Toka shoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa CRDB Bank Board, Mh. Martin Mmari, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk. Charles Kimei, Mkuu wa Huduma mbadala za benki Joseph Witts na Bosi wa masoko na utafiri Tully Mwambapa wakipongezana baada ya kuzindua huduma ya magari ya ATM ya benki hiyo leo jijini dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2008

    kaka Misoup ,Hawa viongozi wanachekesha ujue wanazindua hilo gari halafu wakati wadau wao mpka kesho hakuan card si tembo wala Visa ni mwaka sasa kila siku njoo after 1 month na ni branch ya Lumumba Branch cjui branch zingine ni aibu jamani..............

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2008

    Congratz mtanzania wa 1 kutuma hiyo comment ni kweli jamani Mr Kimei na wenzio ni ajabu mnapongezana huku huduma ni mbaya kuliko maelezo mm nina miezi 6 toka December njoo kesho mapak leo cna Tembo card yangu na hii ni Dar cjui huko mikoani kukoje.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2008

    mimi nina maswali:
    1)Security ya dreva na mteja itakuwa protected na nani?
    2)Haya magari yatakuwa yazunguka jijini au yatakuwa yanaegeshwa sehemu moja kwa masaa kadhaa, nusu siku au siku nzima?
    3)Are these vehicles armored (kwa watu wa usa si mnajua yale madude ya brinks yalivyo)?

    mimi nafikiri idea hii ya kuwapelekea wateja huduma hii muhimu ni nzuri.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2008

    Kuweni serious wazee nyinyi sasa, with fuel costs skyrocketing hizo gharama za kuendeshea hayo magari ya ATMs simta tutupia sisi walalahoi kama banking fees, mtatuua.

    ReplyDelete
  5. ebwana halafu kweli huyo jamaa hapo juu aliyetoa maoni kasema ukweli kinoma,maana mwaka huu nilienda bongo nikasema ngoja niweke vijisent vyangu hapo crdb nilikaa bongo kama miezi mitatu jamaa kila siku wanajiambia mashine ya kutengenezea kadi imeharibika, wakati mashine hizo wala sio ghalama sana ulicompare na wao ni benki kubwa hapo bongo
    yani bongo bado sana ngoja tujikalie huku huku kwa mwenzetu sasa tutafanyaje maana bongo longolongo tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2008

    Sijawahi kupost comment kwenye blog hii lakini ni msomaji mzuri wa blog hii. Leo imeniwia vigumu kuacha kutoa maelezo madogo kunyoosha uelewa.

    1. Watanzania tuna haja ya kujenga utaratibu wa kusifia inapostahili, sio kila jambo madongo tuuuh. Tujiulize tumetoka wapi na tuko wapi na tunaenda wapi?. Sasa hivi benki za wazawa hasa CRDB na NMB zinaongoza kwa ubunifu na faida kuliko benki za kigeni. hili ni jambo zuri.

    2. Maendeleo ya kweli yanaletwa na uwepo wa huduma za kibenki karibu na wananchi. hii inarahisisha mikopo na kujiwekea akiba. kwa waliosoma economics wanajua. Tanzania inajumla ya watu 2.6 million tu wenye akaunti!. wakati kuna watu wenye simu 7.8 millioni!, kuwa na simu ni gharama zaidi ya kuwa na akaunti. sababu kubwa ni umbali wa huduma za kibenki hivyo hili ni suruhiso au mwanzo mzuri kwenda kwenye suruhisho.

    3. Magari haya ni bullet proof, yanatumia 3g na gprs kwa mawasiliano. maeneo lengwa ni wilayani na vijijini.

    Sasa hivi mabenki kama Azania, CBA, CRDB na Stanbic yameanza kufanya morgage finance hivyo ujenzi wa nyuma au ununuzi unakuwa rahisi.

    Ndugu zetu mlioko ughaibuni huku ndio KWENU, lazima mjenge. Nakumbuka nikiwa huko nasoma wazungu walikuwa hawachoki kuuliza unarudi lini kwenu!!!?? MKIWA WAKWELI mnajua hili. Huwa inanisilitisha sana kusoma comments zisizojenga, wala sisizotia ari ya maendeleo!. Ukisikia makocha wa ulaya wanapozungumzia timu pinzani huwa wanatoa positive aspects lakini silikiza makocha wetu!!!.

