maandalizi kabla ya mechi huku bendera yetu ikipepea juu

kocha akiwapa lekcha kabla ya kuingia uwanjani
fc vito kabla ya kuanza mechi yao na ufini

manahodha na refa kati ya uwanja
ufini


mchezo baina ya fc vito na wenzao wa ufini ikiendelea. chini ni kabla ya mechi kuanza
Leo Hii katika mashindano ya Helsinki Cup Finland, Vijana wa Kitanzania wenye umri wa miaka 11 kutoka mtwara FC VITO wameweza kupata ushindi wao wa kwanza kwa kuwafunga vijana wenzao wa kifini wa NUPS goli 5 - 1. kesho wanacheza mechi zao mbili za mwisho za raundi ya kwanza.
matokeo mechi ya kwanza 2 -2 watoto kiwango chao kilikua kizuri ila tatizo size na nguvu hawana mechi ya pili ndio ilikua kazi walikutana na kipigo cha zaidi ya mabao 7 hata nilipoteza mahesabu na wao walishinda 1 mechi ya tatu sikuwepo ila nimesoma kwenye web yao wameshinda 5 - 1 na kesho wanamechi zingine mbili





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2008

    hongereni wanetu!kwa kweli ni wa kupongezwa kwani kutoka mtwara hadi finland na umri huo ukizingatia na mazingira ya huko mimi binafsi nawapongeza sana!
    hembu angalia picha ya kwanza inaonyesha walikuwa na woga flani wamejikunyata au baridi nadhani wakizoea watafika mbali.
    hongereni watoto !itangazeni bendera yetu .

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2008

    Hongera sana kwa wachezaji na timu nzima. Hasa hao walioweza kuandaa safari hii. Vijana watakuwa wamepata uzoefu hapo japo kidogo.

    Kuna vijana wengine wapo Reading wanajiita TYSCO wana moyo kama huu wa kukuza vipaji vya watoto wetu Tanzania. Hebu watafuteni mshirikiane huenda huko mbeleni safari kama hii ikaunganishwa na mechi nyingine hapa UK na kwingineko.

    Mdau UK

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2008

    I hope walionywa kabisaaa wathithubutu KUBADILISHANA JERSEY... Wapi CANAVARHO...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2008

    mmmh vitoto vya kwetu viandunje kidogo.sijui mlo sio wa kutosha?,kama umri unaendana na hao wa finland unaona tofauti kati ya watoto wetu na watoto wa finland

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2008

    Haya mashindano yanafanyika Finland au Norway? Ninavyojua mimi hayo mashindano yanafanyika Finland. Kuna mashindano kama hayo yanaitwa Norway Cup yanafanyika mwishoni mwa Julai

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 09, 2008

    hivyo vitoto vyetu ona vinavyotia huruma hapo juu wakaviacha vinakumutwa na baridiiii!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2008

    Hongereni watoto wetu!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2008

    Watoto wa kwetu andunje sababu ya msosi. Hao wa kizungu wanatia msosi wa afya kuanzia wakiwa wadogo kabisa, hao wa kwetu mlo mara tatu tu kwa siku hakuna snacks wala nini zaidi ya uji chips dume.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 09, 2008

    FC Vito wanaonekana ni wadogo kiumbo ukilinganisha na hao wa ufini.

    ReplyDelete
  10. kwanza kabisa napenda kuwapongeza hao FC Vito kwa jinsi walivyotuwakilisha.

    Kuhusu matokeo mi sioni jambo la kushangaza au kuwalaumu watoto.

    Mara ngapi timu kubwa zipagwa hadi 12(rejea mechi moja ilifanyika kirumba mwanza miaka ya tisini).

    Kwanza watoto wetu unaweza kukuta walipofika tu hata hizo jezi ndio mara ya kwanza kuvaa,Uwanja labda nyasi bandia ndio mara ya kwanza kuchezea.

    Kucheza na "wazungu" ambao hata baadhi ya viongozi wetu bado wanawaogopa ndio maana wanasign mikataba mibovu.

    Kingine "ulaya" mazingira mageni na kabaridi kaufini hakaeleweki.

    Mwisho mbana hata BONGO FC na kuishi miaka yote Ufini walichapwa na wababe wao Tampere hamkusema?

    Mwisho hata mtuma habari mwenyewe ingawa anaonekana kuwa na side bado anatuchanganyia maelezo..mara Norway wakati mtanange ulikuwa ufini.Sasa kama mtuma habari tu kachanganyikiwa na ukubwa wake ..itakuwaje kuhusu madogo

    Hongera waandaaji na timu zima ya Fc ..BIG UP kamanda Dj Ezza naona unawapa mawaidha watoto wetu.

    Naamini tutafika tu

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 09, 2008

    We Edwin naye wacha kuropoka! Kwani Bongo FC inahusiana nini na hii habari? Mara ngapi hao tampere wameshatandikwa na FC bongo. Kuishi miaka mingi ufini ndo nini kwani? Unatia kichefu chefu. Hii ni kujenga chuki! Fikiria kabla ujachora chora hayo madude yako.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2008

    Nategemea Michuzi utakuwa wa kwanza kuwapokea hawa watoto wakirudi huko nyumbani ili kuonyesha mshikamano na upendo kwao kutoka kwa blog hii ya Jamii,maana sijaona hata Gazeti moja la nyumbani liliandika au kuandika kuhusu Safari yao hata maendeleo ya mchezo wao wakiwa nje ya nchi!Muhimu tuzijali timu zote sio Taifa Stas tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...