18/01/87: wanamuziki toka bendi mbalimbali waliojiunga pamoja na kuunda tanzania all stars band wakiwa katika kutekodi nyimbo zao kwa ajili ya kutengeneza santuri na tanzania film company katika ukumbi wa mbowe. toka kulia ni muhidin maalim gurumo (juwata), max bushoke (sikinde), marijani rajab (dar international) melisa na zahir ally (jkt), fresh jumbe (dar international) nana njige (vijabna jazz) mabruki (mwenge) na hamisi (jkt). nyuma kulia ni dj seydou

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2008

    hapa mimi bado sijaanza kuingia mambwewe na mimi nilianza mwaka -79

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2008

    Hii siku sitaisahau. Siku hiyo walikutana miamba wa sauti na kupiga ala. Hili halikuwa onyesho isipokuwa walikuwa wametumia ukumbi wa Mbowe kurekodi nyimbo mbili mahususi: Kumbukumbu ya Samora na Fagio la Chuma.

    Babake, Marehemu Dozza/Doser (Marijani Rajabu Mwana wa Manyema Jabari la Muziki. Mwenyezi Mungu Mrehemu kwa Amani. Amen.) katika nyimbo ya Samora alighani verse ya Kiarabu mpaka vinyweleo vya mwilini na nywele za kichwani zikanisimama.

    Siwezi kuelezea ile kazi ilikuwa ni ya kiwango cha juu mno.

    Mwamba, kila aliyekuwemo kwenye kundi lile alikuwa nguli. Kila safu ilikuwa imewekewa manguli si waimbaji, si wapiga magitaa, si wakong'otaji drums na tumba, si wapuliza midomo ya bata, matrumpet, matrombone. Nilizimia kuona kwenye safu ya brass walikuwa mpaka na mpiga Picollo. Yaani ilikuwa shughuli pevu iliyotayarishwa na kufanikishwa na magwiji katika fani.

    Mzee Mapili kusanya tena watu wa kazi wamwage kitu kingine kama kile. Halafu mrekodi na kufanya tour ndani na nje ya Tanzania. Pia iwe ni fundisho kwa vijana wa sasa na wale wanaopromoti muziki wa sasa. MZEE MAPILI NAKUOMBA TENA WAKUSANYE MANGULI WAMWAGE KITU KAMA KILE. ASANTE.

    Nakumbuka Bassist Chris Kazinduki wakati jamaa wanamaliza shughuli alikubali kwamba lile kundi na ile kazi ilikuwa excellent.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2008

    Tuwekee picha sa mashindano ya break-dance kina mzee bachu,Omari na marehemu Fatuma Disco-Dancer.Na kulikuwa na mcheza show moja kiwete jina limenitoka.Roller boggie pia ilinoga,tuwekee tunaomba

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2008

    Hiki kisanga kilitokea kwenye Bar/club/ukumbi moja enzi za tisini kweusi.
    Nchondo pujo,Remmy pujo,chikinde pujo ukichanganicha purugu.
    Watu wewewe :),:)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...