Salam kwa wadau wote,
Kama kuna jambo limenifurahisha leo nilipofungua blog hii ya jamii ni hili swala la Wana Toledo Secondary kufungua website yao. HONGERENI SANA WANA TOLEDO. Ni juhudi za aina ya pekee mmezionyesha. MWASTAHILI SIFA.
Bwana Michuzi, tunazo changamoto nyingi sana tunakabiliana nazo nyumbani Tanzania. Kwanza, si bei kubwa kuwa website ila jambo moja la kusikitisha sana kuna makampuni makubwa na ambayo ama kwa uhakika walitakiwa kuwa na websites hawana.
Hoja hapa nafikiri kuna umuhimu wa Serikali kupitisha sheria ya lazima kila kampuni kuwa na website, kuna nchi zimefanikiwa sana ktk hili la kupitisha sheria.
Swala la pili ni namna ya usambazaji wa mtandao Tanzania, nilikuwa na wazo la kuweka net nyumba ili kurahisisha mawasilianao ila bei nilizoziona ktk website ya TTCL si za kuwawezesha watu wengi kuwa na net majumbani mwao.
Mfano angalia bei hizi, ni watanzania wangapi wataweza kulipia Tshs 360,000 kupata hiyo ya GB10. Hoja hapa ni kwa TTCL kurekebisha bei zao jamani.
Huku kwa wenye pesa bei zao ziko chini kwetu masikini bei za kuuana, hatutafika namna hiyo. Nitoe mfano nyumbani kwangu nalipa kwa dola ni kama dola 40 kwa mwezi for UNLIMITED TARIFF.
Serikali nayo ingekua mstari wa mbele kuhimiza matumizi ya Teknolojia ya habari nafikiri mambo yangebadilika ila kwa jinsi mambo yalivyo sasa kasi bado ni ndogo sana.
Mdau Amani.


Sita wauawa wakijaribu kuvamia Benki ya NMB Kilosa
ReplyDelete2008-07-20 12:43:41
Na Idda Mushi, PST, Morogoro
Watu sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa katika majibizano ya kurushiana risasi na polisi baada ya kujaribu kuvamia Benki ya National Microfinance (NMB) iliyopo kata ya Kidodi, wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Bw. Thobias Andengenye alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 7.30 usiku katika eneo hilo ambapo kundi la majambazi tisa waliokuwa na bunduki mbili, magari mawili na vifaa mbalimbali walivamia benki hiyo kuvunja milango ya nyuma kwa kukata kwa gesi na kuingia ndani.
Kamanda Andengenye alisema hata hivyo wakifanya kitendo hicho, tayari polisi walikuwa wamezingira nje ya benki hiyo baada ya kupata taarifa toka kwa raia wema hivyo kufyatua risasi hewani kuwataka majambazi hayo kujisalimisha lakini na wao walijibu mapigo kupiga risasi nne wakiwa ndani ya benki hiyo.
Hata hivyo alisema katika majibizano hayo Polisi waliweza kuwaua kwa kuwapiga risasi majambazi sita na kuwakamata wawili ambao walikuwa madereva wa magari hayo huku mmoja akifanikiwa kutoroka.
Alisema walipowapekua waliwakuta wakiwa na bunduki moja aina ya ``Shotgun pump action`` bastola moja aina ya Bereta, risasi 10 za SMG, mkasi wa kukatia nondo, mitalimbo mawili, mitungi mitatu ya gesi ya kukatia kasiki ya kuhifadhia fedha na hirizi tano na karatasi ya maelekezo ya mganga wa kienyeji.
Aidha alivitaja vitu vingine walivyokutwa navyo majambazi hao kuwa ni karatasi mbalimbali za kufungulia kesi katika vituo vya polisi, bisibisi, hirizi, mifuko ya kubebea fedha, kitambulisho cha benki, namba za gari (plate namba) na magari mawili moja aina ya Toyota Hilux pick-up single cabin yenye namba za usajili STJ 6154 lililokuwa likiendeshwa na mtuhumiwa Mwinchande Mikondo (41) mkazi wa Kimara B jijini Dar-es-salaam.
Alisema gari ya pili ilikuwa ni aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T 149 ATL iliyokuwa ikiendeshwa na mtuhumiwa mwingine aliyekamatwa, Msafiri Chitawa (37) mkazi wa Tabata Chang\'ombe jijini Dar es Salaam.
Kamanda huyo wa Polisi alisema gari hilo aina ya Toyota Hilux inayoonyesha kuwa na usajili wa namba za Serikali inafanyiwa uchunguzi zaidi na Polisi ili kubaini mmiliki halali wa gari hiyo.
Alisema miili ya watu hao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya utambuzi na kwamba upelelezi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea ikiwemo kumsaka mtu mmoja anayesadikiwa jambazi aliyetoroka kwenye tukio hilo na wahusika wengine wa mtandao huo.
dola 40 za zimbabwe? that's cheap, man.
ReplyDeleteYale yale ya malikia aliyewashauri watu wale keki mikate ilipokuwa adimu.Watanzania tukosa zahanati,shule watoto wanakaa dawti moja watoto watatu mpaka wanne wengine wanakaa chini.Barabara zetu mbovu na wengi hata hatujui usiku tutakula nini baada ya kugangamala kupata mlo wa mchana.Kwa wenye uwezo sawa lakini priorities za watanzania walio wengi sio Broadband.
