Watanzania wajasiriamali waishio
Uingereza mnakaribishwa kwenye mkutano hapa Ubalozini,
3 Stratford Place ,
London
W1C
1AS.
SIKU: Jumatano 2 Julai 2008
Muda: Saa 12:00 Jioni
Msemaji: Omari Issa ambaye ni Chief Executive Officer wa Investment Climate Facility Taasisi inayosimamia uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji Afrika.(kwa kiswahili:Afisa mkuu mtendaji wa Taasisi inayosimamia uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji barani Afrika
Wahusika: Watanzania wanaojiajiri au wale wenye miradi midogo midogo wanaoifanya hata kama wameajiriwa.
Wale mtakaopenda kuhudhuria Tafadhali mnaombwa kujiandikisha kwa kutuma barua pepe kupitia dilunga@tanzatrade.co.uk ama msanjila@tanzania-online.gov.uk
Pia mnakaribishwa kuja kujiandikisha ubalozini.
Chabaka Kilumanga
Naibu Balozi
ubabaishaji umeshajitokeza hapo hapo. kwani ubalozi hauna barua pee ahdi watumie anwani za binafsi?? Ni dalili za kukosa commitment kweny ehilo jambo au labda waandaaji sio ubalozi bali wao ni ukumbi tu.
ReplyDeleteTuwe serious ili na wengine washiriki kwa ukamilifu. au itauwa mahali pa upata kilaji na kusalimiana na kuondoka?????
Ubalozi u-take initiative na yatumike mawasiliano rasmi ya ofisi hiyo ili kujenga imani kwa washiriki.
Kama ni issue ya kuja kunywa na kupiga picha wengine hatuna nafasi. kama ni issue serious yakujadili ujasiriamali na uwezeshaji tupo tayari kushiriki.
Mshirii mtarajiwa.
Wazo ni zuri sana. tafadhali wahusika tujulisheni ajenda za mkutano na madhumuni yake pia na nini kinatarajiwa baada ya kufanyika huu mkutano.
ReplyDeleteam no happy.mimi nipo Uk na nilidhani naweza nikauhudhuria,sina biashara maana sina mtaji,so i need this kind of seminars to motivate me,ni vipi hapo mrs.balozi?unatuangusha!
ReplyDeletewe nawe anon wa 2,ndio maana mkaambiwa muende kwenye huo mkutano..
ReplyDeleteKWENDENI ZETU, BAADA YA KUSEMWA NA UBISHOO WENU, MNATAKA KUALIKA WATANZANIA WANAOISHI UK SASA? KAMA ALIVYOSEMA MDAU HAPO, MMECHEMSHA TENA. KWANINI MSIALIKE KILA MTANZANIA BASI? HANA MTAJI KWAHIVYO HANA BIASHARA YOYOTE. NA HAPA MMEWAITA ONLY WAFANYA BIASHARA ETI HATA KAMA WAMEAJIRIWA NA WANAFANYA BIASHARA NDOGONDOGO.
ReplyDeleteSHAME ON YOU PEOPLE. KAENI NA UBALOZI WENU.
I don't think this was a right or good place for such an advert as you know here people can say
ReplyDeleteanything, why not posting it in you web/the emabassy web. Also I have an issue with your embassy web, I want to register as a Tanzanian in UK but I could not go through, please activate you web as some people have no time to come physically to the embassy's office..
Anony 1 kasema very sensitive issue ambayo inataka itizamwe kiundani.
ReplyDeleteWhy mtu shughuli ya kikazi atumie private address na sion official address ya kikazi? Hiyo ni sawa na kuweka pesa za ofisi kwenye account yako binafsi........je inakubalika?
Pili, nadhani ubalozi ungelifanya la maana sana kama ungealika Watanzania wote na kuweka bayana agenda ya ualikaji huo.....ili mtu aone je kuna umuhimu wa kuhudhulia aou la?.........sio kufanya kama walivyokurupuka kualika watu tu na watu waende bila kujua linaloenda zungumziwa
Tuache ubabaishaji na tufanye kazi kama Professionals tukiwa tunaelewa njia muafaka za kualika watu ili kufanikisha nia ya kuwaalika
Mwakyembe ang`aka
ReplyDelete2008-06-26 11:58:27
Na Boniface Luhanga, Dodoma
Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harisson Mwakyembe, amewashambulia vikali wabunge wa chama hicho wanaojaribu kuwasafisha watuhumiwa wa ufisadi kwenye mkataba wa zabuni ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.
Dk. Mwakyembe alisema kama wabunge hao wanadhani kuwa kamati yake iliwaonea watuhumiwa hao, anapendekeza taarifa ya kamati yake itenguliwe na kurejeshwa tena Bungeni ili ijadiliwe upya na kwamba iwapo wataonekana waliwaonea, yeye na kamati yake yote, watajiuzulu ubunge.
Hata hivyo, ameonya kuwa, kama itabainika kuwa kweli walihusika, basi watuhumiwa hao nao lazima waachie `ngazi` mara moja katika nyadhifa zao walizonazo sasa.
Alitoa shutuma hizo bungeni jana wakati akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2008/09.
Huku akionekana dhahiri kukerwa na suala hilo, Dk. Mwakyembe alisema kumekuwepo na ujanja- ujanja wa kujaribu kuwasafisha watuhumiwa hao kwa kutaka kuonyesha kwamba, tume yake iliyochunguza kashfa hiyo, iliwaonea.
``Wanajaribu kuwasafisha, unawasafisha nini? Nchi hii siyo mabwege,`` alisisitiza.
