Kikosi kamambe cha Break Point kabla ya mechi yao (juu) na chini ni baada ya kuwasili a-taun. chini kabisa timu ikiwa Kibosho nyumbani kwa mwanachamaDr. Deo Mushi ambapo anaonekana Bw. Fredito 'Mopao' Zacharia (Makumbusho)anaonekana akionja mbege.
Club ya Brake Point veteran ilitembelea Arusha wakati wa sikukuu yasabasaba kwa mwaliko wa Club ya New Executive Eleven ya Arusha na kucheza mchezo wa kirafiki na wenyeji wao. Katika mchezo huo Brake Point iliwabugiza wenyeji magoli 10 - 1, ambapo kivutio na 'man-of-the-match alikuwa Bw. Imani Madega ambaye alifunga magoli matatu, moja akiwa kawala chenga safu yote ya ulinzi ya New Executive Eleven pamoja na kipa wao.
Alopohojiwa na globu hii ya jamii baada ya mechi, Madega, ambaye pia ni mwenyekiti wa Yanga, alisema kilichomuwezesha kufunga 'hat-trick' ni fomyula mpya ya wana jangwani waliyokuja nayo msimu ujao wa ligi.
Magoli mengine yalifungwa na Bw. Ladis Mwamanga (2), Kabuche Muula (2), Rodrick Mwambene (2) na Evarist Hagira (1).


Kaka Lady Mwamanga salam kwako mkuu.
ReplyDeleteKila la heri nimefurahi kukuona.
piusmicky@yahoo.co.uk
Kuala lumpur-Malaysia
hahahahaa
ReplyDeletekweli hiyo ni kali ya mwaka,hongereni break point but pamoja na hayo mbona jezi zenu tshirt na bukta hazifanani namba?au ndo mahesabu yalikuwa hivyo?maana naona mwenye jezi no 10 bukta no 3 then mwenye no 5 bukta yake no 9. hii imekaaje?au ndo ilikuwa kuwachangaya vijana wa half london huko?mtakosa mwaliko siku nyingine mkitoa dozi kubwa hivyo....
ni hayo tuuu