Lady Jay Dee (pichani na wadau wa BongoDjs) tayari yuko London kuwakilisha bara la Afrika katika sherehe ya kuzaliwa kwa Mandela.

Akiwa huko jide atajumuika na masupastaa wengine 15 toka dunia nzima, kumumbia mandela.. jide ataungana na papa wemba na artists wengine wa2 toka africa kwa wimbo maalum wa sherehe hiyo iltakayoongozwa na marafiki wa mandela will smith na oprah katika shoo itayofanyika siku ya ijumaa juni 27.

Mara baada ya shoo hiyo siku ya pili yake, yaani Jumamosi Juni 28, Jide ataingia Reading kwa shoo moja maalum katika ukumbi maarufu wa FACE CLUB RG1 7JF NA KUITAMBULISHA SINGO YAKE MPYA "UKO JUU" KWA MARA YA KWANZA NDANI ya UK.

Habari zinasema Jide pia ataenda nyumbani kwa mdau Baraka Msiilwa wa Twanga Pepeta kusonga ugali kwa spinachi, dagaa, haragwe la nazi.. wadau wa ukerewe mnakaribishwa kujiramba maana jide anayo sifa ya mapishi..

Katika shoo ya reading jide ataweka bayana albam yake mpya ya shurkani, ambayo wimbo wake wa 'siku hazigandi' umemuweka ktk category tatu za tz music awards mwaka huu ... best female artist, song of the year na best song writer... upo hapo???

Jide atatambulisha singo mpya ambayo haijatoka bongo, yaitwa 'Uko Juu'. ataitoa ktk ring tone mwezi julai halafu ndio itaenda redioni. humo amewapa mashavu watu wote walio na sifa nzuri ktk fani zao.. jk, DC wa tegeta, mengi, chifupa (rip), sir kim, kaseja na wengine kibao wamo..

ZIARA YA JIDE YA HUKO READING INAANDALIWA NA BONGODJS

NENDA http://www.bongodjs.com KWA HABARI ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2008

    DC wa Tegeta nilikuwa nashangaa miujiko yote hiyo unayommwagia Jide kumbe amekurusha kwenye "Upo Juu''...teteteee Mheshimiwa Mithupu kwa misifa yani ngoma droo na JK.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2008

    Hongera dada Judith.Kaka Michuzi juzi nilikuwa nafuatilia ule mdahalo wa juzi kuhusu ujio wa Kelly Lowland,ulikuwa mzuri sana.Naona kama hii nafasi ya dada Judith ni nzuri sana kuitangaza nchi yetu.Kwanza tumeambiwa kuna mastaa wa nguvu,mzee mandela ni staa wa nguvu.Wizara inayoshughulikia utalii wamemtumia vipi huyu so-called 'JIDE'??Nafasi kama hii wangeipata akina KQ mngewakoma.HAPPY BIRTH DAY NELSON.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 25, 2008

    ,Msaada kwenye tuta
    Blaza michuzi,wadau na wajuvi, tafadhali nijuzeni ni kweli kwamba, hii dhana ya kuweko kiumbe anayejulikana kama jinamizi ina ukweli? kiumbe ambaye baadhi wanadai eti humjia mtu usingizini na kumkaba? au jinamizi ni ndoto ya kutisha tu kama wanavyodai weledi wengine? Tafadhali msichangie kwa jazba kwani kuna wengi wanaotaka kufahamu kuhusiana na suala hili. majibu yaliyokwenda shule muhimu. Nawakilisha.
    mdau wa Pwani

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2008

    Kuwa muwazi hilo jinamizi likubaka au? kama limekubaka ni jinmizi mahaba hilo.
    VM
    Arusha

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2008

    acheni upuuzi..this is space for lady jay dee mambo ya jinamizi yanatokea wapi sasa?embu acheni hizo amani za kishirikina.soma biblia,Qurani hutatokewa na mambo hayo.kama wewe ni Mkristo,lala na rozali na nyunyuzia maji ya baraka nyumbani mwako,hutasikia cha jinamizi wala babu yake.

    Lady jay dee hongera sana,i love you music and i hope to see you..you are amazing.but i dont like the masai hair.please take it out.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2008

    Peter Ushakuwa DJ kaka???, ebwana angalia career mzazi,na maisha yao kwa sana tu... mwenendo huo washapita wengi na hatujaona mafanikio yoyote....zaidi ya mitihani tu.. its you life ila be serious na life mazee.....
    Mshkaji wako hapa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2008

    Anon jan 25, 3:30 jaribu kuwa mkarimu na mwenye kutoa msaada wa haraka kwa anaehitaji, ikiwa kutoa ushauri m-bahili kiasi hicho je kutoa hela au chakula kwa anaehitaji inakuwaje hapo? mpaka mtu kaja kuweka mambo yake hapa kutafuta msaada ujue kweli yanamsibu hivyo haikugharimu kitu kama utanyamaza kugomba, au kutoa ukali hapa utazidi kumtisha na kukosa msaada kwa wengine ambao wakarimu wanataka kumsaidia walau kwa ushauri tu.

