Michuzi na wadau wote,
Mjadala kuhusu imani katika ndoa umesisimua sana. Nawapa hongera mtoa mada na wachangiaji wote. kwa kweli nimejifunza mengi kama ambavyo nina imani wadau wengine pie wamefunuka macho kwa mengi.Ushukuriwe Michuzi kwa kuweka mada kama hizi kwenye blogu yako ya jamii ambayo kwa hilo na mengineyo mengi sio tu imejidhihirisha hii kweli ni blogu ya jamii, bali pia huna mshindani.

Sasa naomba nami kuwakilisha ombi langu kupitia blogu hii hii ya jamii kuomba mawazo yao wadau wenzangu. Naomba msidhani natania. hii inatokea hivi sasa laivu....

Wadau, ni kwamba mama mkwe wangu kahamia nyumbani kwetu tangu january mwaka huu na ni kama amefika kwani haonyeshi dalili za kuondoka. Yeye anaelewana sana na mwanae, ambaye ndo mke wangu mpendwa.

Swala ni kwamba tangu huyu mama afike hapa anapenda sana kuzungumza na mwanae hata baadaye usiku. Niwaambie wadau kuwa sina shida na mke wangu, ila naona huyu mama mkwe kidogo anaanza kuwa kero, nami kusema lolote kuhusiana na hilo naona sio sahihi, kwani huyu pia ni kama mzazi wangu.

Nitangulize kusema kwamba huko kwake mama mkwe hana shida ya pesa au maisha. Tunamtumiaga pesa, na yeye pia anazo zake. Anachopenda zaidi ni company ya mwanae mpendwa mke wangu. Sasa wakuu, what should I do?

Mke wangu naye naona haoni kuwa kuna ka-distance kanaanza kujengeka kati yetu in terms of intimacy - You know what i am-saying...

MDAU WA MOSHI MJINI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2008

    Wewe kama mwanaume ina bidi upige moyo konde na umwite mkeo pembeni umueelezee yote yanayo kusumbua kuhusu mama mkwe wako na kila kitu kama unataka ndoa yako idumu.ukiwa umekaa kimya na unavumilia yote hayo yatakusumbua moyoni kiasi cha kwamba unaweza ukafanya jambo ambalo litakuaribia ndoa yako .

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2008

    USHAURI WA BURE,YASIJE KUKUTA YALIONIKUTA MKUBWA WAKO,BABA MKWE ALIKUJA AKANIAMBIAMBIA HARAKA SANA MRUDISHE MAMA MKWE WAKO KWAKE,KAMA UNAIPENDA NDOA YAKO,UKICHELEWA NDOA YAKO ITAVUNJIKA,KAMA ILIVYO VUNJIKA YAMIMI NA MAMA MKWE WAKO,NA KWELI BWANA ALIPOONDOKA MKWE TU,MAMA TABIA IKABADILIKA GHAFLA,HUYO ANAPEWA SOMO,AMBALO SIO ZURI KWA NDOA YENU,HARAKA MTIMUE NA MWAMBIE MKEO FAMILIA YENU NI YEYE,WEWE NA WATOTO,WAZAZI MTAWAHESHIMU KAMA WAZAZI NA MTAWAPELEKEA MSAADA HUKO ALIKO EBWANA UKICHELEWA UTAMKUTA MTOMTO SI WAKO MTIMUE CHAPCHAP!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2008

    aha, tatizo dogo, ila una moyo mdogo na wa uungwana ndio maana una hangaika.

    1.Mweleze tatizo mke wako na ajue kuwa huna nia njeam unataka joto lake tu, so tafuteni mbinu amabayo haitakuletea ugomvi kati yako na mama mkwe.

    2.Kwa hiyo tafuteni kitu cha ku mkeep bize, ili nyie wawili muwe pamoja.kama TV,mtafutieni mikanda mizuri.

    3.au mtoto ajifanye ana kakozi fulani amabako inabidi awe bize kidogo.

    KUMBUKA MAMA MKWE ASIJUE LOLOTE

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2008

    pole sana mwanawane, hii tabia hata mie siiungi mkono. kumwambia aondoke huwezi, ukisema uwe unachelewa kurudi home atachonga mdomo hadi basi, na wewe mlete mama yako humo ndani. game inakuwa ngoma droo...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2008

    Au na wewe dini tofauti na mkeo nini? ndo maana anataka kusababisha ka distance.

