Mhariri Mtendaji wa Hali Halisi Bw. Saed Kubenea akiongea na Inspekta Jenerali wa polisi afande Saidi Mwema katika picha hii ya mzee wa sumo iliyopigwa mwezi wa tatu mwaka huu Dar

KLHN imepata nafasi ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Bw. Robert Manumba kuhusu suala la kuvamiwa waandishi wa wahabari. Bw. Manumba hata hivyo amekataa kuhojiwa akidai kuwa tayari wameshatoa statement yao na maelezo yao ndivyo yalivyo hadi sasa.


Nilipojaribu kumbana zaidi Bw. Manumba alikata simu.


Hata hivyo tumepata nafasi ya kuzungumza na Mhariri Mtendaji wa Hali Halisi Bw. Saed Kubenea ambaye ameelezea kwa kirefu kilichojiri na pia kutoboa mambo mengine makubwa zaidi ambayo kujulikana kwake lazima kuwatetemeshe karibu viongozi wote waliowahi kushika nyadhifa za juu nchini.


Mojawapo ya madai makubwa aliyoyatoa ni kuwa akaunti ya Meremeta ambayo inadaiwa kuwa ilikuwa imefilisiwa na baadaye kuundwa Tangold, akaunti hiyo hadi hivi sasa bado inafanya kazi.


Zaidi ya yote Bw. Kubenea amedai kuwa yeye mwenyewe na watu wako tayari kwenda gerezani lakini kamwe hawatota siri ya sources zao za habari na ya kuwa computer na vifaa vilichochukuliwa havina kitu chochote cha kucompromise that sacred trust kati ya vyombo vya habari na vyanzo vya habari.


"Hatuogopi, wala hatutishwi, aluta continua" alisema Bw. Kubenea kwa kujiamini.


Mahojiano ya KLHN na Manumba na Bw. Kubenea yatarushwa leo Jumapili kupitia KLH News na ikiwezekana kupitia Bongo Radio kuanzia saa nane kamili mchana (saa tatu za usiku za Tanzania) katika matangazo yetu ya moja kwa moja ambapo pia tutapokea simu zenu na maoni yenu kuhusu.


Kwa wale wanaotaka kutumia skype kuwasiliana nasi kwa simu watumie contact mwanakijiji007.


Title: KLH News
Episode: "Tutaendelea kuwafunua mafisadi" --- Kubenea


/entry/2008-07-19T21_49_25-07_00


Enjoy!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2008

    Mungu atakulinda Kubenea... Thats what we call a pure Heroic!

    Uko katika DUA zetu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2008

    Jana Jumapili tumepata nafasi pia ya kuzungumza na Waziri wa Habari na Utamaduni Kapt. George Mkuchika kuhusu suala hili la KUbenea. Tutayarusha matangazo hayo yote katika uzuri wake siku ya Jumanne ili iweze kuoana na makala kadhaa zitakazotoka Jumatano.

    For any news update hakikisha unatembelea http://www.klhnews.com kutwa nzima ambako tunarusha matangazo yetu live pamoja na burudani ya muziki masaa 24.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2008

    NBC wamekosea namna ya kuishughulikia hili swala.

    Ilitakiwa benki ikae kimya ila iimarishe kitengo chao cha akaunti za wateja kwa kuweka watu waaminifu na kuthibiti utokaji wa siri bila kumpigia kelele wala kutuhumu mfanyakazi yeyote.Ingefanya mabadiliko ya ndani kimywa kimya.Kutuhumu mfanyakazi na kumpeleka mahakamani kuwa katoa siri ina maana benki ni dhaifu na imehusika moja kwa moja na siri za mteja kuvujishwa na benki.Mteja hajui mfanyakazi wa NBC yeye anaijua benki.

