Tangazo la Mkutano Birmingham, Uingereza

Watanzania Wote wa Birmingham na Miji ya Jirani

Mnakaribishwa kwenye Mkutano wa Watanzania

Tarehe: 26/07/2008
Saa: 12 Jioni hadi Saa 5 Usiku

WAPI:
UKUMBI WA: THE DRUM
144 POTTERS LANE
ASTON
BIRMINGHAM
B6 4UU

Mgeni Rasmi: Balozi wa Tanzania nchini Uingereza
Mhe, Mwanaidi Maajar.
(Atatoa Hotuba Saa: 3 Kamili)


Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na:

Bi Jane Ngereza - 07799362659
Bi Lilian Barongo - 07525175337
Ndugu Raymond Mutembei - 07908124502
Ndugu Moses Katega - 07791584289

Kutakuwa na Vinywaji, Vitafunio na Muziki.

Kiingilio – BURE!!!

Wote Mnakaribishwa




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. WATANZANIA WENZANGU NAOMBA MPUUZE HILI TANGAZO LA NDUGU YETU HUYU SIO LA KWELI. NI KWELI BALOZI ATAKUWA BIRMINGHAM ON THE DATE LAKINI KUNA KINGILIO AMBACHO NI £20 COUPLES NA £10 SINGLES. NA PIA NDUGU MTEMBEI SIO MMOJA WA WAANDAAJI HIVYO MUWE MAKINI NA HILI SWALA. TAFADHAL WASILIANA NA HAWA WALIOTAJWA KATIKA TANGAZO LIFUATALO TU. ASASNTENI NA POLENI KWA USUMBUFU WOWOTE MLIOUPATA KWA AJILI YA TANGAZO HILO.
    ***********************************
    Tanzanian in Birmingham have organised
    Dinner and Dance on Saturday the 26th of July 2006
    The Venue is The Drum
    144 Potter Lane Aston,
    Birmingham.
    B6 4UU.
    Time: 19:00 - Till late.

    Guest on Honour will be
    Hon. Mwanaidi Sinare Maajar
    The Tanzania Ambassador in the United Kingdom.

    There will be an opportunity to ask questions and give suggestions.

    Food will be served between 20:00 - 21:00.
    This is an opportunity to meet with other Tanzanian as well as make your business known among us.


    You are all welcomes.


    Please Contact:
    Bro’ Katty: 07791584289,
    Denis: 07825163358
    Lilian: 07525175337,
    Peter: 07908085100
    Jane: 07799362659
    Stalick:07768183355
    Judy: 07973251851

    CARDS WILL BE £20 COUPLES AND £10 SINGLES

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2008

    mbona waandaji watu wa musoma na bukoba tu?
    wazanzibar mmewatenga? wao ndio wawakilishi wa Tanzania majuu,
    wanajituma sana na kijana wao ADAM NDITI kachaguliwa chelsea hivyo anaitangaza nchi. na kila ukienda Timu za UK lazima kuna vijana wa kizanzibar. hawa ndio wakushirikishwa sio watu wa musoma ambao wana capilize CCM na umoja wa watanzania. wanaingiza ubaguzi wa kidini na ukabila.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2008

    unahusu nini?we have work to go to,and if am going to cancel that for some nonsense al be unhappy

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2008

    mbona watu wote waliotajwa ni wa CCM? au balozi anakuja kwa ajili ya CCM? na sio kwa ajili ya watanzania kama mnavyosema? tafadhali msitubabaishe na uongo wa dinner and dance hiyo ni CCM tu, mwambieni kabisa balozi kuwa ni mkutano wa CCM sio kama mnavyosema.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2008

    mimi namuunga mkono huyo aliyepita hapo juu kuwa dinner and dance kwa wanachama wa ccm kwasababu hao waandaaji ni viongozi wa ccm birmingham na sio viongozi wa jumuia ya watanzania tafadhali tunaomba ufafanuzi zaidi, mkereketwa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2008

    Nyie wana ccm mbina mnajichanganya mara tangazo tulipuuze, mara Raymond si mmoja wenu. Mbona mnaonyesha weakness zenu au mnategemea kufisadi nini, maana huyo aliyetuma tangazo mwanzon lazima ni mmoja wenu haiwezekani akawa na taarifa zote hizo halafu mkasema tumpuuuze. It sis all about MASLAHI. te hehe hehe! mwaka huu wabongo wa majuu mtauana kwa kuandaa vijishughuli vya ulaji ili muwafisadi wenzenu.Mi siji ng'o huko Birmingham kwa nini tulipie hela wakati ubalozi unaingiza vijisenti kwenye visa kila siku, kwa nini fungu lisitokee hapo kwa ajili ya kuwakutanisha WaTz kama sio kuibiana hela.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2008

    Wanamaombi kutinga bungeni wiki ijayo

    2008-07-13 22:26:42
    Na Simon Mhina


    Kamati ya Umoja wa Makanisa ya Kikristo nchini, imemuandikia barua Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, ikimuomba awaruhusu waende Dodoma kulizunguka Bunge kwa ajili ya maombi na kusisitiza kwamba hawaamini taarifa iliyotolewa na Polisi kwamba unga uliopatikana ndani ya jengo hilo haukuwa na uchawi.