Dk. Mwakyembe alisema inavyoelekea, baadhi ya wabunge wamechukulia maamuzi ya tume iliyoundwa na Bunge kuchunguza mkataba wa kampuni ya Richmond kama vile yalikuwa ni yake yeye Dk. Mwakyembe.
``Hapana, yale hayakuwa maamuzi ya Mwakyembe, bali yalikuwa ni ya Bunge hili. Tunajidhalilisha sisi wenyewe mbele ya wananchi licha ya kwamba mwanzoni tulianza kupata heshima,`` alisema.
Kauli ya Dk. Mwakyembe imekuja siku moja baada ya Mbunge wa Buchosa, Bw. Samuel Chitalilo (CCM), juzi kuibuka bungeni na kuwatetea watuhumiwa wa ufisadi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mkataba wa zabuni ya kampuni ya Richmond.
Mbunge huyo aliyewahi kutuhumiwa na baadhi ya wapiga kura wake kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliopita wakidai kuwa alitumia vyeti vya kughushi kupata nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea pia aliwatetea Rais mstaafu, Bw. Benjamin Mkapa kuhusu kuhusishwa kwake na kumiliki mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.
Pia aliwatetea Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge anayedaiwa kuhifadhi dola milioni 1.2 katika akaunti iliyoko kwenye kisiwa cha Jersey, nchini Uingereza ikituhumiwa kwamba huenda `mgao wake` katika sakata ya ununuzi wa rada ya bei mbaya .
Aidha, kauli ya Dk. Mwakyembe, imekuja siku chache baada ya mbunge wa Same Mashariki ( CCM), Bi. Anne Kilango Malecela kutoa wito kwa wabunge wa CCM kusimamia kidete bila woga kuwabana mafisadi waliochota fedha za EPA waweze kuzirejesha.
Hata hivyo, kwa kile kilichoonekana ni kama kumjibu Bi. Kilango, siku iliyofuata, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bi. Anna Abdallah, alisema suala la EPA lisiwagawe wabunge wa chama hicho na kwamba hakuna anayeogopa kulizungumzia ila wanatofautiana namna ya kuwasilisha ujumbe.
Kamati iliyoundwa na Bunge kuchunguza mkataba wa zabuni ya kampuni ya Richmond, ilikuwa chini ya Mwenyekiti Dk. Mwakyembe.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo ambayo baada ya kuwasilisha bungeni taarifa yake, ilijizolea sifa kem kem siyo tu kwa Wabunge bali pia kwa wananchi wengi, ni Bw. Lucas Selelii (CCM-Nzega) na Bw. Herbert Mntangi (CCM-Muheza).
Wengine ni Mhandisi Bi. Stella Manyanya (CCM-Viti Maalum) na Bw. Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni).
``Hatuwezi kila siku kuongelea hayo hayo? Kwenye magazeti pia ni hayo hayo, tumechoka. Wanaacha kuzungumzia maendeleo ya kwenye majimbo yao na kujaribu kuwasafisha,`` alisema Dk. Mwakyembe.
Alisema anapendekeza suala hilo lijadiliwe upya na Bunge na wabunge waseme yote wanayoyaona kuhusiana na sakata hilo lakini pia yeye na kamati yake, watayasema yote hata yale ambayo waliyaacha kwa lengo la kulinda heshima ya serikali.
``Naapa, kama tuliwaonea, tutawajibika na kamati yangu, lakini kama nao watathibitika kuwa walihusika, wajitoe katika nyadhifa zao,`` aliongeza.
Naye Mbunge wa Sikonge (CCM), Bw. Said Mkumba, alipingana na baadhi ya wabunge wa CCM wanaowataka wenzao wasilizungumizie suala la ufisadi bungeni.
Bw. Mkumba alisema ni wajibu wa wabunge wote kuhakikisha kwamba wanakemea kwa nguvu zao suala la ubadhirifu wa fedha za umma.
Alisema kama mtu hataki kusemwa, basi asiibe fedha za umma na akae katika misingi ya uadilifu na kwamba pasipo kulisemea suala hilo, ni sawa na kujidhalilisha wabunge wenyewe na wapiga kura wao.
Awali, Mbunge wa Kyela, Dk. Mwakyembe aliishauri serikali kuhamisha kitengo cha maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na kukipeleka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Alisema hiyo inatokana na jinsi alivyowaona askari wa JWTZ wakifanya kazi ya ujenzi wa daraja baada ya jimbo lake la Kyela kukumbwa na mafuriko miezi kadhaa iliyopita.
Dk. Mwakyembe alisema JWTZ huitika haraka pindi yanapotokea maafa tofauti na urasimu uliopo katika kitengo cha ofisi ya Waziri Mkuu.
``Hakika nilivutiwa na utendaji wa JWTZ tofauti na makandarasi wa kawaida ambao huchukua muda mrefu kufanya upembuzi yakinifu peke yake.
``Makandarasi upembuzi yakinifu huchukua miezi, lakini JWTZ siku moja tu na ujenzi wa daraja siku tatu,`` alisema.
Aliiomba serikali kukihamishia kitengo hicho cha maafa JWTZ na kupendekeza kwamba, baadhi ya askari wastaafu warejeshwe kukiimarisha kwa kuwa bado wana utaalam wa kutosha.
People you have issues. Why do u rush to complain, even before the event has taken place.
ReplyDeleteYou might want to visit the embassy website.
http://www.tanzaniaonline.gov.uk/mission.html