kaka michuzi shikamoo,
Mimi naomba kuuliza watanzania wenzangu wajaribu kunielewesha kuhusu utaratibu unaotumika kupangisha nyumba za msajili zile za magorofa mara nyingi zinakuwa mjini na upanga? kwanini asilimia kubwa ya wapangaji ni wahindi tu nafikiri ni 90% wahindi na 10% iliyobaki ni watanzania?
Tena kinachouma zaidi ni kwamba shirika la nyumba liliamua kujenga nyumba hizo kwa makusudi kabisa ya kuzipangisha kwa wananchi kwa bei nafuu ya kama 100,000TShs mpaka 150,000TShs kwa mwezi, Ili wazalendo waweze kupata makazi bora na kwa bei nafuu (Bei hiyo ndiyo inayotumika kupangishia nyumba hizo kwa sasa, hapo zamani zilikuwa nafuu zaidi).
Sasa inakuwaje wahindi ambao wengi wao ndio wanaomiliki mabiashara ya hela kubwa ndio wapangaji wakubwa kuliko hao maskini wenyewe ambao nyumba hizo zilijengwa kwa ajili yao?

kwa kweli inaumiza sana akili, binafsi nimeshajaribu kutaka kuzipanga lakini wafanyakazi wa shirika hili la nyumba wanazungusha sana kiasi kwamba utaona tuu kama hawataki kukupa nyumba.
Tena wanamasharti magumu ambayo hayana kichwa wala miguu yaani kama yamewekwa mahususi kuwadidimiza wazalendo. Mara nyingi wale wafanyakazi wa shirika hili wanapokuzungusha sana basi ujue tuu kuna muhindi tayari ameshatoa dau kubwa, nasikia madau yanaanzia milioni 5 mpaka hata 50 na kuendelea sasa kweli wazawa tutaweza kuzipanga nyumba hizi hata siku moja.
kwanini tunajibagua wenyewe jamani mpaka nchini kwetu wenyewe?
Tunaona kama sikuzote weupe wa aina yoyote ile ndio wanastahili zaidi kuliko sisi. Wakati mwingine tunawaonea hawa watu weupe wanapotubagua manake sisi wenyewe ndio tunaanzaga kujibagua. kusema kweli inaniuma sana.

Sijui Muheshimiwa rais analionaje hili swala la wananchi wake wazawa kunyanyasika kutafuta nyumba bora wakati zote zimekaliwa na wahindi. Je ni hatua gani atazichukua yeye kama Raisi wa watanzania kuhakikisha kwamba haki inatendeka na rushwa inayotumika kukandamiza wazalendo katika shirika hili la nyumba inatokomezwa?
Wanyonge tunaomba mabadiliko ya kasi mpya, hari mpya na nguvu mpya jamani. Tumechoka kunyanyasika na kubaguliwa nchini kwetu wenyewe.
Sio kwamba sitaki hao wahindi wapangishwe nyumba hizo la hasha ninachoomba mimi ni usawa utumike katika kupangisha nyumba hizo huku wazalendo wakizingatiwa zaidi. Jamani mbona tunasahau ile methali ya kila mwamba ngoma huvutia kwake! Mbona sisi tunavutia wenzetu tuu. Tafadhali muheshimiwa Raisi tusaidie kutatua tatizo hili sugu.

Tafadhali naomba kila alieguswa na mada hii asiache kutoa mchango wake ili tujue nini cha kufanya kutokomeza hili tatizo. Ikibidi wananchi kuandamana kwa amani basi na tuandamane mpaka hapo haki itakapotendeka katika upangishaji wa nyumba hizi.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake bila kusahau baba wetu wa taifa Mwalimi J.k.Nyerere kusema ukweli nafikiri yeye asingeweza kuvumilia unyanyasaji huu kwa wananchi wake.

Wenu Mzalendo Halisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2008

    Zile nyumba za msajili za uhindini kule zilikua za wahindi tangu hapo mwanzoni kabla ya serikali kuzitaifisha na sio kuzijenga. wale wanaoishi kwenye zile apartment walipangishwa kabla ya zile nyumba kutaifishwa ndio maana unaona mpaka leo wapo bado. Apart from that, Msajili hupati nyumba mlala hoi kama huna kitu, wapo wazawa wengi tu wanaokaa kwenye msajili wa majumba ambao wanajiweza na hizo nyumba hawakuzipata bila ya kumwaga hizo milioni ulizozitaja. Kwa hiyo usiwalaumu wale wahindi kama vile walipora zile nyumba, wakulaumiwa ni watu wa msajili kwa kuwauzia watu wenye pesa tu, na hiyo itakuwa unajipotezea wakati tu. Kwenye mlo huwezi kumuambia mbongo usile.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2008

    wahind wanatoa fungu la kutosha kama nyumba inapingishwa 100,000 anatoa had lak 6,so lak 5 za mtu anayefanya kaz hapo aliopekea rushwa,unategemea wewe mzalendo upewe nyumba kalagabao...
    tafuta kiwanya boko or mbwen au mbagala ujenge hizo nyumba siyo za watanzania.
    za wahind ulikuwa ujui,nch ishauzwa.
    kama kila kitu ad migod,bank tumewapa wagen unaona ajabu nyumba kupewa wahind!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 25, 2008

