JK alisalimiana na Bibi Makihiyo Baluah anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 102 wakati alipomtembelea bibi huyo nyumbani kwake mjini Korogwe wakati wa ziara yake mkoani Tanga.

Bibi Baluah ni mke wa hayati Mzee Baluah ambaye alikuwa rafiki yake hayati Mzee Mrisho Kikwete, baba yake JK, ambaye yupo mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi kukagua na kufungua miradi ya maendeleo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Kama nilivyosema hapo awali, matukio kama haya yenye tafsiri katika maisha na jamii, yenye kuelekeza utu na fadhila, watanzania wengi hatuyajali na kuyapa uzito wake. Picha hii iwekwe katika kumbukumbu za kihistoria. Nahuyu mama afuatiliwe ili atoe the other side ya story ya marehemu mumew na urafiki wake na baba wa raisi wetu marehemu mzee Kikwete. Wengi wetu tunapenda kuchangia mambo machafu, kashfa, fitina na uzinzi. Kaka Michuzi hii picha ina tafsiri nyingi na kubwa zenye maana katika nyanja za uongozi na utawala bora. JK is simple, human, down to earth na real. Nimeshindwa kueleza hizo quality kwa kiswahili ili kuweza kupata tafsiri halisi husika. Wangapi wetu tukipata madaraka tunakumbuka marafiki zetu au angalau watu waliogusa maisha yetu eti kupitia kwa wazazi wetu? Taifa lijivunie kiongozi huyu, jamani huyu ni God sent from whatever angle mtu atajaribu kuangalia. Wote tuna mapungufu kwani tu wanadamu lakini kwa mapana na urefu Jakaya Mrisho Kikwete ni 'mtu ' na si kiatu ! Mungu ibariki Tanzania, mungu mbariki JK, na watu wake, Amen.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2008

    Hapa inaonekana raisi wetu anaoshwa nyota na huyu kikongwe, kwani kwenye safu Tanga ilikuwa haijapa mwenyeji. kuna rukwa, bagamoyo, pemba ukiongeza tanga we acha tu.
    Natombe
    Moshi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2008

    I Love You Mr. President because your you!!! Big Up!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2008

    Jazak -allahu Jakaya umetimiza ibada yako na umefanya yaliyoamrishwa na mafundisho ya uislam, kuwa rafiki ya mamako au babako, ni babako na mamako hasa mama au baba akishakufa, unatakiwa uwatendee wema sana na kuwakirimu marafiki aliowaachawa baba au mamako, madaraka yasikufunge kufanya ibada na sunna zote kama unaweza, tulizoamriwa na mitume na maswahaba.

    Mwanamkengwa, wanangachani? wana Makihiyo, hongea!! mnala.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2008

    Kila mtu ana kilema na kasoro yake. Rais wetu kasoro yake kutosahau marafiki na huruma zimemzidi jamani! Hapo sasa lazima amjengee nyumba huyo mama na wasomeshe walioshindwa kusoma kwenye hiyo familia. Mungu akulinda Baba

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2008

    Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni JK anajua kupangilia "pamba" bwana mimi namzimia sana kwa hilo mengine kwangu ni ubinadamu hayaniusu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2008

    Kila siku asubuhi na jioni, naomba Mungu azidi kumlinda Rais wetu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2008

    Mnasema Bongo sio tambarare cheki huyo bibi afya nzuri, she is happy ndani ya nyumba yake ya udogo, maji ya kuteka kisimani napikia kuni, hana cha pensheni ya uzeeni wala kuchambishwa na akinaninihiiiiii na miaka inakwenda.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2008

    WATOTO WEWE, WAZEE WEWE KHA! WACHA NYOTA YAKO IWAKE BABA UNA KIPAJI CHA PEKEE

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2008

    This Photo tells a lot... Am touched by how JK can fit in all situations and lower himself. The snap also shows the life this grandma has been living...am sure JK visit in one way or the other mad her the happiest woman in that day if at all she is in a position to understand everything that happens in such an age coz others do loose memory. All the same Congrats JK for paying her a visit it shows you do remember where you come from and that in itself deserves a credit.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2008

    Watanzania watu wazuri. huwa tunasemana tukibofoa na panapostahili, tunasifiana.

    Hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa. Aliyetoa comments za kwanza kabisa anaongea vizuri sana maneno yake. Katika hii enzi ya "negativity" kwenye jamii yetu, ni raha sana kusikia mtu angalau anasemwa vizuri.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2008

    Asante baba..manake hata mie nimeshindwa kujizuia...ninafurahishwa na Rais wetu anavyofit kwenye mazingira yetu,nakutukumbuka sie tulioko chini kabisa, kutuona tu na kutujulia hali kwetu ni faraja tosha..Mungu akubariki kwa yote yenye mtazamo huo...kwani ni wangapi kati yetu ambao tunashindwa kwenda wajulia hali wazee wetu ambao tumewaacha huko kijijini?

    Hingera baba

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 21, 2008

    Naomba kutofautiana na wengine wote almost japo si kwa ubaya. Sipingi jk kumtembelea huyo kikongwe hapo, nim jambom zuri tu. Lakini kumtembelea huyo kikongwe hapo then ukaacha rasilimali zetu zote zikaliwa na wachache badala ya kumasaidi huyo kikongwe na wengineo wengi its nothing. Wote tunayaona mazingira ya huyo kikongwe hapo yamechoka sana. Ninazo data, kwa rasilimali tulizonazo kama zingeangaliwa vizuri tungweweza kujenga senior citizen centres kama za wenzetu kibao na kuwahifadhi hao vikongwe kama huyu wakaachana na moshi unaopunguza maisha yao. I'm not negative lakini tabasamu la JK wakata watu wachache wanafaidi utajiri wa nchi na wengi wansuffer binafi halinisaidii chochote. Alinde rasilimali zetu then asiwatembelee hao vikongwe its far much better kwani wataliona tabasamu lake kwenye huduma bora za jamii. Mr. President, katiba imekufanya wewe Mungu hebu chukua hatua basi tuone? Muda hausubri. Michuzi hakuna baya kwenye comment endapo tu utaiangalia kwa jicho la kitaaluma. Thanks.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 21, 2008

    anon wa july 21, 09:13 umenichekesha sana.. ''hana cha pensheni ya uzeeni wala kuchambishwa na akinaninihiiiiii'' ....lakini nakuunga mkono bibi ana afya nzuri ndani ya nyumba yake ya udongo.. ''happiness'' that's what matters! na Jk anaonyesha utu wake. nice picture.

    Kay

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 21, 2008

    this photoz is so good enough to get CNN Africa photo of the Year!

    Mbunge wa Kawe itume CNN.

    Take home essay for us..........

    Maisha ni matamu na marefu ukijitunza,mwone bibi anavyowaka waka !
    Jamani anahitaji msaada toka kwetu japo wana kijiji tukijipapasa kwa alfu moja kila mmoja..mbunge ataziwakilisha;mnaonaje HILI!??

    mwisho,waandishi nendeni mkapate siri ya kuishi maisha marefu huyo bibi ili wengine waige.ikiwezekana wale wa tafiti waende kufanya utafiti ili tufaidi sio kila litu kizuri lazima kitoke Ulaya,nasi twaweza kuwafanya watu wengine waige kwetu...

    BIG UP JK....keeeeeeep on !but send segerea MAFISADIIIIIIIIIIIIIiiiiiii wanachafua hali ya hewa ya nchi yako!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 21, 2008

    Nikimuangalia JK anaonekana ni mtu mwenye huruma sana na sometimes aibu. Na kwa hilo mafisadi wameshajua kwamba this guys ni mtu mwenye huruma na aibu ndio maana wameamua kutumia weakness hiyo ya President wetu. Ushauri wangu kwa rais wetu, ni kwamba asiwaonee huruma wala aibu mafisadi, nafikiri anaufahamu ule msemo kwamba ''ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni'' na hiyo ndiyo dawa ya kupambana na mafisadi. Kama JK anapitia blog yetu ya jamii basi ujumbe ameupata, kama atakuwa bize basi naamini wasaidizi wake akiwemo mkuu wa Wilaya ya Nanihii watamfikishia ujumbe! Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 21, 2008

