Watu sita wamekufa jana jumatano katika ajali ya barabarani wakati gari la abiria lilipogongana na gari la mizigo maeneo ya Bungi, kiasi cha kilomita 15 kusini mwa Zanzibar.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja, afande Rashid Seif Khamis, akithibitisha juu ya ajali hiyo ameiambia globu hii ya jamii kwamba gari la abiria lilikuwa likielekea mjini wakati lile la mizigo lilikuwa likienda shamba.
"Hii ni ajali mbaya kabisa kutokea visiwani humu katika miaka hii ya karibuni"' alisema kamanda Khamis.
Shuhuda mmoja katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja alisema pahala hapo palijawa na hekaheka za majeruhi na wafu kuletwa, huku wananchi wakikimbilia hospitali kuangalia ndugu, jamaa ama marafiki waliokumbwa na ajali hiyo.
Alisema shuhuda huyo kwamba walishuhudia gari hilo la mizigo likilivamia la abiria kwa kishindo kikubwa.
Alisema shuhuda huyo kwamba walishuhudia gari hilo la mizigo likilivamia la abiria kwa kishindo kikubwa.
Ajali za barabarani kwa Zanzibar ni chache mno lakini kwa siku za hivi karibuni zimekuwa zikiengezeka sana sana kwa uzembe wa madereva na mwendo wa kasi.
Ni ajali mbaya sana katika historia ya znz, mke wa rafiki yangu wa Paje alifariki na tumemzika jana kijijini kwao Dunga. Poleni wafiwa wote, muwe na subura, kila roho itaonja mauti
ReplyDelete