    Acha Kujichanganya we Mzalendo halisi, waliopangishwa kwenye hizo nyumba ni watanzania wenye asili ya Kiasia. Mpaka uache maneno ya kibaguzi ndo utapata mtu wa kukusikiliza, vinginevyo utaendelea kulalama tu. Nenda NHC uchukue fomu na kuelekezwa jinsi ya kupata Pango na usiwe mchoyo kuwawezesha watumishi utakaowakuta hapo ndo mambo ya mjini, kila mtu kula sehemu anapofanyia kazi vinginevyo watoto hawatakwenda shule upoooo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2008

    habari yako Mzalendo halisi ningependa kukupa jibu kwa kifupi sana ni kwa nini ?unaona wahindi wamejaa humu kwenye nyumba ya msajili kwanza kabisa hizo nyumba zilikuwa zinakaliwa na waswalihi kabisa hapo zamani na kulikuwa hakuna ubaguzi wowote ulikuwepo kipindi hicho na ilikuwa rahisi sana kupata hizo nyumba sasa wahindi siku zote huwa ni wajanja sana na huwa wanaishi kwa mahesabu sana wakawadaganya wafrika kwa hela wawapishe kwenye hizo nyumba na walikuwa wanauzia kwa siri na hao wahindi unapewa milioni zako unamupisha muhindi anaingia ndani ya nyumnba sasa wao wengi wao walikuwa wataka kuwa na nyumba zao ndio anapewa hela anakwenda kujenga huku mbagala sio vibaya kuwa na nyumba yako lakini hesabu walizokuwa wanapiga hao wafrika wezetu zilikuwa sio sawa maana ulikuwa unaweza kujenga taratibu na kuendelea kuishi kwenye hizo nyumba mimi mwenye nimeishi kwenye hizo nyumba mpaka sasa naishi siwezi kuondoka maana najua kupiga hesabu zanagu fresh nikiangalia nikitaka kwenda sokoni ni karibu hospitali yaani huduma zote niko nazo karibu kwahiyo silalamike kuona wahindi wamejaa kwenye hizi nyumba ni ujuinga wa wafrika wenyewe waliondoka wakawachia wahindi siwezi kukuelezea kwa urefu kwa hapo tu panatosha kukupa picha halisi mimi nimejibu sweli hilo ambalo una lalamika kwa nini ? wemejazana wahindi tu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2008

    Dah !IMENIGUSA na imenikumbusha nilivyotapeliwa kwa kutafuta hizo nyumba za NHC. Hayo uyasemayo ni kweli ,mimi binafsi nimeshawahi kutafuta nyumba za NHC kwa kwenda pale ofisi za upanga yani ni usumbufu wale watu wanataka hongo ndio wakusaidie huwezi amini NIMETAPELIWA milioni 3 (3,000,000)
    na baba mmoja ili aweze kunisaidia kupata hizo nyumba anasema aliambiwa alete hicho kiasi na hao watu wa NHC ,sasa sijui ni kweli kwa maana alikua anawasiliana na baba mmoja ambae anahusiana kidogo na rais wetu yupo maeneo ya upanga na huyo baba anapatikana maeneo ya lumumba pale CCM anavaa kofia ya kiislam kila wakati kumbe ni tapeli anaudhalilisha uislam .Yaani siwafichi roho inaniuma sana ila wakati tunakabidhiana hizo pesa hakukuwa na mwanasheria ila nakumbuka nilimwambia hapa tupo wanne hakuna mwanasheria wala shahidi isipokuwa namuweka mungu ndio shahidi wangu ukizingatia huyo baba wa upanga alimuoa jamaa yangu ila sasa wamesha achana ,anyway sina la kufanya ni mnyonge kidogo nilichokua nacho wamekichukua walonacho epecially huyo baba wa upanga kwani kuna siku tulienda mimi na mke wa shemeji yangu tukakuta ameweka fanicha mpya hapo ilikua ni baada kama ya wiki moja toka tuwape hizo pesa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2008

    Wale wapenzi wa Nyota na majini na mauchawi Sheikh Yahya Hussein Bingwa wa Utabiri nchini ameanzisha ukurasa wa Majadiliano ambao utafika kwa kutumia anuani ifuatayo www.astrosheikhtz.com/majadiliano. Hapo mzee anataka watu wajadiliane wazungumze hasa kuhusu chochote, wale wanaopinga nyota waseme, wale wanaounga mkono waseme wenye dukuduku kuhusu chochote uwanja ni wenu. Haya fungueni domo mseme

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2008

    umegusa pale kabisa,,,hili suala sasa limekua sugu izi nyumba ata me nshawai jiuliza ivi ni za wahindi tuu???kwanini wasijenge nyumba zao na ivi walio wengi wana pesa na uwezo mkubwa tu,,kwanini wazalendo tunahangaishwa hivi???afu yan zimepanda bei hivi???manufaa ya nani sasa??
    hizi nyumba zilijengwa kusaidia waTz wasio na uwezo na makaazi mazuri ila sasa ishakua kero afu utakuta uyo mhindi kapanga miaka ata 30,,,JAMANI,,,inasikitisha sana na inakera sana,,izo nyumba nilishafatilia pia km mtoa mada apa yan unaamua tu uache sasa...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2008

