mdau leo allan kalinga akiwa na mai faza wake pamoja na mai maza wamenivamia ofisini kutaka kujua mustakabali wa tawi la liverpool la bongo a.k.a bongoreds a.k.a bwawa la maini. nami ikabidi nimpe ukweli wa tulikofikia hadi sasa.
1. rasimu ya katiba ipo tayari na itakadiliwa katika mkutano mkuu wa kwanza ambao utaitishwa karibuni kwa wanachama wapatao 200 waliokwishaleta majina na maelezo yao
2. baada ya kupata ridhaa ya wanachama wa tawi hilo la bwawa la maini la bongo, uongozi wa muda utatuma hiyo katiba na miniti za kikao huko anfield kwa usajili rasmi.
3. baada ya wanachama hao 200 waanzilishi kuwezesha bongoreds kusajiliwa rasmi kama tawi la liverpool, mchakato wa kuandikisha wanachama utaendelea hadi muda utaokubaliwa na mkutano kabla ya kuitisha uchaguzi mkuu wa kwanza.
aidha, mdau leo alitaka pia kujua nini faida ya kuwa mwanachama wa bongoreds. nikamjibu
a. ni kuunganisha wanachama wa liverpool wenye asili ya bongo popote walipo duniani
b. kupata nafasi ya kufurahi ama kuhuzunika pamoja wakati wa gemu za liverpool ambapo kutakuwa na shoo rasmi kwenye kumbi mbalimbali. hapo memba anaingia bure ama kwa gharama nusu ya kawaida
c.kuhamasisha wadau kupenda michezo na umoja michezoni bila kujali wadhifa ama hali ya mtu. aidha siku ya mechi ya taifa stars bongo reds tunaingia kwa pamoja na kushangilia kwa sauti moja. hapo utakuta hata meneja ama afisa mkubwa akiimba kidedea, na sio kuwaachia kina muchacho peke yao. (na bahatri nzuri muchacho pia ni liverpool damu na wameshajiandikisha uanachama
Mdau Leo naomba kuwasilisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2008

    Good stuff, brainwash them from that very young age then they will be slaves for life. But we should remeber this and be prepared to answer some tough questions from some of these babies, as those of conscienceness will ask one day. Why did you wrap me up on this obsene outfit?
    My idle were people who looked like me, lived the life I live and within my reach. Here Im not talking of Pele, Tigana and Eusubio, but Juma Mkambi, Athumani Chama, Omary bin Jabir Mahadh, Kajole, Pondamali na wengineo.....;
    Natamani kuendelea kuandika lakini wakati mwengine kumfundisha mwanamke malaya aache kupanua miguu kwa kila mtu si kazi rahisi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2008

    hivi michuzi una watoto wewe?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2008

    Hako katoto kana sura nzuri kweli!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2008

    Sasa we anon wa kwanza unaongelea nini?
    Hivi umesoma hiyo 'comment' kabla hujaituma?
    Andika taratibu, kwa kituo, ueleweke.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2008

    Mama yake Leo anani-remind of other girl.
    Mdau, mtoni mashine ya maji.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2008

    Acheni kumfanya mtoto mtumwaa,kwa nini msivalishe jezi ya simba au yangu?bwawa la maini litamsaidia nini mtoto?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2008

    @ Ann. # 1, sijui unazungumzia nini maaana... ila Hukuwa na mfano mwingine mpaka umuongelee MWANAMKE??? kwa nini huwa mnapenda kuongelea vibaya wanawake kila siku na kila mahali halafu mnasema mnawapenda MAMA ZENU NA KUWAHESHIMU????!!!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2008

    kuna watu makanwa yao hayajatulia kbs,,wee anoni nam 1,,,uongee mapointi apa sii ugolo huo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2008

    Wewe anonym wa June 24,5:49pm nakusikitikia sana.Sitaki kuifananisha akili yako na Kinyesi!Kama watoto zako watachukua akili zako basi umekula hasara.Unalo lizungumza tofauti kabisa na maudhui ya picha iliyo tolewa hapo juu.Sijui ndiyo kwanza unajifunza kiingereza au ndiyo kwanza umetoka kubalehe hakika sijui ni lipi.Kati ya Mwanamke na Mwanamme Malaya ni yupi?Mwanamme kifimbo cheza asiyetosheka na mwanamke mmoja kila siku kiguu na njia utamwitaje?Yupo Mwanamke wa kufunua funua mapaja kama hayupo huyo Kifimbo Cheza mwenye shetani la Ngono?Kijana unapo andika humu ujue wapo Baba zako na Mama zako watakao soma huo Ulimbukeni wako!Kumbuka Mdomo uliponza Kichwa!Ulimi ni Mali ukijua kuutumia.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2008

    Alichoongea huyo anony #1 nimekielewa vizuri kabisa. Ingawa ameshindwa kujua kuwa watu wengi wanaoingia kwenye "forum" hii ni wa uwezo mdogo wa kuelewa na ndo maana ameshindwa kuandika ujumbe wake ili uweze kueleweka na hadhira hii.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 26, 2008

    Nawapenda watoto sana. Familia msivunjike moyo na maoni ya huyo wa kwanza. Mlilolifanya ni zuri, kuweni wamoja.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 26, 2008

    Aliyeandika huo ujumbe hapo juu ni mwanaume anayemwona kila mwanamke malaya including his mother, otherwise asingemalizia hiyo point yake na kauli kama hiyo, ninashangaa sna pale mwanamke tu ndio anahesabiwa malaya wakati uzinzi hafanyi mwenyewe kuna malaya wa kiume wamejaa tele na ndio hao wanaolala na hao malaya wa kike. kwanini usimalizie hizo pumba zako na kauli hii
    " Kumfundisha mwanaume kitombi kuheshimu ndoa yake ni kama kumpigia mbuzi gitaa" wanawake hatufurahii kuwa mfano wa kila baya duniani, tuna mengi mazuri ya kuigwa!
    Michuzi usiibanie post yangu am telling the truth.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 26, 2008

    Nawashukuru na kuwapongeza wanawake na wanaume pia wanaoikemea tabia ya kutothamini wanawake, Sisi ndio Mama zenu, mkikimbiwa na Baba zenu tunahangaika na nyinyi mpaka mnakua, mkipigwa mnaita Mamaaa,mkishajiona mmekuwa wanaume Mtukana na kudharau wanawake, kuweni na Busara, hamna heshima na wanawake kwa nini?? Kina dada kina mama Msikae kimya mnapoona utovu wa nidhamu unavuka mipaka.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 26, 2008

    woh woh woh . mnasahau la msingi hapa huyu dogo yuko reading accademy nabaada ya miaka mitano atalamba ganda jekundu. utamu na uchungu unakuja sasa, dual nationality iko wapi ???? angalieni waturuki jana wana mtoto muingereza chelsii wanamjua. hatutakaa tufike huko kama bunge halipitish dual. tumefungwa juzi kila mtu anadai tuanze kuuza wachezaji nje. wanaonunuliwa nje ni yosso nawakifika huku wanapewa uraia. mjiulize wenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...