mbunge wa kyela mh. dk. harrison mwakyembe ametoka kumwaga cheche bungeni sasa hivi, wakati akichangia hotuba ya bejeti ya ofisi ya waziri mkuu, kwa kutoa rai kwamba swala la ufusadi wa RICHMOND ufikie tamati kimoja.

kwa ufupi kasikitishwa sana na kile alichotaja kama maneno kibao yanayosemwa nje ya bunge, mengine yenye lengo la kujisafisha, kuhusiana na ufisadi huo, na kuomba wote ambao hawakupata nafasi kujieleza wakati ule baada ya kamati teule kutoa ripoti yake, wasimame na wajieleze hapo na sio kuzungumzia nje ya hapo.


ametanabahisha kwamba endapo kama katika kujieleza huko hao wanaotakiwa kusema wataweza kudhihirisha kwamba kamati teule haukuwa sahihi basi memba wote wa kamati hiyo wako tayari kujiuzuru.




aidha amesema endapo kamati itapewa muda tena wa kuelezea kila kitu na kudhihirika kwamba wahusika hao wanahusika moja kwa moja basi wao (wahusika) wajiuzulu nyadhifa zao zote.


hii, amesema, ndiyo itakayowezesha mada nyeti ya RICHMOND kufikia tamati na watu kuendelea na mambo mengine muhimu....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2008

    Huyu jamaa alikuwa mwenyekiti wa kamati iliyochunguza RICHMOND na siyo EPA. Kamati ya EPA bado haijamaliza kazi yake;
    Duh!! inamaana mzee wa vijesenti alitaka kumtanguliza shujaa wetu hivi hivi!! Mwakyembe mwambie mzee wa ndumba kwamba mungu bado yupo nawe na hawatakuwa na nafasi ya kukutungia wimbo wa 'TANGULIA NYOTA' kwa wakati huu ambao wananchi wanakuona wewe ni shujaa wao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2008

    Huyu Mbunge ni jasiri! Namuaminia babaake! Anafaa kuwa Rais wetu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 25, 2008

    Mbona mwakyembe umemchomeka kati badala ya juu au nawe michuzi ni fisadi. nami naungana na huyu jamaa mjadala wa mafisadi umechukua muda mrefu bila vitendo na badala yake watu wameanza kujisafisha. kwa vile watanzania tulijaliwa kusahau haraka yaliyopita usije ukaona mjadala unaanza wa mugabe na kuacha mafisadi wakipeta na kuchaguliwa tena kwenye chaguzi zijazo. nadhani ushahidi ni yule waziri mkubwa( mvi cheupe) alisemwa kuwa hafai na raisi wetu wa kwanza lakini jamaa kaona anafaa na matokeo yake ndo haya 'ufisadi'

    Nantombe
    Moshi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2008

    Kweli Mwakyembe ni DUME LA MBEGU kwenye siasa za kisasa hapa Tanzania. Hongera mWAKYEMBE, mwandishi wa habari wa zamani wa DAILY NEWS.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2008

    ndaga malyafyale, jobaga itolo..... gelomanye.... emiheji gelumanye, ne- emilosi gekapite kanunu, Kwala aje na nungwe akwemelege, akusanye, akonosye, akutule mu njela syako syosa.... ndaga michuzi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2008

    richhh woot? richmond
    richhh woot? richmond

    kwa wadau walioenda na kisasa kama mimi(ma braza men) wataelewa what am tokin bout,ma men.kwenye film ya coach carter by samuel l jackson and baby gal ashanti

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2008

    weanony wa June 25, 2008 2:41 PM inaelekea wapenda matusi sana,

    Michuzi "kamchomeka kati" Mwakyembe kivipi??

    Ndo mana jina lako tu nalo limekaa kimatusi matusi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2008

    Nchi kuiendesha Raisi yeyote huhitaji kusaidiwa na Bunge na Mahakama .

    Na Raisi hubidi aheshimu sana vyombo hivyo viwili maana nchi haiwezi endeshwa na mhimili mmoja tu.Sasa bunge likisema hivi au mahakama ikatoa hukumu ikasema hivi na serikali ikakaa kivyake ikadharau bunge au mahakama hapo ujue kazi ipo na nchi huelekea mahali pa kutotawalika.

    Nadhani ni vizuri maagizo ya bunge au mahakama yawe yakiheshimiwa. Kudharau huwa kuna madhara makubwa mno.

    Bunge la Tanzania lina maagizo yake limeishauri serikali basi ni vizuri Serikaliiyazingatie.Isifanyie mchezo.