ReplyDeleteNi kweli kabisa hiyo ni bei ghali sana. Hapa nilipo nalipa Euro 25 kwa mwezi - unlimited tarrif. Na wale wanaolipa kutokana na memory usage wanalipa sawa na Tshs 10.9 kwa MB (tena hii ni kwa wale wanaoishi katika majumba ya hali ya juu). Sasa hebu linganisha na hiyo Tshs 95 kwa MB ya TTCL.
ReplyDeleteWabongo ndio waliwao
Mimi nalipa for DSL US $ 19.99 tu per month bongo hiyo tshs 360,000 is a crap
ReplyDeleteNa huyo anayesema hakuna hospital etc etc ungemuuliza kwanini Bill Gates huwa anakuja kila kukicha Africa kusadia maendeleo na since ameretire amesema hilo ndio litakua jambo lake muhimu la kufanya lakini baada ya chakula bora kwa watoto cha pili anataka kila mtoto awe na laptop? Anajua bila knowledge hayo mengine ni ndoto tu...
Ulimwengu wa sasa hivi bila mtandao ni shida sana. Na ku price up hivyo ni ushuru mwingi wanatozwa na Govt au?
Mdau aliyetoa maoni haya anaweza kutoa mifano ya nchi iliyoweka sheria kwamba kila kampuni iwe na tovuti? Kampuni inapaswa kuona kwamba ili iende sambamba na karne ya 21 inahitaji kujianika mtandaoni, sio mpaka serikali iwatungie sheria. Ndio mambo ya free market hayo.
ReplyDeleteHapa nchini Tanzania viwango vya malipo ya Intermet pamoja na Vocha za Simu za Mkononi bado vya Juu sana!Fikiria katika ulimwengu wa sasa,kila siku mtu atalazimika kupiga simu mara ngapi kwa kutwa na atahitaji kutumia Internet kwa kiwango gani kila siku kwa gharama zilivyo sasa? Its too much.Serikali yetu nayo kwa kutoza kodi kila kitu haijambo.Ukisikika umeanza kuzalisha umeme kwa kutumia Kinyesi cha Binadamu au Ng'ombe hata ikiwa kwa matumizi ya nyumbani tu sitashangaa jamaa wa TRA wakija kukadiria Kiwango cha Kodi utakacho paswa kulipia!Fikiria Airtime za Simu za Mkononi pia zatozwa Kodi!Usipopiga simu sijui watamtoza nani? Watanzania wengi wangependa sana kutumia Internet lakini wanashindwa kutokana na viwango vya ushuru.Hivi sasa Ukiingia katika Internet Cafe Binafsi kwa muda wa saa moja tu utatakiwa ulipie shs.1,500/=,Nusu saa shs.1,000/=.Wangapi watakao mudu viwango hivyo?Hatuwezi kuleta maendeleo ya haraka kwa namna hiyo.Wengi wataachwa na Kasi ya Maendeleo Duniani.Kama ni kuondoka kimaendeleo shurti tuondoke sote kwa pamoja.Siyo watu wachache tu.
ReplyDeleteHuyu anon wa July 20, 2008 5:46 PM, mbona unakuwa na fikra duni? Nyie ndo wale mliosema watu wacheze mak-time kusubiri wenzao wawafikie kimaendeleo. Maendeleo hayasubiri mtu...u get wat u can afford bwana. Sasa kama mtu anaona priority za nchi ni kutoa elimu, sio kudumaza sector nyingine. They all work together katika kuleta maendeleo. U might put more money in one, but that doesnt mean u have no regards to the other. Wat u need is balance! Na ni hilo linalokosekana. Haya makampuni ya simu za mkononi yameweza kuleta maendeleo sana baada ya kuruhusu ushindani katika field ya telecommunication. TTCL ilitesa watu sana...enzi zile walikuwa wanakuja kukufungia simu baada ya ku-spend mwezi mzima kuwaomba! Na sasa ivi imekuwa na hii broadbank inajifanya mbabe...we ngoja waje watu watakaoweza ku-provide equal services at a cheaper rate...they will lose the market. But having said that...they are also using a simple market strategy...wachache wataweza ku-afford hizi bei, lakini kwa sababu wataona ni necessity kwao, wapo tayari kulipa hizo bei za juu. The trick is not to interfere with the market. Open it up, subsides or give other incentives to other companies to provide equal services and hopefully prices will come down. Sema bongo rushwa inasumbua sana. Uwizi na rushwa. Kampuni zitapewa tax cuts kwa miaka kadhaa, alafu zitafanya biashara kwa huo muda na ku-claim loses na kukipa. Mambo ya Holiday Inn hayo. Watu wa juu wanajua hili na wanakaa kimya, kisa wamepewa kitu kidogo. Kweli rushwa itatumaliza!
ReplyDeleteConclusion: Ukumbuke motto ya Kikwete...MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA. Sasa kama kwangu mimi binafsi, maisha bora ni kuwa na mtandao nyumbani...basi nina haki ya kuupata na katika bei nafuu. Kama wewe ni elimu, basi nayo ifanyiwe shughuli, uipate kwa unafuu na ya hali ya juu iwezekanavyo. Lakini sio kusema ehh sijui la muhimu zaidi ni hili au lile!
Nawakilisha!
mtoto