Home
Unlabelled
mambosasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
duh kaputura haikuchanika kweli???aisee..mwanasarakasi huyu..bwana michuzi naomba utuamie kama huyu baba yupo hai au vipi,tungependa kumfanyia mchango wa kifedha sisi wanajumuia wa turkey
ReplyDeleteMakipa wa zamani walikuwa viboko! Walikuwa wanadaka bila kuvaa gloves.
ReplyDeleteHii picha inanikumbusha enzi hizoo! Tukuwa tunakusanya picha za mpira na katuni ya Chakubanga na kuzibandika kwenye vitabu vya simu kwa kutumia gundi ya minyaa.
ReplyDeleteSahihi Au Utomvu wa Michongoma na List Nzima ya Team Zote Ipo Kichwani
DeleteHii ni moja ya picha za kuvutia ninazozikumbuka. Kama si marehemu Ernest Millinga basi atakuwa ni Vicent Urio aliyepiga picha hii. Kaka yangu na mimi tulipenda kukusanya picha na kuzibandika kwenye kitabu kikubwa. Tulizipaka rangi pia. Asante kaka Michuzi, umenikumbusha mbali sana!
ReplyDeleteWe misupu mzuri. wapi Papaa Juma Mensa Pondali kufa kwaja? Hiko ndio kilikuwa chuma....Muulize Ben Kiko.
ReplyDeleteebana nilikuwa sijui kama minyaa inatowa gundi,sisi tulikuwa tunazibandika kwenye madaftari kwa kutumia gundi/urimbo wa michongoma au mikorosho.Nakumbuka nilikuwa na mapicha kibao hasa wachezaji wetu wa kibongo sio kama mitoto ya siku hizi inakuwa ikijali mpira na wachezaji wa yuropa.
ReplyDeleteAthuman Mambosasa ni marehemu, hatunaye tena
ReplyDeletepicha hii sitaweza kuisahau maisha yangu yote.siku hizo tulikuwa tuna kusanya picha toka gazetini halafu tunabandika kwenye daftari.
ReplyDeleteNaikumbuka sana picha hii, kwani enzi hizo tulikuwa tunakusanya cuttings za magazeti na kuzibandika katika daftari, namkumbuka sana MAMBOSASA alikuwa rafiki sana wa kaka yangu, alikuwa mtanashati, siku za mwisho alikuwa Namibia na alirudi akiwa na afya si safi hadi alipofariki, mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, AMINA.
ReplyDeleteAH WAPI BWANA, SIDHANI KAMA YUPO KULIKO MWAMEJA. YULE JAMAA ALIKUWA KIBOKO YA WOTE HATA MAMBOSASA(MAREHEMU) MWENYEWE ANGEKUWAPO ANGEKUBALI HILO NASEMA. ILA BAADA YA MWAMEJA NI YEYE,THEN MAHADHI(BIN JABIR),HALAFU IDDY PAZI(FATHER)NA WA MWISHO KASEJA.KUNA JAMAA MMOJA NAE ILA SI MTANZANIA ANAITWA MAKENZIE RAMADHANI NAE ALIKUWA HATARI GOLINI.
ReplyDeleteHamna chochote. Makipa wote wa siku za nyuma (Mahadhi, Pondamali na Mwameja) walimzidi Mambosasa.
ReplyDeletehii ilikuwa kilele cha soka tanzania, julai 10 1974 simba ilikuwa timo bora siku hiyo, dakika za mwanzo mshambuliaji wa simba saad ally na marehemu gibson sembuli waligongana na ssad ally akapoteza fahamu na kupelekwa bugando, kabla ya kipndi cha kwanza kumalizika elias michael na willy mwaijibe wakagongana nao wakapelekwa bugando hospital, willy alivinjika mkono wa kulia nadhani elias alipoteza fahamu (concusion) cha ajabu sembuli aliendelea kucheza nae ndio aliyewakoa yanga kwa kusawazisha 1-1 katika muda ziada (stoppage time) wakaendelea overtime ndio sunday manara akafunga bao la ushindi ikawa 2-1 nadhani bao la simba lilifungwa na adam sabu.
ReplyDeleteKwa kweli enzi hazirudi, na siku hazigandi.
ReplyDeleteKaka Michuzi leo umeitengeneza siku kwa jinsi usivyojua wewe mwewnyewe, Kaka enzi hizo ilikuwa ni balaa, hamna maneno yatoweza kutosheleza, we acha tu.