    Washauri wa Raisi tunaomba waonyeshe uwezo wao kumshauri Raisi sawasawa vilivyo.Vinginevyo Kama Raisi akionekana kituko mbele ya wananchi na bunge wao wasidhani kuwa nafasi zao za kazi zitakuwa salama kwa kudhani kuwa wao wataonekana safi ila Raisi tu ndiye ataonekana kituko.Raisi akionekana kituko mbele ya wananchi ina maana washauri wake ndio hasa wamemfanya awe kituko kwa kutomshauri ipasavyo.Na nchi nyingi huwaondoa mara moja bila kukawia pale wanapopwaya kiasi cha kufanya Raisi apoteze hadhi yake mbele ya Bunge au wananchi.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2008

    Sisi wananchi tunataka Mwakyembe for President kupitia chama cha mapinduzi na si Laurence Masha wala Benard Membe kama vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti.Na wewe Jakaya Kikwete tunaomba uache wananchi wachague mgombea wao kama Mkapa alivyofanya na usituwekee mrithi kwa matakwa yako kuwa mgombea la sivyo nchi itawaka moto.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2008

    Kwa wale watu wa pwani including Dar sisi wabara huwa tunaiita huu muondoko ni mdundo. Unatembea kwa kuringa kidogo. - by ngedere

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2008

    anon 3:55 huo ni utumwa!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 25, 2008

    wewe anon 5:23 ndio mwenye matusi..umejisema mwenyewe..hahaha..kama yamekushuka vile

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 26, 2008

    Soo la Epa: Mkulo ajiweka pabaya

    2008-06-25 19:30:17
    Na Emmanuel Lengwa, Jijini


    Waziri wa Fedha na Uchumi, Mhe. Mustafa Mkulo amedaiwa kujiweka pabaya kutokana na msimamo wake alioutoa bungeni kuwa mapesa zaidi ya Sh. Bilioni 133 ambayo yalichotwa kifisadi katika Benki Kuu ya Tanzania, BOT kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA ni mali ya wafanyabiashara binafsi na wala si Serikali wala BOT.

    Wakizungumza na Alasiri leo asubuhi, baadhi ya wakazi wa Jijini na pia wanasiasa, wamesema Waziri Mkulo ametoa taarifa ya kushangaza na kwamba hadi sasa, amejiweka pabaya kutokana na maswali kibao kuanza kuibuka na kumuelekea yeye.

    ``Siku zote hizi alikuwa wapi? Na kama ni pesa za wafanyabiashara, awataje majina ili wafahamike waziwazi... majibu yake kuwa si pesa za Serikali wala BOT yanaweza kumuweka pabaya kutokana na maswali mengi yatakayofuata baada ya hapo,`` akasema mkazi mmoja wa Ubungo Jijini aliyejitaja kwa jina la Jesca Francis.

    ``Kwanini Mkulo alinyamaza siku zote hizo na kuacha suala hili liendelee kuisumbua Serikali... kuna utata. Atapaswa kuulizwa maswali mengi ambayo huenda yakamuweka pabaya,`` akaongeza mkazi mwingine wa Sinza, aliyejitambulisha kwa jina la Yusuf Hamza.

    Aidha, Bw. Mbarara Maharagande ambaye ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano ya Umma wa Chama Cha Wananchi, CUF, amesema kauli ya Waziri Mkulo haina msingi wowote na kwamba CUF inaamini kuwa fedha hizo ni za umma na si vinginevyo.

    Akasema maswali kuhusiana na kauli hiyo ya Mkulo ni mengi mno, kwani hata kama anachosema Waziri huyo kikiaminika, bado ukweli unabaki kuwa aliyezilipa ni BoT, tena bila idhini ya hao anaowataja na hivyo kuonyesha kuwa zenyewe ni mali ya Serikali.

    ``Waziri huyu anajiweka pabaya... maswali ni mengi mno kwa sababu hata kama fedha hizo zilikuwa ni za wafanyabiashara, BOT ndio wamezilipa kwa makampuni hewa, wala hao wafanyabiashara anaowasema hawakuwaambia wazilipe wakati ule wa uchaguzi,`` akasema Bw. Maharagande.

    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TLP, Bw. Augostine Mrema amehoji kuwa kauli hiyo ya Waziri Mkulo inalenga kumsafisha nani?

    ``Ushahidi upo kuwa hizo ni fedha za wananchi, sasa tunashangaa Bw. Mkulo kuzikana fedha hizo kuwa sio za Serikali anataka kumsaidia nani? Basi ataje na majina ya hao anaodai kuwa ndio wenye pesa hizo,`` akasema Bw. Mrema.

    Akasema kwa anavyoamini, ni kwamba kuna mchezo unafanyika ili kufuta aibu iliyotokana na ufisadi wa fedha hizo za EPA.

    Akasema Mrema kuwa imani yake hiyo inatokana na ukweli kwamba sasa, hata baadhi ya wabunge wameanza kuonekana wazi wakitoa kauli zinazoonyesha kuwa wamejipanga kutetea mafisadi.

    Waziri Mkulo amerejea kauli yake jana kuwa pesa za EPA hazikuwa za Serikali wala BOT, bali za wafanyabiashara ambao hata hivyo, hakuwataja majina.