    ReplyDelete
  7. ANON 10:11 NAKUSHUKURU KWA MAONI YAKO. TAFADHALI USISITE KUJITOKEZA , MAONI YAKO NI MUHIMU SANA KWANI MAWAZO YA HAWA NDUGU ZETU KWELI ZINAPUMULIA MASHINE. ASIPOONA MAHALI PA KUKOSEA BASI ANANAFIKIRI HANA POINT. MAONI YAKE ANAONA YEYE ANAPOINT KATIKA SEHEMU TUU MTU ALIPOKOSEA. KWA HIYO UKIFANYA MAKOSA MENGI SANA YEYE NDIYO FURAHA YAKE. KWA HIYO MAOMBI YAKE YEYEY KILA SIKU NI KWAMBA WEWE UKOSEE TUU.MFANO ANGALIA BUNGENI WABUNGE WANATEGEMEA KUPATA SIFA NA UMAARUFU PALE AMBAPO WANARIPOTI UOVU UKIFANYIKA. INAMAANA WABUNGE HAWANA UWEZO WA KUJENGA NCHI AU KUWA MAARUFU KWA WANANCHI PASIPO NA MAOVU YA KUWAFAAMISHA WANANCHI. HII NI AINA YA AKILI INAYOITWA LOOSE/LOOSE MENTALITY.YAANI TUKOSE WOTE. INASHAURIWA TUWE NA WIN/WIN MENTALITY YAANI TUPATE WOTE. LOSE/WN AU WIN/LOSE ARE NOT ECOURAGED.LAKINI KILA KITU INABIDI KIWE KAMA KILIVYO ILI KIONEKATE TA KISOMEWE HATIMAYE IKITAFUTIWE UVUMBUZI WA KUDUMU

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2008

    Problem ni kwamba wakati Management inajitahidi kufanya promotion,sametime wafanyakazi wanafanya demarketing,nashindwa kuelewa ni kwa nini? kama uamini jaribu kuomba mkopo pale au itokee umepoteza card na unahitaji huduma ndio utajua namaanisha nini.
    Au ni kutokana na kutokua na motivation nzuri kwa wafanyakazi kutokana na menejimenti kuangalia faida tu bila kuwakumbuka wanaotoka jasho kuileta hiyo faida? Au ni namna tu ya menejimenti kuongeza matumizi ili operating costs zisitiliwe mashaka?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2008

    Anon wa 10:11 PM, umesema sawa kabisa. Lakini swala lilioulizwa hapo ni lile la kwa nini Tembo card inachukua miezi sita kupata na mashine za ATM zinakuwa mbovu kila mara. Hilo la magari ya ATM ni lao katika kuweka mambo yao sawa na tunajua gharama tutabeba sisi watumiaji. Ila pia sisi tunataka vitu wa msingi kama ATM na Tembo card zitoke mara moja bila kusumbuliwa.
    Pili swala la kurudi TZ tutarudi au hatutarudi ila tutajenga au tunajenga au tumeshajenga. Tunachotaka ni mambo mzuri yanao-wiana na ya huku tulipo katika kupata huduma bora kwa wakati mwafaka. Then tuhusike katika kuendeleza nchi, sio lazima wote turudi tukae hapo Dar , ila wengi wetu tuendeleze hili la kuanzisha biashara , makazi nakadhalika huku tukiwa huku.
    Hili la benki kuwa na magari ya ATM inaweza kuwa inapata Hasara na inajua hilo isipokuwa kwa hatua hiyo inakuza jina na soko lake ili-itambulike, kwamba wao ndio bora na kuweza kupata wateja wengi baadaye, na kufidia hasara in future.
    Cha msingi bado tunataka uharakishwaji wa ATM mashine zonazofanya kazi pia Tembo card na pia huduma zisizo na kisirani.
    CRDB mnajitahidi, ila mna kisirani mno kwa wateja na hii sijui ni dharau au ukosefu wa "customer service" nzuri. Kama inawezekana "Fire" watu ambao wanalalamikiwa sana na "hire" watu ambao watoa huduma nzuri. Wanafunzi wenye degree wako wengi sasa hivi TZ waliomaliza business degree, wapatieni kazi katika mtindo huu wa kufire na kuhire.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2008

