Timu ya Tanzanite F.C.ya jiji hapa, ilishindwa kutamba na kutimiza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Indoor kwa mara ya pili mfurulizo richa ya kupewa nafasi kubwa. Timu hii , Ijumaa usiku ilijikuta ikitolewa ktk nusu fainali kwa njia ya matuta na timu ngumu ya Real Tuzus.

Tanzanite F.C iliyokuwa imepungukiwa na wachezaji wake wawili wa kutumainiwa,Elvis "Gazza" na Fred "Capt. Dunga" (kwa kuwa majeruhi), iliweza kuonyesha kandanda safi kama kawaida yao.

Lakini kutokuelewana baina ya wachezaji wa kati na mabeki kulisababisha timu hiyo kuruhusu magoli mawili ya haraka haraka ktk dakika za mwanzoni kabisa za kipindi cha kwanza.

Hata hivyo, hali hiyo haikupokelewa kwa mshituko na vijana wa Tanzanite F.C. ambao walitulia na kuendelea kusuka uelewano baina ya idara zote ndani ya uwanja.

Haikuchukua muda, mshambuliaji Bashiri Chuma "Torres" akamchambua kama karanga golikipa wa Real Tuzus na kuandika bao la kwanza.Dakika sita baadae,mfungaji tegemeo wa Tanzanite F.C, Malik "Goal-Getter" akapachika bao la pili na kupeleka matokeo kuwa 2 - 2 .

Kuanzia hapo mchezo ukawa ni vuta nikuvute hadi mapumziko,toka kipindi cha pili na hata muda wa nyongeza mambo yakawa yale yale.Ndipo muda wa matuta ulipofika.

Kwa mujibu wa sheria za soka ya ndani(Indoor), kila timu ikatakiwa kupiga penati 3. Laaa hauraaaa, siku haikuwa ya Tanzanite F.C. hivyo iliweza kupata penati moja tu kati ya 3.

Penati hiyo iliwekwa kimiani kwa ustadi na kiungo mshambuliaji, Ligalize.Hadi mwisho,Tanzanite F.C ilifunga penati moja na kukosa mbili na wapinzani walifunga mbili na kukosa moja( 1 - 2 ) ,matokeo kwa pamoja ( 3 - 4).

Hivyo ndivyo Timu hii ya Watanzania wanaoishi Atlanta walivyolazwa ktk matuta. Mshindi ktk finali aliweza kujipatia $1,500 taslimu pamoja na kombe na mshindi wa pili alikamata $600 pamoja na kombe.

Tanzanite F.C. kwa sasa inaelekeza mtazamo wake zaidi kuisajili timu ktk Ligi Daraja la Tatu hapa hapa Atlanta inayotazamiwa kuanza mwishoni mwa mwezi wa Tisa.

Mwisho kabisa tungependa kuwakaribisha Watz wote wenye vipaji vya soka kuhamia ktk jiji hili la Atlanta ili tuimarishe timu kabambe na kufungua ukurasa mpya wa historia kwa kuitangaza zaidi Tanzania kwa njia ya soka na madini yetu ya Tanzanite.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Tanzanite F.C.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2008

    Big Up, Tanzanite F.C

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2008

    si mbaya sana.mmekufa kiume wanangu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2008

    Big up TFC.. mmejitahidi sana.. and the BBQ was off the chain.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2008

    Big up 2 you all Tanzanite FC. That bbq was wonderful..... Can we have another bbq b4 summer ends?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...