Bro michuzi,


Lukwangule hapa!


Nakuletea hii picha niulizie kwa wadau wa mambo ya urembo!Jamani nambieni huyu anayeshiriki Miss Leisure World huko China anayeonja chai ya Suzhou (wa pili kutoka kulia) ni nani walahi ?


Hata sijui nani maskini lakini picha hii ninayo. Jamani wadau nani kapeleka mtu huko anaweza kunambia huyu nani na anafanya nini hasa?


Nimeambiwa na mdau mmoja kwamba kuna washiriki wapatao 76 kutoka nchi 70 duniani ambao ni warembio haswaaa wakimsaka Miss Leisure World hii si miss Universe. Mbona nimechanganyikiwa Lukwangule, wadau huu ndio unaitwa msaada katika tuta lakini si kwa dizaini ya Mbagalkka unaweza kuvunja miguu.


Hili ni shindano la kwanza na tayari tuzo ya kwanza ya kutabasamu (Miss Smile),imeshanyakuliwa na Sarah Katrina Miñoza wa Ufilipino. Uholanzi na Venezuela waliibuka wapili na watatu.Sarah Katrina Miñoza ana miaka 23.


Mshindi wa shindano hili anaondoka na kitita cha dola 10,000 na taji.
Waandazi wamesema Miss Leisure 2008 atapatikana Juni 27, 2008.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2008

    Edna Audax Kayozi? Never heard of her. Never-the-less good luck out there! Wakilisha to the fullest!
    http://www.missleisure.com/contestants.php

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...