    Vinginevyo, huwa wa-mamawakwe wanatamani wakati mwengine.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 26, 2008

    weeee mpare nini? acha uchoyo. Kama mke hakupi penzi ndo umeambiwa sabb ni mama mkwe? Muombe akuonee huruma.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2008

    bila uyo mama mkwe ungempata mwanae,ni vibaya mtu akikaa na mwanae,pumbavuuuuuuuuuuuuu,mim nakaa pia na mama mkwe lakin hakuna tatizo lolote,jifunze kupenda ndugu.
    ina maana uyo mama mkwe uwa analala na mwanae chumba kimoja?
    heshimu mama mkwe kijana,jifuze kujali siyo unajiangalia wewe tu.
    mama mkwe ni kama mzaz wako,
    kwan ni vibaya ukihish na mama yako uku umeoa.
    kijana kuwa na eshima

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2008

    pole sana huyo ndio mama mkuu. ninakushauri uangalie filamu ya "mtoto ni haki ya nani" iliyotungwa na afro-dance group. inaweza kukusaidia kupata jibu la tatizo lako.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 26, 2008

    Mzee,hilo soo.Bila kuremba huu unaitwa wivu.Na mapenzi bila wivu hayajakaa sawa.....Technique ni kuwa unaanzisha utani then unachomeka kuwa ungependa kuwa na mkeo pekee kila utakapojisikia hivyo.Na ufanye mara kwa mara....Hii ni bora kwani ukiiendea kirasmi rasmi,utasababisha tension ambayo yaweza kuleta dhana mbaya..Then,baada ya muda muulize mkeo muda ambao mama atakaa hapo.Kuwa straight mwambie unampenda mkwe ila si mipangilio yako kuishi naye milele.
    Goodluck.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 26, 2008

    Pole sana, lakini binafsi ninadhani ni suala la kuongea na mkeo. Sasa swali, kama mama kahamia hapo tangu januari, mumewe kamuachia nani? Ongea na mkeo alione hilo kwa kuwa anawapa wote mateso wewe pamoja na mumewe aliyemuacha nyumbani?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 26, 2008

    POle mdau kwa tatizo unalolikabili, ukweli ni kwamba mimi nilipoona tu kero ya mama mkwe nikajua huyu atakuwa mwanamke anamlalamikia mama wa mwenziwe kumbe ni mwanababa analalamika! mh! kwa mara ya kwanza.

    Sasa mdau usianze kuleta wivu na mamkwe wako . we kaa na mkeo mueleze unampenda sana na unavyojisikia unapomkosa kipindi unamhitaji, pia mkumbushe wajibu wake na aweze kubalance mapenzi yake kwako kwa watoto na kwa wazazi. Mueleze unampenda mama na unamuheshimu kama mamako ila kuwe na kiasi kipindi unapokuwepo awe mwangalifu juu ya hilo, naamini kama utamweleza kwa heshima atakuelewa, ila ukitumia amri na kiburi a.k.a ugomvi, ujue utaharibu kabisaaaaaa.kumbuka huyo ni mzaa chema kwako.

    ReplyDelete
  12. Ndugu yangu pole sana

    me nakushauri jaribu kuongea na mkeo wako tena utoke nae mbali mwambie kwa uzuri na umwambie unakosa uhuru hata mapenzi ya kweli kwake kwani kama unavyojua ndoa ushamili popote sio kwenye kitanda tu mahala popote asipo kuelewa mfuate mama yako wewe au baba yako wewe wamfuate kayemba mwenzao watamwambia madhara ya kukaa kwa watoto muda mrefu lakini jitahidi sana uwe na subira kwa kipindi hiki bila hivyo ndoa itabomoka ndugu yangu kwani nahisi mkeo anamwambia mama yake kila kitu hata mapenzi yenu.....

