeye siyo mtu wa kwanza kufanya research Tanzania wapo wengi ila unaangalia kitu kinachoitwa Target population, then what is your sample size and sample frame.
Kama kweli anania ya kuwaelemisha Wantanzania na wengineo kwaujumla.
Na Resty Mushi SA.
aisee mangi mithupu huyu bwana mushi sasa naona amesapata kisusio cha kutoshea kitabu chake sasa tupumsishe hii weekend vishwa vyetu vijaze mawazo tena tafasali usije na mada moto ingine mpaka jumatano tarehe mbili mwezi wa saba ili tujase jase mawazo na ukirudi sasa ujadili hawa binamu setu wa kipare tafasali kwa nini wote ni wafupi na vithethe ??.......... !!!
ReplyDeleteDeo Mushi kwanza awali ya yote napenda kukupongeza kwa kuwa mtu wa mawazo mapya. Hili la kufanya utafiti na kuandika kitabu nadhani jukumu la wasomi wote watanzania kwa lika mmoja wao kueleza nini anakiona katika jamii inamzunguka.
ReplyDeleteTukiwa na mwamko wa namna hii ndiyo mwanzo wa chachu ya maendeleo kwani fikra nyingi zitawekwa wazi na watu wengi watajifunza kutoka kwenye mawazo ya watu mbalimbali.
Baadhi yetu tunaona kuwa Bw. Deo ana mawazo yasiyofaa na wengine wakidhani anadharauilisha jamii ya watu waliotajwa, ninawaomba mpatieni Bw. Deo mawazo yenu hata kama ni hasi lakini kwa njia ya kujenga imani yake katika kuwapatia wengine maarifa.
Deo, wewe ni mfano tu, wengine wengi wajitokeze kuandika mambo mbalimbali siyo lazima yanayohusiana na makabila yapo mengi ya kuandikwa.
Kwa mfano:
Kuna watumishi wengi tu wa serikali na mashirika ya umma waliokuwa katika utumishi wa muda mrefu wanaweza kuandika vitabu juu ya yale waliyoyaona au kufanya katika muda wao wa utumishi ili kuelezea hali halisi ya wakati huu katika serikali na mashirika hayo.
Kuna wana michezo wengi walioshiriki michezo mbalimbali na wenyewe wanaweza kuandika pia
Akina Tenga, Bayi, Kocha Mziray, Mh. Bendera nk.
Nakupongeza sana Deo.
d
ReplyDeletemisupu, naona watu wa kilimanjaro hii mada inaonekana kuwa tachi sana?looks like hawana confidence na identity yao.mimi ni mhaya na i dont care mtu akisema hakuna wahaya,najua mi ni mhaya tu,period!
ReplyDeleteUnajua bwana unapofanya research au kuandika topic kama hii lazima uwe na definition yako tayari ambayo ndo argument yako inakuwa based hapo. Na hapa naona huyu bwana Mushi anayo tayari. Yeye kasema kuwa "a tribe is made up of ppl who speak the same language and also share the same cultures and traditions". Wadau wamechangia na kuumpa maana nyingine tofauti ambazo nadhani ukizitumia vizuri...itaonyesha kuwa fikra zilisambaa...lakini lazima bwana uwe na a concrete conclusion ya hiyo definition ya tribe na pia uleze kwa nini. mimi naona ndo ishu kubwa iliyozuka hapa. nadhani comments za Anon wa June 27, 2008 3:19 PM zitakusaidia. Maana research yako ni kubwa. Hapa mimi sijaona jibu hata moja nitakaloweza kusema ni swafi kabisa kwa kuandikia kitabu. Mimi katika kuperuzi peruzi nimeona kuwa bwana wachagga hawakuwa kabila moja. Kulikuwa naona wametumia neno 'chiefdoms' hapo. Sasa hizi zilikuwa zinapigana na kufanya biashara. Sasa hapo lazima ujiulize chiefdoms na tribe ni kitu kimoja....au kipi kikubwa, au hata kama kimoja kinaweza kuwa ndani ya kingine. Moja ya definitions zake ni "the territory or people over which a chief rules". Sasa hapo chagua mwenyewe...Sasa bwana waliounganisha hizi chiefdoms ni wakoloni haswa wajerumani. Walikuja kama Wamishionari, nk. Itabidi usome historia hapo. mimi ndo nilivyoona. Sasa kusema kuwa ni kabila au la itatokana na argument yako toka mwanzo kabisa ambayo ni 'what is a tribe?'
ReplyDeleteBwana hii topic ni safi sana. Nadhani itakuwa kwenye historia zaidi. Yani safi sana...tunahitaji kujua historia yetu na sisi wachagga. Ilikuwa namna ghani? kwa nini mimi leo mmachame niwe kabila moja na adui wangu(enzi zile) mkibosho ambaye hata nyumba nilikuwa sijengi mlango ukaangalia huko...
Kila la Kheri
MTOA MADA TUNASHUKURU SANA KWA KUOMBA MSAADA HUU, NENDA KAMUONE DAKTARI UFANYIWE UCHUNGUZI "KIAKILI" KABLA HUJA ISHIA PABAYA.