    Yaani mwenzenu mimi alieniacha hoi ni huyo, Bibi yaani kawaida kinoma kama anasalimiana na mtoto wa rafiki wa mume wake na sio raisi wa nchi. Nimempenda ile mbaya ingekua watu fulani wangeazima hadi viti vya jirani lakini kapewa kigoda akae na JK hana makuu. Yaani Mkuu wa wilaya ya nanihii hili ni bonge la picha, we acha tu. Rais wetu ni mtu wa watu na pia anajishusha sana. Mungu ampe maisha marefu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 21, 2008

    Ano.July 21, 2008 2:18 PM All the same naona unataka kuendeleza kazi yako ya care unayofanya ulipo mpaka home bongo ndio maana naona una...IoI Bababara tu bado ndo centre za wazee wewe acha. watunze hao hao huku ulipo. ukipata mtaji kajenge yako bongo kama mfano then utakuwa umeinvest kwenye new...

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 21, 2008

    Joaquine,siyo kweli kwamba watanzania wengi hawajali maisha na jamii, yenye kulekeza utu na fadhila. President hataki kuwapa credit watu kama hao kwa sababu siyo marafiki wake. Wakati alilkuwa waziri mbona haku msaidia bibi? Alikuwa hana hela? That is the problem. He never gives credit to wananchi. Please do not tell me you have to be a President to do good things. Tuna mkubusha kwamba Watanzania kila siku wana adopt children, wana take care of neighbours, families na hela kidogo tu. Je marafki wake wanaishi hivi? Does he not take of them? Please no fooling.
    I agree, nobody is prefect. JK is simple, human, and down to earth and real only when it applies to his friends. They donot have to worry he takes care of them very well. Anonymous "Mungu ibarike Tanzania, mbarike JK na watu wake" Pia wabarike watu wasiyo watu wake. It is simple those who have it and thoses who do not. All said he does deserve credit, it is never late when helping your own family.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 21, 2008

    hausindile JAKAYA,kwangima sisi powa nakuona hapo uko fresh ile mbaya.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 21, 2008

    Angalia tofauti ya maisha yako wewe Rais wetu na huyo bibi.Maisha ya vijijini ni magumu sana.You have to work Mr Presisent.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 21, 2008

    mzee Michu mbona umebana comment yangu? Au unawaogopa wakubwa. Sikuweka kashfa wala matusi hivyo sielewi kwanini ulibana. Nimeongea ukweli juu ya serikali ya awamu ya 4. Anyway labda matatizo ya kiufundi, ngoja nijaribu tena kwa kifupi (na niache yale ambayo najua yamekutishia kuweka maoni yangu hapa).

    Mi nakubaliana na Anony wa July 21, 2008 2:18 PM na July 21, 2008 5:08 PM. Sipingi umuhimu wa rais kutemebelea wazee, yatima, walemavu, n.k. Ila tunahitaji vitendo thabiti zaidi. Kumtemebelea mtu na kupiga picha inaweza kuwa show tu kisiasa; haisaidii katika kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.

    Tungependa kuona bibi kama huyu hapa anakuwa na maisha mazuri zaidi na anafaidika na rasilimali za nchi yake iwapo utawabana mafisadi na kukuza pato la taifa. Baadhi ya watu wamemntetea mtukufu rais kuwa ni mtu mwema na mafisadi wana-take advantage. Mi napenda kusema kuwa iwapo unayo nafasi ya kuzuia maovu lakini ukakaa tu basi una makosa na wewe. Na ni ngumu kwangu kuamini kuwa Mtukufu Rais hakujua yaliyokuwa yakitendwa. Okay, tuseme basi hakujua; maadam sasa siri imefichuka, tunaomba uwashughulikie mafisadi ipasavyo basi. Ili bibi kama huyu na sisi watanzania kwa ujumla tufaidi matunda ya nchi yetu, na ndoto za maisha bora zitime. Salamu peke yake haitoshi.