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 26, 2008

    ASSALAM ALEIKUM, NDO MAANA MIMI NAUPENDA UISLAM,MAANA UISLAM UMEJENGEKA AIBU, AU HAYA MTU UKIKOSA HAYA SI BINADAMU. PALE NI KWA MKWE YEYE KUKAA MUDA WOTE HUO ANATFUTA NINI TENA ISITOSHE ANAKAA MASAA KIBAO ANALONGA NA MWANAE HATA USIKU, HAONI KAMA ANAMHARIBIA MWANAE NDOA. HUNA HAJA YA KULEMBA MWAMBIE MWANAE KWAMBA ANAVUNJA HAKI YA NDOA NA KWAMBA UNA MMISS SANA NA KWAMBA UNAMPENDA PIA MAMA MKWE ILA KUE NA MIPAKA YAANI MPENDWA WENU NYOTE WEWE NA MAMA MKWE WENU AHESHIMU KILA MTU MUDA WAKE, UKIWA KAZINI ALONGE TU MAMA AKE MUDA WOTE UKIRUDI MZEE NA WEWE NAFASI YAKO KUJINAFASI. MWAMBIE DINI NDIVYO INATAKA MAANA NDOA BILA TENDO LA NDOA HAIPO TENA. AKIZIDI BADILITABIA ANZA KURUDI UMECHELEWA HATA KAMA HUFANYI CHOCHOTE ILA PITIA POPOTE KAA SANA RUDI USIKU MNENE AKIHOJI MWAMBIE HOME HUNA KAMPANI UFANYEJE??? KAMA KWELI MAMA MKWE ANAHAYA NA MKEO ANAKUPENDA ATAJIREKEBISHA. VINGINEVYO KAMSHITAKI KWA BABA MKWE AU UMUAMBIE LIVE, KUOKOA NDOA YAKO.

    WASALAAM MZEE WA BUNJU

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 26, 2008

    Na mimi sijui nikuiteje? Mswahili wewe tena wewe si mchaga maana moshi tunaishi wote hapa na hapo, wewe kinachokusumbua ni kimoja tu: UMASIKINI anza kuhangaikia maisha yako ukae njema we ungekuwa una nyumba kubwa kama yangu ungekuwa na upande mkubwa wa mama mkwe na wewe na binti yako upande wake tena miminimechukua baba yangu mama yangu na mama mkwe wangu (Baba mkwe mishe nyingi hajatulia bado) na naishi kwa raha (ofkozi gharana nene) ila raha sana. UMEKIRI MAMA MKWE HANA CHOCHOTE zaidi ya kupiga stori na bintiye, we hiyo inakusumbua nini maaana km mjanja si unalala samoja afu satano unaamka unakuta mamkwe kaaangusha we unalianzisha n a mkeo, rejea ratiba tu huna haja ya kuwa mswahili kama wanavyokufunza wenzio eti kaa na mkeo muongee, utaanzia wapi? Uchoyo tu huo au umasikini. Nashukuru nimepewa na sijivunii ila naelewa ambaye hajapewa anaumia namna gani

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 26, 2008

    KAMA HANA SHIDA HAPO NYUMBANI SHIDA YAKO NINI??SI UMWACHE AKAE MPAKA ATACHOKA...ATAONDOKA MWENYWE...AU NIKUPE MBINU...YA YEYE AONDOKE?FANYA HIVI...SIKU WAMEKAA WOTE SEBULENI WEWE MFUATE MKEO ANZA KUMPIGA KISS YA MDOMONI MBELE YA MAMA MKWE..ATASIKIA AIBU NA ATAONDOKA MWENYEWE..WACHAGGA WANAOGOPA SANA HIYO KISS YA MDOMONI

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 26, 2008

    oyaa unyumba sii ngono tu. huyu bwana hana muda wa kuongea na mkewe juu mamkwe kachukuwa huo muda.unless kama huyu mkewe ni wale wa yes sir basi kazi. subiri!! nauliza mke wangu juu ya huu mkasa akaniambia alikeni watu babako mamako au shangazi.hope itasaidia

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 26, 2008

    COMMUNICATION-ndio jambo la msingi, kitu kinasumbua ndani ya nyumba TALK ABOUT IT, ongea na Mkeo Kiustaarabu bila kuvunja Heshima yake wala ya Mama Mkwe,tumia baadhi ya maoni ya watu humu yanayoweza kukusaidia changanya na maneno yako mawili matatu mwanangu, mambo yatakuwa mswano.jaribu pia kutoka na mkeokama wkend hivi, ili mpate muda wa kuongea na mai waifu wako..

