MWENYEKITI WA UWT MKOA WA DAR ES SALAAM NA MBUNGE WA VITI MAALUM BIBI JANETH KAHAMA (KUSHOTO) AKIKABIDHI FOMU ZAKE ZA KUWANIA UENYEKITI WA TAIFA WA JUMUIA HIYO KWA KAIMU KATIBU MKUU WA UWT TAIFA BIBI DOMINA NGWADA KATIKA OFISI ZA JUMUIA HIYO MTAA WA LINDI DAR ES SALAAM L


NA MADANGA SHAABAN MADANGA
WA MEDIAWORKS

MWENYEKITI WA UMOJA WA WANAWAKE (UWT) MKOA WA DAR ES SALAAM AMBAYE PIA NI MBUNGE WA VITI MAALUM BIBI JANETH KAHAMA, LEO ALIKUWA MGOMBEA WA KWANZA KURUDISHA FOMU ZAKE ZA KUWANIA UENYEKITI WA JUMUIA HIYO YA CCM TAIFA.

KATIKA SHEREHE FUPI ILIYOFANYIKA MAKAO MAKUU YA UWT MTAA WA LINDI KARIAKOO DAR ES SALAAM, BIBI JANETH KAHAMA ALIFUATANA NA MAMIA YA WANAWAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM KAMA KUPITA ILIVYOKUWA SIKU YA KUCHUKUA FOMU NA KUSABISHA MSONGAMANO MKUBWA KATIKA MTAA HUO AMBAO NI MMOJA KATI YA MITAA INAYOJAA SANA WATU JIJINI KUTWA NZIMA.

AKIONYESHA KUKOMAA KWAKE KISIASA, BIBI KAHAMA ALISEMA ANAWAOMBA WANAWAKE WENGINE WENYE SIFA WAJITOKEZE KUCHUKUA FOMU NA KUZIRUDISHA KWANI HIYO ALIDAI NI HAKI YA KILA MWANACHAMA WA UWT.

BIBI KAHAMA ALIWAKUMBUSHA KINAMAMA KUWA UONGOZI HUWEKWA NA MUNGU NA MGOMBEA YOYOTE ATAKAYECHUKIA WENGINE KUJIINGIZA KATIKA KINYANG'ANYIRO HICHO ANAJIPOTEZEA MUDA WAKE.

NAYE KAIMU KATIBU MKUU WA JUMUIA HIYO BIBI DOMINA NGWADA ALISEMA MPAKA JANA NI WANACHAMA WAWILI TU WA UWT AMBAO NI JANETH KAHAMA NA SOPHIA SIMBA NDIO WALIOCHUKUA FOMU ZA KUWANIA UENYEKITI WA JUMUIA HIYO NGAZI YA TAIFA NA KUTOA WITO KWA WALE WOTE KUFANYA HIVYO KABLA YA JULAI 30 AMBAYO NI SIKU YA MWISHO KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU HIZO.

BIBI NGWADA ALIZITAJA NAFASI ZINGINE ZINAZOWANIWA KUWA NI MAKAMU MWENYEKITI, WAJUMBE WA BARAZA KUU TAIFA NAFASI KUMI ZIKIGAWANYWA SAWA VISIWANI NA BARA NA WAWAKILISHI WA JUMUIA YA VIJANA NA WAZAZI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2008

    Bwana Michuzi naomba sana utangaze hili kwenye website yako...kuna website moja: http://www.pinnacleic.com/ ambayo inajifanya kuchukua pesa za watu bure bure na pia ukichekivizuri kwenye website yake wana representatives Tanzania...hawa jamaa ni scammers wanaojifanya wana chuo Manchester, UK...naomba uwatambulishe watu kupitia glob yako maarufu...otherwise watu wetu watapigwa bao fedha zao...kama huamini sana message yangu naona uwasiliane na hao jamaa kwa style ya kujifanya unataka chuo uone jinsi watakavyotaka kukupiga bao...Mdau

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2008

    mbona uongoz wa sasa ni wale wale,kinachofanyika kuachiana uongoz kifamilia,je mi mtoto wa mkulima ninaosoma chuo sasa iv nitapata uongoz kwel,michuzi usibane

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2008

    How old is she? Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2008

    Ahaaa kumbe huyu ndio mama yake Aveline Ngwada. Ngwada upo wapi nilisikia na wewe unataka kuchukua form za UVCCM

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2008

    Hivi huo u-Bunge haumtoshi? Wakina mama wazee, achieni wengine nao wale kidogo!

    Hii yenu ni skandali!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2008

    ndio walewale...kila pahali ndio haohao...Makabwela,wanyonyaji,makupe wako hai...sasa sisi watanzania mbona hao hatuwachukii???DOUBLE STANDARDS au siyo?hebu angalieni masaizi...yaani nono!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2008

    Jamani makpumzike sasa vijijini. Mzeeke graceful.....Sasa sisi kazi tutapata wapi kama nyie ni nyie tu kila siku.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2008

    She must be in her mid 60's

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2008

    Jamani namtafuta Avelyn Ngwada nilisoma naye Mlimani ...nadhani huyo anayetoa form ni mama yake. Mara ya Mwisho nilisikia yuko Mtwara ni Mhasibu huko ....

    Email yangu ni kitangalinewala@yahoo.com

    Natanguliza shukrani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...