    mzalendo hayo uliyo zungumza yana ukweli mkubwa ndani yake,hapa kuna matatizo mawili kwa uoni wangu kwanza ni rushwa iliyojikita na pili ni umaskini.ikumbukwe miaka ya nyuma nyumba hizi zilikua zikikaliwa na watanzania wenyewe kwa asilimia kubwa sana lkn kila siku zinanyozidi wahindi ndio wanao ongezeka ktk umiliki wa nyumba hizi ni hii yote ni kwasababu watanzania wenyewe wamekua wakiziuza kwa kutaka mapesa mengi kwa hao wahindi ambao hawapendi kukaa nje ya mji kwa ajili ya biashara zao na kwa kuhofia usalama wao maana watu wengi hatuwapendi hawa wabaguzi hivyo wako tayari kununua hizo nyumba kwa gharama yoyote ili wakae mjini au upanga karibu na wenzao.watu wengi wameziuza tena bila hata kuiarifu msajili wa majumba yenyewe na kwenda kujenga nje ya mji,pia nyumba zenyewe ni chache hivyo imekua ni hot cake,kwahiyo tatizo ni sisi wenyewe hata tukipewa tunauza,afadhali wenzetu wazanzibar nyumba zao za michenzani hukuti mhindi hata siku moja.Inabidi tuseme na tamaa zetu tunastahiki vizuri sisi wenyewe sio wahindi tuhata mkibisha lkn huo ndio ukweli, kwanza tujirekebishe tusikae kulaum.MDAU MPENDA AMANI UK.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2008

    Soma Historia, kuelewa kwanini priority ilipewa kwa wahindi, kuanzia kutoka kwa Watawala wa wakati huo Waingereza na mpaka wakati wa mapinduzi ya Zanzibar wahindi wengi walikuja kukimbia discrimination Zanzibar. Wewe unaonekana ni Racist to say the least. Nyumba za usajili ziko kubao na maeneo mengine jijini Dar kwa mfani hamna muhindi hata mmoja. Na sikuhizi bado nyumba zinajengwa na wahindi hawana priority anymore, mimi nawajua wanaofikukuzwa upanga jengo lao linauzwa kwa kujengwa offices. Soma elewa and dont be narrow minded.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2008

    EBWANA NDIO, III HAINA UBAGUZI WALA NINI, ILA NIMETEMBEA NCHI NYINGI SANA DUNIANI SIJAWAI KUONA ETI WANAJALIWA WAGENI KWANZA KWENYE COUNCIL HOUSE KULIKO WENYE MALI. TZ BADO TUNAITAJI VIONGOZI, WACHA TUKUE TU, KUNA WATU TUNA PASSION YA KWELI NA KWETU, ISTOSHE TUMEKULIA KWA WATU KWASABABU KWETU SIO KAMA HAKUNA BALI NI MIJITU YENYE TAMAA NA UKOSEFU WA AKILI.
    BROTHER ISSA MICHU UTAKUMBUKWA SANA KWA ULICHOKIFANYA ATA MIAKA 50 IJAYO. MAANA NAONA SASA TANGU UMETULINK WABONGO KISTYLE YAKO, WALAU ISHU MUIMU TUNAZIJADILI KWA KWELI.SASA NDUGUZETU WAINDI WAINGIE USWAILINI ILI WAZIPISHE FAMILIA MBILI TATU ZA TANDIKA NA YOMBO DOVYA WAHAMIE UPANGA. INASOUND KAMA HAIWEZEKANI LAKINI IKIFIKA WAKATI PRESIDENT WETU AWE KATI YA WATU WALIO ZALIWA MIAKA YA 80 NA. UWEZEKANO WA KUBADILI ILO SYSTEM LA WAKONGWE NI MKUBWA SANA. MREMA ALITAKA KUJARIBU LAKINI AKAZIMWA. JUST THOUGHTS.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2008

    Nakuunga mkono hata mimi nimekuwa najaribu kulitafakari hili swala la nyumba kwa muda mrefu na siyo upanga tu.

    Ukiangalia ki utaratibu Tanzania haina system ambayo inawapa haki wapangaji wa kawaida.

    1. Kila nyumba zinazotangazwa kwa wapangaji kwenye magazeti hata kama ni Magomeni au Kinodoni kinachozungmziwa ni US $ siyo TZ shs. Je ni watu wangapi nchini mwetu wenye uewezo wa kulipia kodi kwa dollars?

    2. Bei za nyumba nchini kwetu ni za juu sana ukilinganisha na kipato cha wanancha bila kusahau standard za nyumba zenyewe.

    3. Kodi inabidi ilipwe kwa mwaka mzima (wakati wanachi wote wanalipwa mshahara kwa mwezi)bila kumsahau dalali anayedai malipo ya mwezi kulingana na kodi itakayolipwa.

    4. Wenye nyumba wanajipandishia bei holela holea bila kuwa na mpangilio.

    Maoni yangu: badala ya wenyenyumba kudai kodi ya mwaka mzima kwanini wasianzisha system ya depost less say miezi mitatu? Kwanza itawasaidia wao (wenye nyumba) kwasabu hii depost ni ya ku secure kwamba mpangaji atalipa kodi on time, na pia kama kuna kitu ambacho kitaharibiwa kwenye nyumba hii pesa itatumiwa ku repair the damages. Hii pia ingewalimit wapangaji ambao huwa wanaharibu nyumba za watu. Nimeishashuhudia kwamba wenyenyumba kawaida huwa inabidi kukarabati nyumba kabla hawajampangisha mtu mwingine kwa sababu ya damages nyingi zinazofanywa, na hii sidhani kama ina faida kwa wenye nyumba kama kweli utalipwa kodi ya mwaka na utumie labda zaidi ya nusu kukarabati nyumba kabla ya kumwingiza mpangaji mwingine.

