mdau obama na mai waifu wake baada ya kulamba dume. wadau mnasemaje, anaweza kuchukua?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2008

    definetely..obviously...certainly...ofcourse atachukua

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2008

    Obama atashinda bila wasi wasi ila akitaka azikombe kura Hilary awe vice president, wanawake watampa kura na Obama atachukua kwa neutral votes,

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2008

    Huyu jamaa ni Next president Of USA, hiyo haina ubishi. Ila kama mdau alivyosema akitaka ushindi tsunami amchukue Hillry yaani iwe Obama/Hillary 08!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2008

    Obama akitakaashinde achague m2 mwingine sio mama clinton,coz mama alikua anamkandia sera zake wa2 ambao hawamtaki mama watamnyima obama kura endapo akimchagua mama.mama inabidi akae chini asubili ata uwaziri.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2008

    Msela hapa ameula ila akitaka kuaribu amchague mama aone,wa2 waliokua hawamtaki mama hawatampa kura kama akimchagua mama.Inabidi mama asubiri uwaziri labda.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2008

    Hapana hawezi kuwa RAIS.Kwani tayari media imeisha anza kujenga mazingira ya mpasuko kati ya mgombea mweusi na mzee mweupe!Wanamuita The first black African -american presiential Nominee for Democratics/he will be the first black president!Hawawezi kumtaja bila the word "black".Na tayari john mccainn ameishakanusha kwamba yeye sio MCBUSH.Kamwe hata endeleza foreign policies za bush.Historia itamshitaki zaidi hasa uislam na experience to make tougher decisions in the white house.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2008

    Bwana Michuzi hutakiwi kuuliza hili,yaani hapa jamaa anatakiwa akubali ombi la mama la kuwa running-mate wake ashinde kwa kishindo.
    Taratibu anaingia zake jumba jeupe.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2008

    hivi jamani Obama kuwa rais itatusaidia vipi taifa letu maana naona tumeshikilia na kufuatilia hili suala as if litatuletea maendeleo nchini mwetu, hapa ndipo wadanganyika tunaponekana wajinga sasa hivi kila mtu amesahau mambo ya ufisadi,epa na mengineo mengi tu, yaani watanzania tunakua kama nyimbo za bongo flava ikitoka inapigwa weeeeeeee baada ya mawiki au mwezi kila mtu keshausahau.....

    tuconcerntrate kwenye mambo ya taifa letu ya USA tuwaachie waUSA

    ni hayo 2

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2008

    Sidhani kama Obama atafikia uamuzi wa kumchukua Hilary kama running mate wake. Hilari japo anapendwa sana na watu wa daraja la kati na wanawake, bado hakuweza kujibu maswali muhimu ya kimataifa kama njia sahihi atakayotumia kumaliza vita vya Iraq na maswala ya Iran na Israel. Obama hapa ana wasiwasi na uwezo wa kujieleza wa Bi Clinton. Pia halikuwa chaguo la Obama tangia awali. Inaaminika seneta wa Virginia Jim Webb.
    www.assenga.blogspot.com

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2008

    Obama atshinda uchaguzi Nov. hata bila ya Hillary, hao wanaoamini kuwa Obama kushinda mpaka amchukue HRC hawajiamini, kwa hiyo in their opinions wanadhani Clinton ni stronger candidate kuliko Obama, waaapi baba...I don buy that.mbona kashindwa kwenye Primary?!!
    kwa wale watafiti wa mambo ya kisiasa(political pundits) wanakwambia kumchukua Hillary Clinton''That will one of the craziest things ever done in the american politics'' by Jimmy Carter. Liabilities za kuwa na Clinton kama running mate are very much higher than the positives she will do to the campaign.Kuwa na Hillary ni kosa kubwa,na litamcost Obama urais,ni sawa na watu walivyoona kuwa Hillary kuwa na Bill Clinton kwenye campaign ilikuwa ni ''a plus factor'' kumbe ilikuwa ni ''a big X factor'' and it finally cost her the nomination.
    Pia watu inabidi muangalie mbali pia,kuwa suala sio kuwa running mate tu,bali baada ya uchaguzi watakuwa wote White House,na hapo factor ya Bill Clinton inaingia tena. The hell will go cold working with Bill.
    EmergencyPoison.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2008

    Trafiki amuumbua afande JWTZ

    2008-06-05 15:56:32
    Na Emmanuel Lengwa, Jijini


    Askari mmoja wa Jeshi la Wananchi, JWTZ amejikuta akiumbuka baada ya kushushwa na askari wa usalama barabarani kutoka kwenye basi la abiria lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza.

    Tukio hilo lilitokea jana mishale ya saa 6:00 mchana mkoani Dodoma, wakati askari huyo alipokuwa miongoni mwa abiria wanane waliozidi ndani ya basi hilo.

    Shuhuda wa tukio hilo ambaye alikuwa miongoni mwa abiria waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Falcon, ameiambia Alasiri kuwa baada ya basi hilo kutoka nje kidogo ya mji wa Dodoma, lilisimamishwa na askari wa usalama barabarani aliyekuwa akiwafuata kwa pikipiki.

    Akasema askari huyo baada ya kulisimamisha basi hilo, alipanda ndani ya basi na kuwasalimia abiria kwa uchangamfu wa hali ya juu.

    Akasema baada ya salamu hizo aliwapa pole kwa safari huku akitoa utani wa hapa na pale, kitendo kilichowafurahisha abiria wengi.

