Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ben Christiaanse akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dk. .Idrisa Rashid wakati wa uzinduzi wa NMB ATM LUKU Recharge.

Leo Tarehe 25 June 2008, NMB imeweka historia mpya katika utoaji wa huduma za kibenki kwa kuanzisha huduma ya kununua LUKU kwenye ATM za NMB yaani NMB LUKU RECHARGE bila gharama yeyote ya ziada . Huduma hii inaenda sambamba na ukuaji wa uwekaji wa ATM nchi nzima.

NMB ilikuwa ni benki ya kwanza kutoa huduma za kuchukua fedha kwenye ATM bila gharama.Hadi sasa NMB ina ongoza kwa kuwa na ATM nyingi kuliko benki nyingine, hadi sasa tayari ina mashine za ATM 115 na ifikapo mwisho wa mwaka huu itakuwa na ATM 200 nchi nzima.
Chini ni bosi wa masoko wa NMB Imani Kajura (shoto) akipeana mikono na mmoja wa wateja wa kwanza wa Tanesco waliotumia huduma hiyo mara tu baada ya kuzinduliwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2008

    ATM bado mbali na uhakika wa kuikuta inafanya kazi si mkubwa kivile. Sehemu 115 kwa TZ nzima? Bado sana ongezeni vituo, iyo Dar tu havitoshi. Nadhani mnaotoa huduma za kutuma pesa kwa simu za mkononi mfano ZPesa na Mobipawa mngefanya hili pia. Amkeni jamani waTz tuna uchumi tunaukalia. Big up to u NMB mpo juu na mmeamka, uyo Marketing wao namkubali. Tatizo hao Tanesko ukiritimba bado haujafutika japo mmeamka, yan leo ndo twaona LUKU ina njia mbadala after kutuweka foleni miaka kibaao. Amkeni! Umeme pia unaweza kuuzwa Online, via SMS au hata calls nmeona sana Mangharibi. Nmekumbuka MPesa pia mngefanya. Sasa je wa mita za kuzunguluka (analog) na za kadi ndo inakwaje? Bongo bwana!
    Mtanzania Mpendanchi japo nmeikimbia: Apakati_ya_chembe_au_kidevu@yahoo.com

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2008

    hongera

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2008

    Is that news, those things are just history now in other countries while in Tanzania are news of the days, in Europe ATM was introduced nearly 100 years ago, in ZIMBABWE more than 50 years ago.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...