    Wewe anon wa 10:11 PM hii uliyosema "Sasa hivi benki za wazawa hasa CRDB na NMB zinaongoza kwa ubunifu na faida kuliko benki za kigeni. hili ni jambo zuri."
    Sikubaliani nayo kabisa.
    i)Faida za kupika vitabu ili waonekane wanafaida na kupata mikopo BOT/au Serikalini?
    ii)Kama ubunifu ni huu wa kununua magari na kuyatembeza kama ATM sio ubunifu kabisa ni kukaribisha hasara ya uendeshaji na malimbikizo ya asset badala ya kutumia fedha katika vitu vya faida. Hapa nilipo, Benki kubwa kuliko zote duniani ambayo ni Bank of America haina hata hayo magari na hata ukimuuliza mtu mjinga atakuambia hilo halisaidii kufikisha huduma wilayani au vijijini, kwani ni sawa na hili la kununua magari-mashangingi ya serikali na kusema yatakwenda vijijini, wakati kila siku yanaishia barabara za lami za miji mikubwa.
    iii)Idadi ya watu waliopo hapa USA wengi wao hawana account za benki. Wengi wao hapa kama ilivyo sawa na TZ wana simu za mikononi na majumbani. Hivyo sikubaliani kabisa na hilo la kununua hayo magari ya ATM kwa kisingizio cha huduma wilayani, thats a bad investment and a bad judgment in Financial management.
    iv)Tunataka basic things za kibenki na sio huge things ambazo zinajulikana kabisa ni hasara. Tutasifia kila kitu cha Tanzania kama wanacopy sawa na nje na kukiendesha kiasi cha 90% sawa na nje, na sio ku-copy then unakiendesha 45% hiyo ni upumbafu.
    iv) Mwisho kumbuka Economics ni kwa ajili ya kutoa mchango au kujua kwa kiasi fulani tunakokwenda, ila hili la CRDB kununua magari ya ATM sio la kichumi, kibiashara, kiuhasibu, kifedha wala kibenki kabisa.Ni la kumuongezea mteja gharama na kupata jibu la kusitisha malipo ya hisa kwa wateja na pia kurefusha asset za benki ili zionekane kuna faida katika mahesabu ya mwisho ya mwaka.
    Kumbuka iga na fanya kweli au iga na fanya katika hali inayokubalika au jaribu kubuni kitu na endesha unavyotaka sio kuiga na kutaka kubuni kwa kuiendesha katika mitindo yako at the same time.
    CRDB inapaswa kusikiliza malamiko ya watu na kuyajibu au kuyafanyia kazi kama inataka kuiga na kufanikiwa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2008

    CRDB kama mnataka basi wekeni ATM katika vituo vya polisi vyote Tanzania. Viko katika wilaya zote TZ. Kuna usalama wa kutosha kwa wateja na fedha zenu pia. Mtawalipa kiasi kidogo cha fedha za kukodi eneo lao ndani kusimamisha mashine ya ATM kuliko hayo magari. Kama ni kubuni basi hilo ni sawa kwani mtakuwa nyinyi tu Dunia nzima kuweka ATM katika vituo vya Polisi kata, wilaya, na mikoa. Nchi zingene zitawaiga kwa kufanya hivyo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 25, 2008

    annon mzalendo wa june 24 10:11 pm, ninakubalian na wewe kuwa pale makampuni au serikali ya bongo inapofanya vizuri ni haki kuwasifia. lakini ninafikiri wadau wengi walioshupalia crdb na mpango wa ATM tembezi wanayo hoja kwamba wakati mwingine tunakurupukia mambo ya juu na gharama kubwa kabla ya kuimarisha yale ya msingi. kama hadi sasa inachukua miezi sita kwa mteja kupata atm card, hiyo atm tembezi itatumiwa na nani? atm tembezi ni hatua nzuri sana lakini haina budi itanguliwe na huduma imara ya kutoa nyezo za kuitumia.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 25, 2008