    Shuhuda huyo akasema simuni kuwa baada ya kuwapa pole, afande huyo mwenye namba F 3082 zilizokuwa zimebandikwa kifuani mwa sare yake, akamwita konda na dereva na kuanza kutoa somo la nguvu kuhusiana na masuala ya usalama barabarani.

    Akasema kutokana umahili wa afande huyo wa kuelimisha huku akitumia lugha ya upole na busara, alijikuta akishangiliwa karibu na abiria wa basi hilo.

    Hata hivyo, baada ya kuwaelimisha abiria madhara ya kukiuka sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na basi kubeba watu wengi kuliko uwezo wake na kabla ya kuamuru abiria waliozidi kuteremka.

    Akasema miongoni mwa abiria waliokuwa wamezidi ndani ya basi hilo, alikuwa ni askari wa JWTZ aliyevalia sare zake za kazi, ambaye alilazimika kutii amri ya kushuka.

    Baadhi ya abiria walianza kumzomea afande huyo wa JWTZ kwa kufumbia macho na kushiriki kuvunja sheria za barabarani huku akiwa amevalia sare za kazi.

    Baada ya abiria waliokuwa wamezidi ndani ya basi hilo kushushwa, basi hilo likaruhusiwa kuendelea na safari, huku trafiki huyo akiwa amezua mjadala mzito ndani ya basi.

    SOURCE: Alasiri

    Habari za Leo
    Tibaigana akabidhi mikoba kwa Kova

    Zombe apumua!

    Moto Dar waua

    Wanaowatumikisha watoto wenye ulemavu kukiona

    Trafiki amuumbua afande JWTZ

    Mbio za mwenge Jijini Dar kuzindua miradi ya Sh. Bil 6

    Binti darasa la saba Dar aanguka ghafla na kufariki

    Wataalam wa mifugo waaswa

    More news....


    -----------------------------------------------
    Maoni ya Mhariri
    Kuna siri gani BoT kuzuia waandishi?

    -----------------------------------------------
    Business bits
    Exchange rates
    Dar Stock Exchange
    Financial Times Editorial
    Financial Watch
    More business

    -----------------------------------------------
    Makala
    Mbinu za kisasa ni muhimu kwa elimu ya watu wazima

    Hali ya maisha ya wananchi iboreshwe

    Mama akimsifia hausiboi kosa, baba kwa hausigeli eti ruksa!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2008

    Atachukua tu hiyo ni lazima. Ila in two years mtasikia kadedi. Maana kuna vimaneno vya chinichini vinavyoendelea huku kuwa oooh- eti ana jina la kiislam na marekani hawataki kuongozwa na mtu mwenye kamguso ka kiislam.Watamuua wamarekani kama atashinda. au watahakikisha in anyway kuwa Obama hashindi. Ila ukweli ni kwamba huyu jamaa anatisha na atashinda.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2008

    Michuzi nataka upost ile mitundiko ya zamani..kama itawezekana especially ule wa baada ya Obama kushinda Iowa caucus January 2008. Kuna "nay sayers" kibao hapa walikuwa wanampa zero chance ya kushinda. Watu walikuwa wako too negative na kwamba atashindwa kwa sababu ya rangi yake. Wow...sijui wanasema nini sasa. Mikutano ya jamaa inajaa five hours kabla ya yeye kuhutubia. The guy is more than a rock star. Na hata kama hatashinda. Ameandika historia tayari.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2008

    in change we can believe in

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2008

    mmmmmmmmh bado sijakubali manake kuna yule jamaa wa kumrithi Mzee Pori..naaamini pia kuna uhafidhina fulani utatumika jammaa akose....ngoja tuone
    yangu macho...

    nyaningedere

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2008

    ASIFANYE KOSA KUMPA HILARY KUWA VICE PRESIDENT,KISHA APEWE ULINZI WA KUTOSHA WASIJE WAKAMMALIZA KWA KUA DEFINETLY,DEMOCRAT WATA SHINDA NA HILARY ALILJUA HILO NDIO MANA AKUTAKA KUAACHIA NGAZI KUMPISHA OBAMA CHAGUO LA WENGI NA MTU WATU,HE HAS A DREAM.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2008

    Yah chance ya kushinda anayo lakini tunaomba ikitokea amechukua 08 wasimfanye kama walivyo mfanyia Kennedy. Maana hawa watu(weupe) sio watu. Sasa hivi matumbo yao moto mweusi kachukua nchi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 06, 2008

    Brek ya kwanza WHITE HOUSE. He's an inspiring fellow. He has changed the history and he's going narrow the gap of racial discrimination, and of course, he's the perfect person to do this because he belongs to both "b" and "w" communities, graduated from the best schools in world.

    We use to admire black-movie stars, sports men and women, musicians, etc etc. But this gentlemen has just gone above all that.

    For sure he'll change America and change the World. God bless Obama. By putting him into the throne you'll be spreading peace on this earth.

