Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2008

    Unafananisha Kifo na Usingizi? Huyo Mugabe anachemsha.Kaanza vema sasa anajifanya yeye gwiji kuliko hata UN. Ujumbe kwa Ndugu zangu huko Zim... Msiwe na wasi, it is just a matter of time. nani alitegemea Inzoka wa kinubi au Nduli atatoka? Sadam kaopolewa kama kambale. Msife moyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2008

    KWELI KAZI IPO? ILA WATAKAO UMIA NI WANANCHI WA HALI YA CHINI.MUGABE WHY, KWANINI?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2008

    Ujasiri alio nao Kikwete kumkaripia Mugabe, leo Mugabe ametoa majibu "Mwenye mkono msafi kati ya viongozi wote wa AU amnyooshee kidole". Kweli sisi tunaweza kumsema Mugabe wakati Zanzibar watu wamenuniana na kuapa haingii mtu ikulu. Tofauti na Mugabe iko wapi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2008

    Hakuna nchi iliyowahi kuharibiwa kiuchumi Africa kama Zimbabwe, hata Iddi Amini na Uganda ina afadhali.

    Bei ya mkate ni zaidi ya Zim Dollar millioni moja......Lahaula Lakwata!!!!

    Sasa hivi viongozi wa Africa wanashindwa kusema ukweli direct.....au ndio kulindana kulekule kwa kusema MWENZETU!!!
    Na msemo wa "Ukiona mwenzio ananyolewa na wewe tia maji"


    Mhhhhhnnnnnn.....Haya, lakini Mandela kesha sema ukweli Mzee haogopi mtu!!!!!


    Jongwe ataishia Mahakama ya Kimataifa kwa anayofanya lazima ashitakiwe tuu!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2008

    Hakuna kitu hapo!AU yenyewe imejaa kina 'Mugabe'wangapi?Usanii tu kibao!Kwa kweli Afrika tunatia aibu.Tutamponza hata mwenzetu Obama apimwe kwa matendo ya viongozi wetu bara la Afrika.Haya,mwenzake wa MDC Morgan kajitoa kabaki yeye mwenyewe Mugabe lakini bado anakwambia Uchaguzi uko pale pale!Mgombea kabaki mmoja yeye peke yake,wazimbabwe watamchagua nani?Huyu Mzee kesha kuwa chizi siyo?Napendekeza AU wampe Mugabe Uenyekiti wa AU wa maisha,Make Mugabe AU Chairman For Life!Mwacheni afie kwenye Meza,si anapenda ukubwa!Umeshindwa kufanya kitu miaka 28 leo hii ukiongezewa miaka mitano utaweza kitu?Hiyo miaka mitano mingine atakuwa na umri wa miaka 90!Anatembelea mkongojo!Kisa,ukubwa!Zimbabwe hivi sasa imezungukwa na nchi zote huru,atakacho singizia nini?Zimbabwe ivamiwe na nani?Huyo mpinzani wake Morgan Tsvangirai kweli haipendi nchi yake awe kibaraka kiasi hicho ambacho Mugabe anataka kutufanya tuamini?Basi hata mrithi wake mwenyewe kutoka chama chake akosekane?Haya ni matunda yetu wenyewe.Kinachotendeka Zimbabwe kipo pia hata hapa nchini Tanzania,tusidanganyane!Tugeuzeni Mambuzi tu,iko siku yatawatokea puani!Afrika ingekuwa na Viongozi safi na sio wanafiki Mugabe angekuwa kesha achia ngazi siku nyingi!Uchumi wake ungekuwa bado imara na watu wake wngekuwa salama zaidi.Kuondoka ataondoka tu apende asipende!Yeye pamoja na huo mlingoti alioushikilia(obsolete ideologies) vyote vitang'olewa na kutupiliwa kwa mbali watoto wetu wasije wakaipata kasumba hiyo!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 27, 2008

    MUGABE,STEP OUT OF POWER PLEASE..UMEZEEKA..ZIMBABWE NEEDS DAMU CHANGA,USIWAFANYIE HIVYO BWANA!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 27, 2008

    Ukiangalia kifaru anavyo muangalia Dume la ng'ombe (zagamba)kwa makini inaonyesha atamfua kwelikweli.Jongwe hilo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...