
Bash hilo ambalo mwaka huu lategemea kuwa bora zaidi ya yale yaliyopita, linaendelea kuboreshwa kwa kuhakikiwa pande zote za Michezo, Burudani, Vyakula na mjumuiko wa pamoja wa kifamilia kwa wanajamii wote wa ki-Afrika waishio maeneo ya karibu na wale wa mbali watakaoweza kujumuika.
Ijumaa ya tarehe 29 mwezi huu (Aug. 29) katika ukumbi wa Mirage Hall uliopo Hyattsville Maryland. Siku ya Jumamosi ( Aug. 30) itakuwa ni JusteLounge iliyopo Bethesda Maryland na kisha siku ya Jumapili (Aug.31) tutarejesha shughuli Mirage Hall kufunga week end.
Jioni za Jumamosi na Jumapili (Aug 30 & 31) kutakuwa na michezo ya soka na nyama choma katika viwanja vya michezo na mapumziko vya Middlebrooke Maryland.
Moja kati ya ahadi za uhakika kwa upande wa burudani ni muziki wa "kufa mtu" toka kwa mkali wa mixing wa clubs mbalimbali hapa Washington DC na pia 93.9 FM (WKYS Radio) Dj Joe.
Joe ambaye ameshathibitisha ushiriki wake, amesema amejiandaa vema kutoa burudani ya aina yake kwa wale wote watakaohudhuria.
Nyote mnakaribishwa
Warning: hapo juste lounge ni padogo sana, tafuteni ukumbi mkubwa.
ReplyDeleteLabda niwe msaada kwa Da'Titi.
ReplyDeleteJamani msiende DC, mie mwenyewe ntakuwepo na mshaniona kwenye blog za utupu. Mtanioneshea vidole bure mkinitambua. Kwa hiyo msiende ili raha nile na wasionijua.
Ni hayo tu kwa leo
TITI
Ndio, namsapoti anony wa kwanza aliyesema Juste padogo. Nishaahirisha maana ndio hiyo niliyokuwa nataka kwenda. Halafu contact ni nani? Tunalipa before or mlangoni, kutolewa nishai sitaki. Na huko Mirage napo michosho ukumbi utafikiri tupo Tip Top, Manzese.
ReplyDelete