    Mbeba box...UK

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 06, 2008

    NO DOUGHT, OBAMA IS THE NEXT PRESIDENT OF THE US OF AMERICA. WHO WILL BE HIS RUNNING MATE? SHOULD NOT BE HILARY CLINTON! ITS BETTER HE CHOOSE ANY OTHER MAN THAT THE CLINTON. GOD BLESS AMERICA, GOD BLESS AFRICA, GOD BLESS TANZANIA

    www.assenga.blogspot.com

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 06, 2008

    it's time for change, hili neno ni zito sana,ingawa watu wengi tunalichukulia poa,unaweza kupataa maana kibao kutoka hapo kwenye hilo neno; ni wkt wa kubadilika si tu kwa utawala wa bush,bali hata kubadili akili zetu kua mtu mweusi hawezi,ndio mana tunabakia maskini kwa ajili ya kuamini hatuwezi kwenda bila wazungu,ndio mana kuna msemo wa keep your body,i'll keep your mind,sasa waafrika wengi tumehifadhi miili tu ila akili zetu wamechukua wazungu,narudi kwenye swali km atachukua nchi? 100% atachukua nchi kwani hakuna mtu yoyote kati ya wale walioshindana nae na hata huyu mccain hamuwezi,sasa wale mnaooongelea kushindwa mtashindwa nyie mjaluo atachukua nchi,na pia siamini km akimchukua mama kua mgombea mwenza ndio atashinda,kwani km mama alikua muhimu si yeye ndie angeshinda basi na la mwisho ni kua kweli watu wengi sana wanaongelea kuuliwa kwa obama,jamani tuache ya MUNGU yafanywe nae,sisi wanadamu tukae kusubiri,kwani lini nyie mnaosema atakufa mlikaa na muumba akawaambia kua atakufa,mbona mnaombea mabaya madala ya mazuri na km atakufa basi ivyo ndio muumba alivyotaka obama afe,acheni kuongelea mambo ya mbele ambayo ni muumba tu anajua,hasa la kifo cha mwanadamu kwani hakuna ajuae siku wala saa,na kusema kua ni muislamu yeye si muislamu ila yule baba yake wa kambo ndio alikua muislamu ila baba yake mzazi ni mkristo ndio mana hata yeye anaenda kanisani,sasa hilo jina la hussein ni la mzee wake wa kambo kitu ambacho kilikua nje ya uwezo wake wakati huo,ila wanataka kutumia hiyo ili asishinde,na watu ambao wavivu wa kufikiri wakiambiwa basi wanachukua tu ivyoivyo.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 06, 2008

    Yes We can...OB '08.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 06, 2008