    Kudai wapangaji kodi ya mwaka inahamasisha rushwa au biashara haramu nchini. Maana siyo watu wote wene uwezo wa kuwa na cash ya kulipa mara moja.

    Inabidi Serikali iliangalie swali la nyumba ki ujumbla. Inapaswa kuwa na bei ambayo inalingana na kipato cha wananchi. Ingawa najua kwamba bie huwa zinaamuliwa na soko(demand), lakini still bei zetu ni too much hata ukilinganisha na nchi jirani.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 25, 2008

    habari zenu,
    Mimi nafahamu katiba ya nchi yetu ni inayojali watu wote bila kuangalia dini, jinsi, utamaduni ama rangi ya mtu. Hivyo basi inapotokea hoja zikajengwa kwa msingi ya wahindi ama wasio wahindi mi binafsi sizikubli saaana. Apa la msingi tuangalie je hao weupe wanao uraia wa Tanzania? Kama wanao wana haki ya kupanga kwa mbinu zozote zile, kwani ktk nchi yetu mbinu-mbinu zipo kila kona, na wala sio NHC tu, kila mtu anakula ofisini kwake!!
    Labda tupambane ili SIFA za upangaji wa maghorofa hayo zibadilishwe na kutazamwa upya na ziwe wazi. Kwa mfano tu, matarajiri(weupe/weusi) wasiruhusiwe kabisa kupanga, wawaachie maskini na wao (matajiri) wakajenge nje ya mji kwa vile wanayo fedha nyingi tu, halafu na usafiri wa kuwaleta mjini pia, umenipata?
    Naomba tusibaguane kwa misingi ya rangi, ukifanyiwa hivyo wewe usijali, ila lipiza baya kwa jema, ndio utakuwa umeshinda....

    aidan mmari, mwanaharakati.
    aidanmmari@yahoo.com

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 25, 2008

    Mto maada nashukuru kwa kuleta hii hoja. Naamini tatizo sio wahandi na ningeomba kuondoa hii aina ya chuki ya kibaguzi inyoonekana kwenye hii hoja.

    Tatizo kubwa limekua kwetu sis wenyewe wazalendo na mfumo mbaya wa kuendeleza makazi mjini Dar es Salaam. Labda waswahili walishafanya makosa huko kipindi kilichopita kwa kuwauzia wahindi haki za hizo nyumba, hili liwe fundisho kwa wengine.

    Kwa upande wa serikali imeshindwa kuandaa utaratibu wa kupatikana viwanja vya kutosha na kupatikana kwa mikopo ya muda mrefu ya ujenzi wa nyumba kwa watu wa hali ya chini. Serikali ikianda sera nzuri za kuendeleza makazi ya watu tutaweza kupata nyumba bora kwenye sehemu nyingi nzuri hapa DSM kama vile kigamboni na maeneo mengi tu. Shirika la nyumba linajenga nyumba za bei mbaya tu, ukiangalia kwenye website yao nyumba zinaanzia mil.70, sasa ni mtanzania gani wa kawaida ataweza kununua hizo nyumba? Na je kwanini mifuko ya pension na bima isitumie akiba za fedha zao kuanzisha mfuko wa kuwakopesha watu wa hali ya chini kwa ajili ya kujenga nyumba? Mifuko hii ya pension ina pesa nyingi ambazo zipo idle na michango ya hawa watu wa hali ya chini na ni wajibu wao kuandaa sera za kuinua maishaya watu hao pia.

    Serikali pia ikiboresha miuondo mbinu kwenye haya makzi kama yetu ya manzese uzuri au hananasif tuatapata upanga nyingine za nguvu!! Haya yote yanawezekana TZ tatizo ni watekelezaji.....

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 25, 2008

    Ishu nyingine ninayojiuliza mbona nyumba nyingi zinazojengwa city centre kwa ubia wa NHC na private companies hizo private companies ni za kihindi tu? Huku NHC inaenda kujenga maporini huko ambako hamna customers? Na NHC inahakikisha vipi kwamba inapata share yake inayostahili kutoka katika hizo nyumba, manake these guys are very clever and corrupt wanaweza kuwa wame-sign contract na NHC kwamba kodi ni TSh200,000/= kumbe wateja wanatozwa TSh 500,000/=, au wanaweza kuwaambia NHC kwamba nyumba haijapata wapangaji wa kutosha kumbe block zima limejaa wapangaji! Mr. Mmari unajiita mwanaharakati, unasema lipiza baya kwa jema, una maana na hela zetu za EPA tusiwadai? In short Indians are our fellow Tanzanians but they really discriminate us, we can't go on tolerating such nonsense for a long time,If they don't change, it will reach a time we will strike back by all means in our possession, it's a time bomb!. This message is clear to our fellow Indians and those Fisadis in power! No offence! This is pure thruth!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 25, 2008

    dah acheni ubaguzi,its open to everyone,wahindi are willing to pay and they have got the funds.thats all