    Hivyo hata kama huyo mfanyakazi wao atafungwa na kukutwa na hatia waathirika waweza ishtaki NBC na kuidai mabilioni kwa uzembe na kusababisha siri kuvuja .Kuepuka hili NBC ingekaa kimya ifanye mabadiliko ndani kwa ndani.Na wanasheria wa NBC wangewashupalia watu wale wa nje wanaodai kuwa benki inavujisha siri wathibitishe kwa kuwa huwezi kujua nani anavujisha taarifa za akaunti ya mtu.Sababu benki ikishatoa statement ya akaunti ya mtu huwezi kujua huyo mtu aliyepewa hiyo statement ya benki kampa nani.Aweza mpa hata hawara yake.Huyo hawara akiipata hiyo statement aweza kwenda akaonyesha watu wengine.Huwezi kumthibiti mteja kuwa akipata statement ya benki asiwaonyeshe watu wengine.

    Kuwatumia Polisi naona wanaiweka NBC pabaya.Ikithibitika kuwa chanzo cha siri za wateja ni NBC iwe kupitia mfanyakazi mzembe kwa uthibitisho wa mahakamani au polisi NBC wajiandae kuumia sababu wajibu wa kuthibiti mfanyakazi mzembe si wa mteja ni wa benki.Mteja aliyeumia atashughulika na benki tu.Wanasheria wa NBC hawakuwa makini katika kushauri .Hasara ya kunyamaza ingekuwa ndogo kuliko ile ya kuonyesha kuwa NBC inahusika na uvujaji siri kupitia mfanyakazi mzembe.

    Sasa wanasheria wa NBC benki itabidi wapigane kufa na kupona kuonyesha kuwa mfanyakazi wake na benki si wavujisha siri kuepuka madhara mazito.Vinginevyo sijui wanasheria wa NBC watafanyaje kuikoa hiyo benki isipate matatizo toka kwa wateja walioumia kwa siri kuvuja.

    Hekima za kisheria hazikutumika katika hili.Na nguvu ya polisi ilikuwa kubwa bila sababu.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2008

    Jamani jasiri wa nchi hii Dr. SLAA amerahisisha kazi sana hasa kwa hao waliozoea kutumia NGUVU kuliko akili(POLISI).kasema nyaraka wanazozitafuta kwa KUBENEYA yeye anazo na nyingine ndio ameompa Kubeneya, wamfuate wakamkamate yeye.Ref www.mwananchi.co.tz

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2008

    Kwa upande mwingine wa kijamii ni bora hao mafisadi wajulikane kwani wanamaliza nchi waumbuliwe Kubenea ashikilie uzi huo huo kwani yeye ni mtoaji habari hivyo habari zozote zinazohusu jamii anatakiwa azitoe, azichunguze na kuzifuatilia kwa kina...Lakini kwa upande wa kiofisi hao wafanyakazi/mfanyakazi wa benki anamakosa hiyo bank inatakiwa ibadilishe mtiririko mzima wa waajiri wake kwani kuna mmoja wapo anayevujisha siri za benki. Na kama ilivyo mtu ukiajiriwa katika sehemu hasa ukiwa mesomea kazi hiyo kuna maadili ambayo unakuwa umefundishwa...Mwajiri natakiwa kutunza siri za Organisation yake na ndio maana hata katika sehemu zingine Mwajiri anatakiwa kula kiapo kutokana na Si kila Organisation hazina siri zipo ambazo zenye siri kubwa hasa kama hivyo Mabenki, Ofisi za Serikali, Mahakama, Hospitali nk...Sasa huyo mwajiri amekiuka taratibu kwa hakika akigundulika amekwisha...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2008

    Tumesikia Bwana Lula Mwananzalu tunasubiri jumapili tupate vitu live.itakuwa KLHNEWS AU huku kwenye podomatic?
    Lula tupe jibu ili tusikose burudani hii.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2008

    Kumbe Lula Mwananzela wa Raia Mwema ni Mwanakijiji. ndio maana kila akiandika kwenye raiamwema anasema nendeni KLH NEWS kumbe anajipigia debe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...