Home
Unlabelled
chifu wa unyanyembe atembelea bunge
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Chifu gani mtoto wa mjini namna hii? Vaa kama akina Kwa Zulu Natal, mbavu nje, pekupeku, mkuki mkononi, usinga kiunoni, n.k. Nyie mnaleta ubitozi wa tai na suti?
ReplyDeleteAsante. Umewaza kama mimi...sasa vazi gani la chief na Tai? Huyo Bitozi tu...!!
ReplyDeletemdau wa kwanza apo umenena,machifu wa sa iv mabitoz
ReplyDeleteAnon wa kwanza baambie, baelesee batalokota benyewe kulunyavu,Ndio tabu hiyo, ya kutawazwa chienyeji cheenyeji, kama kudumisha mila eleweka kisawasawa, usilete maridadi sana maridadi sana tai shingoni ngwabi na skuna.xsizj
ReplyDeleteMachifu, walikuwa zamani, na kwa sasa baadhi nchi za kusini mwa Afrika na Magharibi. Mdau juu hapo yupo sawia kabisa, haya yamezuka lini tena? Zamani machifu walikuwa wana sauti kubwa, labda kama ma gavana wa maeneo yao, sasa huyu brazaman yeye ni kama nani kule Tabora? Au ndio anatumia jina apate ulaji. Maana baada ya uhuru mambo haya yakawa hamna. Vaa kibwaya, ngozi, mapembe, manyoya kama babu zako, au ndio modern chifu? Tuacheni jamani, na mie itabidi nilitembelee bunge maana babu yangu marehemu Pazi Kibasila, nae alikua chifu.
ReplyDeletekha...umangi na uchief si ulifutwa jamani? Inakuwaje leo bunge linamruhusu huyu kutembelea bungeni? Kha...kweli hili ni kofi kwenye shavu la wachagga!
ReplyDeleteSamahani wadau naomba nitofautiane na watu wanaopenda Uchifu, binafsi nachofahamu Mwalimu Nyerere ali-abolish Uchifu, sasa huyu Chifu Bungeni ameenda kufanya nini?
ReplyDeleteMachifu wengine waliotawala Unyenyembe ni Katwanga, Mputa, Mpopo, Kabundi, Nsonso, Mmanywa, Mgalula, Swetu, Fundikira I, Mwasele, Kiyungi,Isike, Nyaso, Kalunde I, Said Fundikira, Kiyungi II, Mkasiwa, Fundikira II na Abdallah Said Fundikira III.
ReplyDeleteIfuma Rashidi Kihiga (Alichaguliwa kwa zengwe desemba mwaka jana, kabla ya mahakama kuu Tabora kutengua uteuzi wake mwezi uliopita na kumkabidhi, huyo yanki pichani)
Ndio ulifutwa na wakina Mwinyi na Mkapa wakaurudisha kwa Azimio la Zanzibar, kimya kimya kwa sababau hawakuamini ndoto hiyo ya kutokomeza u-Chifu!
ReplyDeleteEti, wanatuhubiria wana"muenzi Mwalimu"!
Waache kutudanganya!
Uchifu ni Mawazoni na busara na namna unaishi na watu sio tai wala shanga kiunoni
ReplyDeleteWaheshimiwa naomba nielimishwe. Hivi hawa ni watoto wa marehemu Fundikira? Just curious...
ReplyDeleteHebu acheni ushamba nyie!tunajua rangi yenu nyeusi kama polish ya viatu lakini kwani akili yenu pia nyeusi?watoto wote wa machifu yanasoma kule usa na wanapata elimu boro...nyie mnazubaa kubeba maboksi na kututumia picha zenu za kijinga kijinga...mie nasema bora tuwarudishe machifu kifaragha ili waiokoe nchi hii kutoka kwenye makucha ya wajinga!!!
ReplyDeleteMwalimu alizuia uchifu lakini cha kushangaz anyumbani kwake kwenyewe kuna machifu, si mnaona unafiki wa mzee kifimbo cheza na udikteta humo humo? Kweli mwalimu aliongoza zama za wajinga ndiyo waliowao. Alikuwa msomi msiri sana ndiyo maana Tanzania haitaendelea.
ReplyDeleteNaomba kuuliza. Hiyo ni kidude gani kichwani mwa chifu?
ReplyDeleteHicho kidude kichwani ni taa ya dakitari wakati wa upasuaji ili aone vizuri!
ReplyDeleteAnon 23 july,1:18 umekosea, umekosea, hiyo ni taa ya kuingia nayo mgodini kwenda kujichimbia mwenyewe kwa mkono wake ....
ReplyDeletekadude kichwani kanaitwa SHING'WANDA
ReplyDeleteanon wa July 22, 2008 4:30 PM, sidhani kusema kumuenzi baba wa taifa ina maana tufanye au tukubaliane na kila alichofanya. Imefika muda muafaka sasa ambao inabidi tukae na tumkosoe katika mambo flani flani. Sio kumsifu tu kama makondoo...kha! Kitu kama siasa ya ujamaa ilituumiza sana! Kuvunja u-chief imetuleta pamoja lakini ukumbuke mila na desturi zetu lazima tuwe nazo pia. Sababu kuu za kuvunja u-chief ni katika ku-'consolidate' urais wake. Machief wangefanya kitu isieleweke humu...duh...Unafanya mchezo...kudadadeki? We mchagga amezoea kupata maagizo kutoka kwa mangi mkuu, leo unakuja kumwambia nyerere kasema hichi na kile...atakuelewa?...hehehe! lakini kama wazungu wasemavyo...there are many ways to skin a cat...sasa mimi nadhani hakufuata njia sahihi, katika kutatua hili tatizo. Angeweza kutumia njia nyingine tofauti za kuleta nchi iwe pamoja pasipo kuua uchief kwa makabila baadhi baadhi tu na kubakiza katika mengine!
ReplyDeleteNawakilisha
mtoto