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 25, 2008

    Wewe unayejiita mzalendo halisi wacha leta lawama zako bwana,hebu nenda pale shekilango,au ilala boma kama utakuta wahindi wanaishi,ama ingia magomeni mapipa au ilala kama utakuta hao uliowataja.
    Kinachoendelea hapa ni jambo la kawaida kiuchumi,mahitaji ya nyumba yako juu sana watu wanaohitaji nyumba hizo ni wengi mno,na nyumba zenyewe ni chache mno unatarajia kutakua na hali gani katika upatikanaji wake?
    Siku nyingine uwe unapima hoja zako kama zitaleta madhara gani kwa jamii ili uangalie namna nzuri ya kuiwakilisha,kwani hapa hoja sio kwa nini wahindi tuu na sio watu wa chini,hapa hoja ni namna ya upatikanaji wa hizo nyumba.Kama nilivyosema awali upatikanaji wa nyumba hizo umekua mgumu kutokana na uhaba wa nyumba zenyewe na ukubwa wa mahitaji ya nyumba hizo,kitu kinachopelekea kutumika kwa njia zisizo halali ili kufanikisha lengo.
    Hoja hapa nadhani ingekua ni kwa NHC wenyewe kuamka usingizini na kuchangamkia soko hili kwa kukopa fedha hata kutoka taasisi za kimataifa za fedha na kujenga nyumba za bei nafuu ambazo zingepangishwa kwa wananchi,hakika tusingekua na maeneo kama tandale,manzese,mwananyamala kisiwani nk ambako nyumba zimejengwa hovyohovyo bila mpangilio maalum.
    Yawezekana wapo wanaoliona tatizo hili ila kwa kuhofia mazingira yetu (mnayajua) watu wanakosa ujasili w kuiboresha NHC,ni wazi suala la makazi duni limechangiwa sana na NHC kutojiendesha kibiashara,badala yake kugeuzwa mradi na kina "walewale"

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 25, 2008

    JAMANI MSIWALAUMU NHC WALA WAHINDI WA WATU,KULE PAMEJAA WAHINDI SANA SABABU WASWAHILI SISI WENNYEWE NDO TUNAUZA UPANGAJI KWA WAHINDI,KAMA UMETAPELIWA NI WEWE MWENYEWE UJILAUMU KWA KUTOA RUSHWA,WEWE UTATOAJE PESA MGONGONI??.KAMA UKIENDA KUTAFUTA NYUMBA NHC UNAAMBIA NYUMBA ZIMEJAA NA NI KWELI ZINAKUWA ZIMEJAA,SASA WANAKUAMBIA TAFUTA UKIPATA UJE TUKUSAJILI,SASA WAHINDI WAKIONA WASWAHILI WANAWAFUATA NA KUWAAMBIA WAWAUZIE UPANGAJI SASA NA SISI KWA NJAA ZETU UNAKUBALI KUHABISHWA HATA KWA MILIONI 8-20HIVI UNACHUKUA CHAKO UNAANZA MBELE-MI PIA NIKIHAMIA KWENYE KANYUMBA KANGU NATAFUTA MDOSI AJE ANIPATIE MTAJI,WASWAHILI HAWATOI PESA NDEFU-NI MDAU UPANGA MASHARIKI TENA MSWAHILI NYWELE ZANGU KIPILIPILI

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 25, 2008

    Mdau uliyetundika mada hii,nafikiri kwanza serikali ifumue uongozi mzima wa NHC,iweke utawala mpya ambao utaliendesha shirika hili kibiashara zaidi kuliko ilivyo sasa kama mradi wa watu fulani hivi
    Pili uongozi huo mpya ukague mikataba ya watu wanaoishi kwenye nyumba zile ili kuondoa hali ilivyo sasa ambapo watu (wengi) wamegeuza zile nyumba kam vitegauchumi vyao,kwani wengi wanaoishi kwenye nyumba zile si wapangaji halali
    Tatu uongozi mpya uboreshe nyumba zilizopo na kuongeza uwekezaji katika ujenzi wa makazi mapya ili wananchi wapunguze ujenzi holela kwani ujenzi huu holela unasababishwa na kukosa makazi bora kutokana na serikali kujivua jukumu la ujenzi wa nyumba.
    Wala usiwalaumu wahindi ni shortage ya nyumba ndio iliyosababisha matumizi ya njia zisizo halali ili watu kujipatia makazi.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 25, 2008

    Ndugu mzalendo halisi,hata mimi ni mzalendo halisi. Tofauti zetu ni mbili: 1) mimi ni mwenyeji wa Dar na 2) nina miaka 57. Kwa hivyo, naweza kukuhakikishia kuwa Shirika la Nyumba halijajenga hata nyumba moja "uhindini" Dar (i.e. Upanga, Kisutu, Madukani, Mshihiri, Mtendeni, Kichwele st. n.k. Hizo nyumba karibu zote zilikuwa za Watanganyika wenye asili ya Kiasia; ila 1969 Agosti walinyang'anywa zikawa za MSAJILI WA MAJUMBA. Kilichobaki, waliendelea kuisho humo.Mashamba na viwanda vilitaifishwa na karibu vyote vikafilisika. Ni muhimu uijue historia hiyo na ya Uganda (1972, Iddi Amin). Tujifunze na historia. Tuonyeshe uzalendo wetu kwa kufanya kazi kwa bidii, kuwa waaminifu (pigana na ufisadi) kuwa na uongozi bora badala ya kutafuta target rahisi ili kukwepa ukweli...

