Rais wa Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) Shaban Mintanga, jana amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya kula njama akiwa na wenzake sita ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine kilo 4.8 zenye thamani ya milioni 120 kutoka Tanzania hadi Mauritius.
Rais huyo alisomewa mashtaka yake na Mwendesha Mashtaka wa Polisi,Charles Kenyela.Iilidaiwa na mwendesha mashtaka kuwa Rais huyo alikula njama hiyo Juni 3,mwaka huu.Aidha,Kenyela alidai kuwa katika shtaka la pili,Mintanga mnao Juni 6,mwaka huu alisafirisha dawa hizo kwa kushirikiana wenzake hao sita.
Mintanga alikana mashtaka yote mawili.Mintanga alirudishwa rumande huku akiwa amekosa dhamana kutokana na kesi yake kutokuwa na ruhusa ya dhamana. Habari zaidi soma katika gazeti la HabariLeo kwa kubofya hapa


Haisaaidii kitu nchi kama nigeria watu wanapigania kuingia serikalini kwa msemo wa chuma uondoke hivyo kujiuzuru ni part ya mkataba mtu aliojiwekea kwenye kichwa chake akishapata anachostahili anaondoka kwa gia hiyo halafu hamna lolote linafanyika hata haop kina ed na wenzake walipata ushauri huo toka management ya juu ili kuepuka kuwajibishwa ambapo mara nyingi na si tz unafunguliwa mashitaka....na wewe michuzi tabia ya kutuuliza imekaaje kwa kutusanifu wakati unajua a to z hatutaki hata wewe ukiboronga kumpiga picha jk atakustua ujiuzuru kabla hujawajibsjhwa wewe michuzi unaijua serikali kuliko unavyojijua mwenyewe hivyo tuacheni tu na umaskini wetu tukiweza tutafika kwa kujikongoja hivyo hivyo tukishindwa ndo imetoka hiyo watoto wetu watatafuta makaburi yenu nyie wote.
ReplyDeleteKAKA MICHUZI HII SERIKALI YA KIBONGO IACHE KUTUZINGUA KAMA WAO WANACHUKUA FEDHA ALMOST ZOTE ZA NCHI, HAWASHITAKIWI KWA KUJIFANYA HAWAJUANI, KWA NINI LEO WANAMTOLEA MACHO RAIS WA NDONDI WANATAKA AJIKIDHI VIPI MAHITAJI YAKE NA HAYA MAMBO YA GLOBAL FOOD CRISIS PAMOJA NA FUEL CRISIS????????? MARA MIA YEYE NI MFANYA BIASHARA KULIKONI YALE MAFISADI YALIOCHUKUA MABILIONI NA KUWAAACHA RAIA WEMA HASWA WANAWAKE NA WOTOTO WAKITESEKA.
ReplyDelete