mfalme wa pop michael jackson alipotua bongo miaka ya 90 na kupokelewa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati huo hayati diria. sio kweli kwamba alishuka akiwa amefunga kitambaa usoni kuzuia harufu kama ilivyovumishwa na kama picha inavyoonesha. hii ni mojawapo ya mapicha kibao banda la daily news na habari leo katika maonesho ya sullivan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2008

    kaka michuzi kwakuweka kumbukumbu tu nakusifu hongera sana.
    sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2008

    This has to be the best picture in a long time you have put because i never believed Michael ever came to Tanzania , Michuzi ukooo Juuu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2008

    Japo yawezekana si kweli kama ilivyovumishwa lakini hata hivyo Dar ilikua chafu sana kipindi hicho,ilikua si hatari kukuta mtu kshusha mzigo pale kwenye bustani iliyo mbele ya NBC city cooperate branch.Pia bahari ikichachamaa harufu yake ni soo.Pamoja na hayo mfumo wa maji taka City center pekee ni mbovu sana,na hali imekua mbaya zaidi kutokana ma utitiri wa maghorofa ambayo mengi ama yamejengwa baada ya msingi kuziba mitaro au juu ya mitaro ya zamani zile,mfano angalia pale kwenye jengo la ILO opposite na Africaries, au mvua inyeshe Posta mpya pale nusu saa tu bwawa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2008

    what was the point of the minister to go and collect wako jako from the airport jamani TANZANIA OH TANZANIA what is bloody WRONG WITH US? kwani kina ali akiba walipokelewa na tony blair??

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2008

    Nakupunga Siku aliyekuja michael Jackson, Nilikuwa Bunge Primary School aliishia Kilimanjaro Hotel.

    Nilimuona hapo nikiwa kijana mdogo alipewa mauwa na watoto wawili pale kilimanjaro hotel, kama kumbukumbu zangu sawa.

    Issa Michuzi kama Unasoma hii comment mtafute jamaa mmoja anaitwa Mambo alikuwa akipiga picha sana alikuwepo kilimanjaro hotel, Mambo nafikiri lazima atakuwa nazo hizo picha sababu alikuwa sana pale Kilimanjaro hotel na masuper star wa nje wengi walikuwa wakifikia hapo japo wengi wanachonga hakuwa michael jackson. nilikuwa nayo picha moja sijui imepotea wapi mambo alinipa michael jackson alikuwa kavaa shati la kijani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2008

    Tanzania bwana inachekesha kweli na protocol zake. Waziri anampokeaje mwanamuziki??????
    Kwa sababu anatokea marekani au na ninyi mnategemea Mmasai akienda Marekani apokelewe na Condolezza Rice?!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2008

    Kwa miaka hiyo ya 90 vyombo vya habari bongo vilikuwa bado havijaanza kufuatilia vituko au maisha ya mastaa wa US na hivyo kulikuwa hakuna uthibitisho kuwa Michael alijifunika pua kwa sababu ya harufu mbaya ya mji wa Dar au ilikuwa kinga kwa ajili ya pua yake isije ikamomonyoka akiwa Africa mbali na wataalamu wake ambao wangeweza kuirekebisha bila kuzua gumzo nchini. Tabia yake ya kuziba pua ameendelea nayo mpaka alipokuwa kwenye kesi yake huko California miaka michache iliyopita. Sasa swali langu ni kuwa inamaana hata huko anakoishi na anaonekana akiwa amejufunga kitambaa usoni nako kunanuka?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2008

    MICHUZI KUMBUKA; HUKU MICHAEL JACKSON ANASHUKA.
    NA WANANCHI WANAMIMINIKA KUPOKEA KOMBE LA SOKA LA AFRICA MASHARIKI NA KATI. HAKUNA MTU ALIYEMJALI MPAKA MWENYEWE ALIKUWA ANASHANGAA.
    ALIKAA KILIMANJARO KAMA SIKOSEI.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2008

    michuzi naona hapa umechemsha huyu ni waziri diria au ni raisi wa zanzibar amani karume.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2008