ReplyDeleteDEO MUSHI TAFADHALI HICHO KITABU UNACHOFANYIA RESEARCH KITAKUMALIZA BABANGU FANYA MAMBO YA MAENDELEO SIO KUTAFUTA NANI NI NANI KARNE HII TAFADHALI SANA NDUGU YANGU!! ACHANA NA HABARI ZA WACHAGGA ... WAKIBOSHO WATAKUFANYIA KWELI WEWE!
ReplyDeleteOOOH, MIMI SIPO SIPO MICHUZI MUONYE RAFIKIYO
DEO Unachotarajia kufanya wafundishe wanao sio wanetu sawa heehe!! huo mgawanyo tuliumaliza pale Mangi wote walipo Mchagua Mangi Marialle kuwa Paramount chief sasa wewe unaturudisha wapi?? Unashida gani??
ReplyDeleteHebu muacheni amalize hicho kitabu tu!! Wachagga tutamuonyesha kuwa tu kabila mmoja pale atakaposema ana zindua kitabu akute ni kasha na aende tafuta original akute ni hewa!! Hapo ndio atajua tu wamoja au vipi
ReplyDeleteNDIO TATIZO BLOG ZA WABONGO.
ReplyDeleteHuwa nashangaa hizi blog za wabongo,sijui zina maana gani.Mana utakuta mtu analeta mada ili watu wwamsaidie mawazo.Tofauti na matarajio ya mtu basi anachoambulia ni kutukanwa,kukashifiwa,kuvunjwa moyo na kila aina ya majibu ambayo hayana msingi hata kidogo.Mtu ametaka kujua juu ya mada fulani,basi asaidiwe kwa kupewa majibu mazuri yenye kuridhisha au aurekebishwe kwa kile alichokosea kwa kupewa data zenye ukweli.Wachache wetu wamekuwa wanatoa majibu mazuri yenye busara ila kwa wengi wetu majibu hayaridhishi hata kidogo.Kama huna cha kuchangia basi nyamaza kimya,haina haja ya kutoa majibu yenye kuleta ugomvi.Kama huna idea basi nyamaza.Wabongo tujifunze kutoka kwenye blog nyengine za wenzetu.Haihiji uwe na elimu ndio uchangie.Upeo wa kitu na maarifa yanatosha kabisa kuchangia maada.wabongo tuamke.
Deo Mushi,
ReplyDeleteI have read your comments on what you called HAKUNA KABILA LA WACHAGGA.
I think you have made a fallacious conclusion without making a good research of what you wanted to tell the public. I think I will not be wrong if I say that you WANT TO MAKE A NAME by going against what the world had in her pockets concerning the Chagga tribe. Just to say a ward without much going into details, and making waht we could call a quick generalization the way you made yours, is that There are no Tanzania, but people who live in Tz. It is a shame, "MAKE RESEARCH BEFORE YOU COME TO SUCH CONCLUSIONS."
Kuna taifa la wachaga, ambambo ndani yake kuna makabila ya wasiha, wamachame, wakibosho, wauru, wambokomu, wamochi, waunjo, waseri, warombo. Na ukiangalia historia kila kabila lilikuwa na mangi wao, mfano Mangi horombo wa wa rombo, Mangi Marealle wa Marangu, Mangi Mandara wa Mochi, mangi XYZ wa Uru, Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Mushi wa Machame e.t.c.
ReplyDeleteKwa kuwa huwezi kuwa na taifa ndani ya taifa ndo maana makabila haya kutokana na mila na desturi za utaifa wao kufanana wakawekwe chini ya mangi mkuu [federal king] marealle na huyu ndiye aliyekwenda UN kudai uhuru wa wachagga kama taifa. Hata hivyo baada ya uhuru umangi ulisitishwa na Nyerere na ndipo taifa la wachagga likajulikana kama kabila la wachagga. Naomba uwasiliane na profesa Kimambo atakusaidia na kama unafahamu kijerumani basi wasiliana na mimi nitampatia michuzi kitabu kiliandikwa na Guttmann kuhusu historia yetu. Kwa sasa sisi wachagga ni kabila moja, na ndo maana wote wanatumia msamiati wa 'kyasaka'ambao mchagga hawezi kuutumia dhidi ya mchagga mwenzie.
Naomba kuwasilisha
Mchuku O' njama ya Mangi.
fanya reasearch kwanza, kama huwezi soma vitabu vingi tu vipo vya historia ya wachaga, elimika kwanza.
ReplyDeleteHivi hapa ulikuwa unatoa maoni kwamba jina la wachaga lifutwe au?
manake jina lenyewe lipo, wewe unasema halipo! Kama unapendelueza lisiwepo, basi jitoe kama unaweza.
Kabila gani la asili lina jina la sehemu?
Mfano dar es salaam, waitwe wadaresalam, hakuna, wanaitwa wazaramo, mara hakuna wamara, wanaitwa wakurya, hihivyo Rombo ni wachaga si warombo.
Ona watu wote hata mabao si wachaga walivyokushangaa, soma kwanza kabla KABAL HUJAANDIKA KITABU CHA KUPOTOSHA WATOTO WETU BAADAE.
we umeshasema hakuna kabila la wachagga alafu unaomba ushauri, basi liko kabila la wachagga.
