Ruto awasilisha ujumbe waRais Kibaki kwa Kikwete
Na Mwandishi Maalum,
Kasera, Tanga
JK jana Julai 18, 2008 amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Ujumbe huo umewasilishwa kwa JK na Waziri wa Kilimo wa Kenya, William Ruto (pichani juu), wakati walipokutana kwenye makao makuu ya Jimbo la Mkinga, mkoani Tanga, katika eneo la Kasera.
Katika mkutano huo nyumbani kwa mkuu wa wilaya hiyo, Ruto amewasilisha kwa Rais Kikwete salamu na ujumbe maalum kutoka kwa Rais Kibaki.

Waziri Ruto alifuatana na Balozi wa Kenya katika Tanzania, Mh.Boaz Mbaya.
Waziri Ruto pia amemshukuru Rais Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), kwa mchango mkubwa katika usuluhishi wa mgogoro mkubwa wa siasa uliolipuka kufuatia tofauti kubwa zilizotokana na uchaguzi mkuu nchini humo Desemba mwaka jana.
Ruto alimfuata Rais Kikwete mkoani Tanga ambako Rais Kikwete anaendelea na ziara ya mkoa huo.Ruto ameondoka Tanga kurejea nyumbani Kenya baada ya kuwa amewasilisha ujumbe huo

Tunataka ifike wakati na sisi tumpongeze Rais wetu kwa kusuluhisha mgogoro wa kisiasa Zanzibar! Kwanini Rais anakuwa kimbelembele na migogoro ya watu, wakati ya kwetu inatushinda!!!!!!?
ReplyDelete