
Wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi la London, nchini Uingereza. Viongozi wa Tawi Ndugu Maina Owino (Mwenyekiti) na Katibu wa Tawi Bi Susan Mzee walishirikiana kwa karibu na Katibu wa Siasa na Uenezi Ndugu Moses Katega na Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu Alan Kalinga kufanikisha kikao mjini Reading siku ya Jumamosi Juni 28 katika ukumbi wa 79 London Road.
Tawi la CCM London linaundwa na Mashina ya CCM ya Manchester, Birmingham, London Kaskazini, Southampton, Reading na London Islington.
Pamoja na hoja nyingine zilizoletwa na Wajumbe, kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi la London kilijadili njia madhubuti za kuimarisha mshikamano katika Tawi. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Wako Katika Ujenzi wa Taifa
Soames Phares
Mkurugenzi wa Habari na Teknologia
Chama Cha Mapinduzi
Tawi la London


T-shirt, jamani sio ya Michuzi hio, au ndo pacha mwenzako?
ReplyDeleteHawana lolote wanadhani wakirudi bongo wakigombea uongozi watapata nao nafasi ya kuitafuna nchi. Kama kweli mna uchungu na nchi hebu rudini nyumbani na vijisenti vyenu mkawekeze ili vijana wasio na kazi bongo wapate ajira. Huyo katibu wao tunajua pale mlimani Ukatibu wa DARUSO Ulimshinda akawa anatuuzia vyumba halafu leo mrudi tuwape uongozi si yale yale. Mi nina uchungu sana na hawa watu wanaoendeleza siasa nje ya nchi badala ya kuchukua hatua za kuwekeza nyumbani wanajiandaa kuja KUFISIDI Bongo kwa strategy ya kuwa wana exposure.
ReplyDeleteNchi yetu iliisha pata uhuru siku nyingi, ina amani na utulivu kilichobaki ni tafuteni mitaji nchi za wenzetu na kwenda kuwekeza nyumbani sio kwenda kununulia kura tutakuwa hatufiki. Mi nina mfano wa mtu ninamjua Alitoka uingereza mwaka 2000 na kwenda kugombea ubunge Tabora kwa kisingizio ni PhD holder anakaa london ataleta maendeleo akamwaga vipound vyake watu wakampiga chini kwenye kura za maoni.
Rudini nchini mkaendeleze nchi sio kujijengea majina Tawi la London uingereza halafu mnarudi bongo kutaka uongozi ili Mhamishie Vijisenti vya watanzania Offshore
Mi nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Watanzania wa leo wamekuwa "kunguru" nawaambia ukiinama chini wanajua unaokota jiwe wanaruka hawadanganyiki na maneno wanataka vitendo Rudini Bongo mkawekeze kwenye kuanzisha ajira mpya, muwe entrepreneurs sio kusubiri pesa za majukwaani na longolongo tu nchi inawahitaji sana ndugu zetu hasa katika kukuza uchumi kivitendo sio kimaneno "POLITICS"
Acheni Uzushi nyie bebeni BOX.msitutie kichefuchefu
ReplyDeleteMAALIM ISSA WANAINCHI WENZETU WANAJITAHIDI KWA HALI NA MALI ".KULINDA IMANI YA CHAMA." HAPO UK NA VITONGOJI VYAKE BILA KUSAHAU VISIWA VYA ".JERSEY."...".UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU."
ReplyDeletemambo ya zidumu sera za mwenyekiti hayo! Au sio? Naombeni mnieleze sera za CCM. Mpaka leo nafikiri hamjakana ujamaa ijapokuwa mmekuwa mkifuata mfumo wa kibepari kwa miaka tuseme 20 sasa? Kweli au si kweli?
ReplyDeleteLa pili...kwa nini mafisadi wanaruhusiwa kubaki na kadi za CCM? Tunajenga au tunabomoa? Niwape quote kutoka kwa mmoja wa wabunge wa CCM kuhusu mafisadi..."Mwaka 2010, wananchi hawatatuuliza Richmond wala EPA, watatuuliza maji na barabara tulizowaahidi ziko wapi?" Ndo maendeleo haya?
HUYU JAMAA BAADA YA KUSEMA WAKO KATIKA UJENZI WA SISIEM LONDON ANASEMA WAKO KATIKA UJENZI WA TAIFA
ReplyDeleteWe Peter kama ulikuwa hutaki kupiga picha usingekaa hapo badala yake unaficha uso mbona tumekuona mwangalie mwenzio Maziku,rudini TNT mpige box
ReplyDeletekisa cha kubanana na fremu ya kikwete ni nini? sio wote watakaouona ufalme wa mbinguni.
ReplyDeletenjaa na michuzi ya ufisadi inayowasumbua hao...tafute ufumbuzi suala la zanzibar na cafu..sio kufungua matawi tuu ovyo..isije ikawa kama kenya 2010..mnacheza na siasa nyie..watu wamefunguka masikio na macho siku hizi ..hata mkitoa khanga watu watakula sahani moja na nyinyi..kwanza jk na kundi lake,na mkapa ana kundi lake..humo humo katika chama cha mafisadi.na nyinyi ndio mambumbu wanachama..mpaka london bado mnawababaikia mafisadi..ama kweli nyinyi ni wadanganyika
ReplyDeletekalagabaho..sio fala mimi,
hawa mi naona wamekosa la kufanya! inawezekana ni watoto wa mafisadi hawa, wako wanakula tu hela zetu za EPA na Richmond, kwa hiyo wanafungua matawi kurudisha fadhila! Shame on you!
ReplyDeleteAkhsante sana Mh. IGEMBENSABHO Hawa wanafiki wabeba maboksi wananikera mpaka basi . Eti tawi la CCM London? Kwanza nashangaa kwanini tunawaruhusu kurusha upuuzi wao kwenye blog zetu hizi za jamii. Hawana lolote zaidi ya kutaka kujitengenezea umaarufu ambao haupo ili wakirudi hapa bongo wajifanye wakereketwa kisha wapate ulaji kweny CCM.
ReplyDeleteNimechanganyikiwa hapa, tawi moja lina mashina sita? duu labda ufahamu wangu wa neno shina na tawi ni tafauti na wengineo. Na iweje iweje manchester, reading, birmingham na southampton iwe chini ya tawi la london? hii miji iko nje ya london. Mfumo mzima wa matawi yenu ni wa ajabu, kuna london kaskazini halafu kuna london Islington, mumeweka shina moja kwa london kaskazini yote sasa kwa nini Islington isitambuliwe kwa upande ilipo kama ni kusini au mahariki au kati ya london? what about hackney au camden town? anyway endeleeni kuchuma wana ccm
ReplyDelete