Michu,
Nimezipenda zile picha zako za zawadi kwa wadau wa blogu yetu ya jamii. Nami nimeitikia wito kama utazipenda picha hizi chache nilizopiga njia hiyo hiyo uliopita wewe kwenda Dodoma ila mimi nimepita mchana. Ama kweli bongo tambarare!
Mdau Isaack Kibodya
--------------------------------------------------------
Mdau Kibodya,
asante na hongera kwa kazi nzuri pamoja na kuitikia mwito. Naendelea kukaribisha wadau wanaopenda kupiga picha wajiunge kwenye libeneke hili
Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. bongo mazingira safi san but umaskini tuu ndio unatutatiza.
    naona uko ndani ya benzi boss?? hongera

    ReplyDelete
  2. Happy Birthday Issa Michuzi 28 August is you are Birthday mate.Mbona ujipongezi Wewe..........................hahahaha
    T hapa London

    ReplyDelete
  3. Kibodya hongera naona ulikuwa na Masedesi Benzi.Ndio manedeleo hayo Hongera sana

    ReplyDelete
  4. Bongo tambarare kwasabau kachukua hizo snap kutoka kwenye benzi lake, kwanini hamkuweka image za yule mkereketwa wa CCM pale karibu na Korogwe pale kwenye njia inayoingia kwenye ile restaurant ya highway, jamaa anakaa kwenye kijumba kama kiota cha ndege wakati pembeni pana mnara wa mamilioni wa mtandao mmoja wa simu TZ.
    Michuzi kama watu wote watakua na msimamo kama wako basi nchi hii haitafika kokote, tuna vizuri na vibaya Tz lakini wewe wakimbilia vizuri, tuonyeshe pia vibaya.
    Mficha uchi hazai, bila kuyaweka hayo matatizo hadharani unafikiri watu wataamka lini kuyajadili ili penginepo tupate ufumbuzi.
    Tanzania sio ya matajiri tu, na sisi masikini tunataka tuonekane umasikini wetu.
    Comment uiweke usiiweke ujumbe umeshaupata

    ReplyDelete
  5. mnajua kwanini allien ni most horrific movie? juu director hukuonyeshi allien mwenyewe ila udenda pekee. anawaachia watazamaji wamalizie wenyewe akilini mwao.hivo watu wanamalizia kwa kuimagine ni jinamizi laa ajabu.lol. inaitwa kucheza na akili za watazamaji. hapa naona huo mchezo umetumika. picha nzuri saana na kinachomalizia ni hiyo nembo ya benzi.watu wadau wanamalizia ni bonge ya benzi hawajuu hata benzi ya miaka ya 60 inaweza kuwa na nembo hiyo.. good art. nimependa saana hizi picha

    ReplyDelete
  6. Doo.Kibodya jamaa wanakupiga vidongo.

    ReplyDelete
  7. HAPA UTAKUWA UMEMSAIDIA YULE MDAU ALIYEDAI ETI BARABARA YA DODOMA-DAR INA MIVUMBI (WAKATI WA AJALI YA BWANA PASCAL MAYALA)
    ASANTE, SNEPU ZIMETULIA

    ReplyDelete
  8. mjomba naona uko ndani ya msede, mambo yako mswano. mie naomba kama unayo ile ya keep left cha nanihii

    ReplyDelete
  9. Mimi ninawasiwasi hili gari lilikua la mheshimiwa fulani, kwahio barabara ikafungwa kwa muda ili huyo mheshimiwa apite kwa usalama!
    Mbona hii barabara imekua kama private? hakuna hata gari lolote? tena picha yenyewe ilichukuliwa mchana

    ReplyDelete
  10. Picha ya keep left bado naitafuta katika makabrasha yangu niliipata tutamwomba Issa aiwakilishe. Kuhusu barabara kuwa haina magari, mi nadhani ni uzoefu tu ukizoea kuendesha safari ndefu basi utajua ni wakati gani wa kusafiri na muda gani wa kupita maeneo fulani fulani.Ukiondoka Dar majira ya asubuhi na mapema basi tegemeo ni kuwa utafika maeneo haya kukiwa bado mapema na magari sio mengi hali kadhalika ukiwa umetoka (mathalan) Dodoma saa moja asubuhi utafika Kibaha kuelekea Dar wakati mwafaka na hivyo kuuwahi usumbufu wa Kimara/Ubungo wa foleni za magari.Taratibu hii inapunguza usumbufu, msongamano wa magari na pia hupunguza ajali za kizembe.Wala haina lazima kuwa na dhana ya gari la mkubwa fulani!
    Nawakilisha!

    ReplyDelete
  11. wape kibodya....maana watu mnachonga tuu wakati sanasana mmefika mbali ni ubungo. safari za dodoma tuachieni siye tui-enjoy. dodoma ah, chako ni chako ah...na mtasema ile "Rose Garden" ya dodoma nayo haifai kuwa Dodoma?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...