Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Thobias Andengenye,akionyesha baadhi ya silahawalizotumia majambazi wakati wakitaka kuvunja benki ya NMB Wilayani Kilombero. Nyuma ni magari yaliyotumiwa na majambazi hayo. Katika tukio hilo watuhumiwa wa ujambazi sita waiuliwa na wngine mawili wanashikiliwa na polisi wakati mmoja alifanikiwa kukimbia.
Na Eline Shaidi,
Morogoro
MMOJA kati ya watuhuhiwa wawili wa ujambazi wanaoshikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za kutaka kupora fedha katika benki ya NMB tawi la Kilombero, alikuwa ni Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, imedaiwa.
Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Thobias Andengenye wakati akiongea na Habarileo ofisini kwake.
Andengenye alimtaja Mtuhumiwa huyo kuwa ni Mwichande Mwinkindo (41) ambaye ni Mkazi wa Kimara B Jijini Dar es salaam,katika tukio hilo alikuwa ni dereva wa gari aina ya Toyota Hilux Pick Up,lenye namba ya usajili STJ 6154.
Alisema jambazi hilo,ambalo hivi sasa limeachishwa kazi katika ofisi hizo kutokana na kuhusika na tuhuma zingine za wizi anazokabiliwa nazo, katika kituo cha polisi Mkoani Dodoma.
Hata hivyo kamanda wa polisi hakuweza kuweka bayana tuhuma ambazo anakabiliwa nazo jambazi huyo,ikiwa ni pamoja na nyadhifa aliyokuwa nayo wakati akifanya kazi katika ofisi hizo kutokana na maelezo kuwa bado wanaendelea kufanya nae mahojiano zaidi.
Kwa upande mwingine Kamanda Andengenye alisema mpaka hivi sasa miili ya majambazi sita yaliyouwawa jana katika tukio la kurushiana risasi na polisi,bado ipo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo kwenye Hospitali ya Mkoani hapo.
Alisema majambazi hayo bado hayajafahamika majina yao,na hivyo jeshi hilo bado linaendelea na utambuzi zaidi dhidi ya watu hao,ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya uchunguzi zaidi.
Tangu jana maelfu ya wananchi na wakazi wa Mkoani hapa,wamekuwa wakifika katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti kwa nyakati tofauti kwa ajili ya kutambua maiti za majambazi hayo.
Majambazi hayo yakiwa na vifaa mbalimbali zikiwemo silaha za moto,yaliuliwa na polisi Mkoani hapa,Julai 19 majira ya saa 7 usiku,baada ya kufanikiwa kuvunja benki ya NMB,na kutaka kupora fedha katika benki hiyo.
Hata hivyon waliwahiwa na polisi kabla ya kufanikiwa katika zoezi hilo.


Hongera Jeshi la Polisi - Morogoro.
ReplyDeleteMajambazi yanastahili kufa kabla halijakuwahi. Keep it up Jeshi la Polisi!
Waziri Mkuu Ajiuzulu kwa kutomlipa vizuri mfanyakazi wake hadi ameenda kuvunja Banki. Hiyo ni aibu...!! Just Kidding...!! Ila Lazima serikali ihakikishe magari ya serikali hayafanyi kazi baada ya saa za kazi. Kwanini tunaona hayo ma STJ mitaani, kwenye mabaa baada ya saa za kazi? Kama mtu anaenda Bar, kwanini asitumie gari lake binafsi. Hii ni aibu kuona hadi saa nane usiku magari ya serikali yanazurura mitaani, sasa unaona yanatumika kuvunja ma-bank....tumuamini nani kama siyo serikali....????
ReplyDeleteMdau-USA
Hongera polisi morogoro.
ReplyDeleteNamuona Saba sita katulia kabisa
Wapi na wapi mkuu wa polisi kuvaa "suti" yaani nguo za kiraia kazini, hata huku majuu wakuu wa polisi huvaa nguo za kazi, I mean uniforms hata ma-Generals, hata wakuu wa FBI na MI5, wacha hizo tunataka kuona polisi visible wakivaa uniforms hata kama SAID MWEMA.
ReplyDeleteJamani Saba Sita kiboko yao kumbe upo Moro, sijui anacheo gani sasa?
ReplyDeleteKijana wa Arusha na Moshi, 76 NDIO UMEFANYA MAMBO NINI? MAANA UNA HISTORIA KIJANA
ReplyDeleteThere must be Kenyans inside the scandal
ReplyDelete