    Vivaaa lady jay Jasiri haachi. asili.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2008

    michuzi bwana tehe tehe tehe tehe yani humtoi mtu hewani mpaka akurushe au akupe shavu mimi nimeomba msaaada wa kufungua blog kwako mpka nimechoka kumbe nilitakiwa nikusifien kwanza eeee kwanza hayaaaa huo ni ufisadi mwingine ktk blog wadau. ngoja nikusifie ili na haya maoni yangu uyatoe hewani maana bila hivyo utayatupa kapuni.. michuzi mkuu wa wilaya tegete mzee wa bwawa la maini wa mzee wa bongored uko juuuuu hakuna km ww hakuna wakufikia blog yako teh tehe tehe tehe kwikwiwki. naomba msaada wa kufungua blog

    mdau wa tandale

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2008

    wewe hapo juu ur so insane
    kwani kuwa dj ni dhambi???kakmwabia
    nani ukiwa dj hauna career???how do u know??hau ndo nyie wenye wivu na maendeleo ya watu kama mtu akusaidi
    wala humsaidie achana naye...
    watu wana piga mziki na mambo mengine
    ya career yanaendelea bila matatizo
    i think wewe ni bonge la mwanakijiji
    ambaye hauko civilised
    inshort grow up and ge expossed
    you will understand what it means by that and get ur lazy ass out of that waste of space...dickhead

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2008

    we anon 4:18 acha kijiba cha roho,matter of fact acha wivu na kama huna cha kuongea,usiandike pumba zisizo na kiwiliwili..aliekwambia kalosti life kwa sababu kawa DJ nani.we vipi wewe.mfano tosha ni Dj Clue this man is a millionaire,na kazi pekee ni ya u-DJ.hata ma DJ wa bongo kina Dj Bonylov Dj venture mbona wote wanafanya kazi hiyo na wapo mbali kimaisha?we mpaka mtu awe dokta,sijui loya ndio unaona kazi.we kalagabao nini?nasema usirudie tena kusema kazi za watu.sijakumind wala nini

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2008

    Karibu London Jide
    E-Attack
    Ealing Broadway

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 25, 2008

    A list of African countries and how their natural environments were ranked is shown below.


    African Ranking World Ranking Country
    1 1 Tanzania
    2 11 Uganda
    3 17 Zambia
    4 21 South Africa
    5 24 Kenya
    6 31 Botswana
    7 33 Zimbabwe
    8 34 Ethiopia
    9 38 Cameroon
    10 42 Namibia
    11 51 Senegal
    12 54 Benin
    13 61 Mozambique
    14 67 Burkina Faso
    15 70 Nigeria
    16 74 Madagascar
    17 77 Mali
    18 83 Burundi
    19 86 Egypt
    20 91 Chad
    21 93 Mauritania
    22 94 Tunisia
    23 95 Gambia
    24 97 Algeria
    25 114 Libya
    26 118 Morocco
    27 126 Mauritius

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 26, 2008

    Hata mi sijamind huyo fala anafikiri kazi ni kufanya bank tu ndio mitazamo ya majority bongo.kisa wanataka tips za hela za wizi pathetic kazi popote acheni ujinga kuna alot of careers in this world na hapa (Europe)hakuna kufuatana fatana ndio nyie nilitee fulana kwani huko hazipo? siku moja ukitoka kupangusa jicho lako u will see by ya self tatizo lenu mnaishia Nairobi wakati hilo ni jalala panda uje uone

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 26, 2008

    wewe anon wa 5:29 this is a free world,and theres freedom of speech,dont deprive my rights please.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 26, 2008

    sasa wewe anon wa 10:04 aka anon wa ku copy-paste,TUKUSAIDIAJE NA THAT INFORMATION??ungetueleza basi inahusiana vipi,ili na sisi tuelewe

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 29, 2008

    jamani mbona hatujamuona jd akiimba kwenye bday ya mandela? wambongo mbwana acheni uongo duuuuuu. au kuna mandela mwingine ndio jd alienada kumuimbia?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 29, 2008

    Jamani acheni kutudanganya.JD aliperform saa ngapi on that concert.Na newspapers za bongo nao wanafagilia.Kaka Michuzi please check ur facts before putting anything on the blog.Hata ukicheck list of performers hayupo na hamna jina lake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...