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 26, 2008

    acha uoga mama mkwe sio ndugu yako ni ni mtu mzima mwenzio tu so mwambie anakunyima nafasi au la waende nae bush mkeo mpaka imuishe ndio amrudishe.kwanza kukuaa nae ni mambq ya hatari kwa kuwa kilicho wakutanisha na mkeo yeye pia anacho

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 26, 2008

    Veri veri Simpo,

    Kwani wewe ni Mshika dini sana???????

    Kama sio kwa sana, nakushauru changanya wote tia kibindoni,

    Kuku ni chakula kama ilivyo mayai yake nayo ni chakula,

    Hata muhogo ni chakula kama ilivyo majani yake (kisamvu) nayo ni chakula,

    Ila angalia Mmewe asijue,

    utakosa vyote,


    NI HAYO TU!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 26, 2008

    kaka mimi nimekuelewa sana ila naomba usipanic huyo ni mkeo na yule ni mama yake wape mda. naomba uvumilie tu au na wewe kama unae mama yako mlete nawe uwe buzy nae tuone mkeo atachukuwa uamuzi gani

    ujuwe watu tunatofautiana sana hata mimi napenda kua na mme wangu mda wote kama hatuko kazini sasa tena kama kunamtu ataichukua ile nafasi yangu sitafurahi japo sitamuonyesha.

    au kama unauwezo azisha tabia ya kumtoa auti kila ukirudi kazini akipata banana wine mbili kwa huko moshi najuwa zipo akirudi yeye mwenyewe atakuvutia chumbani bila aibu hatakama juwa halijazama hatajivunga!!

    na mama mkwe kama nia yake ni kukaa basi mzalieni watoto mapacha alee sio zambi wala nini utamzoea na utampenda sana ukimkuta anacheza na mapacha wenu.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 26, 2008

    pole sn kwa ajili ya hy mamkwe, sasa hebu chunguza historia ya huko kwako maaana kuna kabila 1 kama mama mshirikina lazima ampe mtoto wa kwanza mkoba sasa huwezi jua huo usiku huyo mama na hy mtoto wanafanya nini. asije akawa anampa mkoba na kitu hicho si kizuri kabisa. ila kama wewe ni mcha mungu unaweza kusali na kumwomba mungu eemungu niepushie huyu mama mkwe atoke katika nyumba yangu tena unafunga kabisa kwa kusali na atakoka. ama sivyo atakuharibia nyumba hata kama unampenda sisi ni binadamu hatuna mapenzi kabisa tunauma na kupuliza pole sana

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 26, 2008

    kwani huyo mama mkwe mumewe yupo? kama hayupo basi inabidi uelewe kuwa ni mpweke, na kama unasema kuwa fedha sio tatizo basi ujue kuna kitu hapo kwani huyo ni mtu mzima na mara nyingi kama akili zake ni timamu kuna makusudi hapo.usikonde ngoja nikupe ushauri,kulingana na jinsi ulivyo eleza hapo juu kuwa hata usiku mkubwa yeye bado anaweka kiwingu nahisi kama anakawivu fulani hivi kwani anahisi unafaidi mambo fulani.kwani kama ingekuwa sio hivyo angeweza kutafuta mshikaji lakini inaonyesha niya yake ni wewe kwani kuna uwezekano kazungumza na mwanae kuhusu mambo fulani ya kitandani ikaonekana kuwa kaka wewe hujambo.najua unaona kama hatari fulani hivi lakini hayo mambo yapo kaka, kwani unadhani waswahili wanavyosema kuwa kuna kula kuku na vifaranga vyake unadhani huwa wanazungumzia kuku?