ReplyDeletesweet
Arusah.
WEE!!!!!!!!!! SI TUPO SIRIAZI KUJENGA TAIFA LETU WEWE UNAJARIBU KUBOMOOA. UKIMALIZZAA WACHAGAQ UTAFUATA AKINA NANI.TUAMBIEE TUJUE MANA HATA RWANDA NA BURI ILIANZA TARATIBU USIDHANI WALITIBUKA MWAKA 1994 WA KAANZA KUNJINJANA TUUU.
ReplyDeleteNI WATU KA WEWEW WALIANZA KIDOGO KIDO KWAKUA WALISHIWA SERA ZA KUONGEA MBELE ZA WATU. WE BADALA UTAFUTE MAADA ZA MAANA HILI TAIFA LETU LILOKWISHA POTEZA MWELEKEO TUFANYE NINI KAMA WANA KAYA TUKALINUSURU WEWE NDIO UNAJITAHIDI KULIMALIZIA. WEKA MAANA ZAMANA TUKATAFUTE NI WPI TULIPO POTEZA RAMANI YA TAIFA HILI YA KUTUELEKEZA KWENYE MAFANIKIO.L NI HAYO TUU
Nafikiri tatizo linalojitokeza hapa ni watu kuwa overly "protective of their paradigms" hiyo ni kawaida kwani mtu anayetaka kufanya kitu ambacho tunatafsiri kuwa kipya tunataka kupinga kwani anakuwa anatutoa kwenye comfort zone yetu". Tumuache Deo ajenge hoja zake na kureview literature vya kutosha and let him build his case".
ReplyDeleteIn any case there is hardly anything as "absolute truth" duniani-Kumbuka kuna wakati watu waliamini the sun revolved round the earth?sayansi imetupa evidence tofauti. This truth may have been disturbing to some but still this is not conclusive. Tunazidi kujifunza. ( Soma Thomas Kuhn (1970) The Structure of Scientific Revolutions.
Hayo yamepita ila kuna mtu pia anadai kuna kabila la Waarusha sidhani hiyo ni sahihi sana-hawa ni Wamasai. Alafu kuna Wameru na makabila mengine ya mkoa wa Arusha
Mwana Historia,
ReplyDeleteNashangaa sana watu wanavyoandika bila kufikiri. Ninahisi sana watu wana woga wa kujua walikotoka na asili yao. Kwanza, ni nani aliyewapa Wachaga hilo jina? Tafsiri ya Wachaga ambayo baadhi yenu mmeitoa imeandikwa na nani? Inasikitisha kuona kuwa hata watu ambao wamejaliwa kuishi nje ya nchi hawataki kusikia au kusoma ukweli. Nakuunga mkono katika kuandika kwako kwa sababu vizazi vijavyo vitafanikiwa kusoma historia ambayo haikuandikwa na wageni. Nawasihi watu wengine wa Kilimanjaro kufanya utafiti kama huu. Kazi njema ndugu.
Mwanataaluma,
ReplyDeleteNi wazo jema kutaka kujua historia ya makabila mbalimbali na asili ya binadamu. Hii ni kwa sababu makabila yetu, koo zetu na asili zetu kwa ujumla zinatutofautisha kikazi, tabia, uwajibikaji, kurekebishana, na hata kusaidiana. Kwa mfano; hapa Africa mashariki takwimu zinaonyesha uchumi wetu unakua kwa 7% lakini ukitathimini zaidi ya 60% ya utajiri unamilikiwa na wahindi, wachina, wazungu na watu wengine wenye asili ya Asia, japo wao ndio wachache. Mfano mwingine ni kuwa kimaendeleo hapa kwetu Tanzania kuna makabila kama wahadzabe, wamang'ati na wamasai ambao wapo nyuma sana kimaendeleo hasa kwenye taaluma, huduma za afya n.k. Imethibitishwa kuwa wahindi hufanikiwa kwa sababu za kiukabila, pia wahadzabe wapo walipo kwa sababu za kiukabila. Wamachame pia kiuhalisia hutofautiana kwa mfano, na wauru kimaendeleo. Yote yasadikika ni sababu za kiukabila na utofauti wa kiasili. Serikali ambayo inatoa huduma kwa jamii nzima bila kujali kabila, kihekima itasaidia zaidi pale palipoelemewa. Msaada huu sio wa kifedha au vitu vya kushikika tu, bali hata elimu juu ya udhaifu fulani yaweza tolewa na ikawa msaada mkubwa.
Je, bila kujua asili na historia za koo na makabila ya binadamu itawezekanaje?
Mwandishi ana lengo zuri sana la kutaka kupata historia ya wachaga ila nadhani amekutana na watu wengine wanawazia vita vya ukabila kama "RWANDA". Sisi watz hatupo hivyo! Komaa na Kazi
Contact me personally through faceebook @ japh Mbuya i will help
Lafundi ndio tofauti Mila Ni moja mbege Ni ile ile inayotambikia rombo the same tu machame
ReplyDelete