    Hata hivyo, wabunge kadhaa wamekuwa wakipigia kelele pesa hizo zilizobainishwa katika ripoti iliyotolewa na Kampuni ya Ukaguzi ya Kimataifa ya Enrst & Young, ambayo ilionyesha kuwa mapesa hayo yaliyokuwa BOT yamechotwa na makampuni mbalimbali kwa njia za kifisadi.

    Kufuatia ripoti hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete alisitisha nafasi ya Gavana Dk. Daudi Balali na pia akaunda timu ya kufuatilia mapesa hayo , ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Johnson Mwanyika, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Bw. Edward Hosea na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Ludovick Utouh.

    Hata hivyo, timu hiyo iliyopewa muda wa miezi sita bado inaendelea na kazi yake.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 26, 2008

    watanzania tuache masihara jamani kama tunataka maendeleo basi nchi nzima tuwe na huyu mbunge wa kyela mh. dk. harrison mwakyembe. hakika tangu kuzaliwa leo na miaka 50 nashukru lakini sijawahi kuona mtu mwadilifu kama mbunge wa kyela mh. dk. harrison mwakyembe.
    mnajua tatizo ndugu zangu hata tukiangalia maoni hapa kwenye blog ya ndugu machizu hatuwi serious.

    ndugu zangu watanzania nawaomba wote ni kumuunga mkono mheshimiwa kwa hali na mali kuonyesha kuwa huyu ni raisi wetu mtarajiwa.
    naimani ikiwa hakika wananchi tutampata raisi kama mheshimiwa mbunge dr. basi tanzania hatuko mbali kuwa katika nchi zilizoendelea na kwa uwezo wa MUNGU na mheshimwa mbunge basi umasikini kwa mtanzania utakwisha.
    maana tanzania ni nchi tajiri sana tatizo ungozi taabani na ufisadi umeshamiri na samahani kusema raisi kikwete anachangia sana kwa ukimya wake wa vitendo kwa maana wote wahusika na marafiki zake.
    anasahau kuwa MUNGU na wananchi ndio waliomweka hapo.
    Tumuombee kheri aweze kuzinduka.

    ndugu michizu tunaomba number ya mheshimiwa mbunge dr ili tumpe pongeze. MUNGU MBARIKI NA MLINDE MHESHIMIWA MBUNGE DR,

    ReplyDelete
  15. hakuna kama Mwakyembe Tanzania jamanii huyu pekee yake ndyo yuko serious bungeni ndag kalumbu kyala akutule ba mwetu mwe!!!!!
    wapiga kura wa Kyela mpeni kura arudi bungeni tena mwaka 2010

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 26, 2008

    Wabongo naye mmezidi kubabaika! yaani kila mbunge akifanya jambo moja zuri basi awe mgombea wetu wa uraisi, hivi tutakuwa na wagombea wangapi wa urais? Kama mtanzania na pia kama mbunge anawajibu wa kuwatumikia wapiga kura wake na nchi kwa jumla na tunatakiwa tummunge mkono ili awe tena mbunge kwa kipindi kijacho lakini siyo kukimbilia kusema kwamba awe raisi. Walikuwepo wengi wa aina yake kama akina Mzindakaya lakini wakaja kugeuka baadae. Nadhani tulionyesha mabadiliko ni sisi wananchi na siyo wabunge kwani wengi wao sasa hivi wanafahamu uelewa mkubwa wa wananchi kuhusu wajibu wa wbunge wao hivyo ni wajibu wao wabunge kulinda vitumbua vyao vinginevyo tutawamwaga

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 26, 2008

    Hongera Mwakyembe, wewe ndiye unayejua nini kilichokupeleka bungeni. Hao wengine wanachemsha lakini sio wao ila ni tamaa zao, wanapenda madaraka na huku wanakumbatia ufisadi halafu wanataka watu wasiongelee ufisadi. Naona kila mtu anayeitakia nchi hii mema lazima aungane na Dr. Harrison Mwakyembe. Nakuomba na wewe Mkuu wa mkoa wa Mbeya usimpinge Mwakyembe kama ulivyomhujumu katika mapokezi ya kumpokea kama shujaa kwenye jimbo lake. Hii inashangaza sana... yaani mafisadi wengine wanapokelewa na wakuu wao wa mkoa lakini kwa Mwakyembe anayetetea wanyonge anahujumiwa na Mkuu wa Mkoa. Hii ni aibu sana kwa mkuu huyo wa mkoa na nchi kwa ujumla. Mungu msaidie Mwakyembe, mungu ibariki Tanzania. From Michael J. Laiser - Dar.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 27, 2008

    Mwakyembe For PRESIDENCY 2010 if CCM wants to stay ALIVE!Anne Kilango Malecela for PM !nomore Nonsense!and no more Smiling Faces which show no choices AND Wesley Snipes will for the first time smile!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...