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 25, 2008

    tuache kulaumu wahindi wakati tatizo ni ukosefu wa nyumba na rushwa iliyokithiri,kwanza siamini NHC wana uwezo wa kujenga nyumba kutosheleza mahitaji ya watu wote na mfumo mzima wa shirika umejaa rushwa tupu na haueleweki,tunahitaji private investors ambao watajenga nyumba na kutupangisha/kutuuzia kwa bei ya kushindana sio kulaliana kama ilivyo sasa,watanzania wenye pesa inabidi waone hili tatizo na waweke pesa zao maana market ni kubwa sana na sioni kama watapata hasara yeyote,dunia nzima private investor ndio wanawekeza kwenye issue kama hizi na wala sio serikali...kulaumu wahindi haisaidii kitu zaidi ya kujenga chuki tuu isiyo na sababu na kumbuka nyumba nyingi zilikuwa zao kabla ya kutaifishwa,watanzania chukueni mikopo muwekeze kwenye hii biashara tutasolve matatizo mengi sana

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 25, 2008

    Nadhani swala kubwa hapa ni wazalendo na njaa yao na wahindi pia ni wakulaumiwa kwani kutoa Fedha ili kuhakikisha wazelendo hawakai kwenye nyumba hizo pia ni makosa.

    Wakati marehemu Julius Nyerere yupo hai (mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi)upumbavu huu ulikuwa haupo kabisa kwani alikuwa anahakikisha kwamba misingi na sheria zinafatwa lakini pindi mafisadi walipochukua nchi ndio kila kitu kikaanza kwenda mrama.Zile nyumba zilijengwa kwa madhumuni ya watu wenye kipato cha chini na sio matajiri.Sasa iweje tajiri akae kwenye nyumba hizo, hapo msingi mzima umeshakiukwa.

    Kwahiyo basi serikali bado ina nafasi ya kuliingilia swala hili na kuhakikisha kwamba nyumba hizo wahusika wakuu ndio wanapata haki bila kujali rangi zao kama ni mwekundi , wanjano, au wabluu

    Popo

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 25, 2008

    wahindi bwana..where is Mugabe!?!?we need help!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 25, 2008

    BINAFSI NILIBAATIKA KUPA MYUMBA ZA MSAJILI UPANGA,KWA KUFUATA TARATIBU ZAO,1983 MTAA WA KITONGA KARIBU NA MZAMBARAU WA MAPOPO,1988 NIKAJIWA NA MUHINDI,TUBADILISHANE NIENDE KARIAKOO,MTAA WA UHURU 3BED ROOM 2FLOOR,NA AMEIPA PESA TASILIMU 10,000.00 ZA MADAFU,SIKUJIPINDUA NIKAVUTA NA KUNUNUA KIWANJA SH 350,000 KIJITONYAMA TENA BARABARANI NA WENGI WENYE AKILA NA KUONA MBALI TUMEFANYA HIVYO LEO TUNA KULA KUKU KWA MRIJA KULIKO UPANGA NA MAMBO POA,USILAUMU WAHINDI,NA SASA HIVI SI RAHISI KUPATA NYUMBA HUKO KUMEJAA NDUGU,USICHOCHEE VURUGU MBWENI,NDEGE BEACH,KIGAMBONI BADO KUNA VIWANJA VYA SERIKALI KAMA MJENGAJI NENDA WIZARANI UTASAIDIWA.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 25, 2008

    tanzania rushwa ipo kila kona,kuanzia mtu wa juu mpaka mtu wa chini.Hospitalini rushwa,kutafuta kazi ujuano na rushwa,kutafuta nyumba rushwa,airport watakudai kitu kidogo hasa ukiwa unaenda nje ya nchi kwa hiyo pia utaombwa hiyo pia ni rushwa.Kutoa mzigo wako bandarini utatakiwa utoe rushwa,.hao wakubwa ndio usiseme wakipata uongozi jambo la kwanza ni kujilimbikia pesa.Kwa hiyo sio swala la wahindi tu na hicho kitu sijui kama kitaondoka wananchi tutabaki kusema tu na nina uhakika na haohao wanaosema wakiipata chansi wataitumia vilevile.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 25, 2008

    Anonymous wa 12:07 PM, Samahani lakini usiseme kitu ambacho huna uhakika nacho. Mimi naishi Canada na huku bwana ukienda kwenye nyumba za serikali wengi wanaoishi ni wageni kwa sabau wao ndio wenye vipato vidogo. Watu halisi wa Canada wengi wana vipato vizuri kwa hiyo kwao wao it is not worth it kuishi kwenye nyumba hizo. Tatizo la nchi yetu Tanzania ni system mbaya na mbovu tulionayo. Too much corruption kila tunapokwenda mpaka kwenye ofisi za mabalozi wetu nchi za nje.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 26, 2008