    Suala la kuwa na magari ya ATM kwa CRDB bado haliniingi akilini. Kitu cha kwanza wangekifanya ni kutatua suala la kadi Tembo na kuhakikisha ATM mashine zinafika vijijini. Ndio ni maendeleo kwa CRDB kuwa na magari ya ATM na vile vile kupambana na washindani wake....lakini tusitazame Dar pekee yake kuna sehemu kubwa ya nchi inahitaji kuwa na huduma za ATM. Kama ni suala la uchumi na bei ya mafuta inavyopanda ni bora wangeweka ATM mashine kila mahali na pia kuhakikisha hakuna usumbufu katika kupata kadi za tembo. Barabara zetu za vijijini ni mbovu haya magari yakipita mara tatu yatawekwa juu ya mawe bila kusahau usalama wa wafanyakazi wake hata kama ni "bullet proof". Kama ni suala la uchumi na usalama na ushindani wa kibiashara....CRDB wafungue ATM's kila mahali nchini...na wataweza kuikamata sehemu kubwa soko la benki Tanzania.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 25, 2008

    Nadhani kutakuwa na shida kwa matawi ya Dar es Salaam kwa habari ya kadi kwa sababu mimi nilikuwa naishi Morogoro siyo mjini ila wilaya nyingine na ilinichukua kama mwezi hivi kama walivyoahidi kupata kadi yangu.
    Kuhusiana na suala la gharama sa hiyo huduma, hawa waendeshaji wa benki hawawezi kutoa huduma kwa ajili ya kumkandamiza mwananchi na wao wanataka kumsaidia huyo mwananchi. Kwa maana nyingine ni hivi, mpaka wao wameamua kuweka hiyo huduma ina maana takwimu zao zimeonyesha kuwa kuna faida kubwa wamepata na wanaweza kuitumia sehemu ya faida kuanzisha huduma waliyoianzisha wakapata faida zaidi. Pia tukumbuke kuwa watu wanaoweza kufaidika na sisi wateja pia. Kusema kuwa gharama za kuwa na akaunti ni sababu ya hilo inaweza kuwa kweli ila ni mpaka tuhakikishe kima-hesabu na siyo kuhitimisha mapema namna hiyo kwa sababu gharama zinaweza kupanda kwa sababu nyingi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 25, 2008

    anonymous wa 10:24 ni kweli unayosema kuhusu mortgage finance. ila mortgage za bongo interest zake ni kubwa mno, and time period ya kuulipa mkopo ni fupi. unakuta mtu una mortgage ya $200,000 unaambiwa interest rate ni 10% na uwe umemaliza kuilipa in 10 years maximum, at the same time uwe umeweka down payment ya 20%, come one now. thats so unrealistic. mortgage kama hiyo could be streached in a period of up to 30 years with an interest as low as 5%. after all nyumba za bongo ukishanunua au kujenga ndo imetoka, hakuna mjadala wa eti utaiuza baadaye. so them banks need to revise their mortgage terms ili wananchi wengi wafaidike.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 25, 2008

    Jmani naombeni msaada kama kuna mtu anajua swift code ya crdb ya moshi mjini..asanteni

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 25, 2008

    NAOMBENI MSAADA KAMA KUNA MTU ANAJUA SWIFT CODE YA MOSHI MJINI

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 25, 2008

    anoni wa 3.37am,,,umefikiri safi sana,,,huduma zipanuliwe sio hayo magari,,,yatafika adi wapi?kijijini kule itengule?
    anon wa 5.40am,,,ni kweli jamani izp morgage za nyumba sasa iyo interest adi unachoka kbs,,,benki ni biashara tu,,,km wajasiliamali hawamsaidii mlalahoi

