Mheshimiwa mbunge wa Tegeta bwana Michuzi na wadau wote.
Mimi sijambo wa afya, sijui ninyi?

Nawaomba mnipe ‘BIG TOUGH’, namtafuta rafiki yangu ambaye vilevile ni shemeji yangu, kwa jina Dr. IKONJO. Nimepoteana naye toka mwaka 1983, mara ya mwisho kuwa naye ilikuwa huo mwaka tukiwa BONGO, mimi nikaenda zangu masomoni majuu, na yeye mwaka huo huo akaishia Poland. Sijamsikia wala kumtia machoni tena.

Ningependa kokote atakapokuwepo, au kwa yeyote amjuaye ampe habari hizi, kuwa I miss him tooo much, tuwasiliane haraka itakavyo wezekana. Mimi sikama nina shida, lakhasha ila naona muda umefika wakurudisha mbuzi zetu zizini. Ujumbe wake: C. Msuya na I. Mshanga wote hawajambo.

Mimi naitwa Dr. Mdimu Charua Ngoma, niko Manchester, UK, nitakuwa hapa kwa kakipindi kadhaa. Shukurani.

Mtakao taka ripoti za msimu mpya wa premier.ligi ya UK, tuwasiliane wadau wangu. Na tungefurahi sana kama tungelitembelewa na mbunge wetu wa Tegeta, Mheshimiwa I.Michuzi (Umetusahau wapiga kura wako wa Manchester, unaishia London tuuuu, karibu sana, unakosa mengi kutoka hapa).

Mbunge, mpatie Ikonjo na wengineo watakao hitaji hiyo e-mail yangu:
mfumwa@yahoo.com.
Ahsantee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2008

    inamaana kama ni shemeji yako basi hata dada yako hujawasiliana nae au?kama kweli hujawasiliana nao wote basi usisumbuke kwani wameuchuna wanaona unawajazia
    inzi tu

    Mbega

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2008

    Ngoma wa pyschiatric rudi Muhimbili,madokta haba kwenye hicho kitengo. serious! rudi mzee.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 25, 2008

    Na wewe umezidi upare ndio maana wakaona huna dili...ina maana walivyokuwa na shida wakaomba msaada ukawashit sasa ndio unawaulizia?na wao wamesema hawataki basi...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2008

    I bet the correct spelling of the guy's name is Ekonjo if it is the same distant relative of mine I think it could be and he may well be living in Poland. I personally don't have his contacts and my advise would be for you to trace him by making direct contacts with his closest relatives. His elder sister lives in Dar Es Salaam - whom you ought to know since she is your shemeji too and with cousins scattered all over the globe, he shouldn't be hard to trace. This is just light advice as due to data protection rules I am unable to divulge any contacts and I believe Michuzi will be constrained too.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2008

    al musoma acha kujifanya msomi bwana,kama huwezi kumsaidia sema,sio unaanza eti data protection and all that.man stop that

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 28, 2008

    THank you so much for your active blog that releases latest newz,actually unatakiwa kupongezwa, miye ni mdau wako mkubwa ila sijafurahia hata kidogo kwa leo kuona blog yako haina hata habari za vijana wetu wa copa coca cola wanaofunika, hasa wa Kg ambao wamefunika bongo kwa kandanda lao la kutisha, mbona hutoi hata pongezi ili wadau wa kitanzania walio majuu waweze kutoa mchango wa kuinua soka Nchini? hafu nimeamini kweli MUNGU hawezi kumnyima Binadamu vitu vyote, Unajua kigoma, Imenyimwa Umeme, maji shida sana ingawa ziwa lipo jirani, barabara ndo usiseme ukufika utalia, usafili wao wa kutoka ni tren, lile lilobinafisishwa na muhindi, ambalo kwa sasa watu wanajazana - ukiingia mle nadhani utalia machozi, na hutaamini, kama chombo cha kusafilia.

    Lakini cha kujivunia Sir God kawapa vipaji lukuki, watoto wanasukuma kandanda, bila shaka we ni shahidi.naomba mwambie Tinoko, asidhani dar kuna kitu aende magharibi-Kg, hao ni wachache tu ambo kocha amewaona, wapo vijana wengi wanaosukuma kandanda kule, hafu hata wadau wanaofungua akademi za michezo waende Kgm, watapata vipaji vya kuuza nje na hawataamini- itawalipa tu.

    nakutakia siku njema.
    by mdau.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...