    Bwana Michuzi swali lako kwa mtu makini na mwenye kuijua vema siasa na mfumo wa utawala wa hapa Marekani,hawezi kukurupuka na kutoa jibu la jumla jumla kwa sasa.Nasema hivyo,kwa sababu yako mambo(factors) mengi ambayo kwa mchambuzi makini wa masuala ya siasa za Marekani lazima ayaangalie kabla ya kufikia hitimisho kuwa Obama ndiye Rais ajaye wa Marekani.Ingawa itapendeza ikitokea hivyo.
    1.Jambo la kwanza ambalo wadau inabidi walielewe ni kwamba Obama amemshinda huyu mama Clinton kwa wingi wa idadi ya kura za wajumbe(delegates) na wajumbe maalumu(superdelegates).Obama ameweza kupata kura zinazomwezesha kupitishwa na chama chake kama mgombea wake kwenye tiketi ya urais hapo baadaye.Sasa lazima tuelewe kuwa Obama hajamshinda huyu mama kwa kura za jumla za wapiga kura wa kawaida(popular votes).Huyu mama amemshinda Obama kwa hizo za jumla.Sasa hili lazima wadau walitambue.Na kama wakilitambua hili,kwa wale wote wanaombeza huyu mama kuwa hastahili kuwa mgombea mwenza,eti kwa kufanya hivyo itakuwa Obama anajiharibia,watagundua kuwa wanapotoka kabisa.Obama na kambi yake hawawezi hata kwa namna yoyote kulikwepa hilo kama kweli wanataka chama chao kishinde kwenye uchaguzi ujao.Na hata kambi ya Obama ilishaliona hilo mapema kuwa pasipo ushirikiswaji wa karibu wa huyu mama itakuwa ndoto kuingia Ikulu.
    Mama Clinton wakati anatoa hotuba yake jana mjini New York kuwashukuru wale wote waliomuunga mkono,alitamka maneno mazito sana ambayo yanawaumiza vichwa si kambi ya Obama pekee bali na vigogo wa chama kwa ujumla.Alisema kwamba ni lazima sauti ya wapiga kura milioni 18 waliompigia kura zisikilizwe na zipewe uzito unaostahili.Sasa,ninachotaka kusema ni kwamba si sahihi kumbeza huyu mama kama baadhi ya wadau wanavyojaribu kutoa maoni yao.Tukumbuke Obama aliungwa mkono sana na vijana,wasomi,wenye kipato cha juu na watu weusi.Mama Clinton,aliungwa mkono zaidi na wanawake,watu weupe,malatino,na wafanyakazi wa kada ya chini.Sasa kwa anayefuatilia kwa makini siasa za hapa,atakubaliana nami kwamba kundi la watu waliokuwa wanamuunga mkono Obama halina historia ya kumuweka madarakani rais wa Marekani.Ukweli ni kwamba,Rais wa Marekani hupatikana zaidi kupitia kundi la wafuasi wa mama Clinton.Sababu kubwa ni kwamba hao ndio wapiga kura wa nchi hii na ndio wengi zaidi.Vijana hapa Marekani hawana utamaduni wa kujitokeza kupiga kura.Sasa,labda itokee mwaka huu,kwa mara ya kwanza jambo ambalo hakuna mwenye uhakika nalo ingawa wengi ndivyo wanavyotarajia.Kwahiyo hoja ya msingi ni kwamba itakuwa ni kujidanganya kudai kwamba Obama anaweza kushinda bila uwepo wa mama Clinton.Ni jambo tata sana na gumu sana kwa wafuatiliaji makini wa siasa za Marekani.
    2.Sasa, swali lingine la muhimu ni kwamba,je kwa hali hiyo kama Obama na Mama Clinton watakwenda pamoja Democrat wataweza kushinda? Hapa napo panahitaji uchambuzi wa kina.Katika hali ya kawaida na kwa majibu rahisi kulingana na maelezo yangu,naweza kusema ndio,wanaweza shinda japo sio lazima uwe ushindi wa kishindo.Nasema hivyo,kwa sababu uchaguzi wa Marekani ni tofauti sana na uchaguzi kama wa kwetu Tanzania kwamba imekuwa ni dhahiri kujua kwamba mgombea yeyote anayesimamishwa na CCM basi ndiye Rais mtarajiwa.Na hii inatokana na ukweli kwamba bado mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania ni mchanga sana kiasi kwamba sio rahisi kupata mgombea wa kuweza kushindana kwa maana ya kushindana na mgombea wa CCM.Hali ya hapa Marekani ni tofauti sana.Vyama vyote viwili vina nguvu sana.Natukumbuke kuwa huu ulikuwa ni uchaguzi wa kura za maoni ndani ya vyama,sio uchaguzi halisi.Kukubalika kwa mgombea ndani ya chama hakutoi nafasi ya moja kwa moja kukubalika kwa wapiga kura wote.Hilo lazima lieleweke.Nafahamu kuna baadhi ya wapiga kura waliojitokeza kwenye zoezi la kura za maoni za Democrat ambao si wanachama wa Democrat.Baadhi walikuwa ni marepublican na wengine wakujitegemea.Sasa.hawa ni wachache sana na walijitokeza baadhi ya maeneo,na wala sio kila eneo.Sasa,hatuwezi kuwatumia hawa wachache kufanya utafiti makini.Kwa hiyo linapokuja suala la kupambanisha vyama,yako mambo muhimu ya kuyaangalia kwa kina.Jambo moja ambalo wachambuzi wa mambo wamekuwa wakiliangalia japo si kwa njia ya uwazi sana ni suala la uwezekano wa mtu mweusi na mwanamke kwa pamoja kuweza kuchaguliwa kushika madaraka ya juu sana katika taifa hili la wahafidhina.Sasa hili nalo linawaumiza kichwa sana mademocrat.Ingawa hawezi kulisema hadharani,lakini sirini wanalizungumza.Na ndio maana narudia kusema kwamba ili mademocrat watumie mwanya wa ushindi unajionesha mbele yao,ni lazima mama Clinton ashiriki kikamilifu katika kuonesha uzalendo wa kweli kwa chama chake ili kiweze kushinda.Moja ya uzalendo unaopendekezwa na wengi ni kwa huyu mama kujitoa muhanga na hivyo kutoifukuzia nafasi ya mgombea mwenza.Na badala yake apendekeze mtu (mwanaume mzungu)wa kutoka kambi yake wa kuweza kuambatana na Obama kwenye kinyang'anyiro cha urais.Hili wala halina dhana ya ubaguzi wa rangi wala jinsia.Hii ndio Marekani,huwezi kuyakwepa mambo haya,vinginevyo utakuwa ni unafiki mkubwa.Na katika kufanya hivyo ni lazima mtu huyo anapendekezwa atokane na majimbo makubwa ambayo mama Clinton ameonekana kuungwa mkono sana,majimbo ambayo pia ndiyo yaliwapa ushindi marepublican mwaka 2004. Mfano ni jimbo la Ohio na mengine.Katika majimbo haya kuna wafuasi wengi wa mama Clinton ambao kwa kitendo cha mtu wao kushindwa,basi wao hawaelewi somo.Hawako tayari kwa lolote hata kama mama huyu atakuwa mgombea mwenza.Walichotaka wao ni Urais sio umakamu.Sasa watu wa namna hii ambao ni wengi,lazima ipatikane mbinu ya kuwabana wasije wakawapigia kura marepublican,maana wanaweza kabisa kufanya hivyo.Moja ya mbinu ni kuwapa mtu wao,mfano magavana wao ambao walikuwa wanamuunga mkono mama Clinton kwa nguvu zote.
    Kwa hiyo bwana Michuzi,kwa mchambuzi yeyote makini wa siasa za hapa Marekani,hawezi kuja na jibu la mkato na haraka haraka,kwamba lazima Obama(Democrat)washinde uchaguzi ujao,ingawa ni kweli wanaweza shinda.Yapo masuala mengi ya msingi ambayo wapiga kura wa hapa watahitaji kujiridhisha nayo kabla ya kuamua chama gani kipewe dhamana ya uongozi.Baadhi ya masuala hayo mbali ya nililozungumzia hapo juu ni pamoja na kumjua mgombea kwa kina juu ya imani yake,uzoefu wake linapokuja suala la usalama wa nchi (jambo ambalo ni muhimu sana kwa wamarekani),sera za nje,uchumi,afya,ukosefu wa kazi nk.Kwahiyo,swali lako bwana Michuzi bado ni tata kwa sasa.Ngoja tusubiri tuone nani atakuwa mgombea mwenza wa Obama ndipo tunaweza angalau kupata mwanga wa kuweza kuchambua kwa kina kama kweli Obama atalivusha jahazi la mademocrat hapo mwezi Novemba.Hapa pia tutaangalia nafasi ya Obama(Democrat) mbele ya chombo kijulikanacho kama "Electoral College-EC".EC ni chombo muhimu sana kwa mfumo wa uchaguzi na siasa za hapa Marekani kwani kwa utaratibu ndio huamua nani awe Rais na Makamu wa Rais wa Marekani.Tukumbuke mwaka 2000 chombo hiki ndicho kilichowanyima ushindi mademocrat pamoja na kuwashinda marepublican kwa kura za jumla"Popular Votes"Mpaka sasa EC ina wajumbe 538 wanaotokana na idadi sawa na ile ya maseneta na wawakilishi wa majimbo ndani ya Bunge la Marekani.Kwa hiyo,wadau kwanza ndio kumekucha,safari ni ndefu ingawa kila mtu anaweza kutabiri anavyotaka.Lakini,ukweli ni kwamba ushindi wa nafasi ya urais wa hapa unaenda mbali zaidi ya kutabiri.Ni lazima kuwe na uchambuzi wa kina wenye kuzingatia mahesabu halisi pamoja na masuala ya msingi kwa wamarekani.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 06, 2008