    kwanza kaka pole sana kwa mkasa wa nyumba na wahindi kwa ujumla mimi naungana na wewe 1oo% inauma sana. mimi sikai tz ila naijuwa ile nchi haidhamini raia wake bali wageni na tatizo la wahindi haliko ktk nyumba tu bali kila kona kinachouma wao huwa hawapangi foreni ktk sehemu za huduma kama vile hospital,polisi na kwenye ma ofisi ya aina zote hapo nchini zinazotoa huduma za watu. hatakama ni msomi akimuona muhindi anampitisha bila kujali nani alianza kufika. huu ni ushamba na upumbavu na kutotembea kwa ujumla muhindi ni mtu kama yeyote yule ktk kuchangia maada hii ameniudhi anaefurahiya tabiahiyo ya wahindi kutoa rushwa na kuwaona hawana makosa. nakama walikuwepo tangu mwanzo bona hajuwi lungha za hapo?? pili mbona mtu mmoja utamkuta anauraia wa nchi tano??? wakienda kusachiwa ktk wahindi kumi mtanzania anaweza kuwa mmoja tu wengine wote wahamiaji tena na uraia wao ni wakifisadi.tena nawaomba wahindi wote wajiheshimu waache kutoa rushwa kiholela wanachangia kutuharibia nchi zetu, wao wako mjini mguu mmoja ndani mmoja nje wanajua vurungu zikianza wanaondoka na kutuachia vurungu hawa si raia wema na kama ni raia wema na wao wakajenge huko mbweni kwani hela wanazo wamekaa ki uharibifu tu. mtoa ruhwa na mpokea rushwa wote wanamakosa.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 26, 2008

    Hao wadosi wanaoishi kwenye zinazofahamika kama nyumba za Asajile Mwaijumba nao ni Watanzania kama wewe Mdigo. Tofauti ni kuwa Wadigo mnapendelea kumiliki nyumba wakati wadosi hawana noma kuishi maghorofani. Kwa hiyo akiingia humo hatoki na atafanya kila namna kukutoa mswahili kwa sababu kwa miaka atakayoishi mle hicho kidogodogo atakachokupa kinalipa.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 26, 2008

    Mimi ni mhindi na naomba niwajibu wanaolaumu wahindi.

    Nyumba hizo nyingi za NHC zilijengwa na wahindi na sio waswahili.Jasho la wahindi liko kwenye hizo nyumba.Baadaye serikali ilitaifisha.Sasa wahindi kukaa kwenye nyumba zilizojengwa na wahindi wenzao kuna tatizo gani kama kodi wanalipa?

    Mtu ajitokeze hapa aseme hayo maghorofa mengi ya NHC kama yalijengwa na waswahili aseme hapa.Acheni kabisa kuwaonea wahindi.

    Nyumba zetu za familia zetu zilinyang`anywa na serikali halafu sisi tukageuka wapangaji na bado tunalipa kodi hivi hamna shukrani tu?

    Mnachukua nyumba zetu halafu mnatugeuza wapangaji tunalipa kodi za kupanga bila kukwepa halafu bado mnatutukana na matusi juu.Hii shukrani gani Hii?

    Fikria wewe kama nyumba ya baba yako inachukuliwa kwa kutaifishwa halafu wewe unaachwa bila nyumba unakuwa mpangaji na kodi unalipa vizuri halafu unatukanwa na kutukanwa.MBAYA SANA.
    Wahindi waweza kuwa wabaya lakini hili wanaonewa.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 26, 2008

    wewe unaejiita mhindi,nakwamba nyumba zilijengwa na wahindi je unaweza kutueleza vizuri tukaelewa kama wahindi hao waliingia pale na kiasi gani? cha fedha?

    wahindi walijenga na bado wanajenga lakini mali zao zote si harali ni rushwa na wizi na ndiyo maana walitaifishwa na si wahindi tu bali hata weusi

    wahindi wanaingiza hasara kubwa sana ktk serikali kama ni mhindi mfanyabiashara basi ataleta mizingo yake bandarini na hataripa ushuru

    wanakuja bila hela wanatoa rusha wanapata uraia harafu wanaomba mikopo bank wanajenga nyumba hiyo inaitwa ni wizi wa kuaminiwa na ndiyo maana zikataifishwa waliambiwa kila mmoja aeleze njinsi alivyopata mali zake wakashidwa na ndiyo maana nyumba zikachukuliwa na serikali

    tena walikuwa wanauwa tembo wetu ndiyo maana mwalimu mzee wa hekima akawastukia
    walikuja na machacha rumba la kwao limewapinga wakifika wanakaa kidongo wanafanya biashara haramu leo hii walijenga nyumba hela walipata wapi?

    mimi siwachukii wahindi bali nachukizwa na na tabia ya mtu yeyote mpenda rushwa nawaomba tena wahindi waache rusha wafanye mambo halali.

    hata mkapa hivi sasa watu wanamjadili juu ya makaa ya mawe unadhani nae ni mhindi??

    rushwa sio nzuri nyie wahindi na wote wapenda rushwa jiheshimuni jamani ifanyeni dunia ipendeze kama hamsikii mtakimbizwa tena mana watu hawafurahi na hizo tabia za kuwafanya hawana hakili

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 26, 2008

    HEBU NENDENI MKAFANYE KAZI ACHENI POROJO HAPA.

    KAMA MNATAKA NYUMBA KAJENGENI ZA KWENU, EBO!!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 26, 2008

    watu mmeandika insha...looh...au ni novo?embu kalaleni!