Hapo simba, kipa mambosasa , 2 Shaban baraza, 3 Mohamed kajole, 4 Athumani bin Juma 5 aloo Mwitu, 6 omari Gumbo 7 Abasi Dilunga, 8 Haidari abeid, 9 Adam Sabu, 10 Abdallah Kibadeni, 11 Saadi Ali A.K.A WATAKIONA, Kumekucha hapo, Nyamagana vumbi mpaka kwenye Tuu.
ReplyDeletemdau wa saa 10.03 nakusahihisha kidogo kwani mimi ni Lunyasi damu damu, Omari Gumbo kipindi hicho alikuwa bado hajajiunga na Simba na namba sita(6) alikuwa Khalid Abeid akicheza na kaka yake Haidar Abeid namba nane(8).waarabu wa Shinyanga mjini hao baba yao alikuwa akimiliki Zam Zam hotel enzi hizo hapo SHY.
ReplyDeleteCha chandu - UK
Huyo kakosea sana, hapo kipa Mambosasa beki baraza beki kajole, katikati Bin Juma na Chogo, Six Khalid Abeid , wingi Willy mwaijibe wingi Saadi Ali, nane Haidari tisa Sabu na Kumi Kibadeni.
ReplyDeletehalafu kulikuwa na picha moja maarufu sana inayo muonyesha Willy Mwaijibe akipiga mpira kwa kichwa huku Kitwana Manara akimzinga,ukiiona picha hiyo utafikiri kitwana anataka kumtia dole Mwaijibe.Jee,mnaikumbuka?.Halafu naomba kuuliza,ni wachezaji gani wa enzi hizo ambao sasa ni marehemu?
ReplyDeleteHapo Mambosasa ana bonge la Hirizi kiunoni, nakumbuka enzi hizo mechi ya simba na yanga lazima kuna watu wanabebeshwa Majini yakigongana ndio hapo sasa
ReplyDeleteAAAh wazalendo mumemsahau kiboko yao!!!!? "Juma pondamali mensah" huyo ndio kiboko yao.by mlalahoi
ReplyDeleteAnonym wa june 28,2:09pm..Enzi hizo za picha ya Mambosasa yule Pondamali alikuwa "ananyonya ziwa" acha ushabiki.We are talking about real stars!
ReplyDeleteList ilikuwa kama ifuatavyo.
ReplyDelete1.ATHUMANI JUMA MAMBOSASA
2.SHAABANI BARAZA
3.AHMED KAJOLE
4.ARTHUR MWAMBETA
5.OMAR CHOGO
6.KHALID ABEID
7.WILLY MWAIJIBE
8.HAIDARI ABEID MCHACHO
9.ADAM SABU
10.ABDALLAH KIBADEN(KING KIBADEN)
11.MARTIN KIKWA.
Hii ni orodha ya Simba toka mwaka 1974 mpaka 1976.pia hawa ni Simba waliofungwa na Yanga 2-1 mwaka 1974 uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza pia mkitaka orodha ya Yanga iliyofunga Simba 2-1 Nyamagana nitaidondosha mkiomba. MIMI MNAZI MKUBWA WA SIMBA TOKA USA.
"Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni",the best goalkeeper in Tanzania panga pangua piga ua ufe ni IDD PAZI"Father".huyu jamaa ndo aliwapa Simba Hilo kombe huko juu la Afrika mashariki na Kati pamoja na ubingwa wa bara.Hao sijui akina Mambosasa,Mahadhi,Pondamali,Mwameja hakuna kitu just story tuu.Idd Pazi ndo alikuwa golikipa sijaona bongo.
ReplyDeleteCha Chandu - UK
MNAZI MKUBWA WA SIMBA WA USA!Umechemsha kwa sana tu! Martin Kikwa hakucheza Na akina Kibaden.Namba 11 alikuwa Abbas Dilunga.Mwaka 1974 Martin Kikwa(RIP) alikuwa kinda,yeye alikuja kucheza na akina George Kulagwa in 80's.
ReplyDeleteCha chandu - UK
chachandu acha kuchemsha mnazi wa Simba yuko sawa miaka ya 80 Martin Kikwa hakuchezea Simba ILA ALICHEZA MIAKA YA SABINI
ReplyDeletekwa taarifa yako martin kikwa(RIP) hakucheza nyamagana no 11 alikuwa Saad Ally siku hiyo, baada ya kuumia Saad aliingia Kessi Manangu kuchukua nafasi yake, no 4 siku hiyo alikuwa Athumani Juma sio Arthur Mambeta. Martin Kikwa alijiunga na Simba 1975.
ReplyDelete