    HEY MSIMCHAGULIE OBAMA VP.YE ANAJUA WA KUMCHAGUA NA SABABU ANAZO PIA NAONA UMU WADAU WENGINE NI WATU WALIOKATA TAMAA.KUNA MDAU ANASEMA WANAWEZA MUUA.ANATAKA KUSEMA KWAMBA JAMII NYINGINE AMERICA IOGOPE KUGOMBEA NAFAS YA JUU KWA SABABU IYO.
    UO NI UPUMBAVU NA KUTOJIAMIN.KUMBUKEN KWAMBA JESSE JACKSON ALISHAJARIBU KUGOMBEA KWA DEMOCRATIC TENA KIPIND CHA UBAGUZ NA AKUOGOPA.
    TUNAITAJ WATU WAJASIRI NA WANAOJIAMIN PIA WALIOJITOLEA KUTUMIKIA JAMII BILA OFU.
    IVO ONDOEN IMAN POTOFU YA KUSEMA KWAMBA ANAWEZA ULIWA.UO NI UPUMBAVU NA UJINGA.
    PIA MNAOTUITA WA UGHAIBUN KUWA WABEBA MABOKS TUTAACHA KUWATUMIA ELA PUNGUZEN ZARAU.TUTASTOPISHA MISAADA ALA!
    WITO WANGU KWA WADAU NI KUWA WENYE UFINYU WA MAWAZO,UZALENDO,PIA MAFISAD WAJIREKEBISHE.
    TUNAITAJ MABADILIKO SASA.
    NA WATU WA KULETA MABADILIKO NAAMIN SIYO WAZEE NI JAMII YA SASA AMBAO VIJANA.
    VIJANA WENGI WA TANZANIA WANAOGOPA KUGOMBEA NAFASI ZA JUU KWA KISINGIZIO WATAULIWA NA WAZEE WALIOKO KWENYE NAFASI UO NI UFINYU WA MAWAZO NA KUKOSA UZALENDO.
    MWISHO ALIOKO JUU MFATE USISUBIRI ASHUKE KWAN UTASUBIRI MILEE.
    MAISHA BORA YANAKUJA KWA JUHUD ZA MTU,WANAFUNZ MSOME SANA,WAFANYA KAZ MFANYE KAZ KWA BIDII.TANZANIA BADO MASKIN SANA UKITAKA KUAMIN ILO TEMBELEA NCH NYINGINE UONE.
    MUNGU BARIKI TANZANIA
    IN CHANGE WE CAN BELIEVE IN

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 06, 2008

    mdau unaeitwa kada Tumsifu nimekupata mkuu,kila laheri Obama

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 06, 2008

    Jamani tunashabikia Obama Obama!!tunaacha ya nyumbani kwetu,kwani huyo Obama atawasaidia nini?mbona hamuongelei CCM,CHADEMA.TLP NA NCCR MAGEUZI?au mnataka tujue kwamba mko Marekani?mnaangaika bure hata huyo Obama mwenyewe hawajui,tukae chini na sisi tufikirie namna ya kuiangusha Ccm sio kukalia tuu Obama Obama!!mdau Leknes

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 06, 2008

    Kada ndugu yangu, Obama hamuitaji mama clinton kuwa mgombea mwenza. Wewe inaonyesha unaijua vizuri siasa na hostory ya US. Kuna kitu wanaita Balancing of Card kwenye swala la uraisi wa US (government 101), Mama Clinton habalance card bali anakuja na skeleton wake kwenye closet. Unawajua vizuri kabisa GOP wanaongoza kwa dirty politics, so Obama hawezi kurun campaign ya change kama yupo na Mama sababu GOP will crash him to the bones.

    Kingine kama Obama atamchagua HRC then Bill atamuweka wapi? Bill anatabia ya kuvuta Oxygen yote mahala alipo. White house is too small to have two presidents. Bill is always out of control, na Obama hana uwezo wa kumzuia.

    I think Obama inabidi tu amwambie kwamba mama i have alot of respect from you, i will campaign kwako kama unataka ugovernor wa NY au Kama unataka nafasi kwenye suprime court i will give to you. But this is my time let me run this campaign.

    Democratic haitaji majority ya white votes kushinda. It has never happened like that before, nenda kaangalie ushindi wa Democratic legends kama JFK au FDR utaona wote walizama madarakani kwa minory votes + whites. Obama ana potential kubwa sana kushinda kwa 40% ya white na akamalizia the land slide na minority.

    Obama bado ni junior politician, hana experience hata ya miaka miwili kwenye full time senate. Kumbuka amekuja madarakani 2004, then 2006 ametangaza kwamba anagombea kwa kupitia Democratic ticket, bado ana matatizo kwenye foreign policy (center point ya Republican), ili kubalance hii lazima aweke mtu mwenye military back ground. Mtu kama Gen. Wesley Cleark, au Sen. Webb (VA)au Joe Biden. Kumbuka vile vile Obama hana credential kubwa kwenye excutive leadership, hapo ndipo anaweza kumchukua mtu Penny state governor Rendell au Kansas Governor.