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 26, 2008

    MIMI NASUPORT NYUMBA ZA MSAJILI NA ZA WATUMISHI WA SERIKALI, HUSUSANI ZA UPANGA NA MASAKI.
    ACHENI TU WAPEWE WAHINDI. KWASABABU WANAPEWA KWA AJILI YA KUISHI NA WANAISHI KWELI. SIO WATANZANIA WANAPEWA HALAFU WANA ABUSE THE SYSTEM. WANAZIPANGISHA HIZO NYUMBA AMA FLATS. INAITWA KU "SUBLET" WOTE TUNAJUA SUBLETTING IS ILLEGAL. WANAPANGISHA KWA PESA NYINGI ZAIDI YA WANAZOLIPIA PANGO TBA AU NHC. KAMA KWA MFANO HAPA KWETU MASAKI BLOCK B, FLAT 2, CHOLE ROAD. MWANAMKE MPANGAJI, KAIPANGISHA HII FLAT AKITAMBA SASA INAMPATIA PESA ZA KUPATA MTAJI. NA AKITAMBA KUWA "KIMWERI" WA TBA NI SWAIBA WAKE KWAHIYO HATA TUKIREPORT HATOFANYWA KITU, ANAKUSANYA TU PESA.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 27, 2008

    NYUMBA HIZO NYINGI NI ZA WAHINDI WENYEWE ZILIPOTAIFISHWA WALIPEWA PRIORITY YA KWANZA KUPANGA, PIA HATA ZILI ZINGINE WANAZOKAA WAHINDI PENGINE HAZIPANGWI KWA MAJINA YAO NI ZA WATU WEUSI WAMEPANGAISHA WAHINDI KWA BEI YA JUU UKIENDA NHC UTAKUTA JINA LA MMATUMBI SI LA MUHINDI, PIA BEI ZA NYUMBA ZA BONGO NI KUIGA KBEI ZA ULAYA HUWEZI KUJENGA NYUMBA TANZANIA YA VYUMBA VIWILI KWA MILLIONI MIA MBILI NI UOGONGO MTUPU NI KUIGA TU HASA BAADHI YA WATANZANIA WALIO MAJUU WANAJENGA VIJUMBA TANZANIA NA KUIGA WAYAONAYO ULAYA SI KWEILI KABISA NYUMBA YA VYUMBA VITATU TANZANIA IGHARIMU TSHS 300,000,000.00

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 28, 2008

    Sasa naanza kuona "true colours" za watu wanaojiita WaTanzania.
    Aliyeandika hii mada naona kabisa ni "Racist" na ana mawazo mabaya sana ya "Kiracist". Pia Michuzi wewe kui-pokea hii mada na kuibandika ili ijadiliwe kwa aina fulani naona una-support kwa mbali sana mawazo ya "Racist".
    Acha kabisa kujadili racism hapa katika website yetu uungwana. Tumeshaona haya sana hapa USA na sasa wameacha wenyewe kwa sababu suala ni "economy". Kama una complain za kutokupata nyumba ya kupanga "Uhindini" basi kapange Hyena squre- mazense, Sinza, mbezi, kiwalani,kipunguni nk.
    Maana ukianza hili la wahindi utakuja na waarabu, then wapemba, then wachaga, then wa-islam , then wanajifanya wasomi, then ohohoooo, waliosoma nje.
    Soma historia ya hayo maghorofa, then elewa nani aliyajenga, then NHC ilianzishwa vipi na kwa nini, then nani walipata haki ya kuanza kukaa pale na jiulize kwa nini walikaa pale au kwa nini wanapenda kukaa pale.Culture ya wahindi imefanya wakae pale na wenzao pamoja na biashara zao.
    Hawa walikimbia vita vya uhuru wa INDIA mwaka wa 1947 na partion ya pakistan ilipozaliwa taifa huru la india na wengi kuja TZ. walikuta mifumo ya kikoloni iliyowapa mianya ya kujeenga nyumba hizo na kuhimili biashara.
    Nakuomba uache uracist wako kwani
    nyumba zile ni ndogo sana kwa vyumba na wanakaa lukuku mle ndani.

    ReplyDelete
  35. Wabongo tucheni unafiki,
    To be honest waindi its too much!....wakwepa kodi wao,wadhalilishaji wa wafanyakazi wao,biashara za magendo pia wamo, na hata kwenye EPA si tumeona wakina patel!!!!hivi tunawatetea kwa uhindi wao au kweli hatuoni ubaya wao kwa uchumi wetu? RACISM OR NO RACISM.....Indians are a threat to our oppotunities.
    But there are wahindi weusi...our leaders! bila wao waindi weupe wangekula vipi? Wao nao wamejiuzia nyumba za SERIKALI na kujigawia haki kuuubwa ya utanzania huku wakiukana uzalendo kwa matendo yao...la msingi kabla hatujadeal na mlevi tumshugulikie muuzaji wa hicho kilevi lakini ili kumpata huyo muuzaji lazima tumsute mlevi atuambie kanunua wapi(if u get my meaning) so tuanze kwa wahindi ila tuendelee kwa ndugu zetu wanaowalinda hao mabingwa wa rafu kwenye uchumi wetu..WACHA KWETU WAPANGE WATAJENGA KWAO INDIA
    King Kris.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...