    Anony wa 6:10 PM unaongopa sana.
    Mimi nilikuwepo pale uwanja wa ndege na pamoja na Balozi Diria alikuwepo mama chipungahelo na watoto wake pia. Mtu kibao ilijaa uwanja wa ndege kumpokea MJ hadi barabara zote zilijaa watu na hata kilimamnajaro kulifunga. Nakumbuka saa kumi na mbili jioni alifungua mlango/patio wa chumba chake kilichokuwa kinaangalia baharini pale Kilimamnjaro hotel na watu walipiga makelele sana ya kumshangilia hadi ikabidi aombe polisi wawa-ondoe watu pale kwenye majani.Saa moja usiku alipanda benz kuelekea ikulu na aliongea na Mwinyi na kurudi kupumzika hotelini. Nakumbuka siku iliyofuata alikuwa na mipango ya kwenda mbugani na kutaka kutua na dege lake kubwa huko Serengeti na ilishindikana kwa kuwa kulikuwa hakuna uwanja wa kushukia mbugani.
    Alikwenda Sinza badala yake kuonana na watoto yatima na usiku wake kupanda ndege na kurudi USA.
    zaidi nakumbuka magazeti yalisema aliomba pillow za kulalia mpya maana zile alizopewa zilikuwa zinaonekana zinatoa harufu.
    Kumbuka MJ alikuwa tishio wakati ule hata ukimmuliza bibi yangu mzaa bibi mama yake na baba (yaani bibi yangu aliyemzaa mama yake na baba ambaye pia ni bibi) atakwambia wanamuziki aliokuwa akiwajua walikuwa Michael Jackson, Bob Marley , Makeba, Luambo Luazo Makiadi , Tabuley , Morogoro Jazz, etc.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2008

    Na mimi naikumbuka hile siku Michael Jackson kaja. Enzi hizo kino Tambaza A level. Nakumbuka kwa watazamaji, nilikua mmoja wakwanza kum-ona alivyo toka tu nnje ya Airport kabla yakukumbana na umati wa watu barabarani kuelekea Pugu road. Mimi na cousin wangu mdogo nilimpeleka kujipanga kumona. Ilikua kule Airport ya zamani, pale next to the petrol station kulikua na geti kama nakumbuka vizuri. Sisi tulikua pale pale getini kabla ya kuingia bara bara kwenda mjini. Watuwalikua wachache pale maanake ndio ni mwanzo tu wa private entrance ya old Airport. Aikuchukua dakika chache tumejipanga pale getini mara huyo Micheal alikua kwenye four wheel drive land cruiser au kibasi kidogo sikumbuki vizuri type ya gari. Lakini nakumbuka the minute gari limetoka pale kwenye side gate and out of the airport, watu wakwanza yeye kuwaona inje ya airport ilikua sisi na watu wengine wachache. Ndani ya gari, Michael alikua ana move from one side to the other dirisha la kushoto mara dirisha la kulia with excitement zake zakitoto ambazo am sure you've seen him do on tv. na vile vile kulikua na yule mtoto wakizungu bwamdogo nae kwenye gari wakishawishiana, mara left window mara right uku wakipunga mikono. Mara wakatupita na gari kukata kulia kuelekea njia going to town nakutuacha sisi pale kwenye corner by the petrol station ya old airport. Sasa huko njiani ndio kulikua na umati wa watu wakutisha walio isonga gari nakuirukia ukuwakiipiga kama makonda mabasi and the first thing Michael did was kuogopa na kuinama kupiga mbizi ndani ya kochi nyuma kwenye passenger seat na baada ya sekunde chache akajitokeza nakuanza kuwapungia mikono watu. Ata mimi nilishtuka jinsi watu walivyo ivamia hile gari. That is my vivid recollection of that day. Na cousin wangu ambae sasa nikijana mkubwa tu yuko huko bongo akisoma hii kitu atakumbuka na kujua ni nani ameandika hii kitu.

    Na mdau hapo juu umesema ukweli. Barabara ilijaa toka Airport mpaka mjini watu kumuona Michael Jackson. Lakini ndio ile siku watu kule feri na kariakoo walikua wanalikaribisha kombe kuwasili. Na nilielezwa baadae na ndugu waliokua town kwamba gari la kumbeba Michael lilivo pita nadhani ilikua mitaa ya ferri, alikuta watu wamempa mgongo wakiangalia upande wakombe na yeye akujua kwanini watu wanashangilia mitono juu uku wameangalia upande mwingine.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2008

    Anony wa 6:10 PM, namuona Prince Rachi akionekana kwa nyuma - alikuwa ni mpenzi nambari one wa Michael Jackson manake kwake yeye wa kwanza ni Michael Jackson, wa pili ni Ronald Reagan na yeye ni watatu duniani kwa umaarufu enzi zile!!

    Prince Rachi, where are you at?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 06, 2008

    isaah hii ninje ya mada kidogo, picha hiyo pia inanikumbusha mwenzie -mpiga picha Madanga Shaban Madanga yupo wapi?Mlikuwa mnatisha na mpaka sasa wewe libeneke mbele kwa mbele

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...