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 25, 2008

    nyinyi CRDB hamna lolote hapo mmechemka maana kunawateja wengi tu wanapatashida na hizo tembo card zetu eti hapo mnatuambia maendeleo boresheni kwanza hizo visa card zenu ndio mzindue magari, mnaleta hizo ATM mobile wakati card hazifanyikazi? tutumie na nini?
    kama sisi wadau ambao tupo ughaibni tumefungua tanzanite account hapo lakini kutupata visa card zetu ni mwaka sasa umeisha isitoshe ukipata kuactivate tena mpaka mwezi uushe ndio ifanye kazi jamani sisi wadau wa ughaibuni tunaomba mtuboreshee huduma za visa card maana mnatusumbua sana.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 25, 2008

    Mzalendo wa june 24 10:11pm nakubailiana na mtazamo wako napia naamini wale wenye ya negative ni haki yao kuayatoa na hii ni changamoto kwa uongozi wa CRDB, wote wanataka huduma nzuri natunaitakia meme CRDB

    Kwa upande wa CRDB inaonekana kuna 'conflict of interest' kati ya department ya marketing na operation. Kwani inaonekana ubora wa huduma zinazotangazwa haziendani na huduma zinazotolewa kwa wateja. Hii ni changamoto kwenu kuweza kuunganisha hizi sehemu mbili kwenye shirika lenu kufanya kazi kwa ufanisi, kwani inaonekana kuna mapungufu makubwa na kwa ushindani ulio msije mkashagaa kuchemsha karibuni. Barclays inanyatia kama underdogs......

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 25, 2008

    Jamani haya magari ni mbwembwe tu za luchota akili za wadanganyika, na huo ubunifu mnaosema wa crdb mbona sio wao walioanza Exim wanagari la ATM lakini na nina account huko lakini kwa bahati mbaya au nzuri sijawahi kukutana nalo na pia nina acc. CRDB lakini kusema ukweli CRDB mnatakiwa kubadilika haiwezekani benki ambayo kila mtu amekua akiisifia leo kila mtu analalamika huduma ni mbaya Dar mikoani sijui hasa lumumba ikifuatiwa na azikiwe kijitonyama ndio usiseme ni balaa. Ukabila umezidi CRDB hebu ajirini watu wenye ujuzi na sio kimjomba mjomba hata Barclays wanawapita sasa. Card yangu ya tembo imeexpire toka April mpaka leo sijapata nyingine hivi biashara gani hii?. We mdau unaesema Watz hawasifii kitu nakwambia CRDB miaka minne iliyopita ungeuliza kila mtu angeisifia ila kwa sasa ni mdembwedo.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 25, 2008

    anon 10:11 umetumwa wewe!you cant just support that whole system,how do you know the cars are bulletproof??do u work for crdb??

    mi naona ufisadi tu hapa,watch otu tanzanians

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 25, 2008

    wadau dawa ni kuwanyang'anya CRDB market share ya ATM...si mnajua mtu binafsi unaweza kuanzisha ATM yako na machine sio bei mbaya sana,jaribuni kufikiria namna ya kuinvest na ATM ,angalieni kwenye internet mtapata machine mpaka dollar 2000,mkifanya hivyo mtacharge fee kidogo tuu,nakuhakikishia CRDB watatia akili na kuanza kuheshimu wateja...kueni macapitalist mjue namna ya kutake advantage za hawa wazembe

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 26, 2008

    wadau mimi nilikuwa posta benki nikaamua kuhama kwa kuwa ile benki ni mbovu kinoma yaani kichefuchefu nikaona niende crdb azikiwe lakini huu sasa mwezi wa nne sijapata visa card yangu na pale azikiwa ukienda unakuta bonge la foleni alafu kuna joto mle ndani kupita kiasi air condition hazifanyi kazi wameweka vijifeni viwili pale ndani yaani havina lolote na feni moja hivi sasa limeharibika hebu wavifikirie hivyo, pili wadau mkumbuke kuwa kulikuwa na mabasi ya wanafunzi aina ya TATA ambayo yote yamekufa sasa ile migari ya crdb ni TATA kwa hiyo najua itakufa ni bora wangenunua toyota dyna kama exim benk TATA hamna kitu wadau hazimudu tanzania yetu
    mizizi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...