    Mbega hapa

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 26, 2008

    Mdau Mbega; wee sio mchezo kaka naona umeamua kuikandamiza kama ilivyo yani kwani naona wadau wengine wanazunguka zunguka tu wakati issue iko wazi hapo. oya wewe mdau wa moshi mjini inabidi ufanye kama Mbega alivyo kushauri, wamarekani wanasema Touch down

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 26, 2008

    Polee sana, lakini hilo ni swala dogo sana, kwanza mueleze mkeo then kamuweke sawa babamkwe wako (yaani baba wa mkeo)kama hayupo weka chini mkeo na mama yake wape fact maana ndio dawa pekee ukiendelea kukaa kimya itakucost maana yaweza fika maala nawe ukatafuta pa kupumzikia (aka nyumba ndogo) na kama uko smart unapaswa ujue nini kimemleta mamamkwe na pia ni jambo gani hasa wanazungumza. Sifa mojawapo ya mwanaume ni kuwa intelligent na kuweza kusoma na kutafsiri circumstances. Binadamu hawaaminiki na inawezekana kweli akawa na nia chafu kama mdau aliyetangua alivyosema (Naye amekutamani) lakini hata kama ndivyo lakini hakuna justification kimila wala kidini. SO TALK TO THEM.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 26, 2008

    NIMERUDI TENA, MAANA NIMEFURAHISWA NA WACHANGIAJI. BWANAE UBAYA UBAYA TU, SIKU MOJA CHUKUA MKANDA WA NGONO ANGALIA KWA SANA ALAFU TOKA NA BUKTA NYEPESI WAKATI BAGDAD IMESIMAMA MWITE MKEO MBELE YA MAMA KWE ILI AJUE KWAMBA UNAENDA KUMALIZA KESHI, NA HAKIKISHA UNAMLIZA KWA SANA MAMAA, MPAKA ASIKIE YEYE MWENYEWE ATAAGA KESHO YAKE TU

    MZEE WA BUNJU

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 26, 2008

    Jaribu kuwa unachelewa sana kurudi nyumbani kwa siku kama 10 nadhani kwa namna ya kawaida mkeo itabidi akuulize hapo message itakuwa imefika na kitaeleweka.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 26, 2008

    ***** LISTEN TO ME*****

    Kaka , kusema kweli hayo ni majaribu makubwa sana. hata hao wanaozungumza hawajafikwa! kwa wengi kama wamewahi kukaa na wakwe si zaidi ya mwezi, tena kukiwa na sababu maalum kama ya ugonjwa n.k.

    USHAURI: 1: Tafuta shemejiyo mmojawapo, mwenye akili na uelewa mzuri,ambaye mnaelewana vizuri. Mueleze akuelewe, then muombe aongee na mkeo bila kusema kuwa umehusika. Hapa rafiki wa mkeo pia anafaa.ila asiseme ametumwa.

    Baada ya yeye kusema na mkeo, lazima mkeo atakueleza "eti fulani kasema....." hapo sasa na wewe huwi streight kusema ni kweli hupendi, ukisitasita tu mkeo atajua kuna shida but at least hana uhakika! so she will take action kwa kumwondoa ma-mkwe.

    USHAURI: 2: Tafuta nduguyo mkubwa ambaye yuko Idle au anayeweza kukaa kwako walau kwa mwezi mmoja. mpe issue nzima na mwombe akae. hata mjomba/shangazi/ma-mkubwa .... n.k. yaaani hili lazima lilete ugomvi. then wewe una-rule out kuwa... "hapa ni kwetu na watoto wetu tu" ndugu ni kwa emergency tu.

    nitakupa zaidi km hizi mbili hazitafanikiwa.

    PD

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 26, 2008

    sizani kama kunatatizo tena kama kweli ulikuwa nalo kwani ushauri umesha pewa hapo juu, kwani ujue kama kuna unachokipenda au unachokifaidi kutoka kwa mkeo basi hata mama mkwe anacho kwani anasema kuwa "she got from her mama". na napenda kukutadharisha kuwa mama mkwe akiona kama unajifanya uelewi kinachoendelea atahisi unamchora. kinachofuata hapo ni kukubadilishia kibao kwa mkeo kwa madai kwamba unajaribu kumtongoza