    Ila mwishowe, ujumbe kwa Mkuu wa Tegeta. Nimesikitishwa kidogo na kitendo chako cha kuzuia comment yangu ambayo ilikuwa haina hata chembe ya dharau, matusi, kejeli au kashfa. Ila naelewa, we ni mwajiriwa wa TSN inayomilikiwa na serikali, hivyo inapaswa uwaogope wakubwa hao. It is sad maana blog inatakiwa iwe independent source of information. Ni mara ya 1 comment zangu zimezuiwa leo na walikuwa wadau wengine wakilalamika naona kama wana visa tu an kuwa inawezekana labda walitukana, n.k. Ila leo nimegundua kuwa saa nyingine unazuia hata innocent comments kama zikigusa ukweli wa watu fulani fulani

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 22, 2008

    Braza Michu,pale jumba kuu(ikulu) kuna mpiga picha anaitwa Godfrey Baluah,alikuwepo hata kabla ya JK hajaingia ikulu. Je ana uhusiano wowote na huyu bibi?. Wewe ni mpiga picha hivyo ni rahisi kwako kujua. Tafadhali tujulishe.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 22, 2008

    Mimi ningependa kusapoti kitendo cha JK kwenye picha hapo juu na maoni ya wachangiaji wengine.

    Mimi binafsi sina uhusiano wowote wa karibu na JK zaidi ya kuwa ni kiongozi wa nchi yangu. Lakini kunawa kati nilikuwa katika kipindi kigumu ninauguliwa hospitali, nikiwa nimekata tamaa moyoni ghafla nikakutana na Mh. JK (wakati huo ni waziri wa mamabo ya nje) katika ngazi za Hospitali akiwa amemleta mtoto wake ambaye alikuwa anaumwa, alisimama tukasalimia kana kwamba tulikuwa ni watu tunaofahamiana na nikamueleza habari mgonjwa wangu na mahali alipolazwa. Baada ya muda kupita amini usiamini JK alifika alipokuwa mgonjwa wangu na kumjulia hali...nadhani inatosha kuunga mkono waliotangulia kuwa JK ni mtu wa watu ana utu na amestahili kuwa kiongozi. Hana kiburi wala majivuno.

    Ingekuwa ni viongozi wengi kwa kujitahidi kabisa angesema huyu bibi aletwe ikulu nije nimsalimie.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 22, 2008

    Michu kama kweli hii ni blog ya jamii na mtu amecoment bila kashfa au matusi kwanini unaibania???
    hii picha ya prez naona kila gazeti imeitoa kwenye kurasa ya mbele..nini kilichotuvutia?? JK kukaa kwenye kigoda au kutembelea vikongwe kazi ambazo hata mamiss wanafanya au kwasababu huyo bibi ni mke wa rafiki ya babae?? JK ni mpenda sifa na vyombo vya habari kweli vinaweza kukupandisha au kukushusha...Sasa hivi ili swala la znz si nchi linahatarisha muungano, JK sidhani kama ungehairisha hiyo ziara na kuja znz kuudhuria kikao cha ccm kuhusu swala hili sidhani kama kuna mtu angeshangaa. Hili swala limekuwa zito linahitaji fikra za watu wazito kama ww lkn umeona bora kujipigia kampeni kabla ya 2010 kuliko kushughulikia matatizo makubwa...umetuambia tuvumilie shida ni kweli upo serious??? haya maneno ungesema tangu mwanzo sidhani kama ungepata 80% kwenye uchaguzi. JK tumaini lililorejea unataka wananchi tuvumilie matatizo?? ule wimbo wa maisha bora upo wapi? umeingia studio umesahau maishairi matokeo yake umekuja na tungo za papokwahapo ndo umekuja na tuvumilie shida...eteheheee, Mr Prez naomba ifikapo 2010 uachie wengine, hakuna atakae kucheka zaidi ya kukupongeza kwa maamuzi ya kishujaa. Tuombe radhi wadanganyika, umetupotezea muda na umeshindwa kuwashughulikia wabadhilifu wanaotunyona kama kupe maisha bora kwa kila mtz yamekuwa bora maisha. Waachie wenye mawazo mapya tunakushukuru kwa kutufikisha hapa.
    Mungu akubariki na michuzi usibanie.
    Mdau toka Kiwangwa

