Jeshi la Polisi limetoa ripoti yake kuhusu uchunguzi wa kile kilichodaiwa vitendo vya kishirikina Bungeni karibu mwezi mmoja uliopita ambapo ilidaiwa mmojawapo wa wabunge alionekana akimwaga unga kwenye viti mbalimbali.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa (kati ya niliyoyanasa kwa haraka)a. Hakuna Kamera iliyozimwa kuanzia mwaka 2006 (don't ask me walisema zilikuwa zimezimwa)

b. Kwenye mkanda uliodaiwa hakuna mtu aliyeonekana akifanya jambo lolote lile (mkanda mtupu?)

c. Vumbi lililoenda kuchunguzwa halikuwa na sumu yoyote inayotambulika.

d. Hakuna kitendo cha kishirikina.

Hayo yamesemwa na Kamanda huyo wa Mkoa Bw. Omar Mganga alipotoa taarifa kwa Kamati ya Uongozi ya Bunge kuhusu uchunguzi huo uliofuatia matukio ya wiki chache zilizopita. Vyanzo vingine vinasema kuwa kati ya mambo yaligundulika katika uchunguzi huo ni pamoja:a.

Kamera mbili kuwa mbovu kwa muda mrefu bila ya kufanyiwa matengenezo na nyuingine mbili zilikuwa zimegeuzwa (tilted) ingawa sijui zilikuwa zinaangalia upande gani!

b. Na mojawapo ya madai ya kushtua kabisa ambayo wenu mtiifu ameyasikia ni kuwa baadhi ya watu wanaolipwa kuzikodolea macho hizo kamera walikuwa wameuchapa!

Uchunguzi huu unatulazimisha kujiuliza kama kweli bila ya kuwa na mfumo mzuri unaohakikisha uhuru wa taasisi zetu tunaweza kweli kuendesha uchunguzi wowote ambao matokeo yake yakashawishi uaminifu?

Baada ya uchunguzi wa TAKUKURU kuhusu Richmond ambao baadaye ulioneshwa na Kamati Teule ya Bunge kuwa ulikuwa umelenga kupotosha jamii, hatuna budi kujiuliza tena kama vyombo vyetu viko huru na vinaweza kuaminika.

Endapo hatuwezi kuwaamini hawa ambao wamepewa jukumu hilo la kufanya uchunguzi na kutoa taarifa au kufanyia kazi taarifa basi inakuwa vigumu sana kuhakikisha kunakuwepo na utawala wa sheria.

Mfano mzuri ni suala la uchunguzi wa EPA ambao ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi sita. Hadi sasa hakuna anayejua kinaendelea nini baada ya Mwanyika na timu yake kushindwa kutekeleza kazi hiyo ndani ya miezi sita licha ya ushahidi wote kukusanywa na kupelekwa mbele yao?

Kwa mtindo huu sidhani kama tutafika, tutaendelea kuzugwa, kuzugana, na kuzugika. Sikiliza matangazo haya "live" kupitia KLHnews.comTitle: KLH News Episode: Uhuru wa Taasisi zetu, kiini cha Utawala wa sheria!
http://mwanakijiji.podOmatic.com/
entry/2008-07-10T21_27_18-07_00

Enjoy!
http://mwanakijiji.podOmatic.com/mymedia/thumb/13384/300x300_1093106.jpg

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2008

    akuna mtu yeyote amesema unga ulikua na sumu. mtanzania yeyote anajua wachawi wanatumia unga, poda, vumbi na vingine vingi. swali la kujiuliza ni unga huo ulifikaje bungeni na kwa matumizi gani?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2008

    Hii ndo BONGO bwana mwisho wa yote HAKUNA cha EPA , RICHMOND wala nini na watu watajinafasi kwa raha zao ( TATIZO LINAKUJA ' NANI ALIYE MSAFI AMNYOOSHEE KIDOLE MWENZIE '

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2008

    Wadau nawauliza tunawezaje kujua kuwa hapa hakuna ushirikina? Maana mkemia mkuu anaweza kuongelea sumu sijui kama yeye au kamanda wa polisi wanao utaalamu wa kusema hakuna ushirikina!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...