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 26, 2008

    Naomba kaka Michuzi uyaweke haya maoni yangu. Nimeumia sana na maoni yaliyotolewa hapa. Inaonekana wengi waliotoa maoni hawajakomaa kiakili na wanahitaji kufundwa. katika hali ya kukomaa huwezi hata siku moja ukamshauri mwenzio alale na mama mkwe wake eti kwa vile kaja kumtembelea na anaongea sana na mwanaye. Je hawa wanaotoa ushauri huu wanaweza kulala na mama zao? Maana tusiangalie upande wa mke tu. Mimi mama mkwe wangu mzaa mume wangu ana mwaka sasa nyumbani kwangu na anapenda kuongea na mwanaye hadi usiku kama wa mwenzetu sasa nawauliza hao waosha vinywa kwamba nimshauri mume wangu alale na mama yake kwa vile wanaongea naye sana hivo anamwonea wivu? Au baba wakwe wakija wakiongea sana na watoto wao wa kiume na sisi wanawake tuwape uroda?
    utajisikiaje utakaposikia mkeo anampa uroda baba yako mzazi?

    Tuwe wastaarabu jamani. Wazazi wote ni sawa. sio mzazi wa mwanamke akija kwa mwanaye inakuwa kero ageuzwe chakula na mume wakati wazazi wa mume wanapokuja mnawaona kama malaika. Kwani kulala na wake zenu kuna mwisho? mbona mnajifanya mnauhanga sana nyie? wakati hao hao wake zao wakikaa nao siku mbili mfululizo ugomvi ndani ya nyumba na kero kibao. Hapo hakuna lolote mnaloshauri cha maana ni kumwambia mtoa mada aongeze adabu na heshima kwa mkwewe apate thawabu. Huo ndio uvumilivu na hizo ndizo ndoa za kiafrika. Msijifanye mmekaa nje sana hivyo mnataka maisha ya kizungu bado hamyawezi hii ni bongo land tu. Ukiona mkeo anafaidi sana kamlete mama yako uishi naye ili uwe unaongea naye.

    We anon wa june 26 12:41 a.m Mwanamke hawezi kukuacha kwa sababu ya ushauri wa mamake ni matendo yako yalikuwa ya ovyo ndio maana umeachwa usilete visingizio vya kitoto. Na huyo baba mkwe wako hana akili timamu ndio maana alikwambia umfukuze mama mkwe wako. Unategemea umfukuze mama wa mkeo halafu mkeo akuchekee chekee tu. lazima akuonyeshe kwamba umekosea kwa kubadili tabia kidogo. na siku nyingine usirudie. nenda kaombe msamaha kwa mama mkwe wako uliyemfukuza.

    Nyaugu

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 26, 2008

    Shemeji Nyaugu, hivi mama wa mumeo anakaa kwenu mwaka mzima huyo mumewe kamuachia nani? Au ndo wamegombana akaamua kukimbilia kwenu? Huyo baba mkwe wako unadhani anawafikiriaje? Sikia, huyo mama wa mumeo, mama mkwe wa jamaa tunayemzungumzia na wengione kama wao ni wapuuzi. Hawawezi akaacha ndoa zao wakaja kuishai na watoto zao. Kusalimia wiki mbili tatu au hata mwezi ni sawa, lakini kuhamia zaidi ya mwezi ni kero kwa walikohamia na wanaume waliowaacha numbani au hata wadogo zenu ambao wapo bado nyumbani wanahitaji uangalizi na muongozo wao. Watu hawa si wa kufumbiwa macho. Mambo haya mnayaona madogo lakini ndo chanzo cha kushuka mapenzi kwenye ndoa na kusababisha watu waanze kutembea nje na kusababisha maambukizi ya ukimwi endelee. Chukulia mfano, baba mkwe kaachwa mwaka mzima hapati huduma (tendo la ndoa) muda wote huo, unadhani atafanyaje? Apige Nyeto, hapo si lazima atatafuta sehemu ya kupoza? Kinachofuata unadhani itakuwa nini?
    Mama yangu hawezi kuja kaa kwangu mwaka na kumuacha baba nyumbani muda wote huo, mimi nitakuwa wa kwanza kumuelewesha na kumueleza aende nyumbani kumhudumia. Hii si kukosa nidhamu ni kufahamu wajibu wa mume na mke na wao kama wazazi. Kama mama mkwe ana matatizo na mumewe, arudi nyumbani wakayatatue inginevyo ataleta matatizo kwa mwanawe pia. By the way, kasha sababisha shida ndo sababu tunajadili suala hili. Kueni ndugu zangu, mficha maradhi kifo muumbua.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 26, 2008

    Kweli BUBU wameamua kusema leo:

    ukisoma maaoni yaliyotolewa utagundua kuwa watu wana vinywa vichafu mno;

    kwa utamaduni wa kiafrika huwezi lala na ma-Mkwe.