    McCain ana strong experience japo kuwa watu wengi wasio na idea na American experience wana mu-underestimate. Kuna mengi yanaweza kufanyanyika between now and Nov. Kumbuka Barack alikuwa anashinda kuanzia S. Carolina, lakini baada habari ya Jermia Right and Rascoe kuchukua sura nyingine kwenye media, then sen. Obama lost 7 battles i think.

    Kuhusu swala la wanawake they will always vote democratic no matter what. McCain ni antie abotion wanawake knows that, wanajua anapossibility akachagua two or more suprime Judge, which will be conservatives. Na plus Allito and Robert that will be 5 conservative then wanaweza kuoverturn swala la abotion. So, women will vote kwa Obama any way.

    Last tegemea new electro vote Map mwaka huu, usiwaze kabisa kwamba Ohio itakuwa determinant state. Angalia sana Georgia, Colorado, New Mexico, Kansas. Na Obama akimchukua Rendell angalia Penny state itarudi kuwa Blue.

    Goo Obama 08'
    Mdau wa US tawi # 1

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 06, 2008

    Obama lazima atashinda Urais wa Marekani kwa mujibu wa hali halisi ilivyo kisiasa nchini Marekani na Ulimwenguni kwa hivi sasa.Hillary Clinton hawezi kuchaguliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Obama tokana na sababu mbalimbali.Atampa wakati mgumu sana Obama katika kufanya maauzi iwapo Hillary Clinton atateuliwa kuwa Makamu wa Obama.Na Democrats wanalitambua hilo.Kiburi cha Hillary kinasababishwa zaidi na mumewe Bill Clinton kutokana na wadhifa wake kama Rais Mstaafu wa Marekani kwamba anajua sana na alisifika sana kwa kujenga uchumi imara sana wa Marekani na kwamba Obama bado bwana mdogo sana katika siasa na hana ujuzi wala uzoefu wa kutosha kwa maoni ya kambi ya Hillary Clinton.Sasa hoja kama hiyo haina mantiki yoyote katika siasa.Uzuri wa Obama ni kwamba ana 'cut across' hata kwa kambi ya chama cha Republicans cha kina Bush.Na hivi karibuni Rais George W. Bush mwenyewe alisikika akimpongeza Obama mwenyewe binafsi kwa ushindi alioupata dhidi ya Hillary Clintin.Isitoshe Obama anaongozwa na Timu ya watu wazito sana ndani ya chama cha Democrat ambao wasingependa kuona 'majivuno' ya kina Clinton yanarejeshwa ndani ya White House.Hillary Clinton kama ataridhia pengine ataambulia nafasi nyeti kama Secretary of State au nafasi nyingine ya uwaziri katika cabinet.Leo Obama alikutana na Hillary Clinton kwa faragha katika nyumba yao kina Clinton ya Washington DC kuzungumzia mustakabali wa chama chao cha Democrat sasa kwamba Obama ameshinda lakini Hillary Clinton naye akiwa na wafuasi wake wengi sana karibu milioni 18 walio muunga mkono.Kesho Jumamosi Hillary Clinton anatarajiwa kutoa tamko lake rasmi kuhusu ama kumuunga mkono Obama kwa maslahi ya chama chao cha Democrat ili kipate ushindi mnono dhidi ya chama cha Republican cha McCain AU kutomuunga mkono Obama na kusababisha mpasuko ndani ya chama cha Democrat,jambo ambalo halitarajiwi kutokea.Kwasbabu likitokea Hillary Clinton mwenyewe atakuwa amejimaliza kisiasa.Kwa upande mwingine,mgombea wa Republican MacCain japo ni mzuri na ana uzoefu mkubwa sana wa masuala ya kivita lakini anakabiliwa na tatizo moja UZEE ULIOPITA MSTARI ikilinganishwa na mikikimikiki ya shughuli za uongozi wa Urais wa Marekani.Atakacho takiwa Obama kufanya ili kuziba pengo hilo na kujizolea kura nyingi tu kutoka kwa vijana walioko katika chama cha Republicans ni kuwahakikishia kwamba mambo ya kimsingi yanaopiganiwa na chama chao cha Republicans,yeye Obama atayalinda na kuyatekeleza.lakini wakati huo huo bila ya kuwaudhi wafuasi wake wa chama cha Democrat.Suala la Rais wa kwanza Mweusi nchin Marekani halipewi umuhimu hapa kama wengi watakavyo fikiria,cha muhimu zaidi ni Uwezo wa kufikiri,kuchambua mambo,kuyatolea tamko au maamuzi sahihi na hatimaye uwezo wa kuzungumza katika halaiki ya watu na watu wanao kusikiliza wakatafakari nu kuzikubali hoja zako.Sasa Uwezo wote huo Obama amedhihirisha wazi kuwa nao.Kama nilivyo sema Obama anaongozwa na Timu nzito sana ya Wazee wa Democrat wanaokibeba na kukilea chama chao.Obama amefuata nyayo za Baba zake KIFIKRA NA KISIASA kina Marcus Garvey,Martin Luther King,Jesse Jackson,Andrew Young,Condoleeza Rice na wengine wengi.Tumwombe Mwenyezi Mungu amshushie heri na baraka ili apate ushindi.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 06, 2008

    muulizeni shekhe Yahya

    ReplyDelete
  29. Mdau 9.05pm, kazungumza suala la maana. Kweli Obama akichaguliwa inapendeza, ila kushinda kwake sidhani kama kuaisaidia Tz lolote, yeye atakuwa ni rais wa Marekani na ata serve for Americans people and interests of Americans no matter what happen. Hivyo ni vizuri tuangalie mambo yya nchi yetu na bara la Africa kwa jumla. Kama mabadiliko yawepo ndani ya nchi yetu, ya Marekani tuwaachie wenyewe. Labda tujiulize ni Afro-Americans wangapi wamechangia maendeleo ya Tz au kuwekeza Tz? Tujivunieni asili zetu, maana Afro-Americans ki ukweli hawajioni kama wao wana belong kwetu. Ni mtazamo tuu wadau.