    Kadhalika, Kamati hiyo imewashauri mawaziri na wabunge wenye hirizi kuzisalimisha kwao kabla ya kuanza maombi kwani wanaweza kuumbuka.

    Pia Kamati hiyo imesema hatua ya Naibu Spika kufunga mjadala kuhusu `unga wa uchawi` haiwakatishi tamaa kufanya maombi hayo.

    Kamati hiyo imesema taarifa ya polisi imewachanganya na sio sahihi kwa sababu dola haiamini mambo ya uchawi.

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamti hiyo, Askofu Isack Kalenge alisema uchunguzi huo wa Polisi, Mkemia Mkuu, Bunge na Usalama wa Taifa ni batili kwa kuwa vyombo hivyo ambavyo viko chini ya serikali, havina uwezo wa kutambua uchawi.

    Askofu Kalenge, ambaye ni kiongozi wa Kanisa la Pentekoste International, alisema wanaamini kuwa bado uchawi upo bungeni na wabunge wengi wanateswa na nguvu hizo za giza.

    ``Uchawi ni jambo la kiroho, haliwezi kupimwa kwa kamera wala uchunguzi wa Mkemia Mkuu, tunaamini tatizo la uchawi bungeni halijapatiwa ufumbuzi, tunakwenda Dodoma kulimaliza tatizo hilo ili lisitokee tena,``alisema.

    Akizungumza katika mkutano huo, Mchungaji Wilbert Ngowi alisema kamati hiyo haiwezi kufumbia macho taarifa hizo, kwa vile zimeliaibisha Taifa.

    ``Umefika wakati sasa kanisa liseme yale ambayo lilikuwa linayafumbia macho na lifanye mambo ambayo yalikuwa hayafanyiki, japokuwa hatua hii inaweza kutafsiriwa kwamba tunachanganya dini na siasa, lakini si vibaya.

    Kuanzia sasa tumeamua kuchanganya dini na siasa kwa sababu maandiko matakatifu yanasema kufanya hivyo sio dhambi,``alisema.

    Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji Christopher Mtikila alisema iwapo watapata ushirikiano wa Spika wataenda bungeni wiki ijayo.

    Akifafanua, kiongozi huyo alisema wamemuomba Spika awape kibali cha kuingia bungeni kuwaombea wabunge na `kuharibu` nguvu za giza zilizojaa humo.

    Mchungaji Mtikila alisema kabla hawajatia mguu Dodoma, wanawataka Wabunge, mawaziri na yoyote ambaye anatembea na hirizi aisalimishe kabla hawajaanza maombi.

    ``Ni matarajio ya Kamati kwamba wabunge wazalendo, hususan wale ambao hawatembei na hirizi vibindoni, watafurahia kazi hii njema ya watumishi wa Mungu yenye lengo la kuwaponya,``alisema.

    Kiongozi huyo alisema iwapo watakataliwa kufanya mambo hayo, watalizunguka jengo la Bunge hilo na kurusha `makombora ya sala` na kuahidi kwamba hakuna mwanga wala hirizi itakayosalimika.

    Aliahidi kuwa wabunge na mawaziri, ambao ni wapenda uchawi, wataumbuka vibaya kutokana na sala hizo.

    Alisema tayari waumini mbalimbali wameshaanza kufunga kwa ajili ya kujiandaa na sala hiyo.

    Alisema hawatarajii upinzani kutoka kwa Bw. Sitta kwa sababu hivi karibuni Spika huyo alinukuliwa akiwataka viongozi wa dini, kuliombea Bunge kutokana na kuwa katika wakati mgumu.

    ``Sisi tumeamua kwenda kuliombea Bunge kama alivyosema, ila sisi tutaenda na mamlaka makubwa, ambayo yatasambaratisha kila roho chafu.

    Sisi wenye macho ya kiroho tumejua kwamba pale ndani pametundikwa kila aina ya uchawi, lakini hakuna hata mmoja ambao utasalimika,``alisema.

    Akizungumza na Nipashe jana, Spika wa Bunge, Bw. Samweli Sitta, alisema bado hajapokea barua hiyo.

    Hata hivyo, Spika alikataa kuzungumza iwapo atawaruhusu kutekeleza azama yao hiyo mara atakapopata barua yao.

    ``Hilo unalouliza ni jambo jipya, lakini siwezi kulisemea kwa vile sijapata barua yenyewe. Ni vema ukaandika zaidi maoni ya hiyo kamati,`` alisema.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2008

    Mbona inakuwa kama ni Mradi fulani hivi, kwanza wkenye Actual Advert kiingilio bure na waandaaji ni wachache, lakini ilivyokuja kuwa na waandaaji wengi ndio naona na waadaji nao wameongezeka, KUMBUKENI HATUPIGI BOX KWA MAMBO YA KIJINGA................

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...