wadau wakiwa karibu na eneo ambako jengo la ghorofa kumi lililokuwa linajengwa lilipobomoka lote leo. habari mpya toka sehemu ya tukio zinasema watu wanne wameopoloewa na kukimbizwa hospitali. habari za awali ambazo hazijathibitishwa bado zinasema wanasadikiwa kufa baada ya kufunikwa na kifusi cha jengo hilo.
inasemekana watu hao wanne walikuwa ndani ya nyumba ya ghorofa tatu iliyo jirani na hilo ghorofa, ambapo baada ya kuangukiwa na kifusi wakawa wamenasa ndani.
hadi milango ya saa kumi watu watatu walikuwa wameshatolewa, na juhudi za kumpata aliyesalia ama waliosalia zinaendelea.


Dah! habari inasikitisha hii, sipati kusema. Utakuta majengo yote mapya yanayochipua katikati ya jiji la Kandoro ni mwendo huu huu. Nasikia mhandisi wa jiji katiwa korokoroni. Hii sidhani kama inasaidia. Hizi taasisi za usimamizi wa majengo, ikiwa ni pamoja na vyama vya wahandisi, nazo ziwajibike. Maana sidhani kama wanafanya wajibu wao wa kukagua ujenzi unaoendelea zaidi ya kula vijisenti.
ReplyDeleteHalafu nashangaa Haki hajachota habari hii hadi saa hizi. Kaka Mithubu humemuwekea biti nini, maana jamaa kwa kukopi na kupesti habari za wenzie hajambo. Najua Mithubu utaibania hii kumlinda Haki hambaye nasikia ni rafikiyo. Ukweli saa ingine uwe unaachiaga, mana jamaa anaiga kila ufanyalo, tena kwa kubembea mgongoni kwako tehe tehe tehe. Usibane Mithubu kama kweli unajali uhuru wa habari na habari ndiyo hiyo...
Poleni sana kwa tukio hili la kusikitisha sana. Nilikuwa nasikiliza Radio Maria Nimemsikia Kamanda wa Polisi kanda maalumu Dar akisema watu watatu waliopatikana wamepelekwa hospitali, ingawa hakutumia kabisa neno wamefariki. Tuombee wawe wazima
ReplyDeletepoleni sana waathirika. inawezekana wapo hai kwani niliona kwenye picha moja ktk mtandao wa global pulihers tanzania ukimuonyesha kamanda kova akiongee kwa simu na watu waliofukiwa na kifusi hivyo kama waliwahi kuwatoa huenda watakuwa hai
ReplyDelete