    Nyie wachangiaji mnaotoa ushauri huo, muogopeni ALLAH,(Mungu) kwani yeye anawaona na maoni yenu yasiyofaa.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 26, 2008

    Huyu jamaa kukaa Moshi haina maana ni mchaga. wamama wa kichaga hawakai kwa watoto wao wa kike, hata kina baba, wakija ni kusalimia na kama kaka wa binti yuko mitaa hiyo wanaomba wapelekwe kulala huko!My dad never sleep in my house hadi akafariki, mama yangu anakuja akikaa sana ni less than a week, anaomba aende kwa ndugu zake wengine mi nafanya kumtembelea. kwa mila zetu ni mwiko. hawakai kabisa.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 26, 2008

    MICHUZI MIMI NIMEOLEWA NA MAMA MKWE WANGU HUWA AKIJA ANAONGEA NA MUME WANGU MPAKA USIKU WA MANANE ALMOST DAILY. KAMA SIVYO MUME WANGU ANAKUWA AMETOKA NA WASHKAJI ZAKE. nIKIJARIBU KUONGEA NA MUME WANGU ANANIAMBIA KUWA KAMA SI MAMA YAKE NISINGEMPATA. HUU USEMI UNAMAKE SENSE SASA KWA HUYU JAMAA. NA IWE KAMA FUNDISHO KWAKE, AM SURE THERE IS A LOT MORE THAN ALICHOSEMA. ISIJE IKAWA KWAMBA MAMA WA JAMAA HUWA ANAKUJA HALAFU WANAMTREAT MKE KAMA MVAMIZI NA MAMA NDIO MWENYE NYUMBA HALAFU LEO HII KAJA MAMA WA MKE ANAONEKANA MZIBAJI. NI KWA PANDE ZOTE BABA NDOA UVUMILIVU, UKIPENDA BOGA UNAPENDA NA MAUA YAKE.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 26, 2008

    sijui ni kwanini wabongo hawapendi kuwa wazi, naona mtu akisema ukweli basi wanasema hajakuwa kiakili, mpumbavu, unakinywa kichafu,mara humuogopi mungu.kwani ni nani hajawai kusiki mama na mwanae wakigombea bwana?. Kama kweli mama mkwe anajieshimu inakuwaje hata saa za manane hataki kuwapa watu nafasi ya kijivinjari?. kuna mambo kibao ambayo mila na desturi zinakataza lakini mnayafanya sasa ni kwanini mnakuwa wakali kwenye hii kesi ya kanga

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 26, 2008

    Hahaha, Mbega Mbega Mbegaaaaa!
    umenisababishia kufua kwa kicheko! blaza hujatulia

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 27, 2008

    Nachopenda kukuambia ndugu yangu mama mkwe ni sawa kabisa na mama yako mzazi anastahili heshima kam mama yako. Halafu hujajaribu kutatua tatizo likashindikana unaanza kulalamika hiyo si tabia nzuri.Hilo ni kosa la kibinadamu tu .Mweleze mkeo kwa upole bila JAZBA wala HASIRA tena kwa utulivu mkiwa wawili chumbani kwenu.Naamini mkeo si nung'aembe ni mwanamke mwerevu sana atakuelewa tu brooooo.ACHA KULETA MAMBO YA KUKU NA NA MAYAI YAKE KWANI NYIE MNAFIKIRI UKIMWI UNABIPIWA????????MTAKUFA SIKU SI ZENU EBOOOOOOOO.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 27, 2008

    NYIE MNAOSEMA, KUKU NA MAYAI YAKE ITS OKEY, HIVI KWELI, BABA YAKO MZAZI ANGELALA NA BIBI MZAA MAMA YAKO?!!! UNGEYASEMA HAYO?? Ndio Dunia imeharibika ya ajabu yanatokea but PLEASE!! Kwa hiyo nyie mnaweza kabisakulala na WAKWE ZENU.Mungu tubariki.