    Mchangiaji.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 06, 2008

    MDAU KADA, WA 6.32AM, NIMEPENDA UCHAMBUZI WAKO.

    NAOMBA WATU WENYE MAPENZI MEMA NA SIASA SI ZA MAREKANI TU WASOME HUO UCHAMBUZI WAKE NA NADHANI HAPO NDIPO UKWELI ULIPO.

    "YOU DON'T HAVE TO BE LOVED BY EVERYONE...YOU NEED TO BE LOVED BY JUST RIGHT PEOPLE..." LAKINI HII KAULI INAFANYA KAZI KWENYE HATUA HII YA AWALI. OBAMA KAPENDWA NA "DELEGATES" NA "SUPERDELEGATES"....LAKINI CLINTON KAPENDWA NA WAPIGAKURA HALISI KWA KUWEZA KUMSHINDA OBAMA KWENYE "POPULAR VOTES" NA POPULAR VOTE NDIYO INAMCHAGUA RAIS WA MAREKANI KWENYE UCHAGUZI WA RAIS.

    NDUGU ZANGU HUO ULIKUWA NI UCHAGUZI WA MGOMBEA NA SI UCHAGUZI WA RAIS.

    I PERSONALLY LIKE OBAMA BUT HE STILL HAVE A LONG WAY TO GO...AND IF AND ONLY IF WILL DARE TO IGNORE MRS CLINTON I'M SURE HE WILL HAVE TO HAVE EXTRA MILE TO GO, THAT IN MY OPINION...IS GONNA BE HARD WAY.
    SO THE ONLY ATTRACTIVE CHOICE AVAILABLE TO MR.OBAMA IS TO INVITE CLINTON TO BE PART OF HIM.

    THE BOOTOM LINE IS "HE IS A MAN OF JUDGEMENT AND I'M SURE HE'LL MAKE RIGHT DECISSION".

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 06, 2008

    Ni kweli Obama atashinda. Na siku ya kuthibitishwa rasmi kuwa mgombea wa Democrat pale Denver ni siku ya kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. Jiandaeni kusikiliza speech yake. Kwani kuna kundi la wsomi hapa Chuoni kwangu wanasema wataahirisha masomo. Because the guy can deliver. Kuhusu kumchagua Hillary hata mimi simuungi mkono kwani huyo Mama anaoenkana ni mbishi sana. Hivyo atamfanyia ubishi ktk kutekeleza sera zake na baadaye atakaa pembeni na kusema mnaona nilisema msimpe huyu kwanza ni mweusi pili alitaka umaarufu. Lakini kuna tetesi kwamba wanataka kumpa ili ainue uchumi wa nchi kama ataweza which they believe so, but how? That's their question. Kumbukeni siku alipozungumza wakati wa kuthibitisha Jonn KErry 2004, speech aliyoitoa ndiyo wanaokumbuka ndani ya Democrat waliona huyu jamaa anafaa kutokana na historia yake pale Havard.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 06, 2008

    WADAU NI KWA NAMNA GAN TUNAWEZA WATOA MAFISAD KWA NJIA YA AMAN NA UTULIVU SABABU ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA NI WAJINGA WAKIPEWA KOFIA NA MGOMBEA NAFAS WANAAMUA KUMPA KURA WANASAHAU UFISAD ALIOFANYA.
    IV LEO WATANZANIA WALIO WENGI WASHASAHAU KUHUSU RICHMOND.
    NAOMBA WADAU MCHANGIE TUFANYAJE.
    MAMBO YA OBAMA YAISHE TUANGALIE YANAYOTUHUSU KWANZA.
    MNASEMAJE WADAU

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 06, 2008

    mi na mambo 3.

    1. Napenda kupingana na wanaosema Rais wa Marekani hawezi kusaidia Tanzania. Si kweli. Rais wa Marekani anaathiri nyingi nyingi sana kiuchumi. Mfano, Bush kupeleka vita Iraq imeathiri sana bei ya mafuta na kupelekea bei ya vitu kupanda. Mfano mwingine ni tishio la 'Recession' marekani ambalo limeyumbisha uchumi wa dunia nzima ikiwemo mataifa makubwa kama Uingereza.
    Hivyo naamini kuwa kama kutakuwa na Rais bora, itasaidia ku stabilize uchumi wa Marekani na kwa kiasi fulani uchumi wa dunia. Ukumbuke kuwa 'curreny' inayotumika kwenye biashara ni dola ya marekani.

