Miss Vyuo Vikuu 2008, Pendo Laizer, akipiga picha na mrembo wa pili, Johari Abubakary (kulia kwake) na mshindi wa tatu, Siwema Edson (kushoto kwake) baada ya kutangazwa washindi kwenye viwanja vya New World Cinema. Wengine ni mshindi wa nne, Veronica Lukindo (kulia) na mshindi wa tano, Maryce Mzena.
Mrembo aliyefanikiwa kulitwaa taji la umalkia wa Miss Vyuo Vikuu, Pendo Laizer (kulia), akiwa na mshiriki aliyeibuka mshindi wa nne, Veronica Lukindo, wakipozi katika vazi la ufukwenie wakati wa shindano hilo
Baadhi ya warembo walioshiriki kinyang’anyiro cha kumtafuta mrembo wa Vyuo vikuu wakicheza muziki wa utambulisho


Mbona habari imekuja robo robo, hatuambiwi ametoka chuo kikuu gani?
ReplyDeleteHabari bro Misupu, mbona umetupa habari nusu nusu. Hujatwambia vyuo vipi vilishiriki na umetwambia ni nani alishinda lakini hujatwambia alitokea chuo gani, hata mshindi wa pili na watatu pia hatujui wanatokea vyuo vikuu vipi!!
ReplyDeleteMashindano haya ni mazuri, kwanza kwa kujenga ushirikiano wa wanafunzi wanaosoma vyuo tofauti, na pia ni sehemu ya kuendeleza na kugundua vipaji. Hongera kwa walioweka nguvu zao kuyawezesha na kuyandeleza haya mashindano!
Getting sick and tired seeing all these Beauty Contests, can someone find a more constructive things to do with these women than parading them like objects and be judged as who is beautiful than the other?
ReplyDeleteI can see a National Contest to find a candidate to go to Miss World/Universe but all these Miss Kisarawe, Miss Ubungo, Miss Gombero, Miss Shirati, etc what a waste of time and resources !!
Enough is Enough !! Beauty is on the eyes of the beholder, as the saying goes and is only skin deep - please ladies try to invest yourself in more a constructive longterm and durable ventures and projects.
When a man is looking for a wife/girlfriend he does not go to a collection of Miss Nani Who or Miss Nani Where to find one, Got my point? Don't get me wrong I love to see beautiful women just feel we are going overboard with these contests.
Hello Michuzi...long time man.
ReplyDeleteMimi ni hilo vazi la ufukweni tu ndio nina shida nalo. Unless I am wrong lakini naona kama vile hayo ni mavazi ya kuendea gym
Jamani Tanzania inaelekea wapi sasa?! badala ya wasomi kuzingatia masomo na kufanya utafiti ili kuiendeleza nchi yetu inayotopelea kwenye matatizo kibao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, leo wanazingatia mashindano ya kuuza miili na sura tu!? Mwanzoni tukifikiri wanaoshobokea masuala hayo ni watu wasiosoma lakini inaonekana si hivyo. Watanzania tuacheni ufinju wa mawanzo, katika vyuo vikuu ingependeza zidi yawepo mashindano ya kielimu na utafiti na siyo ya miili,ukware na kuimba!Kwani hiyo ndo taaluma tulokuwa nayo pekee! Tuamkeni jamani, mbona mambo ya umiss tunayang'ang'ania sisi tu? kwani nchi hii imekosa masuala mengine muhimu ya kufanywa? mbona hatuweki vikao na vipindi kedekede maredioni au katika televisheni vyakutafuta vipaji vya kielimu, isipokuwa bongo fleva na sura tu? aah jamani msitufanye tukachekwa na majirani, kwa mpango huu ndo hatutafikia leo au kwesho! Bongo Fleva na sura ndo tulokusudiwa, tulale tu na tusijadili lingine lolote muhimu, hebu pitieni blog za wenzetu nchi jirani muone mambo gani muhimu kwa nchi yanyopewa umuhimu.
ReplyDeleteAnko michuni hata ukinibania mi ntasema tu! bora uiweke hadharani!
Wewe anonym 5:24 PM kumbuka kuwa Vyuoni siyo sehemu ya kusoma vitabu na kufanya research peke yake! Urembo na muziki ni taaluma kama taaluma ya sheria ama uchumi. Kila mtu ana kipaji chake na kipaji hicho hicho ndo anachotumia kuibuka na kuwa mtu fulani kwenye jamii. Mashindano haya yamewatoa kina dada wengi tuu, wala hatuhitaji kuwataja hapa. Kwenye taasisi za elimu watu wanahitaji pia burudani baada ya kufanya kazi kubwa ya kusoma na research. Kusoma hakumuondolei msomi sifa ya kuwa mtu asiyependa burudani. Wewe binafsi kama hupendi mambo ya urembo na muzuki usiwatukane wanaopenda kuwa wana ufinyu wa mawazo! Mwenye ufinyu wa mawazo ni wewe unayefikilia kuwa urembo unalenga kwenye ukware!! Pia ukumbuke kuwa Muanzishaji wa blog huwa ana malengo yake, mtu anaweza kuanzisha blog yake kwa ajili ya kutoa burudani, mwingine kuzungumzia ufisadi.... ilimladi mawazo tofauti yanaleta jamii iliyo katika uwiano sawa katika kila nyanja ... uchimi, siasa, burudani n.k
ReplyDeleteMzee, Anon 5:24 PM.
ReplyDeleteHatutakiwi kumlaumu Mzee Michuzi..yeye anatuhabarisha yanayojiri nyumbani. Nasema hivi, YEYE NI MTUMISHI WETU..(No offence Michu, najua umepanipata; usikonde majita). Anyway, kuna blogs hata za Kibongo zinazozungumzia hayo unayotaka yazungumziwe, mfano ni blog mpya ya dogo Peter: http://wakatinihuu.blogspot.com/
Lakini, hii blog YETU ndio mama na baba lao. Sometimes kumfurahisha kila inakuwa ngumu. Halafu huu ndio msimu wa ma-miss Bongo. Nimemaliza.
Niite B.
ps: Nadhani angekuwa anatoa namba za hawa ma-miss watu wasingelalamika (LOL). Ni kipindi cha mpito...