
Leo hii timu kamambe ya Fc Bongo ya helsinki imeweza kuwabamiza timu ya Congo goli 1-0 na kujiongezea matumaini ya kuingia katika nusu fainali za michuano ya PREVENTION CUP HELSINKI.
Kesho Jumanne vijana hawa wa FC BONGO watachuana na Nigeria ambao leo hii wamewabamiza Greece goli 3-0 na kuwa sawa kwa pointi 6 kwa 6 na FC BONGO.
Goli la FC BONGO lilifungwa na sentahafu Ubaldino baada kuachia kigongo cha mita 30 kuelekea golini.. Wakongo walijitahidi kurudisha goli hilo lakini ukuta wa FC BONGO ulikua ngangari kinoma.
KILIMANJARO STOCKHOLM MPOOOOO?


Hili chama nimelikubali, yaani washikaji wamekaa kama wachezaji wa kikweli-kweli.
ReplyDeleteGood on you boys
kilimanjaro fc wanatisha ulaya yote ndio wenye timu nzuri,soma squad 1 kablau, bandari mtwara,machupa simba sc,william john simba sc,ahmed dadi yanga african,kally ongara yanga african,jameel jabir moro utd,abui moro utd,zak dadi kumbukumbu,
ReplyDeleteHongera fc bongo, hivyo ndivyo tunavyotaka, wafungeni huko angalau watu waitambue Tanzania yetu kwamba kitale kipo ila basi tu mafisadi wengi wanaturudisha nyuma.
ReplyDeleteKeep it rollin Bongo F.C.
ReplyDeleteWee anony wa july 21, 2008 1:41 PM,
ReplyDeleteHao wachezaji wako wa yanga na simba watacheua tarehe 16 august fc bongo wakitia nanga huko stockholm. Tutaigeuza fc kilimanjaro kuwa fc Meru. Fc Bongo ni noma, vijana wadogo wamekulia kwenye maacademy huku wanacheza kitale kwa vipimo sio hao jamaa zako chenga twawala.
Haya vijana wetu na wakubwa FC Bongo uzi ule ule. Nakuona Morinyo.... Huyo AK hapo anshtua...
ReplyDelete