    2. Suala la kufurahia Obama kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Democrats si baya. Kwani hili linaweza kutizamwa na katika pande tofauti. Moja wapo ni kuwa ameweza kufika hapo alipo na hiyo inatoa matumaini kwa watu wengi.
    Vile vile, wengine wanafurahi kwa kuwa ni mtu mwenye damu nyeusi, hivyo ni ushabiki. Labdo tujiulize, kushabikia Liverpool, Arsenal, Chelsea ama Man U kunakusaidia nini wewe? Utagundua kuwa ni ushabiki na mapenzi. Hivyo, hali ya watu kufurahia ushindi wa Obama, ni ushabiki na mapenzi kwa kuwa ni mtu ambaye ana kipaji. Kama umeshawahi kusikiliza hotuba zake, utamkubali.

    3. Ni kweli kuwa Obama ana safari ndefu. Na wadau wamechambua kwa kina nafasi yake katika uchaguzi mkuu.
    a. Suala la popular votes ni kweli Clinton kaongoza, lakini ujue Clinton alikuwa anajulikana sana kabla ya Obama. Vile vile popular vote imehusisha majimbo ya Michigan ana Florida ambapo wote hawakufanya kampeni. Naamini kama Obama angefanya kampeni kwenye yale majimbo mawili, angekuwa na nafasi bora zaidi.
    b. Obama alikuwa ni 'underdog' kabla ya uchaguzi wa Iowa. Lakini ameweza kumshinda Clinton (delegates) ambaye ni 'super power' ndani ya chama cha Democrats.
    Timu ya kampeni ya Obama ilijiandaa vyema na ikaweza kumshinda Clinton kimapato.

    Uchaguzi mkuu ni mgumu, lakini naamini si lazima kumfanya Clinton VP ili aweze kushinda. Kwa mtazamo wangu naona atakuwa amejigeuka na kurudisha siasa za zamani 'The way Washington do business' ambazo yeye anazipinga.

    Naamini jambo moja: KAMA AMEWEZA KUFIKA HAPO ALIPO, INA MAANA HAJABAHATISHA. HIVYO, LOLOTE LINAWEZA KUTOKEA KWANI ANA WASHAURI WAZURI NA YEYE MWENYEWE ATAPIMA MAMBO KULINGANA NA WAKATI.

    Maoni yangu ndio hayo

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 06, 2008

    Nyie watu wengine mnaoweka maoni kurasa tano sijui mnategemea watu wayasome au? wabongo bwana kwa ungwini.mnategemea watu wote hawana cha kufanya kama ninyi,au mnadhani mkiandika kifupi watu watajua kuwa hamjui au? ndiyo maana kuna maktaba kwa wale wanaopendele kusoma kwa kirefu, humu tunadonoa tu acheni mambo yenu kama mnamiss shule si mrudi darasani

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 07, 2008

    BARACK (BARAKA - this is the actual name he just airbrushed the spelling as he did not know how to write it in swahili) OBAMA he has a very massive challenge when it comes to choose a running mate, according to political pundits and even from my personal view it will be a mistake to take H. CLINTON on board as a running mate as all the way he was preaching the CHANGE, then what that change will be by taking back to the WHITE HOUSE the former first lady (that means the same gin in a new bottle?), taking her he will as well taken back the former president (Mr Clinton)!!! so by doing so he will be diluting his message of CHANGE which happened to be his winning buzz word, and played a big partin hiss magic winning. Therefore he will remain with nothing to say when the general election comes in and it will be like handingover the presidency to Mr MacCain in a cleaning golden plate as he will be talking about experience he has. To me the guy is brilliant, genius and very clever and he will be the president to remember for the years to come if he wins it. Just today I was reading his book, oooo my GOD he is fantastic!!! HE MIGHT WIN IT WITHOUT SHE. BY THE WAY HE WAS THE BEST STUDENT IN HIS CLASS OF MASTERS OF LAW AT HARVARD UNIVERSITY.

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 07, 2008

    We mdau June 06,2008,10:20pm tuondolee pumba zako hapa.Wewe kama mvivu wa kusoma ni wewe tu.Tuko wadau kibao tunaopenda kusoma makala zenye uchambuzi wa kina.Sio kuja na visentensi visivyoeleweka ili mradi ionekane umeandika.Koma kabisa,acha wadau watumwagie uhondo humu watu tuelimike.Wewe kama unaona ni ndefu skip nenda kwenye vifupi vifupi ambavyo mara zote ni vya kizushi tu.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 07, 2008

    My worst fear is wanaweza kum assassinate hawa Ku Klax Klan coz they are determined to keep any black away from the presidential post.
    I suggest wamuongezee secret agents wengi wamkulinda coz I think yo uko in a very delicate situation.
    Mungu amlinde.
    Am very proud of him.

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 07, 2008

    jamani huyu Dogo ni Genius!
    Nimemvulia sio tu kofia bali hata nguo na kumpa shikamoo!
    Kuna comment niliiona kwa Huffingtonpost inasema "This is the guy who single handedly dismantled the "Mighty Clinton Machine"."
    Mama(na baba pia)wako kwenye mshtuko mkubwa hawaamini ni vipi huyu dogo mgeni kwenye viwanja ameweza kuwanok out? Halafu amehakikisha amezungukwa na ma-Genius wenzie kina David Axelrod Plouffe na Gibbs.
    Dogo alivuta watu 75,000 last month kwenye rally,(wengine 15,000 hawakuweza kuingia!) wakati babu McPori hafikishagi watu 5,000!
    Jamani tusisahau mchango wa Dada Oprah, indozimenti yake ilifungulia njia. Shukrani kwake Dada O!
    Pia jamani tusimsahau Dogo ktk sala zetu mana kuna watu wabaya sana nchi hii, na mama alivochemsha kuhusu kukumbushia yaliyompata Bobby Kennedy sijui alikuwa ana nia gani, she knows better.
    tabunot@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...