

Michu,
Nimezipenda zile picha zako za zawadi kwa wadau wa blogu yetu ya jamii. Nami nimeitikia wito kama utazipenda picha hizi chache nilizopiga njia hiyo hiyo uliopita wewe kwenda Dodoma ila mimi nimepita mchana. Ama kweli bongo tambarare!
Mdau Isaack Kibodya
--------------------------------------------------------
Mdau Kibodya,
asante na hongera kwa kazi nzuri pamoja na kuitikia mwito. Naendelea kukaribisha wadau wanaopenda kupiga picha wajiunge kwenye libeneke hili
Michuzi
bongo mazingira safi san but umaskini tuu ndio unatutatiza.
ReplyDeletenaona uko ndani ya benzi boss?? hongera
Happy Birthday Issa Michuzi 28 August is you are Birthday mate.Mbona ujipongezi Wewe..........................hahahaha
ReplyDeleteT hapa London
Kibodya hongera naona ulikuwa na Masedesi Benzi.Ndio manedeleo hayo Hongera sana
ReplyDeleteBongo tambarare kwasabau kachukua hizo snap kutoka kwenye benzi lake, kwanini hamkuweka image za yule mkereketwa wa CCM pale karibu na Korogwe pale kwenye njia inayoingia kwenye ile restaurant ya highway, jamaa anakaa kwenye kijumba kama kiota cha ndege wakati pembeni pana mnara wa mamilioni wa mtandao mmoja wa simu TZ.
ReplyDeleteMichuzi kama watu wote watakua na msimamo kama wako basi nchi hii haitafika kokote, tuna vizuri na vibaya Tz lakini wewe wakimbilia vizuri, tuonyeshe pia vibaya.
Mficha uchi hazai, bila kuyaweka hayo matatizo hadharani unafikiri watu wataamka lini kuyajadili ili penginepo tupate ufumbuzi.
Tanzania sio ya matajiri tu, na sisi masikini tunataka tuonekane umasikini wetu.
Comment uiweke usiiweke ujumbe umeshaupata
mnajua kwanini allien ni most horrific movie? juu director hukuonyeshi allien mwenyewe ila udenda pekee. anawaachia watazamaji wamalizie wenyewe akilini mwao.hivo watu wanamalizia kwa kuimagine ni jinamizi laa ajabu.lol. inaitwa kucheza na akili za watazamaji. hapa naona huo mchezo umetumika. picha nzuri saana na kinachomalizia ni hiyo nembo ya benzi.watu wadau wanamalizia ni bonge ya benzi hawajuu hata benzi ya miaka ya 60 inaweza kuwa na nembo hiyo.. good art. nimependa saana hizi picha
ReplyDeleteDoo.Kibodya jamaa wanakupiga vidongo.
ReplyDeleteHAPA UTAKUWA UMEMSAIDIA YULE MDAU ALIYEDAI ETI BARABARA YA DODOMA-DAR INA MIVUMBI (WAKATI WA AJALI YA BWANA PASCAL MAYALA)
ReplyDeleteASANTE, SNEPU ZIMETULIA
mjomba naona uko ndani ya msede, mambo yako mswano. mie naomba kama unayo ile ya keep left cha nanihii
ReplyDeleteMimi ninawasiwasi hili gari lilikua la mheshimiwa fulani, kwahio barabara ikafungwa kwa muda ili huyo mheshimiwa apite kwa usalama!
ReplyDeleteMbona hii barabara imekua kama private? hakuna hata gari lolote? tena picha yenyewe ilichukuliwa mchana
Picha ya keep left bado naitafuta katika makabrasha yangu niliipata tutamwomba Issa aiwakilishe. Kuhusu barabara kuwa haina magari, mi nadhani ni uzoefu tu ukizoea kuendesha safari ndefu basi utajua ni wakati gani wa kusafiri na muda gani wa kupita maeneo fulani fulani.Ukiondoka Dar majira ya asubuhi na mapema basi tegemeo ni kuwa utafika maeneo haya kukiwa bado mapema na magari sio mengi hali kadhalika ukiwa umetoka (mathalan) Dodoma saa moja asubuhi utafika Kibaha kuelekea Dar wakati mwafaka na hivyo kuuwahi usumbufu wa Kimara/Ubungo wa foleni za magari.Taratibu hii inapunguza usumbufu, msongamano wa magari na pia hupunguza ajali za kizembe.Wala haina lazima kuwa na dhana ya gari la mkubwa fulani!
ReplyDeleteNawakilisha!
wape kibodya....maana watu mnachonga tuu wakati sanasana mmefika mbali ni ubungo. safari za dodoma tuachieni siye tui-enjoy. dodoma ah, chako ni chako ah...na mtasema ile "Rose Garden" ya dodoma nayo haifai kuwa Dodoma?
ReplyDelete