jeshi la polisi linasaka watuhumiwa sita wa ujambazi ambao kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa dar afande suleiman kova amesema mchana huu kwamba walinaswa kwenye kamera za cctv walipoingia na kupora kiasi cha shilingi milioni 50 kwenye duka la havan's limited barabara ya haile selassie oysterbay jana mchana.
amesema askari wamewatambua kwa majina wawili kati ya watuhumiwa hao sita na msako mkali unaendelea.
wakati huo huo askari wa mkoa huo umekamata kinadada 21 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya ngono maarufu kama machangudoa. hiyo ni katika kutekeleza ahadi za 'kuasfisha jiji' alizotoa mara tu alipotua dar kumrithi afande tibaiagana akitokea mbeya.


hongera baba chapa kazi.
ReplyDeletesweet,
Arusha.
Kwa hili la kamera nampongeza sana kamanda Kova maana itasaidia sana kuwakamata waporaji wa pesa za watu. Hizi kamera zikiwekwa kwenye mabenki,maduka makubwa,nk itapunguza sana uporaji mkubwa wa mali za umma na za binafsi. Well done kamanda Kova!
ReplyDeleteHongera sana Kamanda wa polisi kwa hilo. Wakati umefika wa kutumia technology kupunguza uhalifu kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea.
ReplyDeleteMdau,
Columbus Ohio.
Tupate na kamera za kunasa mafisadi sasa.
ReplyDelete