Habari za shughuli Bro.Michuzi,

Kwanza kabisa pole na mkutano huo wa Arusha. Pili ninapenda kutoa salamu nyingi kwa wadau wote wa blog hii kama kawaida libeneke, nimekutana na jamaa hapa mji wa Perugia-Italy, mtanzania mwenzangu ambae pia ni mpenzi sana wa blog hii, akaniomba tupige picha na kutoa salamu nyingi kwa wote, kwa kua mimi ni mpenzi mkubwa na wala huwa siogopi, nikamwambia haraka sana tutume salamu bila shida.


Jamaa alikuwa mchoraji kijatuni cha gazeti la uhuru hapo miaka ya nyuma, alijulikana kwa jina la mzee MANJE, kikatuni kiliitwa hivyo kwenye gazeti hilo la uhuru kama kuna mtu atakumbuka hilo.


Na huyo hapo dada tulivyo pamoja kwenye picha ni mai nanihii wake wa moyo, basi anatoa salamu sana kwako Bro. Michuzi na kukusifia sana kwa kazi nzuri unayo ifanya kutupa habari motomoto kila siku, na salamu sana kwa wadau woteeee.......!!!!!!!!!!!!!

Pia na mimi nina machache ya kuwauliza wadau hapa, nini maoni yenu kuhusu ushindi wa OBAMA kwasasa? Mimi binafsi nimefurahi kwa hatua aliyo ifikia hata kama bado hajashinda kabisa, lakini ni hatua nzuri sana.

Ni kasi mpya ya mabadiliko na kama kweli atapita basi anaweza kutoa urasimu mkubwa sana kwa pande zote Duniani, maana bado sana haya mambo yapo sana ya kudhalau sana watu weusi kutokujua kitu na kutojua uongozi mzuri, huu ni ukweli wenyewe hata kama kuna mtu atakasilika basi naomba anisamehe, hapa ninapo ishi Italy bado sana mambo haya yapo tu, sio sana lakini yapo.


Na kwasasa wamepata pigo hawaamini kabisa, ndani ya Bunge lao amechaguliwa mtu mweusi kuwa mbunge wa jimbo fulani bado sijui historia yake vizuri ila nimemwona bungeni, mimi ninasema ni pigo kwasababu hawakutegemea kabisa, kwa vijana sio shida sana nimeongea na wengi wao wanasema hiyo ni kawaida kabisa, ila kwa wazee ni shida.


Mimi nitafurahi sana Obama akishinda katika taifa hili kubwa ulimwenguni na akiongoza vizuri itakuwa ni vizuri zaidi na zaidi, kwahiyo ninamtakia kila lakheri nyingi sana ili aweze kufanikiwa. Mimi yangu ni hayo ninasubiri yenu wadau, utani umo lakini bila kuchafua hali ya hewa au sio?

Salamu sana tena sana kwako Mkuu wa Wilaya.

Ni mimi yuleyule wa siku zote!
B.F.CHIBIRITI.
Mdau Chibiriti!
Asante sana kwa ujumbe. Hakika nimefarijika sana kwa kuibuka kwako kwenye globu hii ya jamii baada ya kimya kirefu. Natumai sio mimi tu niliyekumiss na tunaomba uendelee na libeneke kama kawaida.
- Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2008

    Chibiriti wa Chibatali wa Chi Italy, chichi tilijua njomba haupo! Umeibuka, duh. Wapi my nanihiii wako mbona hukupiganae picha safari hii?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2008

    Uyo may wife wa rafiki yako ni bomba sana,nakubali ajaoa uzungu bali kaoa uzuri BIG UP

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2008

    Salamu sana kwako Chibiriti! Tulikumiss sana sana,Husipotee hivyo kaka chibiriti,Sisi Pia tunafuraha kuona huyu Jamaa aliepitia ktk uafrica na uzungu,kwahiyo yeye ni kweli african-american,kwasababu kwao kunajulikana rasmi ni africa na niwapi.Pili kaka chibiriti mie kuna project moja naaindaa iliniweze i`introduce kwa wabunge wetu na wao wajaribu ifanyia kazi,sasa sina mawasiliano yako kaka tunawezashauliana mawili matatu,Dondoo naandaa kuhusu mfumo wa utawala tz ubadilike ktk mikoa,tuwe na majimbo ambayo yanajitegemea kwa kila kitu ili maendeleo ya jimbo husika au Jimbo vivu litabaki na uvivu wao na hakutakuwa na ufisadi,sio sasa mfano Tanga au Iringa inajitaadi kuzalisha pesa zinabaki kuendeleza sehemu nyingine mfano Dar then Tanga inabaki ktk umasikini wake

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2008

    Chibiriti naona umesikiliza maoni ya watu wengi ikiwamo na mimi pia kwamba utulize ball sometimes, sio kila mara kutokea kwa Michuzi na ajenda za kichovu, thumb up kwa hilo.
    So hopefully, utatuliza tena ball and i expect to see you at Michuzi in December.
    Mdau Columbus, Ohio

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2008

    mikonozzzz chibiriti.....mke wa watu...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2008

    jamani mikonozz hailazimishwi huyo dada hapo naona amekasirika kumwekea vikwapa vyenu hata amenuna tuwe wastaarabu! na sidhani kama ana uhusiano na yeyote kati yenu! hii ni kutokana na kuisoma picha. Naomba maoni yenu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2008

    Nimekuelewa Mkuu hapo juu, kuhusu mawasiliano we nipe E-mail yako nitakuandikia, na baadae tutawasiliana zaidi, kwahilo hamna shida kabisa mimi napenda sana maendeleo ya nchi yangu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 08, 2008

    Chibiriti ndiyo yupi kati ya hao? na yeye ni nani? aulizay ataka kujua na si mjinga. shukrani!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 08, 2008

    Sawa kaka nimekupata email yangu ni isackodey@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. hodi hodi mzee chibiritu ukoo tafadhali nifungulie niko hapa nje

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2008

    chibiriti take care na mission town, oohhhooooooo,

    ReplyDelete
  12. DUH CHIBI HAFUNGUI MLANGO NIMEBISHA HODI MASAA 24 YEMEPITA AJAFUNGUA. ITALI HAPA HUWENDA KUNA TATIZO HUKO NDANI NGOJA NI CALL 911, MAANA HUKU ULAYA KILA MTU NA BUSNESS ZAKE. HAWAAJUI YA JIRANI MPAKA WASIKIE HARUFU NDIO WANAWEZA KUANGALIA KWA JIRANI KUNA NINI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...