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 27, 2008

    Jamani mkisikia mahali fulani kunaharibiwa shamba la Bangi, jihadharini msisogelee karibu, ikiwezekana hama mji mpaka zoezi limalizike. Maana kuvuta bangi si lazima uivute huku umeishikilia vidoleni mwako na kupiga pafu, hata ukivuta tu hewa pale inapoharibiwa kwa wingi waweza athirika, sasa hao wanaotoa hadithi za kuku na mayai yake humu bloguni wajue walipitia hako kamoshi si hasha, maana hizi kauli ni za kibangibangi hivi, na hayo matendo ya kuchanganya mpaka mamamkwe ni za watu walio na akili mbovu, na hata kama ni mila flani tuache madhara yake makubwa.
    Kama unataka kutoa msaada kwa mwengine, tafuta busara za kumsaidia, sio utani wa kufurahisha wengine na kukosa kutoa msaada unaopaswa, Mimi masikio yangu yameniwasha nikitafakari mashauri baadhi humu hayana msingi zaidi ya kuburudisha wachache wenye hulka za kupenda kuzungumza upotovu.

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 27, 2008

    humu tunasoma sasa wewe iweje masikio yakuwashe, au mwenzetu wewe unasoma kwa masikio? na kama unavyo dai wewe kuwa kutowa maoni ya mrengo wa kulia(kuku na mayai) ni akili ya bangi basi inamanisha yeyote yule anaeujua usemi huu,au aliewai kuusikia,au kwa waliouwanzisha wako kwenye kundi la wavuta bangi au kuwa karibu na shamba la bangi. sasa sijui kama wewe ulishawai kuusikia au unaujua huu msemo jibu unalo mwenyewe na tunaomba ujichagulie mwenywe kundi. au tunaomba utupe mfano mwingine unaouwelewa wewe kuhusu kula kuku na mayai yake tofauti na ulivyo elezwa hapo juu. na kama unaona huwezi basi ushike adabu yako wewe mwana mtoka pabaya

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 27, 2008

    Hiyo ni united wachaga kama utaki shauri yako hapa ukienda Wales tamaduni nyingine, same to Scotland na Ireland ila wote ni....

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 28, 2008

    Jamani hili swala si mchezo kwa kweli wengine humu majibu yao wanajibu tu ili mradi wameandika.Tatizo la wakwe ni sugu sana kwa familia zetu za kiafrika na siyo wazazi wa kike tu hawa wa kiume ndiyo balaa tena sana unakuta mzazi anangangania kuamia kwa mtoto wake wa kiume eti aje awalee hiyo klweli inakuja?na wakati anawatoto na wajukuu wa kulea hapo ukiuliza unaambiwa toka mwanangu ameowa hanipi pesa kama zamni sasa ngoja nikakae huko ili nione pesa inaenda wapi mammbo ni mengi sana katika ndoa hizi na ndiyo maana unapofunga ndoa unaambiwa utaachana na wazazi wako utaambatana na mkeo.Ushauri tu ni kwa wazazi wetu tuwaache watoto wakishaolewa au kuoawa waishi maisha yao na ubakie upendo sio kila siku kiguu na njia kwa watoto kumbuka wameanzisha familia nyingine hao mamambo ya kwenda kila siku kwa watoto kuna siku hata nyama ikipungua ndani utaanbia alikuja mama yake hapa kachukua nyumbani kulikuwa hakuna chakula hayo si matusi sasa na ukitaka kukaa kwa raha na familia yako mambo ya ndugu yaweke kando lakini ukuiyafuata utachanganyikiwa hauwezi kumrithisha kila mtu ukaweza

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 28, 2008

    Unapomwita mwenzako mwana mtoka pabaya nataka nikuulize wewe ulitokea wapi pazuri tukawatolee na sisi watoto wetu? ila matokeo ya hapo ulipotoka wewe tunapatafakari kutokamna na domo kaya lako linopenda maneno machafu, kelba mkubwa mwanahizaya wee.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...