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 23, 2008

    EPA; IPTL; Richmond; TICTS; Meremeta; TangGold; ANBEM & Kiwira; Mikataba ya madini; Ujenzi wa Twin Towers; Kupanda kwa bei za mafuta na chakula; fedha za per diem kwa kamati za bunge kuchunguza matatizo hapo juu; fedha zinazotumika za per diem zinazotumika kumpatanisha Mengi na Malimana shughuli nyingine zisizokuwa na ulazima; fedha za per diem zilizotumika kutetea bajeti ya 2007; sakata la rada; ndege ya rais; Kuvamiwa Mwanahalisi; Net Group Solutions TANESCO management team; misuse of government & parastatal companies' vehicles; SAA kututapeli ATC; Hali ya Muungano & Zanzibar (mpasuko wa kisiasa; swali la Z'bar ni nchi; kutaka kujitenga kwa Pemba)...

    tunashukuru na kukupongeza kwa kukumbuka wananchi wa kawaida kama huyu bibi, ila bila kushughulikia matatizo hayo juu haina maana.

    tukipunguza upotevu wa fedha kwa ubadhirifu na ufisadi huo juu, tutaimprove maisha ya watanzania wote. Tunaomba angalau tukusikie ukiyazungumzia baadhi ya hayo mambo waziwazi na utoe msimamo wako Mtukufu Rais.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 23, 2008

    We mwenye jina la matusi a.k.a Natomba wa moshi, acha imani za kishirikiana, wewe ndo wale wanaowaponda kwa mawe vibibi vyao wakivituhumu kuwa vichawi, nani kakwambia hapo raisi anaoshwa nyota kama si imani zako za kishirikina zinavyokupeleka? kijeografia tanga pemba na bwagamoyo ni sehemu zinapakana wakwere na wazigua na wasambaa wabondei na wapemba kunauingiliano wa kabila lugha zao wakiongea wanaelewana kwa vile ni majirani na wamesambaa upande mmoja, kutoa hao wa rukwa ulowaingiza kutokana na hisia zako za kichawi, kama vile wewe na mchanganyiko wa wachaga wenzio wa huko moshi we ndo wale wale wa majina ya kubandikana bila kujua tafsiri zake, mkija mjini wanawashangaa na kujibadili majina, tunae mwenzio mwengine huku anaitwa "Mamboro" sasa hapo kumuita hadharani huyo jamaa ni mtihani, ilibidi mpaka akatuelewa kuwa tunatatizika akatuomba tumwite kimiti instead of Mamboro. Kakojoe ukalale kama huna jipya hapa.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 24, 2008

    NANI KAKWAAMBIA HUYO MAMA HANA "PENSHENI" JK YUKO NDANI YA "HIMAYA" YA HUYO MAMA.SERIKALI INATAKIWA "ISAVEI" MASHAMBA/VIWANJA VIJIJINI IYAPE/WAPATIWE THAMANI SAHIHI WAFUNDISHWE/WAPATIWE MIKOPO YENYE RIBA NDOGO SANA ILI WAFIKAPO UZEENI (KAMA HUYO BIBI) WAWE NA CENTI/FEDHA ZA "KIJIKIMU" N.K.

    KITU CHAPILI WAZEE WENGI BADO WANAFEDHA ZA ZAMANI K.M ILE SHs MIA "NYEKUNDU", NOTI YA SHs KUMI "KIJANI" NOTI YA SHs ISHIRINI "BLUU", SHILINGI TANO "GWALA", SENTI KUMI YENYE UMBO LA "MAWIMBIMAWIMBI" (RANGI YA KAHAWIA) NYINGINE ZA KARATASI ZIMELIWA NA PANYA ZIKO NUSU.

    SIKUYA KUBADILISHA FEDHA "REDIO TANZANIA DAR-ES-SALAAM" (RTD) HAIKUMFIKIA HUKO ALIKO.PANYA ALIKUWA AMEINGIA KWENYE REDIO YA MBAO ILE YA "PHILLIPS/NATIONAL" NA BENKI IKO MWENDO WA BASI SIKU NZIMA HAKUWEZA KWENDA AKAAMUA AZIHIFADHI CHINI YA KITANDA CHAKE "TEREMKA TUKAZE" KWNYE MFUKO WA "RAMBO" ALMAARUFU KAMA (MFUKO WA PLASTIKI BEGI).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...